Menu

   

PDF Print E-mail

Waswaha Abroad

 

(C) The Full Picture - 8. Conclusion

 

Majuu

 

Kukhitmisha/Konklushen ya konklushen

(hitima ya marhemu fulani, khitma ya mji, khitma ya nti na khitma ya ulimwengu - mambo yote)

 

Yaliyomo - Index

1. Madhmuni ya nyinyi kusoma makala haya, na Sairas Jirongo

 

2.Waswahili wa "majuu", na kutambua kweli tuputupu

3. Arkitekt Godfri Mwapembwa, na trejik komedi

 

4. Kumwaga mtama, na 'Ich don't think so!"

 

5.Mjaluo Obama, na "No We Can't!"

6. Fairy tales, na ole wako "ahlu matini"

 

7. 99% kusema huu ulioandikwa hapa ni urongo mtupu, na "Mbona hamrudi kwenu basi?"

8. 1% ya wakutia akili, lakini wasipate chansi hao, washainua!

9. 0.1% watakao kuja "majuu", na sababu za kuwaezesha kuja

10. 99.9% na wishful thinking

 

11. The truth shall set you free

 

Konklushen

12. Bichi ile pale, na friza la Amstadamu

13. Laifu besti, na vunga kufa

14. Malindi ni hii, na Hadhramuti ni hii

15. Kupakata mikono, na Ubwete-stan

16. Afrika Maskini-stan, na "Majuu" Kazini-stan

17. Kupakwa hina

 

18. Usiniharakishe, na Tushauriane

19. Mume n'guvuze

20. Mimba changa, na bomba la chooni

21. East Hamu, na makaburi ya Riyadhus Saalihina

22. Kuswali Kishia kwa swihi?

 

23. Obama na bath satafiket yake

24. "Madiba" Mandela, na "Tabu" Mbeki

25. "Chekbobu" Zuma, na Mulema "Mlemavu"

26. "Yazid" Zizu na mango ya Wald Kapu, na Salma bint Said bin Sultan wa Baitul Mtoni

 

27. Maka Kuu, na Maka Chocho

28. Saa za "Majuu"

29. Agro ya "Matini", na mjani wa Moroko

 

30. "Twabibu" D.J., na homa ya maleria

 

31. Milz and Bun, na kutia mato nuru

32. Kenya Pawa, na hongo za Afrika

33. If wishes were horses, then beggars would ride

 

34. Muusini na brek dauni yake, na ngamia wa Ostrelia

35. Tawakkal ya "Majuu", na tawakkal ya "Matini"

 

36. Watoto wa Waswahili walioko "Majuu", na usemi wa "Kumaamako!"

37. Lubna jubna, na mtoto wake Maliha "Mzungu"

 

38. Sababu ya Mswahili kukataa lugha yake

39. Lugha, chombo cha dini, mila na dasturi

 

40. Kujua Kiingereza = edukeshen? "Bollocks to you!"

 

41. Waswahili wasio Waswahili, na Waarabu wa Pemba

42. Mambo ya kushumiana mikono

43. Sindrela na kiatu chake

 

44. "Breaking in the wild horses" shekhe hakuna haa? Hakuna haja

45. Ahmadi usiniweke skwea wee madha faka!

46. Ukweli, shot en shap

47. No preamble hakuna kubembelezana

 

48. Wanyama mwitu walioko zuu (wa "Majuu" wawaonavyo nyinyi wa "Matini")

 

49. Jee, Wazungu wanazo katika zile ila 27 za Waswahili?

 

50. Mtelezo wa Mol of the Emirets, na bembeya ya Maalim Azizi

51. Jee, Waswahili wa "Majuu" watarudi zao Afrika?

52. Coming to terms with msiba wa "Majuu" - miaka 7, 10, 15 na kwenda juu

 

53. Kuchemsha bongo "Majuu", na kula mraba "Matini"

54. Total Football, na Total Parenting

55. Kukazana kwa D.I.Y.

56. Kundalini Yoga

57. Jakuzi la Arusha

58. Faluda ya Dar, na Bintul Mambasa

 

59. Mtu 72, na 'kadi za jumla'

60. Simu mwenga

61. Baskili, na ugumu wa Mdachi

62. Bangi za Amstadamu, na Waswahili mamilionia wakuuza taimu

63. Masafa ya Emerika, na petroli ya Maskati

 

64. "All that is complex is useless, and all that is useful is simple" - Mbuuni mashhuri Kalashnikov huyo

 

65. Tishu za mkono "Majuu", na tishu za chooni "Matini"

66. Ukitaka maendeleo? Jenga barabara Mchina asema

67. Briji, barabara ya pili ya Kichina

68. Waso hili, na Women Fighters F.C. wa Unguja

 

69. Khalifa - Stop the fukri!

 

70. Ramla wa Breda

71. Wafaa Black Beauty

72. Swalaha na "mjakazi" wake

73. Mbaraka na walaloo wake

 

74. Waswahili mafungu sita

 

75. Omani Daakhilia

76. Jinsi moja, na raha ya mrehani

77. Kwanga ya Kongo, na Reermunya wa Hargeisa

78. Kumbe si tende ni mende

79. Watoka mlango gani?

 

80. Bafulani, na Sago la mtaa

 

81. Kutia mkono gizani

82. Kusema kweli badala ya kuwa ma conmen

83. Mazarau

84. Kuanguka kwa hijabu

85. "Ana mdomo mchafu kaa..."

 

86. Ashiki za KiKamba

 

87. Hamster on a treadmill

88. "Neva trast a man with a moogej"

 

89. Kuula huu, na Vicarious Pleasure

90. Matatu za Shuebu, na THabiti "Mcheki" na baa lake

91. Abdurazaki "Mgiriki", na kitabu cha Nchume S.A.W.

 

92. Tom na matumizi yake ya toilet pepa katika hii riseshen

93. J.J.C., na Siri ya iPhone 4S

 

94. Kufungukwa akili kwa Jon Pita

95. Kujisua "Majuu"

 

96. The solution is to change the mindset

97. Prodyuzaz vasiz Konsyumaz, na tembe za maharagwe

98. Utakula au utabeba?

 

99. Gomba la Yemen

100. Falaji za Omani

101. Mateso ya Suudiya

102. BaHamri wa Imarati

 

103. Haki za kinyama, na haki za kibinaadamu

104. Kujitayarisha kwenda Khaliji, na Mechmeka wa Qabusi

 

105. "Majuu" Jahannam namba 7 (Galfu)

106. Motoni Gredi ya 6 (Emerika)

107. Lugha wazimu mtupu na moto Daraja ya 5 (Yurozoni)

108. Gredi ya 4 ni mabuibui na nyoka wa "Oz" (Ostrelia)

109. Daraja ya 3 ni moto wa Kuzungu (Uingereza na Ailendi)

110. Sauna ya kifemeli moto Gredi 2 (Skandinevya)

111. Moto khafifu zaidi, Waislamu wakosa hawa (Kanada)

 

112. Home Sweet Home

 

113. Ushuzi wa Twita, na mabesti wa Fesbuku

114. Skills London, na black entatenaz

115. The glorified lorry driver (pilot)

 

116. Wigi la Gadafi

117. Mek ap basini, na Bwan "Zanga Zanga"

118. Eda ya sku mbili, na bendera ya Shakida wa Tenesii

119. Kamera ya Lytro, na mbio za Abdurasuli

120. Julia Roberts, na mdomo wa kunuka

 

121. Utalii wa ubakazi, na watoto wa Kigiriama

122. Taisiri "soo mbili", na kukata mbuga

123. Kutafta farasi, na dina za "Majuu"

 

124. Teach them how to fish

 

125. Flu jab, na Barzanji

126. Mtumainia cha ndugu

127. Risasi ya EK, na spitali ya MEWA

128. Convinience Store ya Nyuu Yoki

129. Kila mtu abebe msalaba wake

 

130. Cheese Cake

131. Ne'ema ya kiza

132. LHD, na ma Kleva Fools

 

133. Double Dutch & other complications

134. Rusha Hour, na Figa 8

135. Simple life, na Paranoiya

 

136. Adhabu ya kaburi, na ji taa la SAD

137. Udhu wa winta, na mkojo wa swalaa

138. Tobwe ya Messi, na raha ya mitai

139. Mtoto wa shangazi yako, na your last mistake

 

140. "Disprespecting" matineja, na Fuck You ya ji mama

141. Zegere la watoto, na ji bulldog la park

142. Fifti fifti mali ya talaka, na kuwashuku ma in-laws kabla ma out-laws

143. Friidom ya talaka, na dawa za Dokta Mahero

 

144. Waifu jikoni na Devid, na maji chumbani kutonwika

145. Masharubu ya "Movember", na "sexting" ya LMAO

146. Kuharibika kwa woshin mashn, na fundi wa saa

147. Bathdee yako, na bathdee ya Mtume (SAW)

 

148. Suzana Pomed, na wazimu wa Einstein

149. A face only a mother can love, na kuazimana uso wa drama

 

150. "Are You Shuwa?" ya jamaa yangu, na "Uko mpaka lini?" ya Maskati

151. Stock Exchange ya Wahindi, na mawigi ya Waafrika

 

152. Mishinari stail ya Makka

153. "A little knowledge is a dangerous thing", na "Kumaamako!" ya "Matini"

154. Tuputupu ya mwendaazimu, na kishungi na paja la mwanamke

 

155. Kutofika "Majuu", na self-diagnosis

156. Mtoto mchanga kufungika 

157. Mtoto mchanga kufungika choo, na kuja kali kwa Sharifa

158. Goti la Mu'mini, na upaa wa daktari

159. Kuzaa kwa Swabiha, na cutbacks za riseshen

160. 3rd World ya "Majuu", na self-diagnosiz ya mtandao

 

161. Kifafa cha Mzungu, na mavi kunuka ova maiti

162. Tepe za kijeshi, na mdaa wa "Matini"

163. Dabal Kross ya Ambaro, na shaba za Jibuti

164. Hedhi ya Ariji, na mabanati wa Floo

165. Watoto wa skuli, na swala za Ijumaa

166. "Hupendi konda basi", na plawing yuwa oon faro

 

167. Catching my drift, na wigi la Afro

 

168. Waswahili, the extinct dinosaurs

 

169. Chikungunya, na Dongo Kundu

170. Gari la Maserati, dem chuma, na Mazingaombwe ya Mzungu

 

171. Tufunge dirisha, na habari magazetini

1) "M.J." Gaddafi, na mochar ya Misrata

 

2) Feslifti ya Baluskoni, na chama chake cha "Nenda Kuma"

 

3) Mauwaji ya Siiloni (Siri Lanka)

4) Misukosuko ya Yuro, na ulimwengu kuwa taabuni

5) Maandamano ya "Occupy Wall Street"

 

6) Rayana "RiRi", na "It's not like her shit don't stink"

 

7) Majini wa Kizungu, na kwenda tupu

8) Maradhi ya wasiwasi bil khannas, na OCD

 

9) Man City (6) v. Man U (1), na bwamdogo Mario Balotelli

 

10) Kenya kuivamia Somalia

 

172. Wazimu wa Kofi Annan, na ukiskia hiyo Sense and Sensibility

 

173. Ishara ya "Baby on Board", Mitumba, na Saa ya dola 200

174. Kuzibuka, mato tini, Mzungu kusilimu, na kazi manispaa

175. Mimba ya miezi 8, na saikoloji ya kike

 

176. Bodi bilda vitu, na contactless payment

177. Bunaway kids, na otomatik shopping ya Card Case

 

178. Velyu fo mani, na kisahan cha chai cha Jemshidi

179. Taim flaiz, na Mzungu kujikojolea mabarabarani

180. Kunya kwa installment, kuiga maselebritiz, na "a bunch of wankers"

 

181. Mzungu ku blow dry nyele, na kuleta kilio matangani

182. Kulipa teks, na kuowa mwanamwali boko

 

183. The Last Word - Dua ya kuku?

184. Jogoo la shamba?

 

185. Tutie Fatiha

186. Nitumie barua pepe

 

187. Videos

 

 

8. Conclusion

1. Wewe wasoma makala haya, madhmuni yako ata ukayasoma haya ni nini? Tuanze na swala hili muhimu. What do you want to get out of these articles? Jawabu lako siliskii ukilitamka, lakini najua kuna sampuli mbili ya watu wasomao makala haya. Wa kwanza ni walioko "majuu" na wa pili ni walioko "matini". Wale walioko "majuu" hawana ubishi kabsaa. Wajua kuwa yaliomo hapa kuhusu "majuu" ni  kweli tupu 100%. Hakuna mmoja katika wao atakae bishana. The truth is clear, just like daylight is clear from the darkness of the night. Wao wa "majuu" wakisoma makala haya wengine ni kama pas taimu, they are bored. Lakini wote watatokwa na tozi wajua ukweli na utungu wa maneno haya, na yoyote wa "majuu" atakaye sema vengine huyo ni mroo? Ni mrongo kama yoyote atakayesema kua Cyrus Jirongo wa KADDU hana wake 3.

 

2. Kwa hivyo Waswahili wa "majuu" wote wajua reality ilioandikwa hapa ni kweli tuputupu. Washa ekspirians baadhi ya haya, au yote kama haya, au zaidi ya haya. Ata Wahenga walisema, adhabu ya kaburi, aijuae ni maiti. Japo muulize Mswahili 'Wahenga' ni kina nani hawajui, kama ukimuuliza huu msemo wa 'Asema kaa upatu' au 'Asema kaa chiriku' ukimuuliza huu 'upatu' ni nini au huyu 'chiriku' ni nani hajui. Kwa hivyo "majuu" pana hard work tu, and it is not a joke by any stretch of the imagination.

 

3. Tushamalizana na wasomi wa makala haya walio "majuu". Wao wataka ku re-live ekspiriansez zao, wataka konfameshen kuwa pana Waswahili wengine huku kama wao wanaoipata japo hawajuani, na wataka usabba na kupas taim. Ni kama vile kumsoma the failed akitekt na Mbongo Gado (Godfrey Mwampembwa) na katuni zake kwenye gazeti la Deli Neshen la Kenya. Gado ana michoro ya kutekesha, lakini makala haya kwa wasomaji walioko "majuu" si komedi; makala haya yana stinging tail, maana hiyo adhabu ya kaburi ya maisha yalivyo huku wayajua vizuri sana. 

 

4. Jee, wa "majuu" watanipenda kwa kuandika makala haya? Ni kama Yahudi mtekeshaji Sasha Noam Baron Cohen a.k.a. Ali G na komedi zake kama 'Borat' apendao kusema, "Ich don't think so." 99% ya walioko "majuu" watantukia mno kwa kumwaga mtama kwenye kuku wengi. Sasa mulioko "matini" mushatutambua kwamba wengi katika sisi wa "majuu" ni 'fronting' tu, ma feki twasota huku na wengi katika sisi twanuka ndaa kamwe. Do I care kuwa wa "majuu" watakasirika kwa kumwaga mtama huu? "Ich don't think so, shekhe." The truth must be told. Au chembelecho wasemao, "Sema kweli mvua inyeshe!"

 

5. Sasa basi, ni yapi madhmuni ya wanaosoma makala haya katika walio "matini"? Hawa Waswahili wa huku wajua next to nothing of the reality ya "majuu". Wakiona Mjaluo Obama antaguliwa kuwa raisi wa Emerika wao wapiga makofi waona loo, "majuu" anything is possible. The harsh reality wao hawaijui. The daily grind and the daily struggles za huku wao hawazijui. Wao waona ni "Yes we can!" Ukweli ni "No you can't!" lakini wao kutambua hawatambui. Makala haya madhmuni yake ni kukuelimisha wewe wa "matini".

 

6. Kwa hivyo wa "matini" watafta fairy tales hapa, watafta konfameshen kua kweli wa "majuu" wana gud taimu, na inshallah wao wa "matini" wakija zao "majuu" they will live the dream. Sasa hawa huwa disappointed wakisoma makala haya, waona haiwezekani haya kuwa ni maneno ya kweli. Waona mii ni Abdala Moi nna stimu tu, zikinitoka siwezi andika "comedy" hii. Ole wako kijana!

 

7. Kwa hivyo wa "matini" aspokuta fairy tales basi 99% yao watasema huu ni urongo mtupu japo huo "ukweli" wanaoudhania wao doesn't exist. Na Mswahili aliye "majuu" endae tia raundi "matini" na mashaini yake ya kukopa kwa kredit kadi wakimuuliza kuhusu makala haya pengine watazidi kuwadanganya wawapoteze wawaambie "majuu" mambo poa. Mambo ya moto shekhe. Kwa hivyo 99% wata dismiss haya kuwa huku hakuna tabu wala mateso, na Mswahili sku zote atarudi kwenye rizoning yake ya kizembe, "Kama huko kubaya, mbona hamurudi makwenu basi?"

 

8. Haya, wa "matini" waliobakia, wale 1%, watatambua kua haya ni the harsh reality. Hatuko holidee kempu huku, tuko kwenye kupambana na maisha kila leo kama mulivyo huko Afrika bali sisi twapambana na maisha taf zaidi, ajuae ajua. Sasa basi, katika hawa 1%, 99% yao wakipata haf a chens ya kuja "majuu" bado wata rush kuja hivyo hivyo kama ng'ombe wenye kiu kali walioona maji. Wataka kujionea wenyewe, na wajiona wao ni smati zaidi kuliko walio watangulia kwa hivyo they will make a better life for themselves kuliko sisi tulioko huku. Ni shkio la kufa lisoskia dawa shekhe. 

 

9. Kwa hivyo tuangalie statistiks. Waswahili wanaotamani kutoka miji yao waje "majuu" ni 100%. Realistically, watakao pata nafasi ya kutoka kweli ni pengine 0.1% - pengine aje mume wa "majuu" aje mposa na kumuoa amtukue "majuu", au aje binti wa "majuu" aolewe na kijana wa "matini", au pengine kijana au binti wa "matini" ashinde Green Card Lottery ainue, au pengine babake mshefa ampeleke ng'ambo masomoni ndio ashafika, au apate skolaship aje, au ... n.k.

 

10. Sasa basi, 100% wataka kuja "majuu". Only 0.1% will manage to do so, na hawa watakuja yakubali na kusallim amri kuwa makala haya yasema kweli tupu. Na jee wale 99.9% ya Waswahili waliobakia "matini"? Majoriti watajidanganya pengine watapigwa tochi waje zao huku - it won't happen. Kwa hivyo watabaki bure wawahusudu walio "majuu". Hiyo imagineri laif ya 'The Bold & The Beautiful' huku "majuu" hakuna. Kwa hivyo badala ya wa "matini" kuwa na furaha wakiishi hii one life waliopewa na M'ngu S.W.T. wao wenda na laiti na kunung'unika sku zote. Badala ya to put their minds on something constructive wako kwenye wishful thinking na destructive hatred and jealousy sku zote.

 

11. Kwa hivyo, wasomi wa makala hii walioko "majuu" - nyii mwajua haya yaliyomo humu ni reality. Sina vita na nyinyi. I feel you. Tu kwa hisani zenu musiwadanganye walioko "matini"; sku zote mukisema, semeni kweli. The truth will set you free. Na nyii mulioko "matini", the 0.1% mutakao kuja, "Welcome to Hell." Mutakuja nikumbuka. Na nyii 99.9% wa "matini", muna chois - kuweni na umoja mujiendeleze, au zidini kugawanyana na kufitiniana na kuzozana na kuuzana mufilie mbali nyote kumaamako zenu. Na kwa wale 1% ya 1% ya walio matini ambao watatambua ukweli wa makala haya, I salute you all. Go on and make something of your lives. Sasa basi, tuianze hii konklushen.

 

Konklushen

 

12. Afrika pana simpal life - bahari ile pale, buree. Watu wa 'majuu' wayatamani sana maji haya lakini kuyapata hawayapati. Mswahili wa "majuu" yuko kwenye mapande ya barafu ya Saskachewan au kwenye ubaridi wa friza wa Amsterdamu na maji yake ya makanalz yale pale ayaona lakini kuruka chomo haruki au atakufla mbali kwa baridi.

 

13. Weather jee Afrika? Smati, jua la ng'ara gerentii kila siku deli savis. "Majuu" jee? Watu wana ma dipreshen kwa kukosa miale ya jua. Lakini kama nyii wa "matini" hamujaja huku, mutayajuaje haya? Hamuwezi kujua. Na wa "majuu" daima hakupi rialiti angalau mwenzako ukapata kutambua, bali kila ukimuuliza vipi hali huko "majuu" akwambia "Besti" sku zote. Ukiskia "Vunga kufa" ndilo hili shekhe.

 

14. Na uko ndiani waelekea Malindi au Digo wakuta mandhari ya miti na nyasi ya kijani kibichi, kitulizo cha jicho na cha roho. Ukishafika Dubei au Maskati au Hadhramuut ('mauti yashawadia') ukaona jangwa linkaa vipi uta aprishiyet haya. Au ukiona miti yalvyo kaukizana Winta ya Kanada au ya Norway utaelewa haya. 

 

15. Una ndugu, femeli, maswahiba, miskiti, mambo teletele ya kukupumbaza. Yote haya ni bai bai ukifika "majuu". Na wengi walisema potleyambali wakimbia umaskini wa Afrika, lakini hawakufahamu yale mazuri waliyoyaacha nyumba. Uzito wa mambo haya watakayoyawacha nyuma hawakuyatanabahi mpaka ilpokua too leti tena. Ufikapo "majuu" ni "All change" shekhe. Kiss goodbye to all that you used to know and take for granted. Wale waliokua wakidhania kuwa wakifika huku ndio itakua "Welcome to Ubwetestan" wakajatambua kumbe huku "majuu" hukuja likizo eti, bali ndio unkuja jitia nguvuni kwenye kibarua sugu. Kazi "majuu" sku zote hazishi na mapumziko hakuna. Yaya ni wewe na mfanyi kazi ni wewe. Full stop.

 

16. Kazi Afrika jee? Si Afrika ni "Maskinistan", hakuna kazi wala bazi? Na zikiweko hizo kazi basi zapatikana kwa tabu mno. Lakini guess what? Waswahili hawataki kujisumbua ndio maana haweshi kusema 'Afrika kazi hakuna.' Waswahili hawahawa wakifika:-

- Emerika tu watafagia barabara

- Kanada wataosha vyombo hoteli

- Uingereza watawatamba mavi watoto wachanga na wazee wasojiweza

- Ailendi watawatoza faini madreva waliopaki magari vibaya mabarabarani

- Uholanzi watafagia na kupiga madeki mahospitali

- Ufaransa watauza chizi na chiz keki madukani kama kwa Huseni Bekri

- Speni watatunda machungwa, tamata, mahindi na tumbaku mashambani

- Norwe watazoa barafu mabarabarani

- Ostrelia watakama ng'ombe maziwa

- Dubei watakua maaskari gongo eyapoti

- Maskati watakua mesenja wa kupeleka barua za wakubwa huku na kule

- Suudia watakua mayaya majumbani mwa ma amiri

- Kuweti watauza samaki sokoni

 - Qatari watakua waokowaji maisha kwenye mabirika ya mahoteli ya kishefa, wasmama juani kwa masaa mengi mpaka wapige weusi wa makaa.

 

17. Kwa hivyo Mswahili huwa ampakwa hina Afrika, kila kazi is 'beneath him or her', lakini akifika huku "majuu" ile rialiti humpiga kofi la fahamu "Paa!" akawa kazi zote duni azifanya yeye. Kwa hivyo Waswahili ni sharti waamke. 100% ya Waswahili walikwenda "majuu" pasi na kufahamu uhakika wa mambo yatakayo wakabili wakifika huko "majuu". 

 

18. Kwa hivyo, wee ni binti watakaolewa na mtu wa "majuu", ole wako usifanye moto. Tuliza boli. Kaa ufkirie kwa makini. Chembelecho vile vipindi viwili, "Usinharakishe" kilijibiwa na kipindi cha "Tushauriane." Kaa kitako ufkirie kwa makini sana. Mwenye pupa hadiriki kula tamu. Utajizoazoa uje mbio, na mbio za sakafuni sku zote huishia ukingoni. Utakuja "majuu" huku wataka kua Kim Kardashian na utaja jikuta unkua yaya walea watoto, imma ni watoto wa tajiri yako, au ni watoto wako mwenyewe. Kumbuka, ukija hutaweza kumuandika yaya awalee watoto wako maana it's just too bloody expensive. Utawatamba wewe watoto, uwaogeshe wewe, uwapeleke skuli wewe. Hina uliyoipakia usiku wa jana ifikapo skukuu asubuhi ya leo yaanza fifia kwa kuosha vyombo na kubadilisha nepi. Wee si ulikimbilia "majuu" na mayaya wote unwaata Afrika? Chembelecho videmu vya mtaani, "Kula!"

 

19. Unzaa uko hospitali wazaa peke yako; hakuna cha mama wala cha ndugu wala cha mavyaa wala cha wifi. Huku ni rabirabi nafsi. Na kama unao hao ndugu na jamaa zako basi labda wakuangalie sku moja au mbili tu, na sku ya tatu mambo ni 'mume n'guvuze' (japo wee ni mwanamke mzazi mpya). Ubakie ujipikie uji wako wa wimbi kama una nguvu basi na huku wanyonyesha, na usiku ukae mato miezi 6 wahangaika na mtoto mchanga, akikohoa kidogo ushainuka wamuangalia sije akapaliwa na mate, na akilia kidogo huyyo ushaamka, wajiuliza, jee askia joto umfunuwe shuka kidogo au askia baridi umfinike na kijibattania cha sufi.

 

20. Na pana wengine mimba huharibika pasi na wao kukusudia, binti akienda kukojoa chooni akavuja damu kidogo na kutokwa na kipande cha "uchafu", kumbe ambwaga kinyama ambacho ni kitoto maiti kina miezi 2. Kiumbe hicho kwenye shimo la choo, na wengine kutambua kama hiyo ni mimba ishaharibika hawatambui. Kwa ile shoki binti akawa yuko "in denial" akapiga bomba chapchapu akamflashi chooni badala ya kukiokota kimaiti kilotiwa roho tokea siku ya 40 wende wakakizike. Baba akitambua mwanae Mn'gu anamkhitari ahuzunike aanze kupiga simu zake Afrika amtafuta Shekhe, amuuliza amswalie vipi kijimaiti kilicho ghaibu sasa, chiko kwenye mapaipu ya vyooni, pengine ashafika maili 30 sasa au ashaingia baharini kamwe.

 

21. Safari moja nilipita Landan mtaa wa Ist Hamu nikamuona jamaa mmoja yuko maskani geto la jamaa. Samiri huyu anfikwa na msiba, waifu wake anzaa mtoto akajifia sku ile ile. Jamaa shoki, kilio na maskitiko, jamaa wamfanyia mchango. Maiti atazikwa makaburi ya Riyadhus Saalihiin karibu na mtaa wao wa Seven Kings, karibu na kitongoji cha Romfod kilichoko mashariki mwa mji wa Landan. Samiri atafta mchango, maana kupata nafasi ya kaburi ni £2,300 (350,000/=KShs.). Hufi ukapelekwa hobelahobela "Laa ilaha illa lah, Laa ilaha illa lah" barabara ya Abden Nasser magari yakazuiwa trafik tele ukapelekwa kuzikwa Kikowani. Kila kitu "majuu" ni upange na utenge pesa zake kando, licha ya maisha, ata mauti na kuzika yana utaratibu wake maalumu.

 

22. Mwanamke mwengine nlikwenda Sweden akaniuliza jee, aweza kuswali Kishia? Ataka kutanganya Magharibi na Ishai msimu wa Sama, maana Magharibi ni saa 4 na robo usiku, Ishai ni sita kasrobo, na Alfajiri ni saa sabaa unusu usiku. Nnamwambia atafte fatwa kwa shekhe, mii si shekhe wala sina ilmu hiyo.

 

23. "Majuu" sio? Pana mambo sampuli sampuli hujawahi kuyawaza. Ukifika tu, ubaguzi wa rangi wakungojea. Una kisomo usione kisomo chako kitakusev, laa. Maadam wewe si Mzungu utasafa baba, si Dubei, si Uingereza, si Emerika. Au huoni kwamba Obama hivi maajuzi ilibidi aoneshe cheti chake cha kuzaliwa (bath satafiket) ati kama kweli yeye anzaliwa Honolulu wala hakuzaliwa Homa Bay? Ubaguzi wa rangi upo na tena utele.

 

24. Au uamue uwende zako Afrika Kusini ukasomee urubani wa meli kisha ukae huko huko Durban au Keptauni, maana uko "majuu" eti sasa. Afrika ya Kusini si nchi ya kuishi shekhe. Mandela ni mtu na msmamo imara, lakini kazi yake huyu "Madiba" ilikwisha kwa kuupigania uhuru wa Mwafrika. Raisi wa pili baadake akawa Thabo Mbeki (angeitwa 'Tabu' Mbeki) alosomea iktisadi (ikonomiks) Uingereza, lakini akili zake nyingi zilimtuma aseme "HIV does not cause Aids." Watu walikula hepi watiana left, right and center, nchi ikishtuka si ukimwi huo ulivyo enea! Kumbe 'Tabu' Mbeki ajua zaidi kuliko wataalamu wa matibabu, si ni raishi eti?

 

25. Akitoka "Tabu" Mbeki akaja Jakob Zuma ambaye hakusoma skuli kabsaa huyu, ata Kenya asingeweza kuwa hata mbunge. Haya, huyu Yakubu "Chekbobu" Zuma alituhumiwa kua alimnajisi mtoto wa rafki yake. Akiulizwa, jee wajua mwanamke huyu ana ukimwi, jawabu la Yaakubu "Checkbobu" ni kua yeye alioga baada ya 'kulala nae'. Kumbe kuoga kwazuia ukimwi! Na mwana harakati anaefkiriwa atamrithi kiti chake huyu Yaakubu "Chekbobu" ni Julias Malema. Malema hivi maajuzi aulizwa na waandishi wa habari wa kimataifa ampata wapi dola milioni moja unusu kujengea nyumba yake yakishefa ilhali yee ni mwanachama mdogo tu wa kupokea dola elfu 3 kila mwezi, alimjibu mwaandishi wa habari kwa mahamaki, "Mind your own business!" Jawabu ni hili, pengine atakua raisi kesho kutwa huyu, hakuna akauntebiliti hapa, si ni mlemavu wa akili mtu huyu? Tumuite Mulema "Mlemavu". Viongozi ni kama hawa na korupshen ni kama hii, wafkiri nchi hii ya Kizulu yakalika? Haikaliki. Na wee unsomea ubaharia huku wataka ishi huku wakuona ni "majuu"!

 

26. "Majuu" unkuja na Uisilamu wako? The only way is down. Muangalie Zinedine Zidane ("Zizu" kwa Wafaransa wampendao mchezaji huyu wao wa First Class) aliyemtia mango Materazi kwenye kutetea Kombe la Ulimwengu. Wazee wake huyu "Yazid" (niknem walombandika wazee wake) ni Majazairi (Ma aljeria), wakamzaa yeye Ufaransa. Lakini yeye mwenyewe ni "non practising Muslim". Kwa Kiswahili kingine, si Muisilamu mwenye kuamini wala mwenye kufuata. Mkewe Mkristo, na watoto wake wote wanne wana majina ya Kikristo. Na ukiona haya ni ya ajabu, hujafkiria ya amira wa Unguja Salma bint Said bin Sultan. Mzaliwa wa Baitul Mtoni, kisha akaishi katika Baitul Watoro na Baitul Tani, Zanzibar. Akiongea lugha mbili za Kiswahili na Kiarabu. Salma huyu alikacha na mshkaji wake wa Kijermani aliyemtia mimba, akatoroka nae kwenda kwenda Aden 1866 na akabatizwa huko na kuolewa, na akafa Emily Ruete huyu 1924 mjini Hamburg akachomwa kama Baniani na majivu yake yakazikwa kwenye kaburi la mumewe.

 

27. Na wengi mno katika waisilamu, wakiwemo kundini Waswahili pia, wameowa na kuolewa na wasio kua na asli zetu, na wengine wasiokua Waisilamu, na wengine hawana dini kamwe. Au wanati wetu wengine wanaolewa na "walio silimu jina" ili nikah ipite wala kwa hakika kupita haikupita. Lilosilimu ni jina tu, roho i vilevile, haikusilimu. Na Waswahili wengi imma hawafuati dini, au hawawashughulikii watoto wao wakafuata dini, au ni mnchanganyiko wa yote haya mawili. Waswahili wa Toronto na wa London na wa... wana watoto wenye majina ya Kiislamu lakini ni watoto au wanawali (kama ni wanamtuzi tena) au mashababu (kama ni mashanyanyu) wasojua ata nguzo za Kiisilamu ni ngapi wala ni zipi - wasoswali, wasofunga, wasokwenda hija Maka Kuu wala wasokwenda "hija" Maka Chocho (maulidini) wakapiga picha katika hii "Cultural Festival". Na Waswahili wengi walioko "majuu" washafika 3rd jenereshen sasa, na wengi wao, mababu kwa wajukuu, hawaujui wala hawauthamini Uisilamu. Usione ukija wewe leo mambo yatabadilika. Waswahili wakwambia "Mlio wa gude? Ni mmoja." Utapotea wewe kama walvyopotea wao.

 

28. Kwa hivyo waishi "majuu" lakini kumbuka huku ni kazini-stani huku. Wenda mbio saa zote. Na kila nyumba ukienda hukosi saa zaidi ya 2 ukutani. Kuna nyumba za Waswahili wengine pana saa ukutani katika kila chumba katika vyumba vyao 3 watoto wasichelewe skuli, na sting rumu pana moja kubwa, na jikoni pana nyengine mama asichelewe na brekfast, na chooni pia pana moja, mwanya na huku ni tik-tok mwahisabu nukta, saa yakuharakisha. Hamkuja holidee huku.

 

29. Na mukiruka mukenda "matini" kutembea hamupati illa agro (matwaffash). Huyu akupa orodha ya matatizo yake, na yule alalama hana skul fiiz, almuradi kila umskiae ana maprolem. Sasa wee unkwenda holidee wiki mbili kupumzisha kitwa, lakini killa umskiae an maprolem tuu. Shekhe, tuu wiks zako zikisha wataka holidee nyengine ku rikava from your holiday! Ndio mii pasonali huwenda once evri three yaaz, siendi zaidi ya hivyo. Afadhali nende nkatafute jua la Vankuva kuliko uskie dhiki za shangazi huyu na mjomba yule. Au ujiende zako Taki holidee, chip en best. Au uwende zako Kasablanka Moroko ukabarizi. N'na maswaiba huandamana nao wakti mwengine, mimi natafta jua, na wao watafta mjani (Moroko ni World namba 1 kwa mariwana, jamaa zake Bob Mali hawatoki huku).

 

30. Pana Muemerika mmoja nikijuana nae zamani Afrika. Alkua na Pis Kor, anaowa mwanati wa Shela, wakizuia Sheli Bich. Sku moja huyu "aliyesilimishwa" Muhammad (Daniel Jones - mimi nikimuita "D.J.") tunaonana ubayani, kule chini ngomani Floo. Siku zile za jahiliya, twasalimiana, akanivuta kando ya zegere la malaya na mdundiko wa maspika ya disko akanambia nende zangu nyumbani nkapumzike, maana keshoye ntainuka na homa. Mii nkateka. Naskia machofu kidogo lakini otherwise niko o.k. kabisa. Baada ya kuruka majoka, ah, nkenda zangu hom. Asubuhi na'am ammi, n'naamka na maleria. Taharuki, kijasho chembamba, natapikizana, sijiskii kula, n.k. N'kapiga sindano zangu n'katulizana. Baada ya wiki n'kakutana na D.J. Namwambia afan aleyk, unjuaje n'taamkia na homa? Kumbuka, Mzungu huyu si sharifu wala si mganga eti. Anambia "I shook your hand and you were unusually hot to the touch, your face looked lined and haggard, your eyes had that tired look, and you couldn't concentrate much. These are classic signs of malaria."

 

31. Mzungu huyu. Atabiri kwa ilmu, hatabiri kwa nyota za falaki. Ndio ukaambiwa bongo la Mzungu linchoka. Yuwa take taim akasoma mambo yenye faida. Dem mmoja Afrika kila ukimuona ana Mills & Boon mkononi yuwasoma. Namuuliza, ana vingapi kama hivi? Anambia zaidi ya vitabu 3,500 aeza fungua librari khaswaa. Na Swadiki nae hatoki maskani ashufu mandanda yakipita, uso wageuka huku ukishindikiza tako upande huu, kisha uso wageuka kule washindikiza rasa jengine laingia kitotoro cha Yabba. Ukimwambie Swadiki twende tukaswali basi akwambia, "Wee tangulia, mii natia mato nuru kwanza." Ilmu ya D.J. "Muhammad" Waswahili hawana, na hakuna asiyeshikwa na homa Afrika deli savis. Lakini symptoms za homa Mswahili hazijui mpaka ende kwa Dokta Shumi akapimwe. Labda atamani shumu ya Dokta Shumi huyu, haya, jipige mahopu basi.

 

32. Yankumbusha Twalali nlipomuona Afrika. Anambia "Ah, Kenya Pawa pantiwa meneja mzungu. Sasa matransfoma yote barabarani yapigwa savis na kubadilishwa oili. Matransfoma hayajapigwa savis miaka ishirini bwana?! Mzungu kweli ana akili." Mzungu afuata miko na tartibu, Mswahili (na Muafrika in jeneral) hafuati. Sisi twatafta kula tu. Ukinipiga koma zangu mbili bas ntakupigia saini kuwa transfoma nishaisavis, tena naeza kukutilia saini za miaka mengine 50 in advance ukitaka. Korapshen kuruka. Mzungu pia korapshen aijua na aifanya, lakini ni madili makubwa makubwa, si mambo ya health and safety kama kusavis matransfoma, au kucheki matatu za PSV kama ziko road worthy au laa, au utake esenshal savis kama bath satafiket au kitambulisho au paspoti mpaka uhongane, ata ukiwa na chapaa za kutosha Afrika basi kitambulisho chako chaeza wekwa picha ya mbuzi chifu akaisaini yule mbuzi kweli ni wewe.

 

33. Jee, Waswahili wanaoishi "majuu", watamani au hawatamani kurudi zao "matini"? Watamani sana! 99% yearn for the simpal laif and slo pes of laif Afrika, lakini, kwao wao that's too late, it's gone forever. Ni kama ule msemo, "If wishes were horses, then beggars would ride." Lakini those are wishes. The reality ni hawawezi kurudi tena kwa sababu tulizotangulia kuzieleza. Lazma wavumilie na jibaridi na upweke wa "majuu". Lazma wawe kama Wazungu, wawe na forward planning. Wawe na bajet ya nyumbani. The income must be greater than their needs. Na lazma wa satisfy their needs, not their wants. You want many things, lakini that's not necessarily what you need. Lazma wawe na tait bajeting. Wakipungukiwa, hawawezi kumuendea jirani yao au Khalati Amana akawakopesha. As a last resort labda waandike cheki wawape "Checks 4 Cash Converters" - huo ni mshahara wa mwezi ujao washapeana cheki leo wapawe pesa yao, mwisho wa mwezi hawana kitu, mshahara wote na riba kwa juu wenda kwa hawa. "Majuu" haina cha kujuwana wala haina cha huruma.

 

34. Kwa hivyo Waswahili wa "majuu" washa chenj, japo wengi katika wao hawajatanabahi bado. They are not the same. Nilikwenda Ajmani (Imarati) basi niko na korkosi mmoja tumuite Muusini. Mwida gari limmuharibikia kwenye haiwee. Brekdown kava akiicheki ina ekspaya mwezi wa 5 sasa, kwa hivyo hana fowad planning huyu gari tumbakia twaliskuma jangwani kando ya barabara, twamgoja Hamdani amalize shifti yake Gulf Air aje tulifunge kamba tulivute. Mambo kienyeji ile mbaya. Tukakaa hapo 6 hours, bahati twatoka shopping Carrefour tukawa tuna minaral wota na bofulo tukazikalia, tukishikwa na mkojo twakojoa na tukitayammam na mtanga. Na pass taimu kubwa anihadithia ya kuwa huku Imarati usiombe kugonga ngamia shekhe, sallaalaa, si fidya yake utakayo tozwa, afadhali umgonge mtu. Nafkiria, kama maneno hayo ni kweli, basi Arbi bokoboko halimfai. Ati fanyafanya umkose ngamia umgonge mtu! Ikiwa ngamia wana thamani kweli Imarati basi Ma amiri wende zao Ostrelia na makontena maana pana ngamia laki 700 hawana kazi bali watkuliwa ni pests kule, wauawa ovyo kama watu Afrika wauwavyo kombomwiko kwa champali.

 

35. Kwa hivyo "majuu" Waswahili (achana na huyu Musini zuzu badala wa Ajmani; nnapata ripoti kwa swaiba yake mkubwa hivi maajuzi kila akienda Afrika kwa waif wake si piga piga yake hiyo! Ajabu wallahi, waif bita huyu mwenyewe ana washkaji tungu nzima ata sijui kwa nini amfanya mkewe swalihina kuwa ndio panching begi!) - Waswahili wa "majuu" wan chenji, wankua shapu, wana fowad planning. Wana tait bajet, winta ikianza lazma wa set aside pesa zaidi za elektriziti na ges, maana pana long, cold nights ahead. Na wala zaidi, kwa hivyo reshen yazidi. Hakuna mambo yale ya "Tawakkal" tu. Waswahili wa "matini" wapenda sana hii tawakkal, na tawakkal yao sio ile alivyo amrisha M'ngu S.W.T. Kutawakkal kisawasawa ni kujitayarisha vilivyo, kisha u dabal chek, kisha usallim amri, halafu ndio utawakkal. Kabla ya hapo ni kujisoza huko, si kutawakkal.

 

36. Na jee watoto wa Waswahili wa "majuu"? Na jee wajukuu zao? Hawa kwa hakika si Waswahili tena. Kwanza, 99% ya Waswahili hawazungumzi na watoto wao Kiswahili. Shocking, but true. Kila jinsi wengine, Wahindi, Wachina, Manaijeria, Wasomali, Mamoroko, n.k., wazungumza na watoto wao lugha zao. Lakini Waswahili? Wajikataa. Pan taka Kiswahili. Utakwenda Naimeghen (Nijmegen, Holland) na utampata Atika azungumza na watoto wake Kidachi ilhali mume wake ni AbdulWahabu kutoka Mwembe Kuku. Kokote wendapo, mambo ni yayya haya; nenda Bergen, Ozlo (Norwe) na utamkuta Firiyali na wanawe wazungumza Kinorwijiyan nyumbani; nenda Malters Swizalendi utamkuta Fahima azungumza Kijeru na watoto wake; ndoo Brampton, Toronto utampata Hanani azungumza Kizungu na wanawe; nenda Ruwi, Maskati utampata Shuwekha na wanawe wazungumza Kizungu; twaona Kiswahili ni kichafu mpaka tujitoharishe kwa lugha nyenginezo. Watoto wa "majuu" labda wajua "Kumaamako" na "Shoga" wazee watamkayo wakikasirishwa na watoto wao, baas.

 

37. Ndio Lubna hivi majuzi alpokuja Msa nnamuona na binti yake wa miaka sabaa Maliha watoka Uingereza. Ki Maliha chazungumza Kiingereza kwa lahja (eksent) ngumu nusu haifahamiki, na watoto wa sistake Lubna wa Mombasa na watoto wote wa Mtopanga Praimari wanshangaa na kuitana, wote wamskiza ki Maliha chabonga kimombo kwa kustaajabu na kuduwaa, ni kama waliomuona Princess Kate Middleton mtaani khaswaa! Basi Lubna namwangalia ang'ara kwa kuona raha mtoto wake azungumza Kizungu kama Mzungu. Ki Maliha ukikianmbia, "N'doo umshum ankal" ata hakina habari wasema nini. Maskini wa akili mamake, Lubna jubna huyu.

 

38. Kwa nini Waswahili wakataa lugha yao? Pengine mama koko hakusoma skuli sana, basi ile yawa ni prektiz ajifundishe Kiingereza, Kifaransa, n.k. Wengine wajiona wao ni Waswahili "asli dhaifu" kwa hivyo kwa kuzungumza lugha ngeni huwa washapanda daraja. Na wengi waishi "majuu" kwa dhiki na tafash, wangojea chansi ya kushuka holidee Afrika waka shoo off kwamba watoto wao "ni wasomi" kama tulivyomuona Lubna jubna. Au wengine ni "Waarabu" wala Kiarabu chenyewe hawakijui, basi wakhiari watoto wao wajuwe Kizungu kuliko wajuwe Kiswahili lugha yao na lugha ya wazazi wao. Al muradi makhanatha matupu shekhe.

 

39. Hatari iko wapi? Wahindi waliokuja "majuu" wote wajua lugha zao, pamoja na ma Turki, n.k. Lakini still, wao rahisi sana kupotea kidini wakaowa na kuolewa na wasiokua jinsi zao wala dini yao. Sasa basi, upate Mswahili awakuuze watoto wake bila ya lugha ya Kiswahili, huoni ni hatari kubwa shekhe? Maana pamoja na lugha pana mambo mengi yendao na lugha yoyote, kama dini, mila, tabia na desturi. Lugha ndio chombo kinachobeba yote haya yenye faida kubwa mno. Kwa hivyo Waswahili mashosti wenye upungufu wa akili wawanyima watoto wao dairekshen in laif kwa kuwakosesha kitu simpal kama lugha. Umpate Nihadi wa Kanbera Ostrelia azungumza na watoto wake Kizungu saa zote, na Taiba wa mtaa wa Safwa, Dammam Suudia pia yeye ni Kizungu kwenda. Bloody fools. Let me repeat that. Bloody fools. Let me add a little more emphasis. Fucking ignorant cunts.

 

40. Mvlana wangu wa nne sisahau nilipomtukua Msa first taim ana umri wa miaka 8. Tukaingia mskiti Shibu akastaajabu kibla kiko sawasawa, ashazowea miskiti huku "majuu" kibla kiko pembeni mwa mskiti maana 99% ya miskiti huku si purpose-built bali ni house conversions tu, kwa hivyo ile rectangular house si rahisi kupata ubavu wake mmoja uko wima unaelekea kibla. Na miadhini pia, hajawahi kuskia kukiadhiniwa kwa malaud spika, alishangaa sana. Lakini lugha, watoto wangu wote wazungumza Kiswahili sawasawa kama sahani na kawa. Ajua kohozi ni nini, ajua samaki wa kupaka ni nini, ajua shuzi la yai viza ni nini. Lakini Mswahili wa Nairobi tu ataka zungumza na mtoto wake Kizungu, kama kwamba English Lengwej = Being Edyuketed. Waona ukijua Kiingereza ndio utapata kazi na kuheshimika? Haa pata hiyo kazi tukuone basi. Chembelecho msemo wa Kiengereza unao samaraiz mambo yote, "Bollocks to you!" ('Boloks' ni makende, kwa mfano, makende ya mbuzi, n.k. Walokulia Vibokoni wakiskia 'kende' waona ni 'mboo' - no no no no. Boloks to you).

 

41. Kwa hivyo, watoto wa Waswahili waliokulia "majuu" na waliozaliwa huku SI Waswahili tena. Si Waswahili kwa sababu majoriti - 95% hawazungumzi Kiswahili kamwe. Kwa hivyo si dini yao tu iliyodhoofika, bali hawana kalcha yao. Hawajui maana ya 'Kikulacho kinguoni mwako' wala 'Waarabu wa Pemba wajuwana kwa vilemba' ni nini; wala hawajui kupigwa dafrau ni kupi wala kubebwa kwa machera ni nini; wala hawajui siki bin jabili ni nini wala gulab jamuni ni nini; wala hawajui kuteza kibe wala kuteza kode ni nini; wala hawajui kurabu ni nani wala dushi ni nini; wala hawajui jongoo ni yupi wala nge ni yupi; wala hawamjui pweza ni nani wala ngisi ni yupi; wala hawaijui nyavu ilvyo kaa wala uzio ni nini; wala hawaujui mshipi ulvyokaa wala ndoana ilivyokaa; wala hawajui chowa ni nini wala nyungunyungu ni nani; wala hawajui mjiskafiri ni nani wala kivunda jungu ni nani; wala hawamjui kuchi ni nani wala paka duzi ni nani; wala hawajui Makadara ni wapi wala kwa Haji Mwamadi ni wapi; wala hawajui saumu ni nini wala kutoa mkono wa Idi ni kupi; wala hawajui mali kwa mali ni nini wala nguo kuukuu ni nini; wala hawajui chuoni ni wapi wala kukhitimu ni kupi; wala hawajui kisima kinkaa vipi wala baraza inkaaje; wala hawajui kusoma maulidi ni kupi wala kusoma halbadiri ni vipi; wala hawajui kuteza na ringi ni kupi wala kuteza chakacha ni kupi; wala hawajui cha kwenda matangani wenda vipi wala cha kufuata gworide lafuatwa vipi. Watoto wa Waswahili walioko "majuu" SI WASWAHILI.

 

42. Kwa hivyo akija mtoto wa ndugu yako wa "majuu" usimletee mambo ya amshumu mkono wa "ankal Alii" wala "anti Warda" - kalcha yake huyu kijana au binti wa "majuu" ni "Hi" and "Bye". Si mtu aaga yuwenda zake wamwambia "Karibu" - logic yao watoto hawa ni "Bye see you later"- kwaheri kitowe bwana, sio "Karibu" na huku mtu ashaaga yuwenda zake. Different kalchaz. Na mambo ya kushumiana mikono ni unhygienic - mikono ina jamz, haishumiwi shekhe!

 

43. Kwa hivyo watoto waliozaliwa "majuu" kwa jumla huwa Makanedianz, Waemerika, Waingereza, Madachi, Maswizi, n.k. Wana a common culture. Culture za wazee wao hushika 30% au chache kuliko hii, na watoto wa Waswahili wasiofundishwa Kiswahili wala mila na desturi zao huwa 90%-100% SI WASWAHILI, full stop. Na wale watoto waliozaliwa Afrika na kukulia huku, wengine wao waliozwa makazin na nin na nini, lakini wengi katika wao merij zao haziku last. Wale walio olewa na kuletwa walikumbana na reality ya laif "majuu" wakaja kuta kuwa huku hapana Fairy Tales sijui cha hadithi za 'Cinderella and her magic slipper' wala hapana cha laifstail ya Richi na Brooke ya "The Bold" hupigwa na shok. Binti ya mtu akatanabahi huku ni Kazini-stan from day one wakiingia; mpaka wakajiuliza, "Naosha vyombo ata hina yangu ntokayo nayo Afrika haijafutika?!"

 

44. Mpaka watoto wa Waswahili wa huku wengi washatambua kua it's better tuowe na tuolewe na wa hukuhuku "majuu" kwa sababu hawakuweka pochi mbele kama jamaa zetu wa Afrika, wala wa huku hawana hizo unrealistic expectations kwa sababu tayari wajua "what the score is". Kwa hivyo this being the case, wa "majuu" ni bora kuwaowa kwa sababu hawana haja ya tuwa "break in" hawa Waswahili wa "matini" kama vile ma cowboy wanavyo wa break in ma wild horses wapate kuwa tamed wasallim amri. Wengi walioowa waschana wa Waswahili wanao kulia maSuudia na maOmani, pia wakakuta mambo ni haya haya, na wengi wao maspidi wan twenti shekhe, wanwashinda hata kina ma Suzan na kina ma Viktoria wa "majuu". Kwa hivyo, watoto wa Waswahili wa "majuu" SI Waswahili, maana thinking yao wao ni ya Kizungu kabsaa.

 

45. Na hata wazee wao, wale waliokuja "majuu" miaka 10, 20, 30 au kuzidi, wale pia ni Waswahili jina tu, si Waswahili namna mulivyo nyinyi wa "matini." Waswahili hupigwa na maisha huku mpaka wakachenji. Wana foward planning, wenda mbio makazini, mpaka wakija kutembea huko once in a blue moon, wakaagana na Ahmadi wakutane kahawani saa moja asubuhi Ahmadi awaweke skwea asitokee, Waswahili wa "majuu" huchizika kwa hasira. Na mobaili kila ukimpigia waskia, "Samahani, mteja hapatikani." Ukimuona utamwambia, "Wee Ahmadi madha faka, usiniweke skwea tena mwana kummala mamaako!" Ule ubwege Waswahili wa "majuu" uliwatoka zamani, kwa hivyo hawana taim na kule kupotezeana wakati wa hawa vinyang'arika wa "matini".

 

46. Ndio ile sistem iliyoko "majuu" yambadilisha Mswahili akawa kama Mzungu mambo yake. Short and sharp. Jamaa awa efishent kabisa. Kila jambo lenda kwa taim yake. Basi yenda kwa taim tebal, utalikuta liko steji saa moja unusu kamili. Ukija saa moja na dakika thalathini na moja basi lishakwenda kitambo. Kwa hivyo Mswahili ageuka awa kama Mzungu, mpaka nyii wa "matini" mukimuona mwamsema, "Ah, ajifanya ankua Mzuuuuungu kweli." Hajifanyi, ndio sistem ya "majuu" inavyo oparet. Uspolipa kodi kwa taim yake nyumba wafukuzwa na virago vyako utavipata untupiwa nde ya mlango, simpal.

 

47. Kwa hivyo Waswahili wa "majuu" kila wakizidi kuishi huku waatana na urata wa Kiswahili, ule uchafu usokua Uisilamu, kama kutotimiza ahadi, n.k. Ata kusema kweli. Jambo haliwezekani Mswahili wa "majuu" hana preamble au kuanya anya, atakwambia stret. Ukiudhika udhika tena udhika sana, lakini taim westing hakuna hapa. Si masala ya kuchelea ati sije aka ku hurt your feeling or not. Ndio watoto wa "majuu" hawasemi urongo. Huwezi kumtukua skiing? Humdanganyi na kumpa ma ekskyuziz. Wamwambia stret, "I can't take you because I can't afford to. I've got the electric and gas bill to pay today, the car mortgage on the 15th, and rent at the end of the month." Na mtoto aambiwaye ana miaka 6 tu.

 

48. Kwa hivyo watoto wa "majuu" hawajioni wao ni Waswahili wala Waafrika, no bwana. Wao 100% ni wa "majuu". Wakija holiday, pengine 2 or 3 times in their lifetimes, wankuja holiday tu kama kwenda Jamaica wakaogelea bichi au walokwenda Egypt wakaona ma pyramids. Afrika wankuja it's no big deal. Nyanya yupo, shangazi yupo, ammi yupo, kazin yupo, etc., hawa wote ni ma aquaintances wa dakika mbili tu. They don't really know you, and they don't understand how you think or behave. As far as they are concerned, nyii mwahusiana na baba yao au na mama yao tu, lakini they don't really identify with you. Their family ni baba yao na mama yao na ndugu zao, na nyinyi ni kama walokwenda zao zuu wakaona wanyama mwitu haya wakarudi zao tena. Na wao si Waswahili wala si Wakenya. Samjo bwana?

 

49. Wala usione zile ila 27 za Waswahili ni ila za Waswahili tu, laa. Ata Wazungu wanazo nyingi katika ila hizi hizi. Masabasi namba wan ni Wazungu. Jirani ajua taim utokayo na urudiyo, sku gani unkorofishana na waif wako, watia gange gani, na una afeya na nani. Kugoana na kuoneana kunjaa. Ukiwa una watoto wako maskuli utapata ripoti kila siku. Na ikiwa ubaguzi u tele. Na ikiwa ni pochi lapendwa sana huku. Wataka nini jengine? Uganga Wazungu waufanya pia, wataka zaidi? Na watu ova weit hawana mazoezi wanjaa. Na pita barabarani baadal magrib na kila nyumba utakuta watu wamuagalia Kadeshian ankwenda Dubei kuipromote "Millions of Milkshakes" ya Kim Kardashian kwenye T.V. Ila 27 Wazungu pia wanazo.

 

50. Kwa hivyo, watoto wa Waswahili wa "majuu" SI Waswahili. Ata wale waliokwenda Suudia, Imarati na Maskati, mkondo ni huu huu. Japo hawa wanaoishi huku (ispokua baadhi yao Omani) hawana uraiyaa, na hawaupati ata wakazaana vijukuu kwa vitukuu, kupata ata bath satafiket au kitambulisho hawapati shekhe. Waonewa na kunyimwa haki zao, si watu wazima, si watoto. Hawa ni gest wakaz, any taim waajiri wao au serkali ikijiskia wawafukuzla mbali. Kwa hivyo watoto wao wanaozaliwa huku na wakuliao huku wana a big disadvantage sababu wanakua na kalcha za nchi hizi bila ya kuwa na raits zozote, ata when they have had enough, warudi "kwao" Afrika lakini wajikuta they can't really fit in huku "kwao" maana kalcha walio kulia nayo si ya Kiswahili. Wata i miss Skiing ya Mall of the Emirates (ushaskia wapi kuna barafu jangwani ispokua kwa wendazimu hawa maImarati?! How big is their carbon footprint shekhe? Ni kama Ulaya wa recreate Desert conditions ili watu wa camel-ride. It does not make any sense whatsoever!), na mukienda nao watoto hawa wa "majuu" Makadara wataona Maalim Azizi na bembeya yake ya vikapu is actually a circus act.

 

51. Na wa "majuu" tushaona 99% watamani kurudi zao "matini", lakini slowly, slowly, waanza ku-rialaiz kurudi hakurudiki. Wakijicheki wajikuta wana makaratasi na mapaspoti ya huku "majuu" (Kenya mazuzu mpaka leo hawakubali 'dual-citizenship' kwa hivyo they're missing out on investment kubwa kutoka kwa Wakenya waishio ng'ambo), na wana moogej na watoto wako maskuli na ma unii, na wengine ni wagonjwa long term wahitaji matibabu kama kubadilishwa damu kila wiki n.k., na almost all Waswahili wa "majuu" hawana ata kibanda huko Afrika licha ya kuwa na nyumba ya makao wala kazi ziwangojao wakirudi. Kwa hivyo Waswahili walioona they'll make money huku "majuu" kisha warudi kwenye raha ya kwenda mfungo Kanamai waanza kutambua mdogo mdogo kua kurudi hawawezi kurudi japo watamani. They are coming to terms kua 99% yao ndio washa selehea huku, hawarudi tena waishi Afrika, neva, eva.

 

52. Kwa wengi realization hii yawaletea huzuni kubwa, lakini ni kama msiba, you have to deal with it and move on. Kurudi hawawezi tena kurudi, kwa hivyo washaanza kuzikana humu humu makaburini wakifa. Ukiona otom infika na majani ya miti yapukutika huwa ni a very depressing taim katika mwaka wao wa kwanza huku "majuu". Afta about 7 years waanza kuona ni normal. After 10 years you are looking forward kuona hizi seasonal changes. After 15 years yote haya ni normal and part of life khasaa, and you can't have it any differently. Your mental metamorphosis is complete. You are a totally different person from the one who left Africa.

 

53. Kwa hivyo Mswahili wa "majuu", awe ni mzaliwa wa huku, au ankulia huku, au ankuja ni mtu ana 20, ana 30, ana 40, mtu na fahamu zake, akikaa huku hubadilika akawa si Mswahili tena. Fikra zake zawa advanced. Ajua Uswahilini kuna mengi mabaya na mengi ya kuregeshana nyuma, mambo ya kubaguana na ya kuvundana kila siku. Sasa yuko in a new environment, a new culture, na yuwa absorb that new culture. Awa sharper, more progressive. Ajua the future of their kids is in their hands. Aatana na gati na kutafta kujua ya watu. Ashika kwenda mbio kazini na kusomesha watoto wake. Na ku pass taim aanza kuwa na hobi akazamia kwenye hobi hiyo. Ndio ukaskia bongo la Mzungu lintumika sana. Isabu nyingi, hobiz nyingi, mpaka aja vumbua jambo kama iPhone which takes the world by storm. Na watoto wa Waswahili wa "majuu" jee? Ndio 100% mabongo yao yafanya kazi kama Wazungu. Usione ajabu mtoto wa Mswahili huku "majuu" akaja akavumbua kitu ulimwengu mzima ukapata habari. Nyii wa "matini" endeleeni kula mraba huku mukichimbana kila siku.

 

54. Basi walioko "majuu" wa straggal. Wana majukumu makubwa makubwa kuliko nyinyi wa "matini". Wahakikishe wawapeleka skuli watoto wao wenyewe (hakuna cha watoto kwenda skuli peke yao, au waandamane na watoto wenziwao kama Afrika), kisha jioni wawapitie wawaregeshe nyumbani, kisha wahakikishe wafanye nao homwak, kisha wawasmamie na kuwasupavaiz waangalia vipindi gani kwenye TV japo ni kaatuni, na wakiwepo kwenye mtandao wa chati na nani. Na wenye muamko wahakikishe watoto wao wenda chuoni, na nyumbani wawasmamie kila kipindi cha swala watawadhe na kuswali. Haya yote wayafanye na juu ya baba na mama wote kwenda zao kazini. Yaani ni kama ile "Total Football" philosophy ya timu ya Holland ya Ayaks (Ajax) na timu ya kimataifa ya Kidachi, na timu ya Asenali ya Venga (Wenger) na "tiki-taka" ya Baselona ya Cryuff (kila pleya aeza cheza attack, mid-field au difenda) - basi wazazi Waswahili wa "majuu" pia wateza "Total Parenting" - wafanye A to Z (Waemerika wasema A to "Zee" - Zed ni zee kwao, ndio Jay-Z ni Jay Zee si Jay Zed na Zebra tumjuae ni Zibra huku Makdonald-stan).

 

55. Kwa hivyo kwa watoto wako, nyii wazee ndio ni baba na ni mama, na nyinyi pia ndio marafiki wao na ma playmates wao, na ndio ni waalimu wa chuoni, na ndio ni waalimu wa tushen, na ndio ni wapumbazi na ndio waliwaza na ndio ma psychologists, na ndio makocha wa football, na ndio makocha wa swimming, na na na... Nyinyi kwao wao ndio mambo yote. Na ukiwa nyumbani mfereji wa vuja humuiti Alii au Babadi aje autengeneze. Laa. Costs too much money which you can't afford. Utaurekebisha mwenyewe. Utafanya risachi yako kwenye kitabu cha DIY (Do It Yourself) au mtandao, uwende hadwea shop ukanunue vifaa vyako vya mipira na ma rench ujitie kazini. Au busati la ukuta mpaka ukuta (wall to wall carpet) lataka badilishwa utajifundisha mwenyewe namna ya kulitia. Au nyumba yataka kartasi ya ukuta (wall paper), au kuta zataka kupigwa rangi shekhe utanunua mwenyewe gundi, makartasi, rangi, brashi, n.k. ujitie kazini. Au gari yataka kubadilishwa oili utaibadilisha mwenyewe. Au baskili ina panchari utaitia kiraka wewe. Ndio ukaona bongo la Mzungu lintumika sana. Hangoji kufanyiwa, and part of the reason is ikonomik - a sevu pesa. Na ndio ukaona Mswahili wa "majuu" akija Afrika hangoji kufanyiwa, ataosha vyombo mwenyewe pindi akimaliza kula, atajifulia nguo zake azianike, na kumbadilisha mtoto kibinda atambadilisha otamatik hamgoji yaya, n.k., sababu ya mazoea. "Majuu" hakuna kufanyiwa, na ubwete nduu zangu I'm sorry hakuna.

 

56. Ikonomik rizonz ndizo zinazomfanya Mswahili wa "majuu" asiwe ji lezi. Huku ni "amka twende" - hakuna kujizoazoa au kujiskiza. Mswahili wa "majuu" mwisho wa siku, kama bado ana afiya, afanye Kundalini yoga ili a chill out. Nyii wa "matini" mukiskia Kundalini Yoga mwaanza kuteka, mwaona ni sampuli ya matusi. Ndio maana Waswahili wa huku hawana taimu na nyinyi kabsaa. Nyii wa "matini" mikono wazi mwataka kupewa tu. Mtu akitoka safari ni, "Unniletea nini?" Hamujiulizi ndani ya nafsi zenu, "Nimpe bradha man au sista doo kitu gani ili afurahi nae atoka mbali mno na watoto, Ulaya hukko kwenye mijibarafu na ma dipreshen?" Laa, fikra hiyo hamuna kabsaa. Nyii sku zote mwataka "zaka zenu" tu. Mwangoja kupewa, wala kutoa hamtoi. 

 

57. Nilikwenda Arusha kumpelekea mamake Eddie dawa zake, kama alivyoniagizia huyu swaiba yangu. Nkifika nkaona jambo la ajabu. Nyumba ya madhake na ndugu zake femeli ya watu 14 ni ya wastani, nyumba ya Kiswahili na bati lake, lakini mashallah chooni panjengewa jakuzi shekhe. Nyumba zote za Waswahili wa huku "majuu" nilizoingia - si Kanada, si Maskati, si Emerika, si Afrika Kusini, si Uingereza, si Swizi, zoote, sikujaaliwa kuona Jakuzi shekhe. Jakuzi nnaliona Arusha! Na Eddie amenyeka kwa kazi Edomonton, sabuni akioga hatupi hata ibakie kipande cha mwisho kaa usondapo peremendi kwa muda inyayuka kweli ibakie myayuko wa mwisho, na dawa ya meno Eddie aikamuwe aitowe uhai wote, sababu? Eddie asevu kuwapelekea femeli yake Afrika, lakini jamaa zake ata habari hawana. Wana daladala (matatu za Tz) mbili za kazi, lakini sku zote haweshi kulilia hali. Sting rumu wana plazma TV inchi 42, makochi ya ledha, busati zito ata Maskati pia hakuna, na dirisha la jikoni uskumapo chapati waona vyuu ya mlima wa Kilimanjaro. Na ukichoka ati waumwa na sijui na bega, hilo Jacuzzi lakungojea shekhe! Na Eddie? Amenyeka, yuko IKEA afanya kazi, abeba mafanicha na mapaipu kwa forklifti shekhe atia mzigo 16 hours a day 6 days a week!

 

58. Ndio Ti zedi jamaa washaerevuka. Waume wa London wakija kutaka kuowa waambiwa, "Niowe mpenzi, lakini mie niache hapa hapa." Mume ende akachume huko, amletee yeye bibiye huku Dar, ala mafuluda akitremsha na mapeshen. Maana Wabongo washagundua uhakika wa "majuu" = hard work. Binti amwambia mwenzie, "London sitokwenda shogangu, labda niende shopping tu, kisha nirudi zangu hukuhuku Afrika. Sitofanywa yaya mie kule, nikibadilisha vibinda usiku kwa mchana." Na Bintul Mombasa nae pia karibuni will learn this same lesson. Atamwambia mume aliyekuja kumposa, "London sendi nkawa boi wako kule, niwe nkifagia na kukupigia deki usiku na mtana. Kuniowa niowe, lakini niate nikae hapa hapa kwa mamaangu, au ninunulia nyumba Nyali nkae." Na amwambie jirani yake, "Skiiza, mii mume hatoni kantroli kabsaa."

 

59. Ndio ntkulie mimi kwa mfano. Niko hapa sasa mwaka wa 28 huu. Idi ya kwanza nilikua na listi ya jamaa na marafiki 72. Nawakorogea simu duka la Mchina downtauni, si Minal Aidini hizo na amkua amkua zake nyingi. Kila wakti ukipita, napatikana na misukosuko na mitihani kutoka kwa hawahawa jamaa zangu na marafiki. Baada ya kila mtihani napunguza listi, baada ya kila fitna napunguza listi. Nkipeleka kadi za Toronto za CN Tower (hapakua na kadi za ming'aro wa sparkalz za 'Eid Mubarak' muzijuazo nyinyi huku zama zile) napata feed back naambiwa, "Je, hizi kadi anzinunua kwa jumla?" Hizo zao za rejareja sikuziona, wala haitokei siku mtu wa "matini" akanikumbuka akanikorogea simu angalau akanipigia akansalimia tu. Bali nlimpigia jamaa yangu mmoja atia mzigo Abu Dhabi, nkampata anaipokea Tanga yuko holidee, akiipokea anambia, "Kama una jambo lolote la muhimu, sema chapchapu, maana ntachajiwa roaming chajiz, wantia msumari shekhe." Mpaka leo sijampigia tena simu kumtia msumari wala kumtoa mwiba, na mwaka ni wa 12 wendao tena huu.

 

60. Kwa hivyo, listi ya jamaa na marafiki mwaka wangu wa kwanza Toronto ulikua ni mtu 72. Wengine walokua na simu za nyumbani (hakuna mobaili sku zile) kuwapigia niliwapigia, na wasokua nazo wote walipata hizi "kadi za jumla". Jee 28 yaaz leta, mambo yakoje? Simu niipigao ni moja kwa hisabu. Na hii nampigie rafki yake marhem mamaangu tu, bas. Mtu mwema ambaye mamaangu aliniusia nisimtupe, baas. Na waifu nae? Simu moja vilevile. Ampigia mamake tu, ni "Jambo?" "Jambo." Babake wumanaiza, mara yuko nyumbani, mara hayuko. Akiweko nyumbani na yeye pia ni hiyo jambo jambo tu, na aspoweko basi huwa ni asiyekuwako, na lake haliko. Laif hiyo.

 

61. "Majuu" basi ndio namna hii. Wanaokuja bado wageni mato yawan'gara, jino la mwisho waliona. Washazoea wasmamishwa na mapai saa moja ya usiku Posta waulizwa kitambulisho. Au wakaa miaka 30 Dubei na hawana raits zozote. Hapa wapata sheria ya kukaa na kila jambo. Huwa na furaha telee. Lakini wape taimu kidogo wa adjust. Kisha ile rialiti huwapiga. Wakitanabahi hapa wako Kazinistani hufanya akili. Ndio usione Madachi wapenda kupeleka mabaskili ati ni hobi ile, laa. Madachi wapeleka mabaskili kusevu pesa, maana hiyo petroli yenu ya Arabuni ni ghali mno. Ule ugumu wa Mdachi ni kwa sababu they can't afford to run a car. Ata zile tulips maua yao si kuzidi malav bwana. Tulips ni biznez, na maua haya yaliletwa kutoka Taki miaka 500 iliyopita, ikawa mbegu zake haba 5 wanunua nyumba kwa watu wanavyoipigania biashara ya mauwa. Ndio mpaka leo maua mengi Ulaya nzima yatoka kwa hawa Madachi. Ni kazi hii, si lavu wala starehe. Au huoni viatu vyao maarufu ni vya mbao kama mitawanda (waziita clogs), ata soli hazina? Na "going Dutch" ni maarufu dunia nzima maana yake ni "twende fifti fifti", twenda mii na wewe mchumba wangu kula Abasi Kefu, lakini mii nalipa bili yangu kando na wee walipa yako kando. Haa, kula unenepe basi!

 

62. "Majuu" ni ikonomiks. Mambo magumu. Na maua ya tulips ya Kidachi ni hayo, na maua yenye pesa zaidi si tulips ya ofisini au kutengeza ma bukee (bouquets) za harusini, bali maua yenye pesa zaidi ni bangi. Au huoni Akasha andenguliwa Holland? Basi ingia kafee yoyote uvute stimu zikujae kitwa tele, na ukitaka ufanyiwe uji wa bangi ukae unwe ndoo nzima pia utafanyiwa, bora pesa yako tu. Na watu Afrika wangojea hagallwa zetu, wakiskia "majuu" wao waona sku zote sisi tuna pawa shawa (power shower) na hayo majakuzi vyooni, mapresha kuka na ma maikro wevu jikoni, ma dishwosha na ma woshing mashin majumbani, wala kwa hakika watu wa "matini" hawana haja ya vitu hivi maana hivi ni taim seving devices, na wao taimu ya Ulimwengu mzima wanayo, hawajui ata waifanye nini. Pengine Afrika fanyeni biznez yakuuza taimu yenu mutakuwa mamilonia.

 

63. Na ukiona Emerika kila mtu ana gari usione ni starehe ile, laa shekhe. Ile ni necessity. Masafa ni marefu. Wakaa Mazeraz na dukani kununua maziwa ni Kibokoni, utakwenda kwa miguu kweli? Huwendi. Na ukisema utapanda basi mabasi, Emerika ruti zake undeveloped. Itabidi upande pengine mabasi 5 tofauti utie na lundi kwa juu ndio ununue painti yako ya maziwa. It's mo ikonomikal ununue a beat up car - gari sekan hendi lilochoka - likupeleke wendako. Ni kama Maskati vilevile. Huna gari basi kazini hakwendeki, simpal. Wakaa Ruwi uwende shopping mtaa jirani wa Matrah ukanunuwe samaki ni kilomita 5 kwenda kurudi, halafu uwende kazini Azeba hizo ni kilomita 20 kwenda na 20 kurudi. Utapiga mguu na jua la 40 digriiz? Na watu Omani wapeleka magari maana maji ghali kuliko petroli. Petroli ikisha (na kwisha itakwisha, Qabusi asema 2020) Wamanga watapanda ngamia. 

 

64. Ndio binadamu lazma aishi na filosofi katika maisha yake. Mrusi Kalashnikov aliunda bunduki first klass, ishamaliza zaidi ya miaka 50, and still no one can match it ulimwengu mzima, ata Muemerika na teknoloji yake yote hana mfano wake. Maturkana wasokwenda skuli waeza ipiga bunduki hii sawasawa kama maofisaa wa kijeshi waliosomea vyuo vikuu vya Nato. Na filosofi yake huyu bwana ilikua ni hii, "All that is complex is useless, and all that is useful is simple." Nyii wa "matini" mwataka kuja "majuu", na wote wa "majuu" watamani waje waishi hukuhuku kwenu "matini". Alfajiri wenda baharini kuogelea, saa 2 asubuhi wenda tia mzigo wako, na ukirudi zako nyumbani saa 11 uko ndiani unkujaona mkungu watafta jiwe upure kungu zako ule. Simpal, enjoyable laif. Simpal is good. Lakini binaadamu hatosheki. Ndio Mzungu akakwambia "The grass is always greener on the other side of the fence." Wee wataka haya mambo kompliketed ya "majuu", wala ukifika hutayaweza, yatakutumbukia nyongo. Ndio Wazungu pia wakakwambia, "Be careful of what you wish for." Sababu? It may come true, na hapo basi huenda hizo wishes zako zikakutumbukia nyongo.

 

65. Ndio mikono michafu si ioshe na maji itakauka wenyewe Afrika kwa jua na joto? Ha ah. Wee wataka tishu ndani ya gari. Tishu zinwekewa "majuu" kwenye ubaridi wa friza, upate kufutia mikono kwa tishu sije mikono ikafriz. Nchi zenye joto za Ulaya, kwa mfano Spain, wajitamba kwa maji. Lakini wee M'ngu atakujaalia nyumba yako Nyali ushatia tishu chooni, wataba tu kaa nyani wala akili hutumii. Kama unadhifu ni kutamba na tishu, basi mbona huogi na tishu pia?

 

66. Afrika kuna raha. Ndio ukaona Mchina atamuova teki Muemerika kiuchumi kabla 2020, na hivi leo yuko namba 2. Na filosofi yake ni simpal. "If you want to develop your local economy, build a road." Sasa Afrika ya leo si China, manake barabara hakuna. Pesa zinazotengewa kujengwa au kuimarisha barabara zapigwa. Hiyo ni korapshen ya Kiserikali. Na Waswahili korapshen yao ni kuwa mahasidi wakihusudiana na kuvundana sku zote. Jee, wee waona hata ndugu wawili waliozalika tumbo moja wakishikana, wakawa wanchanga senti zao na kushauriana na kushirikiana kusmamisha miradi? Labda ni ndugu 2 katika alfu 20.

 

67. Ndiyo hiyo barabara ya Wachina, si barabara ya lami tu. Ni briji pia. Na briji yenyewe si briji ya chuma, ni briji ya kimawazo. Lazma muungane kimawazo, where there is a "meeting of the minds" ile briji iwaunganishe, pawe na barabara au briji yakuwaunganisha kimawazo baina yenu. Kushirikiana is the key. Nyii mwataka panda ndege tu mwende mukalete bidhaa za China muje muziuze kwa kutamani tu, kabla nyoyo kulingana? Hamuwezi, sababu hamuna filosofi wala guiding light ya Kichina ya kushirikiana. Ikiwa mumbakia mwatimbana na mwazozana, huku kuendelea mutaendelea vipi?

 

68. Makosa yetu wenyewe Waswahili. Na Waswahili ni "Waso hili? Wana lile." Twataka kwenda "majuu" lakini Kalashnikovu akwambia simpal is best kama maisha ya huku huku "matini". Twataka maendeleo, lakini ukienda Unguja utakuta "maendeleo" ni wanawake kuwa na timu ya mpira yaitwa "Women Fighters FC" (si ni ugahba tu huu?). Na twataka maendeleo yet Waswahili tuna korapshen yetu spesheli ya kudhulumiana na kuzozana sisi kwa sisi. Mbona hatuji chalenj, tukasema wajua nini, tutaanzisha biznez sisi kwa sisi and this is how we will do it, let's go.

 

69. Jamaa mmoja aitwa Khalifa aliniomba laki 7 "tushirikiane" kwenye biashara ili aanzishe matatu ya kuzungusha Wazungu mbugani. Kwa sharti moja lakini. Anambia, "Pesa nipe, lakini usiniulize kitu kwa muda wa mwaka mzima." How he plans to run this one matatu, maana pana cha maspeya, pana cha redio komyunikeshenz hapa, pana kutafta hao watalii, pana ku advertaiz, pana kupata kibali, pana inshurens, pana first aid, pana logistics za petroli, maji ya kunwa na lanchi, pana Wazungu wakishikwa na mkojo au mavi wende wapi haja, pana kuwa na jeki na maspana na maspeya taya, pana knowledge sasa wanyama wako wapi sizon gani saa ngapi, pana mambo ya wedha na ilmu ukisakama topeni utajitoa vipi, pana pesa za mkononi za emajensi na pesa za kuhongana ukipambana na trafik, pana, pana... mambo tungu nzima. Na ekspirians ya kupeleka watoto wa skuli kutoka majumbani mwao kuwapeleka Staa of the See tu Khalifa hana, lakini ataka anzisha "biashara" ya kuzungusha watalii Tsavo na Masai Mara. "Usiniulize kitu"? Jamanini eeh, STOP THE FUCKERY! Au kwa Kiswahili kingine, ateni ushoga.

 

70. Tuwaangalie watoto wa "majuu" waowa na kuolewa na nani. Pana Ramla aishi mji wa Breda ulioko karibu na Rotterdam, Uholanzi. Ramla ana Mdachi wake mweusi aitwa Desi Wijdenbosch, kutoka Suriname, Emerika Kusini. Wao hawakuowana, bali waishi "saman vonen", kama galfren na boifren tu. Wana watoto wavlana wawili wazuri, wamfuga marasta kama baba yao. Kuvuta bangi kwa Desi ni katika ibada muhimu. 

 

71. Wafaa black beauty ansomea u byutishen mjini London, nae anolewa Eindhoven na Henri Geert, Mdachi wa Kizungu wa Zandvoort (rafki zake Wafaa wa London wauita 'Zen-mavuzi'), mji wenye bichi maarufu Holland. Geert ati aitwa "Jamal" sasa baada ya "kusilimishwa". Madachi na lugha yao - a bastard language of German & English, lugha hii hawana "J" basi waitamka "Y". Wafaa nae anzaa na huyu 'Yamal' wake watoto watatu. Ijumaa mosi na ijumaa pili awapeleka wote music lessons - ni kutwalii piyano na vayolini.

 

72. Swalaha anamtia mimba Mjameka akazaa nae. Mara mbili. Wao waishi Birmingham, Uingereza. Madhake ankataa asimuowe "mjakazi" huyu au hampi radhi zake, kwa hivyo Swalaha sasa andunga sindano ili asipate watoto wengine. Wanaharamu wake awaona kila wikendi, na Daloris anamshkaji wa Kijameka, lakini Swalaha vitu kupewa bado apewa now and again, kwa siri, "if he behaves." Na maana ya ku bihav ni kukoboka, amnunulie toaster this week, na mobile phone next week.

 

73. Mbaraka hensam boy nae anamuoa Msomali. Mtoto mmoja wanzaa, lakini merij haiku wak, wanaatana. Kesi iko kotini, Aminoo hataki Mbaraka amtembelee kijana wao Ga'al. Basi tu katika kumuonesha matungu. Na child support money kulipa alipa kila mwezi. Kosa la Mbaraka, asema Aminoo, ni kuwa Mbaraka soft sana. Na huu ulatifu wake ndio ulomtongea, maana hakujaaliwa kumuinulia mkono akampiga Aminoo ata sku moja. Kisomali, hiyo can only mean 1 thing - Mbaraka kwa hakika does not really love her. Mbaraka sasa yuwenda Afrika, waif hanting. Ampambana na dem wa Kiswaha ngomani Pirates. Buse yake inammaliza. Hivi ashapeleka maneno kwao Zaragoza, na harusi itasmama kabla mwisho wa mwaka huu, inshallah.

 

74. Hii mifano 4 yatosha. Hii ni reality. Mtu huowa jinsi yake. Yoyote mwenye ekspirans atakwambia haya. Why? Waepukana na mizozo na misukosuko mengi. Asojua ataleta kifua hapa apinge, lakini ajuwae ajua kuwa utaepukana na unnecessary heartache. Kabla hatujaendelea zaidi na maudhui haya, tu difain tena Mswahili ni nani. Mswahili ni mtu aliyezalika "matini" ambaye lugha, mila, na dasturi yake ni ya Kiswahili. Yale makundi 6 ya Waswahili - Waswahili wa kiasili kama Wabajuni, na Wamanga, na Washihiri, na Wabulushi, na Wahindi Mabadala walioingiliana na kukulia na wengine kuowana na Waswahili katika mitaa ya Mkanyageni na Kuze na mengineyo, na makabila mengine yaliyoingiliana na hawa Waswahili kwa kuwa ni majirani wa miaka mingi na wengine wao kuowana na hawa Waswahili, wote hawa ni Waswahili. Ukimtukua Ammaari Mshihiri wa Kidogo Basi umbwage Yemen mji wa Seyuun au kijiji cha Al Jurbaa kilichoko majabalini, Ammaari atakuwa kama 'a fish out of water'. Ata kama lugha aizungumza (very doubtful to begin with), zile mila na dasturi za kule ni totally alien to him. Kwake yeye he might as well kuwa unambwaga katika boma la Kimasai lilioko Narok. Kumbuka, mila na dasturi pamoja na lugha ndio utamaduni (kalcha). Ni kama tukutwae wewe uzungumzae Kizungu tukupeleke Swindon, Coventry au London, Uingereza. Wafkiri ufikapo ni otamatik Wazungu ushawajua maadam wazungumza Kizungu? Laa bwana. Watakutia skuli wakupe na mitihani mpaka utawatukia mwenyewe. Safiri ujuwe. Sku zote vishipa na wenye uzembe na ubwam'ba'di ni wale wasosafiri.

 

75. Hal kadhalika Mmanga wa Msa au wa Unguja ukambwaga Omani. Maskati atakaa no problem kwa vile kokote endako azungumza Kizungu, signs zote za barabarani zinaandikwa Kizungu, etc. Na Waswahili ni wengi mno kule, khasa Maskati. Swali kokote mitaani, tagua mskiti huu au ule, utakuta watu waamkuana Kiswahili, baada ya pambaja wakatia stori hapo za paukwa pakawa hataa... Lakini mbwage Wilaayatud Daakhilia huku huku Umangani, atakua ni kama paka aliyenyeshewa na mvua. Lugha huku ni Kimanga kuruka, na mila na dasturi ni za kuamkuana kwa kupiga pambaja za pua na kusonga haluwa za tende. Same goes for Wabulushi ukiwabwaga wilaya ya Baluchistani Pakistani, na Mabadala ukiwabwaga sehemu ya Kutch, Gujirati India, utawakuta wako lost. Kwa hivyo kwetu sote ni Uswahilini, amkeni! Watakaungu kina Bin Jelebi na kina Bin Haluwa, hakuna mwenye kwao katika hawa illa ni huku huku Uswahilini - mashiko yao yote yaku huku. Ndipo wakipozalika, ndio lugha waizungumzao kama kunwa maji, mila na desturi zao zote ni za huku. Waswahili ni sote sisi kwa sisi tuliozalika na kukulia Uswahilini. Sasa tuendelee na stori yetu ya posa na kuowa huku "majuu".

 

76. Watu uzuri kuoa jinsi zao for a simpal rizon. Ndoa ni furaha jana na kufuriana leo, na ni kuteka kesho na ni huzuni kesho kutwa, na ni kusheherekea mtondo na kuomboleza mtondo goo. Pana ups and downs. Ukiowa au kuolewa na mtu jinsi yako, utajua protokolz of bihevya. Mke amskize mume Kibla chake aongoze nyumba. Ramadhani hiyo angalau upate pikiwa mahamri na matobosha. Mukiwa nde na hamutaki mtu ashike mita inyi mwanena iye, mwabonga Kindau au Kimvita. Mukitoleana joksi angalau mufahamikiane muteke pamoja. Na sku nyengine mke akufukizie chumba na nguo zake azitie mrehani, na ukitaka akutezee chakacha chumbani mwenu akukatishie kiuno. Na muhimu zaidi kuliko jambo lolote, pakitokea kutoelewana kwa sababu yoyote, pawe angalau na marefarii kutokamana na jamaa zenu wawakulishe.

 

77. Sasa hawa Waswahili walio owa na kuolewa na wasiokua jinsi zao - yaani wasiokua na kalcha ya Kiswahili - wengi hukumbwa na matatizo ambayo yangekuwa more easily solved wangekua waelewana lugha na mila. Saadie yuko Los Angeles anaolewa na Mkongo Pierre Mubenda aliyesilimu kikweli. Lakini wagombana kwa upuzi mara nyingi, na vyakula Mubenda avipendavyo ni fufu, kwanga, mwambe, na tshitekutaku. Waif kuvipika haviezi, heshi kuviunguza. Au mchkulie Ratibu aliyemuowa Msomali Ayan. Wanwatana baada ya miezi 13, na sababu ya ukabila wa Kisomali. Ayan ni katika Ma Is-haka, Wasomali weupe kutoka Hargeisa, na wamuona Ratibu ni katika ma "Reermunya" au 'Waafrika'. Basi femeli yake ikimwita Ratibu 'adoon' sku zote mpaka yakamtaffash, na talaka aliitoa sababu Ayan amtaraji mumewe ampe yeye mshahara wake wote, kisha yeye Ayan ampangie yeye Ratibu bajet azitumie vipi.

 

78. Kwa hivyo uzuri uowe mila yenu; if marriage is a gamble then you bloody well better improve your odds! Kwa hivyo wazazi wa wavlana na waschana wa "majuu", make shua mwanzo wawapa ilimu nzuri ya Kiislamu. Uspofanya hivi, maswala wenda jibu wewe, si mimi, kesho mbele ya M'ngu. Ukisha fanya hivi, kisha jaribu umuoze mwanayo mtoto of the same kalcha ili a improve his/her odds of a happy merij. Muoze watoto wazuri wa mwendo na tabia kutoka hukuhuku "majuu" maana utakao waoza watakua washazoea hii "rat race" ya "majuu", kwa hivyo hawana cha kuwa na kazi ya ku adjust. Kama hukupata, fkiria umtaftie wa "majuu" ya Dubei na Maskati. Na unshindwa, wataftie wa "matini". Lakini fanya hom wak yako uzuri, sije ikawa ni kisa cha ile nyimbo, "Kumbe si tende ni mende, kimdara kakimbia." Sije ukapatwa badili ya kupata.

 

79. Ndio ile risachi waliokuwa wakiifanya wazee wetu zamani. Watachunguza binti/kijana atoka mlango gani. Kama baba ni mzinifu au ni wife beater, mvlana wake ana a high statistical probability kuwa atafuata mkondo huu huu. Kama mama ni spid boti haiyumkiniki kutoka binti swalihina illa kwa nadra sana. Mlango wauchunguza kwanza ata kabla hujaja kwa mtoto mwenyewe. Kama mlango mbovu, ata you don't take it any further. Watizama mlango mwengine ulio madhbuti. Na ukiupata mlango imara, ndio wamchunguza yule mtoto sasa. Jee, ana washkaji? Jee, ansoma? Jee, ana adabu nzuri? Jee, aswali? Jee...

 

80. Mlango wa nyumba ukiwa mbovu huna haja kamwe ya kuangalia dirisha. Japo wengi Waswahili sku hizi wameharibu maana ya kuangalia mlango. Sku hizi waleta mambo ya mlango mzuri ni wa kina AlBaBin (soma kifungu nambari 12 cha "Illa 27 za Waswahili") ilhali yakua waeza kumkuta kwa mfano Ba-fulan binti zake wote wanaharibika, ni wazinifu, washawahi kutoa mimba mara kadhaa, haweshi kusema watu na masabasi na wazuzi na maswalata namba wan, pamoja na pengine upate mzee wao aliala na binti yake, au ameua mtu majabalini huko, au wana ndugu wa kiume mashoga wankwisha kazi, au wana sista mmoja jisago, au wana hababa magati, au femeli ina upungufu wa akili ndugu mmoja mwendawazimu wa kutiwa pingu, na ndugu mwengine ana maradhi ya wasiwasi tabia yake ni kufunga na kufungua milango usiku mmoja mara ishirini, au... lakini maadam ni kina Ba-fulan bas, wahishimiwa hawa, na kuwaoza binti yako utawaoza chapchap. Haa ah, hapana bwana. Hii ni kamba mbovu itakukatikia ndiani, atana nayo shekhe. Wee tafta sana huyu Ba, lakini sije ukapatikana na baa lenyewe tu.

 

81. Lazma uuchunguze mlango vizuri sana. Uukague kwa hikma na busara. Mlango ukiwa ni mzuri na unkuafiki, kisha sasa umuangalie huyo kijana au binti. Asiwe atafuta pochi. Vipochi "majuu" vina tundu, sije akaja akakupa hedek mukaatana ndiani. Hapo ukimaliza uchunguzi wako wa mambo ya ndani na ya nde basi ndio sasa mutawakkal tena. Na usisahau shekhe, there are no guarantees in life. Kwa hivyo mwanangu, uutiapo mkono kizani, fungua mato vizuri, tena tukua na tochi. Sku zote mwanangu uwe na tahadhari.

 

82. Na mukienda kuposa huko "matini" sema kweli jamani. Ukimpa kijana au binti ya mtu wa "matini" illusions za "majuu" akawa na false hopes and expectations, jua ya kua you will inevitably run into problems, au sivyo? Kwa hivyo, do not mislead Waswahili wa "matini". Wakija wajuwe exactly what's in store for them. Laa sivyo watakuja tambua munwa"con"i and they will give you hell. Wataka salama yako, lay your cards on the table, face up. Kusudi wajuwe na mapema reality ya huku "majuu" ni nini, ili wasije na mafantasi tele huku kisha wakaja furizana bure. 

 

83. Tuzungumzie kuhusu madharau kidogo, prejudice. Tuchkulie Wasomali kwa mfano. Kwa wale wajuao, wajua wanawake wa Kisomali wengi mno ni materialistic. Mpaka malaya wa kwanza wa waziwazi wa kujitembeza mabarabarani wakisega nguo utadhani wataka ruka tope Msa walikua ni hawa "Walaaloo" au "Wasonga". Na mpaka leo wapo, hata juzi nilpokwenda Msa nnamuona kiruka ndia mmoja, jishangingi jizuri kweli kweli kama hulijui kazi yake na wapita ndia ukaliona dirishani utafanyafanya ukapeleke posa chap chap. Jisupu lenyewe laitwa Almasi, watu wa kwenda ma Floo wote walijua. Material beings hawa. Hata pana msemo wa Kisomali kuwa mwanamke wa Kisomali akilifuata pochi lako atakwambia hata mavi yako yanukia aluhudi. Wajuao wajua. Je, ni haki kusema wanawake wote wa Kisomali wamo katika kundi hili?

 

84. Laa. Wanawake wa Kiswahili pia wamo. Hizi ni katika zile ila 27 tulizoziangalia kwa kirefu. Wengine watakwambia 99% ya wanawake wa Kisomali wanamshinda "I'm a material girl" Madonna. Namii n'takupa figa hiyo hiyo ya 99% ya wanawake wetu wa Kiswahili kupenda pochi. Mwengine atakataa, ata i revise down this number to 60%. Zote hizi zategemea bahati yako na khibra (ekspirans) yako katika laif. Sisi tuliokaa "majuu" twajua wanawake wa Kizungu wengi ni material women. Kwa hivyo lipigishe breki ji konvatibal lako na mademu Wakizungu watacharukwa na kukuangalia kwa midomo wazi na mato yao kuwang'ara Oxford Street; na wanawake wa Kiswahili watakupa bonge la smaili na huku waziwate hijabu zao ziwaanguke kusudi uzione nyele zao wakiwepo barabara ya Digo Rodi, na wa Kisomali watayakaba magontina yao kusudi uzione shepu zao downtown Mogadishu.

 

85. Kwa hivyo tusiwe na upuzi wa ku generelize - let's stop tarring people with the same tar brush. Umskie mtu, "Ah, Mdigo ni mzigo." Mswahili na vitimbi vyake unsahau ndio ni mzigo mzito zaidi? Au uskie, "Mgiriama ni Mgiriama tu." Na jee Mmanga? Mmanga si ni Mmanga bwana, au yeye si Mmanga? Au usikie, "Ah Wa Kuze n'mahasidi mno." Kweli wengi watu wa Kuze ni mahasidi mno, lakini, si Waswahili wote ni mahasidi, twajua au hatujui? Twajua vizuri sana. Au uskie, "Ana mdomo mchafu kama Mgunya." Hujapita Kidogo Basi au Guraya ukaskia waume kwa wake wa Kishihiri midomo yao michafu inshinda mitaro ya mavi?

 

86. Twapenda kutukana watu, lakini mambo hayohayo tutukanayo watu tunayo sisi wenyewe, na mara nyingi tunayo zaidi ya hayo! Ndio M.J. akakwambia, "I'm starting with the man in the mirror. I'm asking him to change his ways." Tuanze na nafsi zetu tuzitakase mwanzo. Ni kama uowe Mkamba. Katika shughul utafurahi shekhe, maana si kelele za ashki hizo. Sawa sawa na Mhabashi. Na Mswahili hako mbali nyuma. We're all the same, more or less. Labda kalcha za Mhabashi na Mkamba jambo hili la ku-advertaiz love-making yashajishiwa, na sisi wengine twakatazana tusisikikane maana mambo ya chumbani lazma yabakie chumbani. Na Msomali ni kimyakimya, pengine ni kule kutokuwa na feelings nyingi kwa sababu ya kukatwa kinembe na kushonwa kabsaa, kukafungwa ndia kukabakia tundu ndogo sana ya kupitisha damu ya hedhi tu, ata ukimuowa mke huyu taimu ya kumuingilia utashindwa hiyo shughul, nkama mtaimbo ulokita kwenye jabali. Huna namna, ndio ni mpaka umpeleke sajari kwa daktari shekhe akafunguwe barabara. Lakini wanawake wa Kisomali wa "majuu" hawakatwi ndini, basi kelele zao majirani wote watapata khabari.

 

87. Kwa hivyo tuataneni na huku kutukunana. Let's concentrate our efforts on what we can achieve and what we can change for the better. Khaswa hawa 99.9% tulioko "matini" ambao they will never come huku "majuu". Ya hawa wa "majuu", yao yankwisha. Wao wankuja ma Emerika na nchi za Ulaya na Khaliji na wako kwenye mabio ya kutafuta rizki Wazungu waiita the Rat Race. Wenda mbio huku Kazini-stan wala hawana cha kupumua, kama hamster on a treadmill. Jamaa wote huku wako mbioni walipa kodi wakienda makazini, na jioni wao ni kuwasmamia na kuwasomesha watoto wao, maana maskuli huku ni bure tu (yani wasiwasi bil khannasi tu), kwa hivyo mzazi yoyote akikupa siri yake atakwambia lazma watoto uwasomeshe wewe mwenyewe wakisharudi kutoka maskuli au watakua mabunga wa mwisho sku zote washika mikia tu. Kwa hivyo wazazi risponsibal huku "majuu" ukienda majumbani mwao ni kama uloingia tushen ya Pujara.

 

88. Kwa hivyo walioko "majuu" laifu zao zinkwisha. Maisha yao hayana tamu wala nyamu. Wako bizi walipa mogej, kushikika hawashikiki. Ata rafki yangu mmoja alintekesha sana. Anambia Junior Meneja wetu atayaangalia maslahi yake kwa kumskiza mkubwa wake yeye kazini, au atayaangalia malalamishi yetu sisi wafanyi kazi wadogo, ati ayapeleke mbele kwa wakubwa ili yatatuliwe? Namuuliza kwa nini? Akanipa katika hizo hikma kubwa kabisa. Anambia, "Never trust a man with a mortgage." Maadam nyumba ailipia, lazma ayaangalie maslahi yake na ya bosi wake, sije akafutwa kesho akashindwa kulipa mogej. Kwa hivyo sisi watu wadogo ni potelea mbaa? Potelea mbali, tukae na shida na matatizo yetu, tuselehee.

 

89. Waswahili wa "majuu" wao wenyewe hawainjoi maana sku zote wana kumbukumbu za fifti fifti. 50-50 ndio nini hii? "Leo ijumaapili, Afrika n'gekua niko bichi nala hepi, huku kumaamake ndio mwanzo niko mzigoni". Au "F'tari ya vitalifa na figili yashuka kweli, na huku ata harufu ya Ramadhani huisikii kamwe!" We are all a product of our childhoods. Kuna wale walioko Maskati sasa washamaliza miaka 30 tokea waondoke Afrika, lakini bado kumbukumbu hizi huwajia na wao wako majangwani kule. Kwa hivyo huku hawako, na kule pia hawako, sisi watu wa "majuu" kwa hakika ndio tuliokula huu. Kwa hivyo, "majuu" tuko bizi twalea the next jenereshen, watoto na wajukuu wetu ambao wako fully adjusted huku, manake utoto wao wakifunua mato hawaijui reality nyengine ispokua hii walokulia nayo huku "majuu". Kwa hivyo Waswahili wa "majuu" washa rizain kua yale mazuri wayakumbukao ya zamani are gone for ever, ilobakia wazidi jitihada wawalishe, na kuwavisha, na kuwasomesha watoto wao, hayo ndio yalobakia sasa. They take pleasure kuona watoto wao waendelea - hii Mzungu aiita "Vicarious pleasure". Yaani kufanikiwa kwa watoto wao na wajukuu wao ndio huwa furaha kwao, japo locked away in their memories is the pleasure of a simple life ya Afrika that is gone from their lives and which they will always miss. Upo kijana?

 

90. Na pana wengine wanaojaribu kurudi zao Afrika na wakashindwa. Shuebu alipeleka matatu zake mbili akapigwa pande na madereva wakimteza shere pesa zake mpaka akaziuzla mbali zote, at a huge loss. Mwishoe aliamua arudi zake "majuu". Na wachache mno hu succeed wakirudi zao "matini", kama Thabiti aliyeowa Mcheki (Czech). Mzee huyu ana baa yake pale Mtwapa Creek, auza mchuchula na nyama choma baada ya 32 years kuishi Ureno.

 

91. Laifu hii. "Majuu" ikamfanya mtu asahau mpaka dini yake khaswaa, na yeye ni mtu mzima, si mtoto. Kisa cha jamaa mmoja n'limkuta Uyonani (Greece). Niko na waif twazuru hekalu la Akropolis mara jamaa akaanza kutubongesha Kiswahili. Tunstaajabu. Kumbe ni mkaazi wa Athens wa miaka mingi, anaowa Myonani na anzaa nae watoto. Tukapiga nae kahawa pale kafee, na nikampa kijitabu cha Mtume Muhammad S.A.W. nlichokua nacho mkobani nikikisoma mara kwa mara, n'kampa yeye kama kijizawadi. Haya, Abdurazaki akatualika jioni sku ya pili kwake nyumbani. Tukenda mimi na waif. Mkewe ana tabia nzuri, na watoto wao mabarobaro pia tukawaona. Baada ya dina, tunkaa siting rum, wakaleta mvinyo, waka toast hapo wakanwa wote. Ata tukiagana twatoka tena, jito langu likaangukia kwenye pipa la taka lilokua wazi pale mlangoni mwa jikoni (jiko hili hapa na mlango wa kutokea huu hapa), n'kakikuta kitabu nilichompa jana yake kimo juujuu ndani ya pipa pamoja na maganda ya vitunguu. La haula walaa kuuwata!

 

92. Kwa hivyo, Waswahili wa "majuu" yetu yankwisha. Tuko kwenye ma konkrit jangal huku, tuko katika mbio za marathon twalipa mogej na huku tukibadilisha vibinda na kuwapa watoto tushen majumbani mwetu. Mahisabu mengi - college fund ya mtoto, jee mwezi jana tulitia kitu bengi? Jee n'linunua tishu supamaket jana? Afadhali n'taje ya tishu. Nimemgombeza waif sababu annunua tishu ya ughali juzi kushinda jana. Ukiishika tishu yenewe koliti koliti kweli, na ni 'frangranced' yanukia asmini. Sijui Wazungu wakisha jifutia nazo hunusana matako hawa au nvipi sijui. Sisi twanunua sababu vyoo vya Kizungu ni sharti uweke karatasi kwanza, au unyapo, shonde likitumbukia majini mle maji hukurukia ukajitia najisi, kwa hivyo itabidi kila ukibwaga bomu uinuke kidogo. Bila ya kwanza kutandaza tishu mle itakua ni eksesaiz hiyo si kunya tena. Kwa hivyo watia toilet pepa kwanza. Mii si maindi sana, hutia mpaka magazeti tishu zikisha, n'kawanyia viongozi wote wa ulimwengu. Basi juzi tuko kazini, twatia stori na swaiba. Sote twalalama ya kuwa recession ni kali, yatuumiza. Mambo mabaya, wakuta watu 500 wakimbilia nafasi za kazi 10 tu namna mambo yalvyo haribika. Namwambia, "Tom, I've change all the lights in my house to the energy saving bulbs." Tom akanijibu, "Listen, things are so bad that last week I was down to my last roll of toilet paper, and as you know, we're not getting paid until next week. Know what I did? I took the two-ply toilet paper and separated it, and used one ply at a time. When I'm done, damn it, I got to wash off the fucking brown skid marks that are all over my fucking hand!"

 

93. Waswahili wa "majuu". Yetu yankwisha bwana. Twazeeka, sasa hivi tutapelekwa old peoples homes watoto wakianza college. Ndio utatembea barabarani umkute jamaa bleki hapunguzi gari lake spidi wala kusimama hasimami kwenye zebra crossing, ushajua huyu ni JJC (Jojo Just Come), fresh kutoka Afrika. Mpe taimu atastaarabika. Lile gari hatojiona kuwa ati he owns the road. Atatambua gari is just a tool to take you from point A to point B. Mpe taim, na pengine atakuja kua texi draiva kamwe, apeleke wateja huku na kule, mpaka lile gari litamtumbukia nyongo. Ndio ataa akienda Afrika kutembea, hataki skia neno "Gari" abadan - atakhiyari ende zake Lamu akapande punda, au apige mguu kuanzia Ngomeni mpaka Changamwe, ende akanunue maembe kule arudi zake mtaani. Hataki cha magari wala hataki cha simu. Nyii wa "matini" ndio mukiona kwenye CNN pantoka iPhone 4S mwachachawa mwaitaka. iPhone S, na ile 'S' stands for 'Siri'? Mbiombio mwaitaka hii simu, mwaona hii simu ya voice command application pengine itakuWezesha wewe upate siri za watu wa ulimwengu mzima, including mke mwenzako. Lumbukeni nyii.

 

94. Ndio yoyote alioko "matini" huwa bongo lake linfungika, mpaka asafiri. Waambiwa edyukeshen haiko vitabuni; safiri uelimike. Wote waliokwenda "majuu" wana mtazamo mwengine wa maisha, si kama yule ambaye hajasafiri. Muangalie John Peter, kwa mfano. Huyu alikaa "majuu" miaka 15, akasomea London School of Economics (kama Sefu wa Gadafi), na akaowa mpaka Mzungu, kabla ya kuamua kurudi zake Kenya aupiganie uhuru. Kama hujamjua bado Joni Pita ni nani, yeye si mwengine ispokua ni Kamau wa Muigai mzaliwa wa kijiji cha Kikuyu, aliyejibadilisha jina akajiita Jomo Kenyatta.

 

95. Pesa, na raha, na utajiri, zote hizi ziko Afrika, haziko "majuu". Mukizipigania hizo Green Card muje Emerika, jua ya kua mwapigania utumwa, lakini nyinyi kujua hamujui. Hakuna uneducated people wajao. Emerika hawa uneducated people ni wengi, wataka edyuketed & motivated people, fresh blood, walio na hamu na ghamu ya kutia mzigo. Ndooni mujisuwe huku muitajirishe nchi, lakini mwishoe mwaja realise you're only working to pay the bills. Kutajirika urongo hutajiriki. Utajiri wa pesa uko Afrika, na umakini wa roho pia uko Afrika. Tatizo la Waswahili na Waafrika kwa jumla ni kuto yatanabahi haya!

 

96. Ndio solushen yenu nyinyi 99.9% ya Waswahili ambao hamtokuja "majuu" ni mukae kitako, mupange. Kidole kimoja? Hakiuwi tawa. Lazma vidole vishirikiane, na lazma Waswahili washirikiane. Washauriane mawazo, kisha wachange pesa. Na u lezi tuuwateni jamani! Mukiwa na huku kushirikiana basi jua ya kuwa mutajijenga, na mutaishi katika mustawa wa hali ya juu ya kimaisha. Is this wishful thinking? Yes. It's very unlikely to become a reality. Why? Because if you want to know where you are going, first you have to look where you are coming from. Historia ya Waswahili wao skuzote ni kutengana na kuzozana. Kwa hivyo, fyucha itakua ni hii hii. Ispokua thruu edyukeshen. Na edyukeshen nduu zangu, sikusudii mupawe vitabu muvidurusu na muvitwalii, ha ah. Nakusudia muwe na soshiyal enjiniyaz, yaani ma community workers, ambao ni watu wenye kuzunguka na kuwapa fikra mpya kama hizi ili angalau mambo yabadilike for the better. My estimate? Pengine 1% tu ya wale 99.9% waliobakia "matini" waeza ku chenj.

 

97. Lazma nyii wa "matini" muamue mu move on from consumers muwe producers. Manake nyii sku zote ni makonzyumaz, mwataka kula tu. Na mwangoja kupewa hizo "zaka zenu". Lazma muchenji, dunia ya leo ni swim or sink. Muwe imma mwatengeneza vitu mukiviuza, au muwe wenye kuleta huduma (yaani either producing goods or producing services). Mjukuu wangu wa miaka 8 sama iliyopita alipanda tembe za maharagwe katika mchanga ulokuwemo ndani ya mkebe, na baada ya miezi 2 hii Agosti iliyopita, akavuna maharagwe yake, akayachemsha, akayala. Hakuna aliyemtuma. Jee wewe baba mzima hapo ulipo, ushawahi kupanda haragwe moja? I can gerentii that hujawahi kupanda, na kama ulilazimishwa skuli, hukuwa na intrest ya kusubiri ukavuna ulchopanda. Hujioni kuwa ni konzyuuma wewe, wataka kula tu?

 

98. Hebu fkiria Msa hiyo hakuna hata kiwanda cha kuunda baskili? Hata basi kiwanda cha kutengeza msumari shekhe? Lazma tuungane, na lazma tuwe maprodyuzaz. M'ngu huleta baraka kubwa katika kushirikiana. Kushirikiana ndio kwaleta mashirika, companies. Mabiashara haya. Mwauza vitu - mfano viatu hata kama ni makirikiri - au mwauza huduma (service) kama waalimu kufundisha watoto hisabu. Kushirikiana kwa kheri kote M'ngu akupenda. Kushirikiana asokupenda M'ngu ni kushirikiana kwa shari, kwa mfano uulizwe, "Gati ya Kolombo freshi n'taipata kwa M'meru gani?" basi hapo umlekeze mtu, na shirki ya kumshirikisha M'ngu Mwenye Utukufu, Aliye Mkwasi, Mwenye Nguvu, Mwenye Uwezo Wote, Asiyemhitajia Yoyote, Mfalme Aliyeshinda Wafalme Wote, Asoshindwa na Lolote  - Huyu kumshirikisha usimshirikishe, au utakwenda ona moto wa milele kwa dhulma hii kubwa kabisa. Lakini kushirikiana baina ya sisi kwa sisi, sote tupige kasia kidau chetu kiende mbele, shirki hiyo M'ngu anaihimiza. Sio mpango wetu wote skuzote ni "mpango wa papa", twafkiria kwenda kununua chipsi tule, na the only taim we use our brains ni weta akituuliza, "Bos, utakula au utabeba?"

 

99. Sasa tuangalie kidogo, wee ni wa "matini" wataka olewa na mume wa "majuu", au linkuja toto kutoka "majuu" linkutunuku, toto lataka uliowe likutkuwe "majuu", au pengine wewe wa "matini" wataka kuja huku kusoma, au wataka kuja kufanya kazi, wapi katika nchi nyingi za "majuu" ndiko bora? Tuanze na Yemen. Huku si pahali shekhe. Pana ndaa, pana ukabila, pana misukosuko ya kisiasa, na kazi zenyewe hakuna, wenyeji 35% hawana kazi hata yakuuza vikoi. Wako about 2 centuries behind the rest of the world. Yemen ni pahali duni kuliko Afrika. Ata gati waiabuduyo karibuni haitopandika tena huku kwa sababu ya uhaba wa maji chini ya ardhi (receding water table).

 

100. Jee Oman? Si mbaya, nchi ya vyetezo na mabuli ya kahawa, lakini huku ni wrong namba pia. Omani na Bahraini wana ukosefu wa kazi wa 15%, na wote wameingilia Omanization na Barainaization - kazi zipewe wenyeji wenye nti kwanza. Na ukiangalia Omani, mafuta yao yesha 2020, hiyo ni kesho kutwa tu, na 80% ya nchi hii ni jangwa tupu la majabali, hapana fyucha huku. Wao waliringa kutoa mabuku yao kuwapa wenye asli za Kimanga wa Afrika Mashariki kwa miaka mingi, na karibuni watafungua milango yote wazi ili watu waingie mijini maana waanza kuishiwa. Wajua baada ya gesi ya kupikia walonayo, hapana tena kitu chengine cha kuendesha uchumi wao. Wajaribu kuvutia watalii, lakini ikiwa Riyali moja ya Kimanga = dola mbili unusu za Kimarekani (ukilinganisha na 1$ US = 80K. Shs), kompitishen ya Kenya jee Wamanga waiweza, maana Kenya is much, much cheaper, na pana wedha bab kubwa na wanyama mwitu fogo bin tele. Kwa hivyo wee ufkiriae "majuu" ya kwenda Omani hebu zindukana. Kweli utawata mpunga wako, na minazi kupepeya, na bahari ya Msa, ukajitie kwenye jangwa, na mitende ya kunyunyiziwa maji ya majabalini kwa mitaro ya falaji ? Bali Wamanga karibuni  watakuja omba vitambulisho vya Kenya katika kutafuta maisha bora.

 

101. Suudia kuna wenyeji wasio na kazi 10%. Na katika nchi zote ambazo utanyimwa haki zaidi pengine hakuna mbaya zaidi kuliko nchi hii. Hata KTN pia ishaleta habari nyingi za waliofungwa bila ya hatia, walioteswa, na hata walio adhibiwa mpaka mtu akauawa japo hatia moja hana.

 

102. Imarati jee, kina Dubei na Abu Dhabi? Hiki kinchi kidogo kina watu milioni 9, na wenyeji ni kama milioni moja unusu tu. Ukosefu wa kazi kwa wenyeji wafika 12%. Wageni wafanyishwa kazi kama mahayawani, na haki hawana, ata afadhali ngamia wao wana haki zaidi kuliko wewe. Ikibidi tena kwenda ndio uwende, utafanyaje tena, ndio itakua ule msemo  wa "Lisilobudi hutendwa." Kumbuka Mzungu ana mshahara mara 2 au 3 kuliko wewe, na pengine wee unsoma kama Mzungu au unamshinda khaswaa, lakini ndio katika ule ubaguzi wa rangi utakao ukuta, japo wee pengine ni katika kina BaHamri, na kina Al Borawiya, na kina Qufuli bin Funguo. Kwa Muimarati huna hadhi, and they don't give a shit.

 

103. Pengine nchi nzuri kwenda ni Qatari, in pesa kaa njugu. Lakini kote huku miji ya Kiarabu utapambana na reality nyingi. Pana unsuria, na kubaguliwa, na kunyimwa haki zako za kibinaadamu. Haki za kibinaadamu kwa hakika ni haki za Kiislamu, na kunyimwa haki hizi utanyimwa tu. Au ushaskia wakimbizi (ma refyujee) wangapi waliopewa makaratasi ya kuishi nchi hizi, au uliskia lini wao kupewa uraiyaa? Hakuna, ata kesi moja pia hutapata. Labda uwe Stiven Chirono aliyepigwa dola milioni moja yake ili awe raiyaa wa Qatar kusudi iiwakilishe kwenye Olimpiks. Lakini kama mbio za Chirono (Sefu Saidi Shahini kama ajulikanavyo na Makatari) huna, basi kwa Arbi huna namba wewe. Aibu na fedheha kwa Waarabu wallahi, wanshindwa na Mzungu. Leo utakwenda London waeza kuta mtaa mzima una Wahindi sehemu za Upton Park, au sehemu yote ina watu weusi kama Lewisham, na wote ni raiyaa wana haki kamili za kisheria, na kuja wankuja juzi kushinda jana tu!

 

104. Kwa hivyo wenda Khaliji (Gulf) hakikisha umesomea kazi. Na kwa kusomea ni unfanya akaunts zako mpaka mwisho wa kisomo, una CPA zote, ndio uwende ukashindane na Wahindi waliojaa kaa nzige kule, na wote wansoma sana "like there's no tomorrow". Na kama huna kisomo cha vitabu, basi hakikisha umesomea kazi vizuri, kwa mfano, una satafiket mia za kuzamia majini (PADI diving), au ni dereva sio wa matatu tu, bali wa trekta na forklifti na... Pana dem mmoja edyuketed nilimkuta Afrika, kazi yake kupaka watu hina. Anambia ataka kwenda Omani awe Wedding Matchmaker. Namuuliza, ashafanya rishachi yake vizuri? Hujiamkii tu, ufkirie wataka kuwa mechmeka. Uliskia Qabusi ana haja ya kuowa? Qabusi hana haja ya mke bwana. Ukifanya, fanya risachi yako sawasawa, usiwe kwenye hadithi za alfu lela ulela bwana. Bila hivi utakua weta hoteli, au utafagia barabara manispaa, au utakua yaya nyumbani kwa mtu, au utawatamba mavi watoto walemavu wa kiakili speshel skuli. Kwa hivyo zindukana.

 

105. Tushaangalia nchi za Kiarabu. Huku ndiko utakuta viongozi wala hepi ile mbov mbaya, lakini wafanyikazi wao  wa kutoka makwetu na Wahindi wasota kwa mishahara ya chini, kubaguliwa, kudharauliwa, na kunyimwa haki zao. Viongozi wa huku wajiita "mashekhe", lakini si israfu yake hiyo walionayo ya kupita mipaka, kwa mfano, mti wa krismasi wa lulu na almasi hoteli ya Emirates Palace ya Abu Dhabi ungharimu dola miloni 11, mwengine "Sheikh" Hamad (aitwa "Rainbow Sheikh" huyu) anchimba makanalz kwenye kisiwa chake cha Futaisi yana upana wa kilomita 2 na urefu wa kilomita 1 lakini hayapiti majahazi wala hayana faida yoyote ila fakhri tu, yanaandika jina lake HAMAD lasomeka mpaka mwezini, na "Shekhe" mwengine ana plet namba ya gari "1" iliyogharimu dola milioni 14! Kwa hivyo, nchi hizi za Kiarabu ni "majuu" nambari ya 7 katika orodha ya nchi za "majuu" bora. "Majuu" yote ni kama jahannam na daraja zake 7 za muwako wa moto na mateso. Kwa hivyo tunmalizana na daraja mbaya zaidi na ya chini kabisa ya kina Firauni na makafiri wasoamini kitu na wanafiki wanaojidai ni Waislamu, ndio hii "majuu" ya Arabuni Gred 7. Wala usisahau janna haiko "majuu" - hapana bwana. Janna ni Afrika, wenye kujua wajua.

 

106. Tuangalie "majuu" ya gredi namba 6. Hii ni Emerika. Uzuri wake ni kuwa huku wewe tayari wazungumza Kiingereza kama wao, kwa hivyo huna haja ya kujifunza lugha mpya. Uzuri kwenda, lakini usisahau hutotajirika. Watia mzigo ili ulipe kodi na mahitaji mengineyo. Watia jobu and pay your taxes to keep the country going. Ndio ukaskia nchi za Kiafrika pana brain-drain; wale waliosoma sana kama madaktari wenda huku wakizitajirisha nchi hizi na kuzimaskinisha nchi zao za asili. Emerika you will work yourself to death. Kama waona wenda holiday camp huku mwenzangu think again. Kama ni daktari afadhali utibu wagonjwa wa maleria utapata pato zuri Afrika, watoto utawasomesha vizuri, na stress yako ndogo si kama huku. Na kama wee ni mwana walilia wembe, haa tukua Naset hii kateze nayo, lakini ikikukata utalia na nani?

 

107. "Majuu" namba 5 ni Eurozone. Huku ni kama Ujeru, Uholanzi na Ufaransa. Sitii kundini nchi za Poland, huku kuna umaskini na unsuria (ubaguzi wa rangi) mkubwa. Shida ya Ujeru, Uholanzi, na Ufaransa, kwanza hizi ni nchi hazipendi wageni, kwa hivyo utaskia dhiki kwanza. Waeza pita na ndia zako mtu barabarani akakuangalia kaa ulooza. Wazungu waita hii "Giving you a dirty look." Pili, wana lugha usizozielewa, kwa hivyo utakaa miaka mingi wajifunza tena upya kusema kwa lugha yao "Kikombe" na "Kisahan cha chai". Ujeru kwa mfano wana lugha kali utadhani uko militari, lugha ya Kidachi hujui ni Kijerumani, hujui ni Kiingereza, lugha yenyewe konfyuzd, na Kifaransa wazungumza kipuapua kaa ulojawa na kamasi, na pozi zake ni za kikuchu, na lugha yenyewe ina kiume na kike katika kila kitu, si mtu, si kombomwiko, si buli la chai, si kitujio, shekhe kukuchokesha itakuchokesha tu. Na nchi zote hizi zina mizozo ya pesa zao za Yuro, kwa hivyo pana uhaba mkubwa sana wa kazi. Kwa hivyo, ata usitie kwenye hisabu zako Uispania wala Uyonani (Gris) - huku hupati kazi hata yakuwalisha kuku mtama wala kazi ya kuwalisha paka maderere.

 

108. Namba 4 huku "majuu" ni Ostrelia. Ukienda huku uwe na kisomo, maana kompitishen kali, lakini uzuri ni kwazungumzwa Kiingereza, na laif ya huku spidi yake mdogo mdogo. Sema winta yao watu wote wa ulimwengu wako sama na huku kwao Ostrelia the opposite is true, kwa hivyo mambo yao huwa ni ya kipekee pekee, na msemo wa "mate" (yatamkwa 'meyt') unzidi, na lazma utapenda mtezo wa ragbi maana ndio uchizi wa nchi nzima. Na kama waogopa buibui na nyoka na vidudu 200 vengine vya hatari, basi Ostrelia usende mwanangu nakuusia au utapanda presha bure.

 

109. Namba ya 3 katika orodha yetu ya Jahannam ya "majuu" ni Uingereza na jamhuriya ya Ailend. Huku Mswahili tayari wazungumza Kiingereza, basi huna shida ya lugha. Ailendi inaharibika kwa kuanguka kwa Yuro, lakini watu wenyewe makarimu na hali ya ubaguzi iko chini. Na watu polait, si kama kumbokumbo za Landan kwa mfano. Na usisahau ukiwa ushakua mwananchi, waeza kujivuta ukaenda nchi yoyote ya Ulaya. Uingereza saa nyengine utafkiria uko Afrika, kama ukienda sehemu za Lewisham kusini mwa mji wa Landan au mji wa Baming-ham (Birmingham), au utadhani uko Bombe ukienda sehemu flani katika mji wa Bredford au mtaa wa Tower Hamlets mashariki mwa mji wa Landan.

 

110. Namba 2 katika orodha yetu ni nchi za Skandinevya. Hizi ni Denmak, Noowee, Swiden na Finlend. Hizi haziko Eurozone, na zavutia kwa sababu japo zina tax za 55-60% (kwa hivyo hutakua na sevings za haja wala uwezo wa kuwasaidia sana jamaa zako Afrika), tax ile waiona faida yake ukiwa na watoto kuwapeleka baby-sitting walipa malipo madogo mno, hospitali zao zakutibu kweli, sio kwa mfano Uingereza yenye hospitali za bure lakini matibabu yenyewe ni bure (yaani wasiwasi bil khannasi), au Emerika ambapo kama huna inshuarens utapukutika meno yeshe yote na daktari wa meno huwezi kumuona, au utajifiliya mbali kwa T.B. au kensa lakini matibabu hupewi maadam huna inshurens. Ubaya wa nchi hizi za Skandinevya? Kwanza ni lugha - lazma ujifundishe alif-bee tena. Pili ni baridi, ukivaa jinz winta ni kama ulovaa suruali chapachapa yaanza fuliwa msimu wa mivua Afrika. Sharti uiweke suruali kwenye hita kwanza itoke mzizimo ipate umoto, kisha uvae andawea ndefu zaitwa long johns Kiengereza. Bila ya hivyo, kuswali huswali, maana utatokwa na mkojo bila ya kutaka kwa kuzizima suruali shekhe. Na pia, usisahau kuchukiwa Uislamu. Norwee mwaka huu Breivik aliuwa watu 77 sababu apinga wageni, khasa Waisilamu.

 

111. Namba 1 - ile Jahannam ya "baridi" kabisa watakayoingia Waisilamu waovu kesho akhera - Mn'gu astutie katika wao wala walio waovu kuliko wao, amin. Nchi bora katika hizi za "majuu" ni Kanada. Mii ni mtu mzima sasa, kwa hivyo nikiritaya na wewe pia ukija ukiritaya, waangaliwa vizuri sana na serikali, si kama Uingereza kwa mfano pana "fuel poverty", yaani waliostaafu hawajui pesa kidogo walizo nazo jee wanunue mkate wale au walipe bili ya gesi inayotia umoto ndani ya majumba yao ili wasife kwa baridi. Ndio kule utakuta wazee waingia sekan hen bookshops, wajinunulia mijitabu ya kizamani kwa pesa duni, wee waona hawa kweli watu wa huku wapenda usomi, kumbe wenda ziwasha peji kule majumbani mwao ili wapate kuota moto! Fyuul povati ndio hiyo. Tukirudi huku Kanada, makazi hapa ni mengi kwa sababu wananchi wenyewe ni wachache wafika milioni 35 tu (linganisha na Kenya, ina watu milioni 40 japo ardhi ya Kanada inshinda ardhi ya Kenya kwa ukubwa mara 20). Kwa hivyo ukiangalia nafasi ya ardhi ilivyo kunduka, masomo bure, matibabu bure, makazi yanjaa, na hapa tuna sistem nzuri za kupinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kidini, kwa mfano, ukipatikana wambagua mtu hakika uko mashakani. Kanada? Ikija posa ya huku irukie.

 

112. Hizi Jahannam daraja 7 ndizo the rest, lakini what's the best, narudia tena? Home is best. Afrika bwana. Muna raha zote huko, mwaishi your one life kwa starehe kubwa. Bora tu muwe na kushirikiana. Hiyo ndiyo key. Watu wasomee makazi ya udaktari, na watu wawe ni wenye maduka, na muwe ni maseremala, na... Kila mtu awe na ujuzi (trade, or skill) flani, ata kama ni kufuga kuku, na muongeze kushirikiana kwa kuchanga pesa, na kusaidiana kimawazo, na kitanfidhi (practically, doing something constructive). Ukiwa munlaza damu mwajidanganya ati mwangoja "an easy life" muje "majuu", basi kaa ukijua ikiwa utajaaliwa kuja Landan basi, utaukuta uwanda wa mpira wa Arsenali ule pale, kukifungwa bao na wewe uko jikoni waskia shindo la mashabiki latetemesha ardhi, lakini kwenda kuitizama mechi hata sku moja hutokwenda japo watamani, roho yakutoka. Kwa nini usende? Kwa sababu lazma mwanzo uwe shabiki uliyejiandikisha na klabu hiyo iliyo na waiting list ya miaka 10, na ukiimaliza hiyo miaka kumi, utowe pauni elfu 2 kujiandikisha tuu, wala tikiti hata ya mechi moja hujanunua (kama hizo pesa unazo basi), na wakti huo ukifika, basi uwe na hiyo taimu yakwenda unayo, na hapo pengine wewe kila ijumaamosi na ijumaapili uko mzigoni wamenyeka kuosha masufuria jikoni mwa hoteli.

 

113. Kwa hivyo Afrika besti, nishasema haya zaidi ya mara alfu moja, natumai taka za mashkio zishakutoka by now. "Majuu" ukichelewa kazini leo, na ati kesho, na kesho kutwa pia, jua kama kazi kufutwa wafutwa, no ifs, no buts. Hakuna ekskyuziz ya kusingizia basi linchelewa kwa sababu kila chombo cha usafiri chenda kwa taim. Ulochelewa ni wewe, si chombo. Na baada ya kazi, watu wako kwenye Twita saa zote. Sijui unchemua? Watia kwenye twita, ulimwengu wote upate khabari. Unkuja teuka, watia kwenye twita. Unkunguwaa barabarani, twita hiyo. Unshuta? Twita. Na marafiki wako wakubwa wako kwenye Fesbuku. Wakuta mtu ati ana marafiki 8,213. Ukimwambia, hebu ntajie majina yao 20 tu katika hawa bila ya kuangalia kompyuta hawezi. Rafiki wa kuonana ana kwa ana mukakaa pamoja, mukazungumza, na mukanwa na kahawa hakuna. Wataka rafiki? Yuko kwenye kompyuta. Ni kama mjukuu wangu. Anaulizwa spelling ya 'Opera' (yatamkwa 'opra' - ni kisa chenye kuhadithiwa kwa nyimbo), yeye akaandika "Oprah". Too much T.V. hiyo.

 

114. Mwaka jana nilibahatika kwenda "Skills London" nilpopitia mji huu. Maonesho haya yalikuweko mtaa waitwa Custom House ulioko mashariki mwa mji huu. Nikakuta jiwea hauzi kubwa mno - kama Nakumati ya Likoni mara 10 hivi. Ndani hapo wana maonyesho, sehemu moja ni pa kuripeya magari, na jirani yake pana sehemu ya kuunda mapikipiki, kwa kule wana kumardadisha mahadika (gardening and landscaping), na mbele yake pana ufundi wa ma T.V. na maredio, na kando yake pana ufundi wa spaki, na mbele kidogo pana ufundi wa ma kompyuta, na kwa kule pana ushonaji wa feshen, na mbele yake pana namna ya kutengeza sukari, na ubavuni wa hiyo pana namna ya ujenzi wa matofali (bricklaying), na kwa hapa pana upigaji rangi, na kwa kando kuna usonara, na kule mbele pana vimeza vya kolej za ufundi na pia vimeza vya univasiti visopungua 100. Skills. Wakupa maonyesho ya saa kwa mfano, watoto kwa watu wazima wajaribu kuunda saa hapohapo under supavision, kisha ukipendelea laini hiyo ya kazi wakupa mwongozo. Basi utakuta watoto wa Kizungu tele wanletwa na wazee wao, na wa Kihindi, na Wakichina pia. Watu Weusi huwaoni kokote ispokua kona ile ya mwisho kulee steji, wako kwenye jukwaa, waimba.

 

115. Na huku kutaka kuwa D.J. au muimbaji huku "majuu" ni kama kwa watoto walio "matini". Hawana uwongozo, ndio hupoteza taim yao kwa kutafta upuzi kwa kutojua ndia ya kupitia wakapita. Kubwa letu ni Mombasa Show, twende tukanunue ndoo na mabeseni ya plastiki kwa bei nafuu, si ni makonzyumaz sisi? Show inwekewa wakulima, lakini Mombasa hao wakulima wawapi? Twabaki twenda nunua makopo ya uji huku tukitia kozi. Umskie dem aseme, "Ya ukwaju hiyo?" na mwengine amjibu, "Ha ah, ni ya mbirimbi hiyo". Waswahili twahitaji 'Skills Show' kama hii niliyo iona ya 'Skills London'. Ndio kama sehemu niliyo izuru ya marubani wa ndege. Nnamkuta rubani anvaa tepe zake zote awashajihisha watoto na huku awaonesha aircraft instruments kama ma air speed dials, na ma joysticks, n.k., na huku awaambia, "A pilot is nothing more but a glorified lorry driver."

 

116. Haya Gaddafi huyo ashauwawa. Alkua anjifita ndani ya mtaro wa maji ya mvua. Panya ndio hupenda kujifita kwenye mitaro sampuli hii, na yeye aliyeonea na kuwauwa raiyaa wake na kuwaita panya, ampatikana yeye humu mtaroni, kaa panya. Angalia binadamu na kibri, the irony, M'ngu SWT akamtia kwenye mtaro yeye akapigwa shaba ya tumbo. Jeraha ya kitwa alkua nayo na damu ilimvuja kitwani - sijui kama antiwa risasi ya kitwa - lakini yaonekana kilichomuua khasa ni risasi ya tumbo aliyotefuliwa na wanamgambo. Sasa ukimwangalia anvaa wigi (tupee) sababu afita upaa, na kila mtu ajua mzee wa miaka 69 hawezi kua na sura za kijana, kwa hivyo afanyiwa upasuaji wa plastiki usoni (plastic sajari) au kuinuliwa uso (face lift). Uzee haukimbiliki wala hauna dawa, kama yalivyo mauti pia, kasema Mtume SAW chembelecho maneno ya Al Marhum Shekh Abdalla Farsi.

 

117. Pointi hii muhimu sana. Waswahili waishi "majuu", na utamuona mwanamke yuko kwenye basi au treni injaa watu tip top, yuwenda kazini ana kiyoo chake mkononi, ajipaka mapoda na huku chombo chenda, na wasafiri wenzake wamuangalia free show na yeye hana habari. Na Waswahili nao pia wamo, watafta kufurisha midomo kama ektres Angelina Jolie kwa ma botox, au wainuliwe matako wawe wan marasa kaa Jenifa Lopezi (ma bum lifti hayo), au wapunguzwe mafuta ya tumbo (ma tummy tuck hayo), au watiwe jeli za silikoni matitini (ma breast enlargement hayo), au wapunguzwe mafuta ya matiti (ma breast reduction hayo), na... Twendapi jamani? Huyo, Gaddafi na vitisho vyake vya "Zanga zanga", aliyezua hili zanga aliliweza baa hilo?

 

118. N'doo "majuu" na utakua kwenye "Rat Race" kama walivyo mbioni Wazungu wa "majuu". Ukizeeka sura na wewe ni sekretari au ni msomaji wa habari, huna tena maket, mpaka upelekwe back room ukafanye typing huko. Ukija kazini na uso "necheral"? Utasemwa, mpaka ujitie ma mek up. Na ukiamka kuchelewa, lazma ujipake mafaundeshen na huku treni yaelekea katika safari yake abiria tele. Na ukifiwa na mumewo, usione utakaa eda yako ya miezi 4 na sku 10 - kwani hiyo ni kazi ni ya babako, itakungojea wewe? Sku ya tatu warudi zako kazini, na matozi yakikuzidi, tishu zinjaa chooni, nenda huko ukajifute, urudi kwenye deski lako risepshen, simu zangoja jibiwa. Wee ulioko "matini" utaletewa picha ya Shakida yuko sijui Tenesii, Emerika, ankaa sting rumu yake, na kwenye kimeza cha kahawa (coffee table - hapana cha pambo la jigoma la ngozi ya mbuzi ati ndio pambo huku) pana kibendera cha Emerika waona ala gud taim, laa, ala bad taim bwana. Utadhani ni sheria Emerika, karibu kila gaden na kila nyumba ina bendera ya Emerika. Au ifike Alkhamisi ya tatu mwezi wa Novemba, watu washerehekee Thanksgiving wale bata mzinga, Waislamu kwa Wakristo, siku isherehekewe hii ova Idul Fitri au Krismasi. Hiki kijibendera, na bata mzinga wa 'Siku ya Kushkuru', wee ndio waona ushafika? Kodobwe. Na usemi wao skuzote ni "God Bless America." God bless Kenya bwana. Usisahau na Tanzania, na Naijeria pia, na... "Majuu" mwaona pana raha? Pan karaha shekhe.

 

119. Kwa hivyo, usione teknoloji mpya kama ya Lytro, wapiga picha pengine gari lapita sehemu spidi ukute picha yatezateza. Kamera ya Lytro wewe wajipigia shaghala baghala, kisha itajifokas wenyewe baadae, itoke picha shap kabisa. Unkaa na Deli Neshen lako Msa, wasoma habari hii roho yakutoka. Haya, koboka basi dola 500 uinunue, halafu uifanyeje? Nilishukia kwa swaiba mjini Nyuu Yok. Jamaa atia mzigo Mande tu Sande - kwa ufupi hana ofu huyu. Jobu tatu, alala masaa 4 kwa siku. A sevu ajipeleka kolej asomea Crime Scene Forensics. Nkifika, reshen anai stoki ndani ya double door American fridge lake, na annibandikia instructions nende wapi na wapi sait seeing, nitafurahi. Sasa huyu Abdurasuli mpe hiyo kamera ya Lytro, apige nini na hana taimu hata ya kula baga kingi hapo takeaway? Atakwambia hiyo Lytro itie huko "tini" - watu wako mbioni na maisha taf huku. Na nyii mwasoma Deli Neshen mwataka kamera hii "letest". Nyii ni wagoo? Wangonjwa.

 

120. Ndio mtu "majuu" hajizalii tuu. Utaona mke anaolewa na huku amiza tembe miaka 10 kabla kuzaa mtoto wa kwanza. Lazma upange uzazi, hujizalii tu kaa kuku wa gredi atagae mayai twenti foo seven. Na ukiskia mtu anzaa pindi akiolewa tu, basi jua femeli planing infeli. Labda mtoto akizaliwa most laikli atakua anshika koili mkononi sababu ile koili ilifeli, au kama hana koili mkononi, basi mama alikosea hisabu za kumiza tembe, au kama koili hamna wala tembe hamizi, basi mpira wa shughul uliotumiwa labda ulipasukia ndiani. Na Mzungu usione ni supa mzuri, hanuki, laa. Ata ektres Julia Roberts intavyuu moja alisema katika snema moja anainuka kitandani asubuhi nyele matimtimu, hana mek ap, na auziba mdomo wake kwa mkono. Asema hii ndio reality ya kila mtu, ma ekta wengine haya hawayaoneshi. "Mdomo asubuhi jamani waleta," asema Julia. Na nyii mwaona Mzungu hana "morning breath", anukia aluhudi tu saa zote. Mii pasonali nishaingia kwenye lifti ya jumuia katika ofis block moja, barobaro wa miaka 18 akatushutuia bwau shuzi wa kelele ndani ya hiyo lifti, kisha akamuelekea barobaro mwenziwe wakateka kwelikweli. Yaonekana ilkua ni mambo ya "Rii, rii?" Na Wazungu wote kunya wanya, na wote kukojoa wakojoa, na wote kuteuka wateukizana, na wachemua, na watoa makohozi ya gredi, na watokora pua, na hunuka waspooga, na wengine wan tawa haweshi kujikuna utosi. Nakuona wee wa "matini" waduala kuskia haya. Uliskia si binaadamu ni malaika hawa?

 

121. Na wanaume wa Kizungu pia hupatikana wenye kuharibu watoto, kama mashekhe wetu wengine na waalimu wa vyuoni na wauzaji kareti masokoni. Wazungu na utalii wa u paedophile ni mwingi. Ata ripoti intoka hivi maajuzi ya kuwa Wazungu wampunguza kwenda Cambodia kuharibu watoto kwa sababu vyama vya kupambana nao vimeimarika. Wazungu hawa sasa wabadilisha hewa. Wendapi? Waja pwani ya Kenya. Ripota mmoja, undercover, akaingia kijiji cha Kigiriama, babae watoto akapewa Yuro 5 "akawaazima" watoto wake wawili - kibinti cha miaka 6 na kijana wa miaka 5, wende tauni kwa gari "wakapigwe picha na Mzungu". Amkeni jamani. Na Waswahili kujiuza, waume kwa wake, kunchacha, na mambo haya yako tokea zamani Msa, Malindi, na Takaungu, na Watamu. Tunlala twangoja "zaka zetu" tu.

 

122. Kuna safari moja niko Msa. Kijana mmoja ajua mie natoka "majuu". Simjui, anambia aitwa Taisiri. Anambia yeye dereva hodari apeleka malori Uganda, Rwanda na Burundi. Lakini ampoteza leseni yake, na anaishiwa, ataka msaada angalau ende akapige picha atengeze leseni mpya, kwa hivyo nimshtuwe soo mbili. Najua sasa nataka pigwa dharba hapa, hana cha draiving wala cha walking huyu. Hapo tuko uwanda wa Makadara, na jua ni la saa sita. Namwambia wapi pahali rahisi pakupiga picha? Anambia Foto Rama, iko Gulshan. Namwambia, "Twende." Twende ni mguu shekhe, tukapiga lundi mpaka Gulshan. Anambia haya basi, nimpe senti ataingia apige mii naeza kwenda zangu. Namwambia, "Usijali." Tukaingia, nikampa mwenyewe Baniani senti mkononi, akampiga picha, akampa picha zake. Basi tukitoka Taisiri anambia, "Basi nipe fifti npande tuktuk." Nafkiria, "Huyu anjunukwa? Ni ile pajero nilompa Baniani akanregeshea soo 3 ndio ishamzuzua." Nkamjibu, "Sori, sina pesa za kutezea. Miguu yako unayo sio? Kata mbuga shekhe."

 

123. Hebu fkiria. Watu "majuu" wamenyeka, na wa "matini" wangoja barakallah sku zote. Fucking cunts. Wataka kumdroo huyu, na wampige pande yule, na wamdhulumu huyu, na wamrushe urathi yule. Na huku haweshi kuzozana na kuhusudiana. Watu wasoshikana, wakawa kitu kimoja, wakazua miradi mizuri mizuri, wakayafanya fanya wakajiendeleza, wao wako katika kutafta farasi na ma mishen saa zote. Musiskie kuna kisima cha pesa huku, ha ku na. Mii sijala lanchi muijuwao nyinyi wa "matini" sasa ni mwaka wa 19; huku twala dinner sku zote, wala si kwa kutaka sana Uzungu au kwa khiari yetu ndio twala dina, laa bwana. Twala dina kwa sababu taimu ya lanchi huwa tuko mbioni makazini, hatuwahi kurudi majumbani tukala mtee, kisha tukafumba jito dakika mbili kaa nyinyi. Tukila ki sandwichi au kijitekaway cha chipsi huku unsmama barabarani, au uko ndani ya basi laelekea kazini, pia twashkuru. Kwa hivyo twarudi nyumbani saa 3 au 4 ya usiku kama tunrudi mapema basi, na hapo ndio tule hiyo dina munayoitamani nyinyi majuha musojuwa illa kutilifu pesa na kuzikana tu.

 

124. Lazma Waswahili wawe na mabadiliko. Na mabadiliko yenyewe yaanze kitwani. Manake mabongo yetu mengi yana mavi ndani yake, hayana akili. Tuanze na saikoliji mpya, a new way of doing things. Kwishe huku kunyosha mikono kupokea zaka. It must stop. Hii ndio yatufanya tuwe waziavu. Hapana bwana. Taimu tena hii tuamke. Kwa hivyo the apporach must be, "Teach them how to fish." Free fish wote wankwisha, walobakia ni wa kununua. Mfundishe ende ufuoni akafukuwe choa, kisha umpe na ndoana atie kile chambo. Kisha aurushe mshipi hapo jiwe la mbu askize mdono. Samaki akidona, auvute mshipi kwa nguvu kusudi amnase samaki. Hapana tena cha barakallawa zisokwisha, twangoja kupewa mpaka lini? Ata kisima mwisho kitakauka, ubakie wachota mtanga mtupu.

 

125. "Matini" muko katika raha, lakini "you can't see the forest for the trees." Ndio penye miti, hapana wajenzi. Hivi winta yaaza na mifupa yaniuma - arthritis hiyo. Na hivi nina appointment ya kwenda kwa daktari anipige flu jab, sindano hiyo. Hii ni yakuzuia homa ya mafua. Viungo huwa kama vilokufa, uko kitandani wiki nzima, kama ulopigwa na maleria kali. Na homa hii ya ndani huuwa wazee wengi kama sisi, kila winta pana fungu maalumu lenda shekhe. Na "matini" muko kwenye Barzanji na Makasida, mwakutamani huku? Ndooni, lakini juweni na mapema ya kuwa hakuna maboi wala mayaya huku. Mwawawata wote eyapoti, mwaja kujitia kwenye majuto huku.

 

126. Kwa hivyo skills bwana. Waswahili wafundishwe makazi. Hapana cha suti na tai hapa. Roll up your sleeves and get down to do some serious work. Hakuna tena kubembelezana wala kuraiyana, wakti mbaya huu. Mtumainia cha ndugu? Hufa maskini. Na mtumainia cha jirani? Utampata kuzikani. Huko matangani amfuata tangalizi, hana haja ya kilio. Kwa hivyo, zizuwiyeni hizo tangalizi. Kila mtu ajifundishe kazi, pasiwe na nyumba isokua na watu wawili au zaidi wafanyao kazi. Na walobakia wawe wako katika kusomea kazi, watafta ujuzi (hizo skills). Tusbakie nyuma twatoleana hadithi na vitandawili, tukae tukipeane mithali sku zote, au upite maskani wamskia jamaa amwambia mwenzake kimatani, "Fanya hishima mbele ya watu wazima," au "Fanya adabu mbele ya Waarabu." Taim mbaya.

 

127. Safari moja nlipita MEWA hospital kumtembelea jamaa. Nkakuta kesi moja mbaya. Bwam mdogo ampigwa shaba, hali yake mbaya. Ahitaji upasuaji, au Zraili yu tayari kutwaa haki yaki any taim. Basi kijana kwao pesa hakuna, na antefuliwa risasi kwa bahati mbaya alpokua awatoa mbio majambazi Kongowea waloivamia bucha mtanaa kwa ma AK 47. Basi patakikana laki moja unusu ili afanyiwe upresheni risasi itolewe. Pana vifaa vitumike, pana dawa, pana gharama za chumba, pana pesa za madaktari. Mchango unfanywa mtaani kwao, na wengine wakatia walichonacho, hata mskiti Musa pale jirani pakatangazwa. Mchango sku ya tano unfika elfu 14; siku ya sita kijana M'ngu alimkhitari. Nliskitika sana, lakini ndio mambo Afrika ni mpango-less. Amkeni jamani.

 

128. "Majuu" watu wako mbioni. Muhindi ana corner shop auza maziwa, vibiriti na magazeti mjini Landan. Afungua duka masaa 18 kila siku. New York, kalasinga ana convenience store, alifungua masaa 24 - masaa 12 asubuhi ni zamu yake, na masaa 12 mengine ni zamu ya nduguye. Akiwa mgonjwa, waif wake ashika zamu. Lanch brek ni kwa kusimama, nusu saa tu, waif aje asmamie kidogo. Mwenendo ni huu 7 days a week, 365 days a year. Pita Diwali yee yuko wazi, pita Krismas, yee yuwazi, pita na New Year yee yuko wazi. Wewe utaweza kuwata kwenda Letahauzi Nyuu Yaa ukale "Hepi Nyuma"? Huwezi. Bali ukipawa nafasi ile, nusu ya duka utalifuja reshen uipeleke nyumbani kwako. Na duka utalifungua saa 4 asubuhi, na ukishakula pilau ya ijumaa, utalala fwaa, ute wakutoka, duka hulifunguwi kamwe. Fanyeni akili jamani.

 

129. Ndio maana ya bath kontroli kuzidi huku "majuu". Hujizalii tu, bila stepu. Afrika wajizalia ovyo kwa sababu hapo zamani za kale, watu walpokua na mashamba, more hands in the field = more food on the table. Na ukiangalia, magonjwa ya watoto ni mengi, na wengi wao wafa kabla hawajatimiza umri wa miaka 5. Utazaa "majuu" ufkirie, hebu ni mbwage mtoto Afrika kwa bradha au sista amuangalie. Ntampa pesa nzuri amwangalie mtoto wangu, na pesa nyengine zimsaidie yeye na watoto wake. Namba wan atakataa, atakwambia kila mtu abebe msalaba wake. Na hata akikubali, atamsunduga na kumsimanga, amfanye mtoto kama yatima, or worse, bradhako aeza mfanyia u bii kamwe, akamuharibu. Au hujaskia visa namna hii? Kama hujaviskia huwa basi wewe hujavitafuta.

 

130. Haya basi, "majuu" uwe ushafika. Ushajua cheese cake ni nini. Ushazijua sampuli zote za kahawa sasa - pana kapuchino (capuccino), pana moka (mocha), pana espresso, pana latay (latte), pana caffe lungo, pana caffe freddo, na pana caffe mokiato (macchiato). Usha improve kutoka kwenye kahawa utungu, kahawa tamu, na ntilie tangawizi. Nyama si nyama tu sasa. Pana 'Rump' (tako), pana Prime Rib (mbavu), pana Sirloin, T-bone, Rib-eye, Fillet, Porterhouse, na pana Chateaubriand. Na nyama choma, ile ungua ungua sasa pia wajua yaleta kensa. Sasa shekhe, ok, ushajua yote haya, ndio tukupigie makofi? "Majuu" mambo ni mengi na ni kompliketed, mengi ni unnecessary, huna haja ya kuyajua, wala hayakuzidishii starehe yoyote illa inkua ni homework sasa, lazma uwe msomi, na wee unkwenda kafee and all that you want is to order sahani ya nyama moja, na kikombe chako cha kahawa, bas. Huoni una simpal laif "matini", kwa hivyo haya mengi yakuzungushana akili yaso maana ni ya kazi gani? 

 

131. Kuna vitu vingi sana utakavyo vimiss. Mojawapo ni kiza. "Majuu" utakaa mjini na kwawaka mataa usiku wa manane utadhani ni mtana. Au sama pana muangaza saa nane za usiku mpaka saa tano za usiku. Basi ujiandae kulala, ufunge pazia zako, na bado pana muangaza wa sama au taa za barabarani zapenya kwenye pazia, bado waiona saa hii hapa, na kimeza kile pale. Lile giza la Afrika ni ne'ema, lakini utajuaje kama hujaja huku? Na pana zogo la vin'gora vya magari ya mapai full taim, si mtana si usiku wa manane, kama tuk tuk zenu zilivyo na zegere wakti wa mtana, non-stop. Ndio usiku wa Afrika huwa kimya. Hiyo ni ne'ema kubwa, maana madaktari wajua kua continuous low-level zogo in the background lapandisha presha. 

 

132. Ndio ukimuona mtu Afrika apeleka Left Hand Drive waona loo, ashafika huyu, maana ndinga hii lazma yatoka "majuu". Nyii machali. Bakieni hivyo hivyo mwataka kutudroo tukija, mwajiona makleva kwelikweli, kumbe nyote ni makleva fuli tu.

 

133. Turudi "majuu". Pana kischana kimoja cha Waswahili chenye umri wa miaka 4. Kinvalishwa kijinzi taiti, kisha chamuuliza dadake mkubwa, "Does my bum look big in this?" Huku ndiko kuendelea? Au tafauti ya keki na biskoti ni ipi? Keki ukiiwata wazi kwa muda yawa ngumu, na biskoti yawa laini. Sasa utangoja iwe ngumu au iwe laini, si wewe kula tu, utatambua palepale ipi ni keki na ipi ni biskoti bwana? Au alamu ikilia asubuhi, bado huamki, waibofya "Snooze" button ili ilie mara kwa mara. Kwa hivyo huku kujua kuitia saa "snooze" ndio ushaerevuka sasa? Alaam ishalia, si uinuke kushakucha tena? Masnooz hayo ni ya kazi gani, postponing the inevitebal? Au ukishajua Kidachi ndio ushatukuka? Ata Wazungu wana mtezo wa lugha waitwa "Double Dutch" - yaani mtezo wa kupotosha lugha, maneno yakawa hayafahamiki tena, lugha ikawa haina kitwa wala miguu.

 

134. Twenda au twatoka kazini huku "majuu" twapambana na vurumai la rush hour. Rash awa sku zote watu wako kwenye rush but nobody's going anywhere fast. Trafik jam kuanzia Msa mpaka Malindi. Kweli utafika nyumbani leo wewe? Kaa kwa muda "majuu" utakua smati, utaerevuka kwa mambo mengi. Ata ukiwa chek bobu la mtaani hubanduki kibarazani utabadilisha mawazo yako. Namba wan kibaraza ukikiona huku "majuu" hukikai - smiti baridi kaa ulokalia barafu. Kisha, mawazo yako mengi yata chenj. Si zamani ukiona dem aliyejaa kishtobe ndio yee sio? Fika "majuu" na utatanabahi uzuri wa mwanamke si hili furushi la kukalia tu, laa. Bali mwanamke lazma awe na hips zenye shepu nzuri. Ndio hiyo figa 8 uiskiayo. Hakika alama kubwa ya mwanamke ni hips - mwanamume yoyote hana shepu hapa, hata mashoga walokwisha kazi. Mume M'ngu anamuumba kiume, na mke anaumbwa kike, vitu viwili tafauti kabisa. 

 

135. Jambo n'nalo likariri saa zote ni kuwa pana ilmu kubwa nyii wa "matini" hamuijui. Ni uzuri kuijua, nyingi ina manufaa. Lakini at the end of the day, yaani mwisho wa kwisha, ata ukiijua, simpal laif mulonayo is the best. Bora tu, mufanye kazi kwa bidii and live your life. Kwa hivyo shkuru uko mtaani na misemo ya kupass taim ni kama haya ya "Kishiste kina vahuro." Bora musome magazeti na mabuku yenye manufaa, na mwaangalia dokyumentri zenu, na huku muna kazi mwaziendea mbio, ndivyo hivyo laif goes on. Angalau upate kujua kuwa paranoia, kuogopa pasi na sababu ya kikweli, ni sampuli ya wazimu ambayo haimpati mgonjwa yoyote mpaka apitishe umri wa miaka 30. Na Baniani atembea tumbo wazi wala hakoziwi wala hakosewi adabu, lakini vininja vyetu vya koziwa saa zote, ujiulize kwa nini? Hiyo ni edyukeshen. Waja "majuu", na ukute pana riots barabarani, kama kule London hivi maajuzi, watu wapore maduka ya mobaili na maduka ya ma TV na maduka ya vyakula, lakini ma bookshop hayadarwi kabsaa, maana wengi mno hawajui kusoma, wala hiyo ilmu iliyo vitabuni ndani ya bukshops hizi hawana haja nazo.

 

136. Nshakwambia sana kuwa "majuu" kubaya, maana adhabu ya kaburi, aijuae ni maiti. Lakini kila ukikanywa mwana mkaidi wewe, wapinga na kushupana, mpaka yakupate ndio utajua ni kweli maneno nkwambiayo. Ntakupa mifano mengine hapa. Huenda tukaelewana mwenzangu. Kukaa utakaa huku, na vazi la huzuni litakuvaa. Utakua na depression. Samya nnamkuta Sweden, kila otom na winta atumia taa ya muwako mkali ya SAD, aiwasha kama saa tatu asubuhi. Iwake wee, saa nzima, na yeye yu hapo asoma gazeti au aangalia TV, almuhimu miale ya taa yampiga kistepu matoni, kama jua la kawaida liwakavyo huko Afrika. SAD ni Seasonal Affective Disorder, watu kuhuzunika nyakati hizi za kukosekana jua na kiza kirefu, miezi 6 au zaidi. Wee uko Afrika wajua cha mshipa wa ngiri tu.

 

137. Au winta hiyo, yaja kesho kutwa. Utatawadha chooni na maji yako ya moto, lakini winta ni winta, pan baridi, hujafika mswalani chumbani kwako, mkojo kidogo huo ushakutoka bila ya kutaka. Haa, kajioshe basi, kisha utawadhe tena, halafu baadaye uje ufuwe kikoi au leso zako sasa.

 

138. Au wakaa "majuu" na huwezi ku affod kwenda cheki mechi bolini, wala huna chapaa za kulipia setilait TV, angalau ukaicheki mechi nyumbani. Afrika? Uko kwenye DSTV, grupu kubwa la watu, si viteko vyake hivyo, mwaangalia La Liga, Baselona yateza na Rial Madrid. Waitisha soda ukitaka, kahawa ukijiskia, mitai ukiyatamani. Messi antiwa tobwe? Si goa yake hiyo, mun raha na viteko kwenda. Na kukiadhiniwa magharibi,  huyyo, ushainuka, wenda zako kuswali, raha mustarehe.

 

139. Wenzako Afrika washerehekea bao la Messi, na wewe ulioko "majuu" uko mzigoni. Preshaaaa! Lazma u pafoom, au you get the sack baba. Hakuna cha unfanya kosa kazini, lakini wee sijui ni mtoto wa shangazi yangu, kwa hivyo, I'll look the other way, noo bwana. Mzungu akwambia, "You're only as good as your last mistake." Tia gange miaka 10 no mistake, you're ok. Make one mistake, ushabandikizwa kuwa you're good for nothing. 

 

140. Na uko ndiani watembea? For your own safety, chunga watu sampuli mbili, wavlana ma tineja, na madem/wanawake sampuli zote. Matineja wampawa umbele sana nchi hizi. Vijana ukiwaona waleee waja, mtu mbili, au kikundi cha mtu tano, dakia barabara upesi, utembee upande ule. Au watakudundia, wakupige kumbo kusudi, kisha wakuvamie na wakushindilie magumi for "disrespecting" them, au wakuchanje visu kisha haoo, wende zao, ata habari hawana. Au wakutolee vyuma wakutefulie shaba. Na hatari ya wanawake jee, hasa ma bleki? Wakuona wee waja, ndio mwanzo, watajimwayamwaya barabarani, watembea kwa maringo, wajua utawapisha tu. Haa, wajilete vibaya na wewe uwapige kumbo, kama huoni chamtema kuni wee. Si ma Fuck You yake hayo utakayopawa, na mapai uitiwe, uambiwe unamu assault huyo mwanamke (na aliyejileta ni yeye), na vibangili kabakaa uvishwe, utiwe ndani ya 99, upelekwe mbele.

 

141. Na stress hazishi barabarani. Unwatoto, fujo na zegere nyumbani? Waona hebu nwatukue hapo paki (uwandani/magaden) wakanyoshe miguu, wa burn some energy. Uko kule, mwida jamaa ankuja na ji bulldog hillo, anliwatilia kamba, lawajia mato mduara, meno wazi, labweka kichizi. Mwaona ni mzaha? Kweli tupu hii. Hapo kama kutishika mutishike, kama ni kuumwa muumwe. Na msomee jamaa mwenye huyo mbwa hatari kama hakung'owi meno. Mzungu akwambia, "Damned if you do, and damned if you don't." Au msemo mwengine, "Caught between a rock and a hard place." Rudini kwenu, huku si kwenu bwana.

 

142. Na "majuu" wanawake wampawa umbele sana, yatukiza khassa. Ati munaatana? Mali uliyoyatolea wewe jasho mwagawanya, mwenda fifti fifti. Na wee untia mzigo miaka 40, na ex wako kazi hakufanya hata sku mbili, ankaa ala visheti kutwa nzima. Na mahkama itaamrisha utozwe na senti za kumuangalia huyo eksi, ndiyo hiyo alimony uiskiayo. Na watoto? Utawalipia mpaka wafike 18 (child support hiyo). Basi uwe un'watoto watano, ikifika mwisho wa mwezi, pesa hata huzishiki mkononi, zatolewa juu kwa juu. Ukicheki kilichobakia, hata pesa za kununua pakti ya Embassy huna. Ndio utaskia visa huku vya ajabu. Mzungu mambo yakuwatana yako kotini, yee antukua bulldozer, ankwenda ibomomlea mbali nyumba yake, ukiicheki, yote chini, fleeet. Na gari anlikata pande mbili kwa msumeno wa spaki. Haya, huyo ex sasa aje atukuwe sheya yake ende nayo zake! Ndio ukiskia mke wa mtu andedishwa, sku zote wale wachunguzi humshuku mumewe/mshkaji wake kwanza. Wakwambia, "Before you suspect the outlaws, suspect the in-laws first." Ndio hiyo kikulacho kinguoni mwako uiskiayo.

 

143. Na ukiwa wee ni mwanamke, na unaatana na mumeo, ushajipatia hizo "haki" zako na mali tungu nzima, ndio ushaupanchi? F'kiria tena dadangu. Watoto uwalee peke yako, mkono mmoja huo. Uwaogeshe, uwavishe nepi, uwalishe, uwapeleke skuli, uwende shopping, uwende kazini... Hiyo "freedom" iwapi? Kweli huna huyo mume wakumfulia hizo soksi zake, mbona wajuta sasa? Mbona hiyo "freedom" inkutumbukia nyongo sasa? Maana ulkua ukitamani sana hiyo "freedom", wakaa ukimfanyia mumeo inda mpaka talaka zako 3 kwa pamoja anzitoa, moja yako, moja ya mamako, na moja ya ukoo wako mzima? Mbona raha basi huna? Hiyo si fridom, bali ni kifungo cha maisha hicho. Si uliambiwa kauli ya Mtume S.A.W. ya kua mwanamke aombae talaka pasi na katika zile sababu tatu makhsusi za kisheria huwa anlaaniwa, lakini wewe kuskia uliskia? Ukijicheki kitwa mvi tele, uso unjaa makunyanzi (pliti za uso), na dawa za dipreshen watumia asubuhi na jioni, na uspozila, utachiziklambali, sasa hivi utkuliwe ukapelekwe kwa Dokta Mahero au Pot Rizi.

 

144. Na wee waishi na waif wako katika a shared accomodation – fleti moja, wapangaji 50. Basi waif yuko jikoni na leso yake, apika. Na David wa kutoka Kot Divwaa (Ivory Coast) nae pia yuko jikoni, apika. Kweli wee mume ulioko chumbani kwako, kule kukaa chumbani kwakalika kweli, au hata kunwa maji kwanwika? "Majuu" hii.

 

145. Au usome kwenye Coastweek ati "majuu" mwezi ujao wa Novemba pana "Movember", mwezi wa wanaume wa Kizungu kufuga masharubu. Mzungu hunyoa masharubu yote kiparaa, ukimuangalia mdomo unkaa kaa ninihihiyo ya bata. Illa Novemba, wengi hufuga mijisharubu hayo kama uskani wa baskili. Ati hii ni katika kuchanga pesa ili kupambana na kensa ya kiume (prostate cancer). Na wewe uko "matini" wang'arisha mato ukiisoma stori hii kwenye jarida la Kostwik, watamani ati kuwa huku, na wee pia ufuge masharubu yawe mwitu khaswaa. Chochote cha "majuu" wewe zidi kukitamani tu, lumbukeni. Au uwe bachla boi huku "majuu" na saa zote kazi yako ni "sexting" - wamtumia kipusa chako text (sms) za ukosefu wa adabu, na kila ukimtumia sentensi, akujibu kwa kukwambia LMAO - "Laughed My Ass Off" - na wee waona raaha, wazidi kumtumia ukware mwengine. Tamani haya, lakini kaa ukijua kuwa hii "majuu" wewe kuijua hujaijua bado.

 

146. Basi uwe una woshing mashini, inharibika. Humuiti fundi. Waitupla mbali, ununuwe nyengine. Sababu? Kuiripeya, lazma umlipe fundi masaa yote atakayoyafanyia kazi hiyo, na umlipe na vifaa kama spea atakazotumia. Definitely more expensive kuliko kununua woshin mashin mpya. Saa inharibika ukanda? Same thing, tupa, nunua nyengine. Sijui kioo cha mobaili kimpata ufa? Tupa, nunua mobaili mpya. Au... fuata mkondo.

 

147. Na mambo ya Kazinistan ushayajua vizuri. Usione birthday yako utapata ofu, au pengine utatoka gange mapema. Laa bwana. Mii miaka yote s'japata bathdee yangu ofu ata sku moja, wala kupata ofu ya bathdee ya Mtume (SAW) hata moja s'japata. Bathdee kula keki nyumbani kwako ushibe, kisha toka uwende zako kazini, na idi mosi na idi pili zikifika, zote utazila kazini. "Majuu" sio, kaa ukijua kua hukuja holidee hapa.

 

148. Ilmu, ukiitaka huku "majuu" (kama huko kwenu pia, ukiitaka), iko. Ata advataizment hapa zakufanya uchemshe bongo, ufkirie, si kama zenu za "Suzana Pomed kwa urembo wa kudumu" - ni hizo kwa hizo miaka nenda miaka rudi. Waeza kuoneshwa Einstein na manyere yake kama simba mwitu, anshika choki mkononi, aandika ubaoni "E=mc2", kisha wakaleta maandishi pale chini yasema, "Aspergers' is more common than you think. Don't discriminate against those with mental health issues." Na ukimuona Babadi M'ngu anamjaalia ulimi mzito, nyii mwajiropokea tu, "Anshutiwa tumboni huyu."

 

149. Na kama ilmu huitaki huku "majuu", watafta ku waste taimu, basi upuzi pia huku uko, tena u fogo. Matineja huku wengi hawajui ya kuwa mkatano waleta ukimwi, amini usiamini. Na kugoana kutele. Waeza mskia mtu amsema mwengine, "He's got a face only a mother can love." Ni kama nyinyi mtaani huko "matini", n'shamskia jamaa amgoa mwenzake amwambia, "Hebu niazime uso wako kwa hisani yako, leo tuna drama skuli."

 

150. Na tushasema pesa ziko tait, watu hawana pesa za kutezea. Niko Msa, bwam mdogo, jamaa yangu. Namdadisi, n'kakuta anazo pesa zake mwenyewe za kujiendeleza katika mradi alioutaka. Nilipotambua ya kua ajiweza, nkamwambia, "Huna haja ya msaada wangu. You can manage all by yourself." Anniambia kwa maskitiko, "Are you shuwa?" "Matini" watu wataka tu, without understanding kuwa hizi pesa za kutezea sisi wa "majuu" haaa-tuuu-naaa. Yoyote aliyewahi kwenda Maskati atakwambia akikutana na sijui Mzee Zahor au akikutana na Bibi Salma, na hapo aanza ingia Maskati, swali la kwanza watakalo kuuliza ni, "Uko mpaka lini?" Kisha watakukacha, ndio huwaoni tena. Wakizuka sehemu zile uloshukia, basi hapo itakua ni baada ya ile tarehe uliyompa ya safari yako. Watu mawaya, wenda na tait bajet, nyii mwaona kila mmoja wao ana kisima cha petroli?

 

151. Wahindi sirias utawakuta huku "majuu" waja kazini shifti za kuchelewa, maana asubuhi saa moja mpaka saa mbili wako kwenye mtandao, wa study NYSE au FTSE100, waangalia soko la hisa leo likoje? Kengele ikilia tu kufunguliwapo stok ekschenji, waanza kununua na kuuza hisa, ata ifikapo saa 4 asubuhi washatengeza dola zao mia 2, wazime kompyuta, wajitaarishe kwenda makazini. Mableki? Pia wapenda shifti za kuchelewa, lakini wao washughulikia kujiseti mawigi, wayatengeze vizuri, kila unwele uwekwe pahali pake. Na Waswahili nao wapiga usingizi wao mpaka saa sita, kabla kujizoazoa, ndipo waelekee makazini mpaka mausiku tena.

 

152. Si dini, si dunia, sisi Waswahili tuko nyuma. Pana kijana mmoja ankuja huku "majuu" miezi 6 haipati, ana 30 hivi, anniuliza mas'ala ya kuowa tulpokutana mskitini sku moja. Nikamuhadithia kwa kadri ya nilivyoweza, kisha nikamwambia lazma baina ya mume na mke pawe na foreplay kwanza, kule kuteza teza na waifu kabla ya kumuingilia. Na nikamwambia pia, ilmu ya Uislamu ni kubwa, lazma afanye risachi zaidi, maana kwa mfano, maswahaba muhajirina wa Makka wakifanya kile kitendo wakipendelea missionary style, na ma Answari wa Madina wakipendelea doggy style, na stela zote hizi mbili, Mtume S.A.W. alisema ni sawa, bora tu mtu asimuingilie mkewe palpokatazwa, nyuma.

 

153. Sku ya pili alasiri, swaiba yangu Muradi annikuta mskitini, akapasua sana. Anambia ankutana na yule kijana, nae asema mii sina ushekhe wa usiku wala wa mtana, bali ni mkosefu wa adabu kamwe mtu mzima mimi. Na swahibu Muradi anijua vizuri. N'kamuhadithia Muradi yalojiri, tukakaa tukateka sana. Kweli Mzungu ansema, "A little knowledge is a dangerous thing." Kijana atoka "matini" fresh huyu, ataka kuowa, na maneno kama haya, ya ilmu ya foreplay, missionary na doggy style kuyaskia hajawahi kuyaskia juu ya mimbar wala jamvini darasani, na Mtume S.A.W. yote haya na zaidi ya haya aliyazungumza na maswahaba wake ridhwanullaha aleihim, lakini "matini" ilmu iliyoko ni dhaifu, yaishia kwenye maulidi yafaa au hayafai na ukitokwa na madhii jee uoge au usioge janaba, baas. Mengi ya manufaa kuzungumzwa hayazungumzwi. Yazungumzwayo utakayo yaskia ni ya "Kumaamako!" na "Shoga mkubwa wewe!"

 

154. Jee ningemwambia huyu kijana ya kuwa afadhali mwanamke akutembelee tuputupu kabsaa kuliko akuangushie hijabu kukuonesha nyele au kusega rinda kidogo akakuonesha mwanzo wa paja kidogo, si angeniona ndio nnazibuka kabisa?! Maana hakuna asimikae akimuona Nana mwendaazimu atembea tuputupu, au yuko? Uzuri wa mwanamke ni ile "suggestion" tu, maanake shetwani ni pure mind games. Mwanamke akivaa skin tait wee huwa tayari ushachajika, uko tayari kuingia ngomani. Lakini nenda nudist beach ukaone watu watembea tupuu kama mahayawani, na hata kutamani hutotamani. Ndio nyele zifiteni sawasawa kwa hijabu enyi wanawake, na buibui ukilivaa lisikukabe ukawa kaa ulotiwa kwenye kifumbu, sije ukawa watembea barabarani kumbe huku una mijidhambi mikubwa mikubwa, wenda huku ukiyarokota.

 

155. Ukishafika "majuu", usione ndio ushafika, bado hujafika bwana. Umgonjwa sio? Nchi nyingi walipa kumuona daktari, na dawa wazilipia. Na mshahara wako wenda kwenye neshnal kontribushen kulipa matibabu ya ghafla – emajensi, kama kupigwa dafrau. Juu ya haya yoote, and most important, lazma uwe shapu, uwe wajifanyia self-diagnosis. Uwe daktari wa nafsi yako. Kwa nini jambo hili ni muhimu sana?

 

156. Ntakupa mifano 4. Madha mmoja yuko Manchester, anzaa mtoto. Sku ya kwanza, hapati choo mtoto. Siku ya pili, choo bado hapati. Akimaliza sku ya tatu na mambo ni haya haya, mama ammuita nasi, amwambia something's wrong. Nasi ampuuza. Amwambia saa nyengine ndivyo ilivyo kwa watoto wachanga. Sharifa amwambia, ha ah, hiyo si kawaida. Akafanya zogo mpaka akaitwa daktari, nae daktari pia amuondosha ndiani, ajipurukusha. Sharifa anleta nduru, niitieni meneja sasa hivi. Ikabidi mtoto wende wakampige cat scan. Kwenye rizalti wakaona kumbe matumbo yake yankoteka, ikabidi palepale wamfanyie upasuaji wa haraka. Kama Sharifa hakuja kali? Ki Hamdani kingekufla mbali. "Majuu" hii.

 

157. Kisa cha mwengine, Fakii, mwenye umri wa miaka 52, yuko Landan. Afanya na manispaa. Ana pumbu (hania). Matibabu yenyewe Fakii atakikaniwa afanye ni simpal – atiwe kama kitujio na stepla sehemu 4 baina ya ngozi na misuli. Dokta Mzungu, na Fakii ana praivet inshurens, kwa hivyo afanyiwa simpal prosidya privet hospital. Ammaliza upasuaji salama, ankwenda zake nyumbani. Hapati choo sku tano, kisa cha kiji Hamdani, kile kitoto kichanga cha Sharifa. And worse, atapikizana. Akimpigia simu daktari wake, daktari amwambia, "These things happen. If it clogs up some more, go to the chemist and buy yourself some laxatives." Msahala akanwa Fakii, akasubiri.  Bado choo kupata hapati. Ata rafki yake Musa akija mtembelea jioni yake, amuona hali yake taabani sana. Akam rush emajensi, akipigwa ma X-Ray, ampatikana kuwa kile kitujio na zile stepla zintiwa baina ya misuli na matumbo, si baina ya ngozi na misuli kama inavyopasa. Kwa hivyo vitu hivyo vinkaba choo. Wakamfanyia emajensi sajari kufungua ndia. Bila hivyo, Fakii angekua ni marehemu tena. "Majuu" hiyo.

 

158. Mwengine ni Mu'mini, yuko Paris. Aumwa na goti, limfura. Daktari wake ashampa pain killers, na japo mfuro unshuka, ampata side effect ya alsa. Na aspomiza dawa, goti larudi kufura. Akangoja muda mrefu, waiting list, kisha akenda MRI scan, halafu akafanya apointment kumuona daktari wake. Akimuona baada ya mwezi, daktari ana picha zake 200 za MRI ziko kwenye kompyuta. Mu'mini amuuliza daktari, goti lake lina shida gani? Daktari amwambia anlitumia sana, linzeeka tu. Mu'mini amuuliza, mbona goti la pili liko sawa, na yote yana umri mmoja? Daktari hajui. Mu'mini amuuliza, hizo hapo picha 200, shida iwapi amuoneshe? Daktari amwambia haoni shida, mpaka wamfanyie key-hole surgery ndio watajua tatizo liko wapi. Mu'mini amuuliza, sasa tufanye lini? Daktari amwambia pana waiting list kubwa, kwa hivyo, aendelee kumiza zile tembe za kupunguza mfuro zimleteayo alsa, nothing else can be done. Mu'mini auliza, nothing else can be done? Daktari ajibu, "Look at my head. You see there's no hair on it, Mon Ami Monsieur, I'm bald. Can I do anything about it?" Matibabu ya "majuu" haya.

 

159. Na kisa cha mwisho ni cha Swabiha. Anzaa Birmingham, Uingereza. Chumba cha kuzaa hospitali akiingia labour? Anwekwa kwenye kitanda, na chini kwenye floor pana damu ya mzazi mwengine aliyezaa half an hour kabla yeye kuletwa. Si ni riseshen na cut backs kuzidi hizo? "Majuu" hii.

 

160. Kwa hivyo, wewe ukishafika "majuu", kaa ukijua ya kua bado kufika hujafika. Matibabu ni namna hii uyaonayo, kama ya 3rd world. Mifano hii minne ni real. Kwa hivyo usijidanganye. Uko "majuu" na ni mgonjwa? Self-diagnosis ni muhimu. Spend taim, uko kwenye mtandao (intanet) wafanya risachi yako. Daktari akiku bull-shit, mwambie hiyo ni bull-shit, katafte second opinion. Lau sivyo, utajifilia mbali, uwende ukafanyiwe post-mortem kesho kutwa.

 

161. Na musione Wazungu hawana vifafa, laa, wanavyo. Ndio kama kuna katika khabari kwenye TV, ati mtu maarufu apigwa mapicha na waandishi wa habari, na fleshi zitakua ni nyingi, lazma utaonywa mwanzo ya kuwa, "The following news item contains flashing images." Ili mwenye kifafa asiangalie, sije akaanza kutatarika na kutaataa. Na wengine mavi yao yaleta mno. Mmoja gange,  n'naingia chooni na yeye atoka anambia, "I'm so sorry, it's like somebody's just died. I've got Krohn's disease, and that's why I always use this upstairs toilet." Na pana maradhi kila sampuli huku, mengi mno Afrika hujawahi hata kuyaskia kamwe. Utaskia mtu ana M.S. – maradhi yamfanya awe anchooka 24/7. Na mengi mno huko you will never come across.

 

162. Kwa hivyo "majuu" mambo yake tafauti na huko, but it doesn't mean ni bora kuliko huko. Miezi inayo kuja haya ya kukaribia Krismasi, si  mwezi wa sherehe ya dini huku, laa, ni shopping opportunity, na pia femeli membaz wa get together, maana hawa jamaa moja waeza maliza miaka 20 hawaonani, na pengine wakaa mji huo huo mmoja. Kwa hivyo ikifika Novemba na Disemba,  utaona magazeti si advataizment za saa hizo. Kawaida. Wanaume wababaishwa na saa, na vi gadgets kama remote-controlled helicopters, na video games. Ndio utaona wanajeshi pia wapawa vi gejets na vi toys pia kuwaridhisha, nazo ndizo hizo medals kuvaa vifuani mwa mashati na hizo chepe mabegani kuonesha huyu ni brigediya na huyu ndie jenerali. Wanawake wao wazuzuliwa kwa julryi (jewellery) – ki lakti hivi, au kiboksi cha chakleti hivi. Watoto ni toys za sampuli nyingi. Zote hizi ni shopping opportunities hizi, kwa hivyo maduka ya advataiz kwenye magazeti ili yauze mali. Ndio waifu pengine akununulie electric toothbrush – Afrika wataka ng'arisha meno, waifu akikununulia md'aa meno yatang'ara vilevile, lakini wewe waona, laa, it's not the same thing. 

 

163. Pana jamaa mmoja wa hapa Toronto, Ahmedi. Alkua na waifu wa Kisomali, sasa wanaatana. Wanzaa, mashallahu, watoto wanne. Sevings zao za miaka ishirini, wanzipeleka Jibuti, wanjenga nyumba yao ya kishefa na kiji shopping centre cha maduka 10. Madhmuni wende waka settle huko. Kumbe Ambaro anam dabal kross, kila kitu ankiandika katika jina lake. Ahmedi kibahati aliletewa an anonymous e mail, yaonesha maandishi kwa Kifaransa. Akamuonesha frendi wake Pierre kazini wa kutoka Quebec. Pierre akampa hiyo shoki. Amwambia hii ni khati ya nyumba moja na maduka 10 yalioko Jibuti, na yote mwenyewe ni Ambaro, waif wake. Confrontation nyumbani, na kupelekana kwa jamaa zake Ambaro hukuhuku Kanada, mpaka ukweli ukadhihiri. Kumbe Ambaro ana mshkaji wake Jibuti, wampendana toka maskuli, na waifu akenda kuzuru kwao kumbe enda titigwa kule. DNA zikafanywa, na talaka zikatoka. Mambo ya propati kugawanya ndio bado hayatatuliwa. Na jamaa washamuonya Ahmedi kwenda Jibuti asende, aeza pigwa shaba kamwe.

 

164. Kwa hivyo, ishi "majuu", na kuona utaona mengi. Pana dem mmoja asoma kolej, na mmoja katika marafki wake ni mtoto wangu. Huyu ni mmoja katika wanafunzi, ni Msomali Asharafu (waitakidi ni katika masharifu hawa). Mtoto wangu katika kuzungumza nae huyu binti, ikadhihiri ya kua hajui kuwa pana cha kuoga ikisha hedhi. N'kashangaa sana. Histri yake binti huyu ni ankuja Toronto ana umri wa miaka 2, sasa ana 20. Babake yuko Yemen, lakini madhake yuko hapa, na sista zake 2 pia wako hapa.  Wote ni majinzi kuruka, wana ma wowowo kiyama. Sasa huyu Arij kama kuoga hedhi hajui, atajua kuoga janaba, na ngoma kutoka hatoki, na sharabu kupiga apiga? Kisa hiki kikikustaajabisha, basi utastaajabika kwa mengi, maana watoto wa Waswahili wengi huku hawatoki ngoma. Ni kama ukiingia Florida au Pirates huko Afrika, mabanati zetu kibao. Mii nakisia ya kua 70% ya mabanati zetu maklabu kwenda washakwenda Afrika. Na mabanati wa "majuu" jee? 90%. Reality hii.

 

165. Na utamlea mtoto, ujitahidi umfundishe dini, lakini swala ya Ijumaa hawezi kuiswali. Saa 2 asubuhi yuko skuli, na akitoka ni saa 9 jioni, kisa cha Ijumaa Tatu mpaka Ijumaa hiki. Huoni ya kua Ijumaa ashaikosa hiyo? Mpaka labda summer holidee ya miezi 2, ndiyo pengine ukimshkilia,  apate mawaidha kidogo hapo mskitini. Lakini miezi 10 iliyobakia, yee hajui cha imamu wala cha maamuma huku.

 

166. Kwa hiyvo, Afrika wapita ndiani waskia, "Hupendi? Konda bas!" Na ukinwa chai "bora" ni mpaka iwe ni ya maziwa ya mkebe - Ideal Milk hiyo  - au bado hujanwa chai bora. Au mtu achemue, badala ya kumwambia, "Arhamukallah" (M'ngu akurehemu), wamwambia, "Afya! Kula juu, tini kumoto." Au upite mtaani, umskie mtu ajiendea kitotoroni, na huku ampaza sauti aimba, "Nauza kuu, nauza kuu, nauza kuu-ngu. Nauza mboo, nauza mboo, nauza mboo-ga." Ubasha ndio oda of the day. Jamaa washinda maskani kutwaa, mazungumzo ni ya boriti na misonobari, na hisabu kubwa walonazo ni kula kwa mdomo wa juu, na kula huo mdomo wa tini. Mambo gani haya? Hawa bado hawajaona tupa ya asali inwatwa hapo nde mlangoni mpaka ika freeze kwenye baridi ya -10 digriiz bado. "Majuu" ni lazma, chembelecho Wazungu, ufanye kitu kimoja. "You must plough your own furrow." Ndio watu wa "majuu" s'ku zote utawakuta wana pliti za nyuso – mafikra mengi hayo. Saa zote  wao wachemsha bongo, wajitahidi, wajaribu kutatua matatizo yao. Hakuna wakukusaidia huku, kila mtu ni rabi rabi nafsi. And failure is not an option. Huku sio? There are no excuses.

 

167. Kwa hivyo, tumalizie makala yetu hii ilokua ndefu. N'na mengi ya kusema, lakini natumai "you have caught my drift." "Majuu" si kuzuri. Watu waipata mno, lakini hakuna mmoja atakae kwambia kweli. Kweli mii n'shakwambia, sasa kuijua kidogo waijua. Ukitaka kuja wee ndoo tu, hakuna aliye kuzuia, lakini kaa ukijua utakuja lia sana huku. A better deal ni ufanye akili. Soma vilivyo huko huko Afrika, ushike kazi yako huko huko, kama ni udaktari, au ni mchoraji plani za nyumba za ujenzi, n.k. Na kama kisomo sampuli hii huna, someya kazi. Pata ujuzi (skills), kwa mfano wayaring, au ushonaji, ujiangalie maishani mwako. Ukija huku "majuu", utalazimika ufanye yayya haya, whether you like it or not. Usizuzulike na kutafta makubwa ya mobaili mpya na ya kiatu kipya kiloingia mjini. Na kama Mzungu wala Muhindi havai wigi la nyele za Afro za Kiafrika, basi kwa nini dadako akanunue nyele nyororo za Kikoreya azivae?

 

168. Na lazma tushirikiane. Bila ya kushirikiana, we're all on a sinking ship. Na tuateni ushoga wa kubaguana. Let's be proud of who we are and where we come from, bila ya kuwa na "vibri" na kujiboresha kishosti. Nilimuuliza jamaa mmoja annizidi mimi umri sana. Namuuliza, Modi mtezaji maarufu wa timu ya Mwenge ya zamani, yeye ni Mswahili wa kabila gani (zamani Mwenge ilkua ni timu ya mpira ya Waswahili wa Kiasili, na Feswal ni ya Waswahili wa Kishihiri), anijibu, "Wallahi sijui." Na naamini kweli hajui. Watu kuogopa kujulikana kabila lao kwa vile ni "duni" la Waswahili wa Kiasili, mpaka twajikuta tunkulia na mtezaji huyu hodari kama Maradona, na bado hatumjui kama yeye ni Mtangana au ni Mkilindini au ni Msiu au...! Lazma tuchenj, au tutakua tumo ndani ya vitabu vya historia tu - iwe ni mambo ya, "Once upon a time, a very long time ago, there used to be a people in the coast of Kenya called the Waswahili. These extinct people..." Au waona ni mzaha? Reality hii.

 

169. Wa "majuu" are better than wa "matini" kwa sababu washajua "majuu" ni upuzi mtupu. They have really got an education now, kwa sababu wansafiri wakauona ulimwengu, sasa waujua ulimwengu ulvyokaa, washauona. The world is their teacher. Wambakia wako bizi, na wakiwa dipressed, hutafta hobi wakafanya. Mimi hobi yangu kubwa ni body lengwej. Nkiingia risepshen kwa dentist, siwaangalii mademu na meno yao msumeno, laa. Nawaangalia machekbobu wanapoingia hapo risepshen. Chekbobu akishamuona dem chuma, ile bodi lengwej yake yapeleka signal zakutekesha mno kwa wajuao. Ndio n'takaa na cheki dokyumentri kuhusu Chikungunya Tanzania. Wee msomaji pengine you don't have a clue Chikungunya ni nini; licha ya kua maradhi haya yapatikana Tiizedi, huna habari hata huku Dongo Kundu ni wapi (vuka Mtongwe next wikendi ukakuangalie).

 

170. Kwa hivyo, niko kwenye kuangalia dokyumentri, mwida pana advataizment ya ndinga wazimu, Mazerati (Maserati). Gari hili ni laki 4, dola za Kimarekani, si shilingi za Kenya. Basi sku zote kwenye advataizment za ma sports cars, utakuta dem chuma yuko kwenye bonet. Fast cars and beautiful women, what's the connection? Najua wee wafkiri wanawake huchachawa na magari, kwa hivyo ukiwa na Maserati ndio mwanamke ushamuokota. You are right, to a point. Na wale wenye fahamu ya ndani zaidi, wao watambua kuwa a fast car to a middle-aged, balding man is like viagra, an extension of their dicks. Pia ni kweli. But these 2 reasons are not the main point for advertisers here. Saikologist akwambia, wewe mwanamume ukimcheki dem mzuri, pale akili hukuruka. You as a man cannot reason properly for upto 30 seconds baada ya kumcheki huyu binti mrembo. Taimu ile ndio wee ni fala mno, utaitoa hiyo black credit card yako, ukoroge simu, and place an order. Ndio Mzungu akaitwa Mzungu, sababu yeye kazi yake ni kuzungua watu sku zote. Wee ukiskia mambo ya kuzungua humfkiria Mwalimu Alii tu. Mzungu ndie mwenye kuzungua watu khasaa. Na sku zote hajifanyii tu jambo bahati na sibu, ati "akatawakkal" kijinga tu; laa, kila jambo lenda kimahesabu. Haya ndio mazingaombwe ya Mzungu.

 

171. Sasa tuangalie khabari magazetini. Hebu mwanzo nifunge dirisha. Pana vin'gora vya magari ya mapai. Ishi "majuu" katika mji wowote mkubwa saa zote ni noo-nii tuu, hakwishi. Huyu andungwa jisu, yule ampigwa shaba. Haya, dirisha n'shalifunga, silence sasa kama tulioko laibrari.

 

1) Habari magazetini. Gaddafi yuko mochari, mji wa Misrata. Huku ndiko alikouwa watu wake wengi mno. Si mlolongo wake huo wa wananchi wanaoingia wakimuangalia Frauni wao na wakimpiga mapicha kwa mamobaili. Gaddafi alkua ajiona ni Maikal Jeksen wa viongozi. Kila kitu alichokifanya Maikal, na yee ankiigiza. Plastik sajari ya uso, wigi kuvaa kitwani, na unifomu za kijeshi zenye min'garo min'garo; hata akiingia katika mahema yake ya kibedui majangwani, siajabu alikuwa akiingia reverse kama 'moonwalk' ya M.J. mtangani hapo.  Na hakuna ajuwae kwa nini alikua 'Colonel Gaddafi' sku zote, kwa nini hakujipandisha cheo akawa 'Brigadier General Gaddafi'? Sijui akizikwa atasomewa Qur'ani au katika zile "aya" zake kwenye Kitabu chake cha Kijani (Green Book). Laa'natul Lah aleih.

 

2) Baluskoni nae, mwengine mpenda ma fes lifti huyu. Kesi yake iko kotini. Waziri mkuu huyu mwenye umri wa miaka 75 atuhumiwa anamlala malaya wa Kimoroko mwenye umri wa miaka 17; kumlala mschana mdogo hivi, hata awe na umri wa miaka 14, si kinyume cha sheria huku Utaliani. Kuvunja sheria na uwe na khatia ni kumlipa pesa binti aliye na umri wa chini ya miaka 18 kwa sababu ya kumkaza. Kwa Kiswahili chengine, mwanamke akipokea pesa kwa kitendo cha uzinifu (malaya) si haramu huku; haramu ni malaya kuwa na umri wa chini ya miaka 18. Lau Baluskoni mwenye kupenda ufa hakumlipa kitu huyu Karima El Mahroug ("Ruby"), basi pangekua hapana kesi. Haya basi, Baluskoni asema, ati kimzaha, kuwa chama chake cha kisiasa cha 'Forza Italia' au 'Nenda Itali' (Go Italy) kibadilishwe jina sasa, kiitwe 'Forza Gnocca' au 'Nenda Kuma' (Go Pussy).

 

3) Pana uchunguzi wa vita vilivyopiganwa kisiwa cha Siri Lanka miaka 2 iliyopita. Palitokea mauwaji makubwa ya kabila dogo la Kitamili, kila mtu ajua kuwa walio sarenda waliuawa hivyo hivyo kinyume na sheria, na waliuawa wanamgambo wapinzani, na waliuwawa raiyaa wengi mno, waume kwa wake, watoto kwa watu wazima. Jee, Jumuia ya Madola itaishtaki serikali ya Siri Lanka, au Mchina mwenye kiti cha kudumu katika Kikao cha Usalama atapinga kushtakiwa kwa viongozi hawa, na sababu ni kuwa amepewa bez ya kuweka meli zake za kivita?

 

4) Pesa ya Wazungu ya Yuro iko taabuni. Kuzoroteka kwa uchumi kunzidi, na Mayonani wanshindwa kulipa riba ya mikopo yao. Wakiambiwa riba ni haramu kubwa si hawaskii? Kwa hivyo, pana presha kubwa ya viongozi wa nchi za Yuro zizidi bidii zizuie kuzorota zaidi kwa hii pesa yao ya Yuro, au uchumi wa ulimwengu mzima - zikiwemo nchi za Emerika, Uingereza, na Uchina - zote zitaumia vibaya. Tatizo ni kuwa Ulaya pana pesa moja ya Yuro lakini nchi zilizomo kwenye muungano huu hazina ushirikiano mkubwa wa kiuchumi, wala Benki Kuu ya Ulaya haikupewa nguvu kamili, wala muungano wa kisiasa si wa kupigana pambaja na kushikana na kushirikiana vya kutosha. Kila nchi katika muungano huu yafanya mambo kivyake. Suluhisho ni muungano wa kisiasa wa karibu zaidi na ushirikiano zaidi wa kiuchumi, au sivyo Yuro itavundikla mbali. Mambo yalivyo sasa ni ya kukhofisha - ni fifti fifti.

 

5) Maandamano ya 'Occupy Wall Street' Nyuu Yok yazidi kasi. Landan na miji mengi ya Ulaya waigiza. Shirika lisilo taraji faida la Adbusters la Kanada ndio wanaoshajiisha maandamano haya. Na sababu ni simpal - kuzorota kwa hali ya kiuchumi kunkua kubaya zaidi, na watu wa kawaida wazidi kutanabahi kuwa matajiri wakubwa - mabepari - ndio wanaosababisha hali hii yenye kuumiza kila mtu.

 

6) RiRi (Rihanna) antoa nyimbo mpya yaitwa, "We Found Love". Huyu ana nyimbo za R&B nzuri, lakini ankua mwerevu, sasa apiga nyimbo mdundo wa Kizungu sababu pesa nyingi wanazo Wazungu. Anyway, model wa kiume kwenye vidio yake ni ex-boxer, Dudley O'Shaughnessy, 'point 5' baba bleki na mama mu Airish. Basi huyu hensam boy aulizwa yeye anaingiliana na RiRi, ammuonaje? Asema RiRi yuko down to earth, na maneno aliyotumia kutujulisha kuwa yuko down to earth asema, "Despite her fame and all, she's not like her shit dont stink." Waswahili wafkiria stizai waijua wao peke yao. Let me tell you something, nyii watu wa "matini". Mzungu humshindi kwa stizai, humshindi kwa kugoa, wala humshindi kwa usabasi. Ajuae ajua, na asiyejua usimuulize. Ni kama kazini kwangu, ukiingia chooni pana ilani yasema, "Flush when you are done. And no floaters please!" Floaters si zile za swimming; floaters ni mavi yanao olea.

 

7) Pana jizinga la muvi la Holiwudi latengenezwa. Mada (sabjekt)? Poltergist. Haya ni mambo ya majini. Nyumba haikaliwi, na ukiingia waona vituko, viti venda wenyewe, taa zawashwa na aziwashae humuoni, n.k., vituko tungu nzima. Mambo yote Mzungu anayo, musione huku mambo haya hakuna. Ndio ukiingia chooni, usome dua Mtume S.A.W. aliyotufundisha; na ukiogelea baharini, usiogelee tuputupu; na ukiwa tayari kumuingilia waif wako, usome dua spesheli ili shetwani asitwae fungu lake maalumu katika yule mtoto atakayezaliwa. Nyakati zote hizi tatu ni mwanaadamu anapokua tupu. Pana dua zake tunwekewa, sababu malaika wa M'ngu waliowekwa wakulinde wewe binaadamu huondoka ukiwa tupu, ndio waomba dua M'ngu Mwenyewe akulinde. Na pana watu huwa tupu, wakazini na wake za watu vyooni na baharini. Huoni huku ni kutupa mawe polis steshen? Hapana cha mambo ya kalamu na kusajiliwa kwenye O.B. hapa - ni marungu kwenda tu. 

 

8) Jamaa mmoja ana maradhi ya wasiwasi Winipeg anjiuwa. Alkua extra clean, lazma aoshe mikono yake mara 30 baada ya kila saa. Kama jamaa mmoja Nairobi alkua kila mtu akimpa mkono lazma akaoshe mkono. Ata ile sabuni yenyewe lazma aioshe kwanza, na jamaa si wawajua hawana kazi, kila wakimuona basi wakimbilia kumuamkua, wampe mkono kisha wakae wakimteka. Wazungu wayaita maradhi haya OCD - Obsessive Compulsive Disorder. Yaskitisha, maana yana dawa yake. Ata kazini pana jamaa hivi yuko katika matibabu. Ana locker (kabati) lake gange, na akishalifunga, atapapasa loki mara 50 kabla kwenda zake. Ata akitoka nyumbani kwake, atafunga mlango ende zake, akifika kona atarudi tena acheki ahakikishe kweli mlango anaufunga. Aeza rudi mara 10 shekhe. Ndio ukaambiwa wazimu ni nta arbaini. Ata Albert Einstein, Isaac Newton, Michael Jackson, Wolfgang Mozart, Henry Ford, Mark Twain, na wengi zaidi, wote waliugua/waugua maradhi ya upungufu wa akili ya Asperger's Syndrome, aina ya autism.

 

9) Timu yangu ya Man City inwajaza Man U mabao 6 kwa lao 1 nyumbani kwao Old Trafford. Aliyeanza kuwabikiri ni Mario Balotelli. Balotelli ni bwamdogo wa miaka 21 tu, mzaliwa wa kisiwa cha Sisili, wazazi wake ni Magana, lakini walimpeana kwa serikali wamlee sababu ya umaskini. Yes! Rizalti hii ni mbaya zaidi, hawajawahi hawa "Mashetwani Wekundu" kufungwa vibaya namna hii na sisi tokea 1926!

 

10) Na mtandao habari za Kenya. Wanajeshi wa Kenya wamvamia Somalia, hivi wako kijiji cha Afmadow sasa, waelekea Kismayu. Mambo yakutekesha, na ningeteka kama hayaskitishi. Hebu tumulike tochi kidogo:-

1 - Aliyeamrisha kuvamia ni waziri, kisha baadaye ndio akawaarifu wenziwe. Sasa, raisi na waziri mkuu wa barazara la mawaziri (kebinet) ndio wenye kukata shauri (in charge), au waziri ndio mambo yote? 

2 - Kenya yavamia nchi nyengine, na kila mtu ajua war needs funding. Sasa shilingi ya Kenya imeanguka vibaya hivi karibuni, watu wenda madukani asubuhi na huku wakhofia bei ya leo itakua si kama ya jana, jee mkate ushapanda tena? Kisha Kenya yenda vitani? Pesa hizi zitatoka wapi na pesa hakuna? Na kama pesa zinzidi, mbona waalimu wagoma wataka ongezewa mishahara?

3 - Raiyaa wa nchi nyengine zisokua Kenya wanshikwa mateka. Na huu uharamia wa baharini (piracy) uko miaka mingi, haukuanza jana, kwa hivyo why now? 

4 - Je, yawezekana ya kua wanasiasa wetu wa Kenya wajaribu kuondosha kumulikwa kwa mwenge (attention) mbali na mahakama ya kimataifa ya The Hague na wale 6 wanaoshtakiwa na Ocampo?

5 - Au ni wanasiasa waona hii ni kampeni ya uchaguzi wa 2012, maana wanasiasa wa ulimwengu mzima wapenda vita wakti wa uchaguzi, wajua watapata sapoti yenye nguvu kabisa katika uchaguzi?

6 - Na ikiwa Kenya yataka kuwakhasiri hawa wendaazimu wa Ash-Shabaab, ndio watangaza magazetini na bungeni kuwa dhamira yao ni waingie Kismayu? Mwenye kutenda si hutenda tu, mbona kwapigwa mbiu kuwapsha khabari na mapema?

7 - Halafu, hawaijui saikoloji ya Msomali? Msomali atazozana na mwenziwe wa kabila na ukoo mwengine kufa kutozikana, ata nduguye atamuuwa, lakini akiingia asiyekua Msomali kati, wote wataungana na kumgeukia asiyekua ni Msomali. Si huoni Muemerika alikimbia mwenyewe? Na M'habashi pia akakacha? Wanshindwa hawa wenye pesa, NA vifaa vya vita, na ujuzi mkubwa wa kupigana, wataeza wanajeshi wa Kenya, wao waona wenda piknik? Na wataka pigana na hawa wanamgambo and they've nothing to lose, kweli muta win nyinyi Wakenya and you have everything to lose?

8 - Na Kenya ikiona vita basi vinkwisha, wataandikiana na nani mkataba huo? Na hawa wanamgambo machizi? Mkenya aki cease fire, jee machizi wa Ash-Shabaab kweli watahishimu haya maandishi kwenye karatasi?

9 - Na wanamgambo sku zote vita vyao ni vita vya 'hit and run' - Kenya wataviweza vita hivi? Wana khibra (ekspirans) ya kuwashinda Mahabashi waliokimbia wenyewe? Mfaransa antekwa nyara, Wakenya wampeleka boti ya polisi kuwafkuza, inkuja penduka, kikosi cha wanamaji chote (nevi nzima) wambaki waokolewa na wavuvi wa pweza na wa samaki! Au wavamia, mwida hiyo helikopta inaanguka wenyewe, wanajeshi wanjifia. Khibra ya vita iko wapi hapa?

10 - Jana nasoma Neshen, lasema usalama umeimarishwa Likoni Ferry, na leo gazeti lasema watu wa usalama wakhofia sehemu za Kitui wilaya ya Kaskazini Mashariki, wakhofia magaidi wa Kisomali wapenya kuelekea mjini Nairobi. Jee, Kenya iloingia vita hivi bila ya hisabu kali, yaweza kuwazuia wendaazimu hawa kweli?

11 - Au utalii ni namba 1 Kenya, na watalii baada ya utekaji nyara wa Wazungu Kiwayu na Manda, Wazungu watakata guu Kenya wasije. Sasa, waingia vitani khaswaa, na machizi ni hawa waliorepua makombora Kampala hivi majuzi, kweli usalama Kenya utazidi sasa au utapungua? Au utalii ukifirika, si nchi nzima ishakhanithika tena? Maana just like no one can exist in a vacuum, huu utalii pia doesn't exist alone. Una konekshen na usafiri, ukulima, n.k. Vita hivi kweli vina 'national interest' ya Wakenya, au vina 'national loss' kwetu? Mbona hili bongo la Mwafrika siku zote linlala, wala kutumika halitumiki?

12 - Na Kenya kwanza yavamia Somalia, kwani waliowateka nyara Wazungu wa MSF kutoka Dadaab ni Ash-Shabaab kweli? Ushahidi hamna, na kila Mhalili mwenye kuijua hii nchi na kuwajua Wasomali akwambia makao makuu (hedkota) ya ma pairets iko Haradhere iliyoko kilomita 300 kaskazini mwa mji wa Mogadishu, na amiri wao (the man in charge) ajulikana kama "Afweyn" au "Big Mouth", na kijiji hiki cha Haradhere hakiko kamwe katika mikono ya hawa wendaazimu Ash-Shabaab. Kwa hivyo, Kenya invamia Somalia kweli kuzuia Pirates, au pana ajenda nyengine hapa?

13 - Sharif Sheikh Ahmed, raisi wa sasa wa Somalia, mbona alipingwa alpozuia kumwagika kwa damu Somalia kupitita mahakama zao za ICU (Islamic Courts Union)? Mbona Mhabashi aliivamia Somalia kumuondoa yeye na hii ICU, na Umoja wa Kimataifa mbona haukumzuia Mhabashi? Umoja wa Kimataifa si waendeshwa na nchi chache tu? Kwa hivyo nchi hizi ndizo zipigazo twari ndio zamuni ikaanza? Waona siasa hizi? Apendae, tongo huita kengeza, na jee atukiae, si huwa ni kinyume na haya? Jee, hizi ni siasa za uadilifu? Kwa makosa haya wakaja machizi wenye siasa za kichaa hawa ma Ash-Shabaab.

14 - Haya, Wasomali wa Kenya wako karibu milioni 1, na pana nusu milioni ya wakimbizi wa Kisomali walioko Dadaab. Wangapi katika hawa watakao shikwa ovyo, watakao pigwa, watakao nyanyaswa, watakao najisiwa, watakao kuuawa, watakao pawa mateso makubwa, na watakao  nyimwa haki zao zote za kibinaadamu? 

15 - Au watu wangapi wasio husika na rapsha hizi watatiwa kati, raiaa wa kawaida, kina mimi na wewe, pengine mtu anfanana na Msomali tu (licha ya kuwa majoriti ya Wasomali hawahusiki kamwe na ugaidi huu wa Ash-Shabaab) basi ndio ashashikwa, ateswe, ili atoe 'kitu kidogo' tu? Wangapi katika Wabajuni wa Lamu kwa hivyo watashikwa ovyo? Na wangapi watashikwa kwa kushukiwa kwa sababu wao ni Wasilamu tu? Na wangapi wasio na hatia watafinywa Nyati House?

16 - Au Wasomali wa Kenya, raiyaa kamili, kwa nini wakandamizwe, na wao wana haki kama Wakikuyu, Wajaluo na Makalenjini nchini? Au ni nani kama si Naibu wa Amiri Jeshi (Deputy Commander Major General) Mahmoud Mohammed, Msomali wa Kenya ambaye hakumaliza hata shule ya msingi (praimari skuul), nae ndiye aliyekua na ushujaa zaidi na akaokoa jahazi katika kuzuia majaribio ya mapinduzi ya Agosti Mosi, 1982? Au si Mkenya huyu? Kwa hivyo, kwa nini pawe na vita na Wasomali wa Kenya wateseke?

17 - Na T.K.K. ilivyo mbaya mno Kenya (mojawapo katika nchi zishikazo mkia ikiwa nambari 150 ulimwenguni), kweli maafisa wa usalama wakiwashika magaidi, hawa maafisaa wakifungiwa chao, kweli hawato wawachilia huru hawa walioshikwa? Brauni na bangi mabilioni ngapi kwani yashikwa mijini Kenya kila mwaka, kisha yawachiliwa na kuwaregelea hawa hawa ma Drug Lords, na sababu ni hii hii 'chai' isokua na sukari?

18 - Na Kenya yaingia kati sasa katika vita, itaweza mkorogo huu wa studio? M'ngu asijaalie, mambo yakikorogeka Kenya, nchi ngapi za Afrika Mashariki zitakhasirika? Uganda, Rwanda, Burundi, Kongo, Sudani ya Kusini, na Ethiopia - nchi 7 kwa jumla. Jee, vita hivi vaingia akilini?

 

172. Ni kama wale watu 19, wakiwemo kina Kofi Annan mwenye kiti mstaafu wa Umoja wa Mataifa, na pia Sir Richard Branson wa shirika la ndege la Virgin, hawa wote 19 katika Tume ya Kimataifa kuhusu Sera ya Mihadharati (Global Commission on Drug Policy), wasema kuzuiwa kwa madawa ya kulevya kumfeli, kwa hivyo suluhisho lilioko ni wahalalishe mihadharati ("let's legalise drugs."). Ati iwe bangi na unga wa brauni ukijiskia wenda zako kununua hapo dukani kwa 'Father Reshen'. Ndio ukaambiwa, "Akili nyingi huondoa maarifa." Haya ni maneno ya kiwazimu. Ni kama vita hivi vya Kenya na Somalia, haviingii akilini kwa yoyote mwenye kufkiria sana. Nakhofia nchi na sehemu yote ya Afrika Mashariki kupatikana na mchafuko na misukosuko. Na haya yakitokea - siombi wala M'ngu asijaalie - hawa viongozi wa Kenya na mawaziri walioamrisha vita hivi lazma wabebe mas'ulia na lawama kamili. Hapana cha sense wala cha sensibility hapa.

 

173. "Majuu" musije, na kaa munlazima kuja, basi ndooni nyote mujionee wenyewe, si mwana sku zote akililia wembe mpe? Ndooni, lakini kuja kwenu ni mas'ala ya kilio kukileta matangani. Mtakuja jijutia bure. Mtajua kweli mukiona kibeji kimbandikwa kwenye gari, "Baby on Board", kule si kujionesha wee bado waeza kuzaa, hapana. Kibeji unkibandika ili ukipatikana na ajali barabarani, angalau wamtafte huyo 'baby on board' wakisha waokoa nyinyi majeruhi au nyinyi maiti. Pana upweke nchi hizi, watu hawajuani, na jirani yako wa miaka 30 pia hamujuani hata majina. Na musione mutakuja vaa mavasachi na ma Kelvin Klein huku; hizo nguo besti moja mbili zitakaa makabatini, na feshen yake ikisha huzivai tena. Utakuja vaa mitumba ulonunua Charity shop, uvae wewe na umvishe na waif, na watoto wakuwao chapchapu pia shopping ya majaka na viatu mutazifanya maduka sampuli hii. Na ukijaaliwa kuvaa saa ya ughali ya dola 200, inayo kwambia sijui leo mwezi uko phase gani, sijui maji ya baharini yanjaa au yankupwa, ina alarm tafauti 10, ina stop watch mpaka 1,000 split seconds, na waeza ifanyia deep diving umbali wa mita 300, na ikakwambia North Pole iko wapi, na ina gerentii betri haishi miaka 10, mambo yote haya na utaingia kwako nyumbani sku moja ukanda wa plastiki ujikote na tumbuu, ukanda huo ushakatika, na saa ndio haivaliki tena. Ni mbio za sakafuni hizo huishiya ukingoni.

 

174. Ikiwa ni huku "majuu" musijidanganye kabisa, maisha ya upweke hamuko tayari kuyakabili. Kwa hivyo, musiyaombe wala musiyatamani, yatakuja kuwashinda bure. Ndio utamuona Mswahili atembea barabarani na huku mambo yanamshinda, yuwenda na huku azungumza peke yake, wala mobaili mkononi hana wala 'hands-free' pia hana. Umuone forena ansmama peke yake barabarani a repu kweli, ukiitafuta simu mkononi huioni, ukionacho alchokishika ni yai mkononi, alishtakia kwa sauti ya juu kabisa kama kwamba anshika maikrofoni atangaza, mtu ashazibuka. Na ukitembea ndiani, utembee na huku wa avoid eye-contact na mtu yoyote upishanae barabarani, sije akakukemea, "What are you looking at?" Kwa hivyo huku "majuu" ukitembea ni "mato tini" saa zote, wala ushekhe huna. Waangalia tini au wajifanya waangalia kwengine ili usilete 'woo' na mtu yoyote. Au uone Mzungu akisilimu ashakua malaika, laa bwana. Aja na begej ya pasonaliti yake ile ile - akiwa mjeuri ataendelea vile vile na ujeuri wake. Wangapi wansilimu na kuswali hawaswali? Wengi. Na wengine wajiita ni ma "Black Muslims" au" Neshen of Islam" - wao wavaa ma suti na matai utadhani wenda dinner. Kwa hivyo, ukishamuogesha mtoto wako na shampoo ya "No Tears Formula" isiyowasha mato, ndio ushafika? Au unlazima ya "majuu", na ukija waja fagia barabara, na kazi hiyo hiyo ya manispaa hutaki ata kuisikia jina Afrika, mbona hamtumii akili?

 

175. Mwakuwania huku "majuu", mwaona ndiko kwenye ustaarabu mkubwa, lakini mkeo atakua na tumbo la mimba ya miezi 8, aingie kwenye treni, wala hakuna mmoja atakae mpisha kiti akae. Au ukute feshen yabadilika ikibadilika, waona huku ndiko kuendelea, lakini yaregelewa tena yale yale kila baada ya miaka 18. Kwa hivyo hiyo mini skati uringao nayo sasa, kesha tangulia kuivaa mamako zamani. Au uwe kwenye hafla ya kazini, na mwanamke amkute mwanamke mwenziwe anvaa nguo kopi rait kama yake, basi mara nyingi ataibadilisha kistepu, pengine afunge hanjifu kwenye kola ndio ashaibadilisha kidogo, au ataimwagia tembo kusudi iingie doa, almuradi isiwe anvaa sare kama mwenziwe. Hii ndio saikoloji ya kike ilivyo Afrika, na ukija zako "majuu", utakuta mambo haya ndivyo hivyo hivyo yalivyo huku pia. Kwani hyuman necha yachenji? Haichenji.

 

176. Au utaona jipandikizi la bodibilda, lashindana na Shuzi Niga, kumbe jamaa ni vitu. Au umalize siku nzima - uko nde masaa 16 ndiani na kazini, na usiwahi kutabasamu na yoyote hata kwa nusu dakika, unnuna tuu, sku nzimaa. Hii ndiyo "majuu". Kwa hivyo, usihadaike ukiskia watu huku sasa wako katika "cloud computing", na wewe ukayatamani haya makompyuta ya mawingu. Au ukaskia pana kwenda shoping na kulipa kwa "contactless payment" kwa kutumia mobaili tu, watu wengi pesa taslimu hawazitumii tena, na wengi waanza kutupla mbali kredit kad zao hazina tena kazi, na wewe uyatamani haya. Wala usibabaike ukiskia msimu wa otom pana matufaha kibao mitini, haya huanguka wenyewe mpaka yakaozeana, mwishowe wakala ma deer, wakawa wenda wakiyumbayumba, wanlewa chakari. Wala usihadaike ukiskia watu wa Maskati na wa Mississauga wanwa chai magarini na wee pia ukayatamani haya ya kunwa chai garini. Wao wako mbioni wenda zao makazini, hawana hata taimu ya kushuta.

 

177. Na kuzaa huku mwazaa watoto, lakini huna kontroli yoyote, ukasema wawafundisha hishma na adabu, wawakuuza kisawasawa, laa. Mazingira ni ya kikafiri, mtoto any taim aeza kuamua akitowe, yuwenda zake akaishi kivyake. Twazungumza watoto wa kutokea miaka 8 - runaway kids. Emerika, kwa mfano, pana watoto karibu milioni 3 wakimbia makwao killa mwaka. Pengine wantukanwa kidogo nyumbani, bas, mtoto huyyo, ashakacha. Au ampigwa kidogo, atiwa adabu. Huyyo, ashainua. Au ana mshkaji. Wamkataza? Bye bye ashakwenda, na ndio humuoni tena. Na wanao ingilia maisha ya umalaya, na ugahba, na ushoga, na ugawadi, na wao ni wenye umri mdogo wa miaka 10 hivi wapata watoto 300,000 kila mwaka huku Emerika. Wee zidi kuangalia MTV tu ikuzuzuwe. Mwatamani "majuu", manake mwaskia kila siku mwaskia jipya la kuwapurukusha, kwa mfano kuna 'Card Case' sasa, waingia zako dukani na makamera hapo mlangoni otamatik yashakusoma wee ni nani, kwa hivyo huna haja tena ya kubeba pesa wala kredit kad sasa, wafanya shopping yako, ukisha, wenda zako till wamwambia kastama assistant jina lako tu - ndio konfameshen hiyo - malipo ni otomatik duka la toa pesa kwenye akaunti yako benki. Sikia haya basi utamani kuja. Ndoo tu, ewe uliye junukwa, kama hutokwi na mvi za tini. Nakupa sku mbili tu.

 

178. Na kumbuka kwenda kwangu Afrika sku zote ni Ikonomi Klas, kama ilivyo kwa Waswahili wote wengineo. Hatuingii First Class, licha ya hiyo Business Class ya kina Zubedi (mashallah). Pesa "majuu" sku zote ziko tait. Ndio wee wa "majuu" ushapanuka akili, sku zote watafta 'value for money'. Kwa hivyo Mswahili wa "matini" akitaka kukupiga dharba, wee wamuangalia kaa aliyooza. Ataka kukufanya wee n'kuchu? Kila jambo lenda kwa mahisabu, hujifanyii tuu. Mambo kwa mpango, si kama fala Jamshid bin Abdullah, Sultani wa mwisho wa Unguja aliyependuliwa 1964 kwa uziavu wake. Alipoonywa kuwa kuna njama ya Mganda John Okello na chama cha Afro Shirazi kuipindua serikali ya Zanzibar (Nyerere, Kenyatta, na Jaramogi Oginga Odinga, wote hawa walikua wajua kuhusu njama ya mapinduzi haya, na hakuna aliyeyapinga, yakaleta kuuwawa kwa Wamanga na Wahindi elfu 17 katika usiku mmoja - ndio hayo mauwaji ya kimbari, hiyo jenosaid unayoisikia sku zote), Jemshidi alijibu, "Kwani serikali ni kisahani cha chai, yaeza pinduliwa tu?"

 

179. "Majuu" kwa hivyo pana fowad planning saa zote. Hapana cha kubahatisha, wala hapana cha kutawakkal kijinga. Waswahili wa "majuu" wanchenji kwa jambo hili ambalo ni central to saikoloji ya Mzungu. Yuko mbioni kuhakikisha kila jambo liko pahali pake - meticulous planning and covering all angles hiyo - ndio kila aliyoko "majuu" ahisi "time flies". Tuko bizi, wahakikisha ya kuwa every little detail is in place, na nyinyi wa "matini" hamu plan chochote, muko kwenye falsafa ya "Ponda mali kufa kwaja" na kuteza Lele Mama tu. Kwa hivyo "majuu" yote haya ya ku "make hay while the sun shines" yako, lakini haimfanyi Mzungu kuwa ni malaika, wala haimfanyi Mzungu kuwa ni pafekt. Laa. Mzungu huyuhuyu utampata barabarani anlewa chakari, apita akijikojolea surualeni, si waume, si wake. Na kushuta hushuta, na kuteuka huteuka, akatokwa na kamasi, na akatema makohozi. Akiwashwa hujikuna, na saa nyengine, hutokora pua, na wengi waeza maliza siku moja, siku mbili, na saa nyengine wakamaliza wiki na kuoga wasioge. Hujayaona haya kwenye "The Bold & The Beautiful", au ushayaona? Hujayaona kwa sababu hawakuoneshi reality. Wewe kwenye The Bold uko kwenye make-believe tu, vunga kufa. Ni kama kupikwa sima (waiita 'asida') mjini Tai'iz, Yemen, pia hujaiona sio, japo kuweko iko. Wee zidi kupoteza wakti wako kwa kuangalia misalsal usiku na mtana.

 

180. Wewe huku "majuu" ni kama mfungwa tu, uko locked in kwenye treadmill, wenda mbio huku mwalipa mabili tu, ndio kazi kubwa hiyo ulonayo. Maisha yalivyo na kasi, hakuna cha kudiriki, ata ukinya pia huna taimu ya kukaa ukanya sawasawa kwa makini, wanya chapchap, kwa installment, ujiharakishe ukate choo au utakosa basi kwenda kazini. Na taimu ya kufanya chapati - sijui kuzikanda, na kutia tabaki, na kuzichoma - taimu huna, na hata ungekua unayo hiyo taimu, cha kuskumia chapati huna. Labda utafte tupa ya tree top uskumiye nayo hizo chapati. Kwa hivyo riyaliti ya watu makamo ni kazi kwenda tu, na waliozeeka ni nyumba za wazee, na riyaliti ya vijana, wao wataka kuvaa mikufu na vipuli waume kwa wake, wawania kuwa ma celebrities tu. Too much T.V. hiyo. Hawana aspirations kuwa ma scientists, wala.... Akili zao finyu. Nilikua kwenye dabal deka la Landan sku moja, katika safari zangu, nenda mtembelea mtoto wa mjombangu. Naskia wanawake matineja wazungumza kwa lahja yao ya Kiingereza iliyo ngumu, "After all that I done for them, what do I get? Fuck all! A fucking bunch of wankers, innit?" Hii ndiyo edukeshen yao - 'I get fuck all = I get nothing'; 'Wankers' (yatamkwa 'Wenkaz') = mwenye kujipiga mkwenyeto, beshen yaani mijifala; na 'innit?' (yatamkwa 'ini') = 'isn't it?'

 

181. Kwa hivyo usihadaike wala usibabaike, tuliza boli kijana. Dem wa Kizungu nyele zavutia kwa sababu azitia stretna, laa sivyo mapindi na kukotana kwake kutakua ova mchafuko wa mawimbi ya bahari. Na akishaoga hajitokei tuu, lazma amalize wan awa nzima, nyele azi blow dry (azipiga heya draya). Na hair ekstenshen, na mawigi, na kuzitia dawa, na kuzitia rangi, Wazungu nyele zao kuzifanya yote haya ni bai oda. Na ulapo makoroni (pasta), kumbuka si Mataliani ndio walio ivumbua, hapana bwana. Wataliani wameiiga kwa Waarabu wa Kaskazini mwa Afrika, kina Malibya na Mamoroko. Na ukija "majuu", vidole vya mikono na vidole vya miguu vitakuzizima saa zote kwa baridi, japo glavz unvaa, na soksi za sufi nzito pia unvaa, na hata ukijifinika mablangeti mazito mawili mawili, kuamka usiku utaamka tu, pengine mara 2 au mara 3, ushururuwe chooni ukabwauwe. Kwa hivyo, riyaliti ikikupiga ukishafika huku "majuu", sijui uanze kuangua kilio cha majuto uliye wee, huwa it's too late shekhe, waja leta kilio matangani?

 

182. Kumbuka "majuu" munkuja kufanya kazi tu hapa, muzitajirishe hizi nchi za "majuu" kwa kutozwa kodi (taxes), nothing more, nothing less. Ni kama Zaharai mschana mmoja wa kwetu, aanza olewa Saskatoon baada ya kuishi Dubei miaka kadhaa anambia, "Angalau hapa muna rights, si kama Dubei." Kweli raits munazo, lakini ukishatanabahi kuwa "majuu" ni Kazinistan, na mpango ulioko ni mmoja tu, nao ni wa kushika pesa za 'hand to mouth' tu, wengi hata sevings za saba unusu wala za pesa nane hawana, hapo utafanya akili. Afadhali mukae huko huko kwenu "matini", lakini mupunguze upuzi kama wa Jamali namwambia, "Wewe waowa demu, wajua si bikra huyu?" Jamali anijibu huku ateka, "Ah, si ndio uzuri bwana? Aliyembikiri si ashanipunguzia kazi?" Upuzi, na uppuuzi, tuuwateni jamani. Kaeni vizuri huko "matini", na kuweni na kushikana, muwe kitu kimoja, mujiletee nafsi zenu maendeleo. Na M'ngu awape salama. God bless Kenya.

 

183. The Last Word

Mwanamke wa kiBaniani atembea tumbo wazi sku zote, lakini kukosewa adabu hakosewi, wala kuvundiwa hishima havundiwi; avundiwae hishima sku zote ni ninja ya Kiswahili. Ushajiuliza kwa nini? Makala yote haya yaangalia the reality kavu kavu, hakuna cha kustahiyana kishosti hapa. Kwa hivyo, wewe ikiwa ni Mswahili mwenzangu, na ati unaudhika kwa sababu fulani ya jambo au mambo lilivyo/yaliyoandikwa humu ndani, wahisi ati nnakutukana kwa sababu ya ule ubwamba'di wako, au ule u unsuria wako, au kasoro yoyote nyengine katika zile kasoro 27 tulizozitaja hapa za Waswahili, ukaona nnakupigizia wewe binafsi, na nnakuwata tupuu kama nlokuvua nguo zote, basi sikupi pole ndu yangu. It's hai taim tuambiane kweli; tuseme ukweli, tena tuseme ukweli wote, tusifitane, wala tusipakane mafuta nyuma ya tupa. Kwa hivyo udhika nduu yangu, tena udhika sana. Udhika mpaka upasuke, na apizo pia ukitaka apiza, lakini usisahau, "Dua ya kuku haimpati mwewe." Katika watakao udhika kwa sababu ya yaliyoandikwa ndani ya makala haya hutapata mmoja katika wao mwenye akili, wala mwenye fahamu nzuri, wala mwenye wingi wa busara, wala mwenye kutanabahi. Watakao kasirishwa na haya, hao wote ni madubbash watupu, wenye kupenda ubwamb'adi, wingi wa isti'mari, wepesi wa kukejeli watu pasi na haki. Yaani ni kisa cha nyani asioona kundule. Kwa watu sampuli hii nawaambia, "Sit on my middle finger, then spin on it."

 

184. Na ikiwa unaifurahia hii reality check iliyomo humu, ulkua kabla ya makala haya ni "jogoo la shamba lisowika mjini", lakini sasa umpata faida moja, mbili, au zaidi, basi kazi yetu impasi sote tulioshughulikia makala haya. Basi imma wewe uwe ni mtu wa "matini" ukajua vizuri sasa reality ya huku "majuu", au wewe ni mtu wa huku "majuu" na sasa ukayajua mengi zaidi ya watu walioko huku huku "majuu" ulokua huyajui, au wewe wa "majuu" ukayajua mengi zaidi ya watu wa kule "matini" ambayo pengine ulkua kuyajua huyajui kwa sababu pengine ukija huku "majuu" ulkua bado una umri mdogo na vitimbi na abal hakama za Waswahili ulkua bado hujazijua vizuri, au pengine Mswahili wewe kukaa na Waswahili ulikaa sana nao lakini Uswahili wenyewe ulkua hukuutanabahi kwa sababu imma hukua ni mshtuko au pengine ulifwata sana sunna saa zote wewe ni 'salama alekum' kwa kila mtu upishanae na wee ni mato tini tuu saa zote wafwata ushekhe na maamrisho ya Mtume SAW saa zote (Waswahili humteka mtu sampuli hii, wakamfanyia na inadi na stizai, wallahi ajabu ya Rahmani baadhi ya majuha hawa wavundifu kumamaa maa zao ma imbwa hawa!), kwa hivyo ulkua unlala usingizi mzito, na sasa unsoma moja mbili ya makala haya na mato yako unyafungua sasa na ile full pikcha ishakujia shapu sasa, basi tuombea M'ngu mwandani ndani ya nafsi yako soote tulohusika na kazi hii, "tukapoteza" masaa mengi mno kuyaandika na kuyaratibu yoote yaliyomo humu. M'ngu atupe sote kula la kheri hapa duniani, na kesho akhera pia twende tukakute mazuri matupu yatungojea huko, aamiin.

 

185. 

- Al faatiha.

- Allahumma aatina fiid dunya hasanatan wa fil aakhirati hassana, wakinaa adhaaban naar, aamin.

- Rabbana hablanaa min azwaajinaa wa dhuriyaatinaa kurrata a'yunin, wajalnaa lil muttakina imaama, aamin.

- Rabbanagh firlanaa wal ikwaaninaa ladhiina sabakuuna fil iiman, walaa tajalna fii kulubinaa ghillan liladhiina aamanu Rabbanaa innaka Raufur Rahiim.

- Rabanaagh firlanaa waliwaalidiina walmuuminiina walmuuminati innaka antal Ghafuurur Rahiim, aamin.

- Waswalli Allahumma alaa Rasuulinaa, wal hamdu lillahi Rabbil Aalamin.

 

Omar "Auni" Bunu.
Dedicated to my late mother, Somoe Mwana.
 

Toronto, October 2011.

 

186. Tuma Barua Pepe

 Ukitaka kuyasifu au kuyashifu makala haya,

Ukitaka kunishkuru au kunitukana mimi usinbakishe, uutanganye na ukoo wangu mzima,

Yoote hayo, na nyoote nyinyi, mwakaribishwa,

Nitumie barua pepe hapa:- 

< This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it > (baina ya 'omar' na 'bunu' pana 'desh' kama hivi, "omar_bunu")
 
 

 

 

187. Videos

1. Gado on CNN

2. Cyrus Jirongo & Karusi the 40 Shs Note

3. Kalonzo Musyoka & Raila Odinga wateta chooni

 

4. Obama & his official birth video answering Donald Trump

5. Fishing for bicycles, Amsterdam

 

6. Bichi, Lamu

7. Kupaka hina

 

8. India Cricket World Cup win celebrations, East Ham

9. Zinedin Zidane Worldcup Headbutt

 

10. Julius Mulema War Talk

11. Jacob Zuma

 

12. Makka Kuu

13. Makka Chocho

 

14. How to use Twitter

15. You need to get off Facebook!

16. Baby on Board car sticker

 

17. Mjani Morocco

18. Mario Balotelli

 

19. Part-Time Day Trading set up in an average Joe's home

20. Microsoft Flight Simulator X set up at home

 

21. Ali G - Interviewing David Beckham & Posh Spice

22. Ali G - Interview with Shaquile O'Neil

23. Ali G - Feminism

24. Ali G - Drugs interview

25. Ali G - Dangerous Weapons Interview

26. Ali G - FBI Interview

27. Ali G - James Baker Interview

28. Ali G - L.A. Gang Interview

29. Ali G - Animal Rights Interview

30. Ali G - Interview with a Physics Professor

31. Ali G - Interview with a Chemistry Professor

 

32. Mzungu picking his nose on a train

33. Woman shitting in public

34. Farting everywhere

35. Chris lighting a fart on a train

36. Artist refused to take pictures at a train station

 

37. Kenyan Runner loses his feet to frostbite

 

38. L.A. Riots 1992

39. 1993 London Race Killing of Stephen Lawrence

40. English Riots: People, Police & Politicians

41. Racist rant on a tram, London

42. Racism in European Football

43. The Hijab - French Xenophobia & Intolerance

 

44. London's Metropolitan Police - Take the knife?/Don't take the knife? - Choose A Different Ending

 

45. Massive Strike - UK

 

46. 1997 Bank of America Robbery Shootout, North Hollywood

47. Situation Critical - Real Hollywood Shootout (National Geographic)

48. Call of Duty: Modern Warfare 3

 

49. Contactless Payment

50. World Skills, London 2011

51. Tissot T-Touch watch

 

52. Barons of Kandahar, Lamu

53. Kenya Lamu islanders protest Somali kidnappings

54. Kiunga Village - Kenya-Somalia Border Post

 

55. Mayor of Mogadishu

56. Somali Gangsters

57. Mogadishu 2009

58. Somali-Sijui interview in a car in Nairobi

59. Migrating Kitchen - Somalia

 

60. Truth, Lies & Asylum Seekers

61. Next Door Neighbours - Somalis in the USA

62. Shukri, Somali Woman in Turin, Italy

63. Naima, getting out of poverty in Norway

 

64. FGM (Female Genital Mutilation) of Pokots (& Somalis)

65. Somali girls in England

66. Somali girls fight in the USA

67. Somali girls on a night out fight on Bus No. 29, London

68. Somali bad-boy in America (LOL)

69. Mbarawa "Drug Dealer" showing off his car in NY

70. Minneapolis ghat bust

71. Canadian Somali girls land in jail in Jamaica

72. Somalis caught up in turf wars in Edmonton, Alberta, Canada

 

73. Anti-Tribalism Movement, Wembley, London

74. Why wear the hijab? USA

75. Worldwide Somali Students

76. Mo Farah the British Champion

 

2Pac - Ghetto Politics - Great lyrics to help you to understand the harsh reality of"Majuu"

(Parental Advisory - Explicit Lyrics)

 

77. Dear Mama (Poor single mother on welfare)

78. Brenda's Got a Baby (Do whateva it takes to resist the temptation)

79. Keep Ya Head Up (The blacker the belly the sweeter the juice)

80. Changes (My stomach hurts so I'm looking for a purse to snatch)

81. Till The End of Time (Ain't flashed a smile in a long while)

 

82. Nigga Nature (Fake hair, fake nails, fake ass too - buy me this/buy me that syndrome shit)

83. Skandalaz (I went from hell to living well)

84. Wonda Y They Call U Bitch (Keep ya head up legs closed eyes open)

85. I Ain't Mad At Cha (I keep my Glock beside my head when will it stop)

86. How Do U Want It (All I want is the money fuck the fame I'm a simple man)

 

87. Fuck Friends (Understand this, they ain't no nigga like me, fuck Jay-Z)

88. Only God Can Judge Me (Paranoid from the weed/Trying to focus but I can't see)

 

89. Lil' Homies (Got my diploma but didn't learn shit in school)

90. Ambitionz Az A Ridah (My attitude was 'Fuck it')

91. Heartz of Men (Grab your bulletproof vest nigga cause its gonna be a long one)

92. All Eyez On Me (Bitches pursue me like a dream, been known to disappear before your eyes like a dope fiend)

93. Picha Me Rollin (Picha me rollin in my 500 Benz/My dreams are censored, my hopes are gone)

94. 2Pac - Till I Die (Bury me in pieces 'cause they fear reincarnation)

95. Hit 'Em Up (Grab your Glocks when you see 2Pac, Call the cops when you see 2Pac)

 

96. Get Rich or Die Tryin (Reality in the Streets - 50 Cent)

 

Since this topic - the true "majuu" - has been so serious & frankly, a little depressing, let's say our goodbyes with this collection of one liners. You gotta laugh!

 

97. 100 funniest 1 liners