Menu

   

PDF Print E-mail
 
Waswaha Abroad
 
 
(C) The Full Picture - 6. Wayajuwayo walio "majuu
 
moon phases
 
6. Wayajuwayo walio "majuu"
 
Yaliyomo:-
A. Swalaa za kimnya huwaje, na ombi la Ayyub A.S.
B. Alama 3 za mwanamke kuwa tayari kukinyaka
C. Ndege haipigi stati, utaishtuwaje?
D. Msuaki wa Mdaa, na mato ya Kizungu
E. Kusoma gazeti chooni, na kanda ya ngono ya Kadeshian
F. Jeket Potetoz, na "House Full" ya Regal
G. Mkojo kikombeni, kutiwa tobwe mpirani, keepy uppy, "ndoo nkutome" ya Madonna, na swalaa ya Norwe
H. Drying Room na Blackbrii, na maswala 150 najua utayafeli tuu, nakwambia "Rii!"
I. Silence! Exam in Progress (150 multiple choice questions)
 
1. Samaki wa tafi na wa tangu, na kushutisha na kukutia riyahi
2. Kengele ya chuma ya Serani, na kengele ya kanisani
3. Mwanaharamu n'yupi, na baba haramu n'yupi?
4. Kuvunda ungo 8-13, na kuruka blada
5. Shuzi la mwanamke, na fanya hishma yako
6. Kuowana karatani, na 'henz up' ya shatranji
7. Kumpa mwenzio siri, na kunong'onezana
8. Mafta ya ndege, na mafta spesheli kabisa
9. "Bisbasa" ya Mambasa, na Kenya=TKK
10. Kwenda Milima ya Shimba, na kujaza magurdumu upepo fogo
11. Kuingia moto nyumbani, na moto huo kukuuwa
12. Shakli ya mwezi mpya, na shakli ya mwezi mkongwe
13. Shababu akimuona RiRi, na kiungo kumfura palepale
14. Kumshika panya, na mtego wa jubna
15. Nyoka hatari Mamba Mweusi, na kasi ya misamba 5 kwa nukta
16. Mboo ya binaadamu, na urefu wa ikilala na ikiamka
17. Kuma ya mwanamke, na shimo lisilojaa
18. Mbwa, na kumpa nyama ya nguruwe
19. Kujaa na kukupwa maji, na kunwa maji ya chooni
20. Mitaa 10 ya Mambasa, na mtaa wa Mwanakwerekwe
21. Meli na manuwari, na serikali na mskiti
22. Magarmachi, na "Watoto Nyara" ya Baba Ziro
23. Kuvaa sana kofia, na kutokwa na upaa
24. Breki ya meli bandarini, na kuchumpa kwa lori la Skeniya
25. Kiumbe hatari zaidi Afrika nzima, na mashetwani wa Kibokoni
26. Kulegea kwa mwenye mimba, na jee mimba ni ugonjwa?
27. Kuharibika kwa Lend Rova kwenye mbuga ya wanyama, na shahada ya simba
28. Mzamiaji kukatika na shaza baharini, na bahari kugeuka kuwa nyekundu
29. Mkeo anung'unika Shekh Abdalla hawezi kazi, na kula kungu manga na mabungo
30. Breki kufeli Likoni Feri, na kusubiri Nguvu Mambasa ije
31. Ovadozi ya Teja, na hatari ya kula pilau kabla ya kutumia unga
32. Azamae Madubaha, na inna lilahi huyo ni wa Kikowani
33. Kupunguza gharama mskiti wa Mazeraz, na kutojenga choo
34. Mti wa kahawa, na rangi ya buni ni buni bwana!
35. Ubaya wa kahawa, na ashki za ovyo ovyo
36. Simu za iFoni, na kulazmika kuzungumza Kizungu
37. Kula mayai kila siku, na kuzidi presha na kufanya maradhi ya moyo
38. Kuamka usiku waangaliya 'taimu', na kukoboa mato ya glopu
39. U 'long saited' na u 'shot saited' ni upi, na upumbavu na hikma ni ipi?
40. Kuzikwa Kikowani, na kilio kurudi matangani
41. Dereva 'Wan Twenti', na Malindi Basi 'kuondoka' kwel kweli
42. Guum Shekhe Uwende (GSU) ya Kenya, na Fanya Fujo Uwone (FFU) ya Tz
43. Gari la Shela ya Malindi, na kuandikwa 'Domo Kaya'
44. Samaki wa Tini ya Mvungu, na samaki wa Juu ya Dari
45. Ngumi kuumbiwa MuAfrika, na Miyereka ya kiMandingo
46. Bunduki maarufu ya EK47, na risasi alfu moja
47. Jambazi kukushkia cha moto, na kubingiria kwako ujifite nyuma ya gari
48. 'Henz ap', na kuiskia risasi ya kitwa kabla kifo
49. Ngome ya Siyu, na ujenzi wa Sultan Barghash au wa Bwana Mataka?
50. Wa kwanza kunyoa ndevu, na Mzungu kushika bendera
51. Kuingia mskitini kwa swaliwa, na kutiwa ndoo uzirai
52. Yasofaa kumzuiya mtu, na kukimbia chuo cha Maalim Shaishi
53. Glasi mbili za tembo, na shilingi mbili za riba
54. Umbile la mwanamke, na kutoweza kushusha "mzigo"
55. Tahajudi za maswahaba, na sunna ya Qailula
56. Anayesilimu, na kukatwa mzunga
57. Darasa za Shekikh Lai mskiti Mwijabu, na kazi ya Mtume S.A.W.
58. Kulea mayatima, na kuwapanga kama watoto wako khasaa
59. Tungu Suleiman A.S. alomskia akinena, na nyuki wa dhakari au wa untha?
60. Kuvaa kanzu Umangani, na hatari yake kubwa iliyoko
61. Wanawake waloolewa wa KiYahudi, na kuvaa kwao hijabu za roho
62. 911 ya polisi wa "majuu", na 999 yetu ya Afrika
63. Nyota za bendera ya Marikani, na fegi 20 ndani ya Pakti ya Embaasi
64. Ulaya na Uingereza, Welz na kwa Maskoti
65. Sama na kharifu, na 'foli' ya ya kupendana
66. Hebu n"fleshie" ya Afrika, na nvulie nguo ya "majuu"
67. 'Habari za Ulimwengu' gazeti la Uingereza, ramli ya 'pinging'
68. Kutokua na tawa huku "majuu", na vikoto na peni la alkhamisi pia ni zii
69. Nyusi za malaya wa Mwembe Tayari, na 'beji' ya Serani
70. Raisi kupanda ngazi ya ndege chap chapu, na kuzikimbilia keki zilizomo ndegeni
71. Waanzilishi wa  'Leba Dee', na sababu nti hii hai iadhmishi siku hiyo May 1
72. Kensa ya matiti, na matiti ya mwanamume
73. Miale ya jua ndani ya gari, na vitamin D ilo pyuwa
74. Gari la petroli la "n'g'aang", na mlio wa fattaki wa gari la spaki
75. Kukaa nyumbani kipofu wa Afrika, na mato ya baiyonik ya kipofu wa "majuu"
76. Kuingia chooni "majuu", na maji na tishu za 'Stabaks'
77. Namba za Kizungu n'zipi, na namba za KiTaliani n'zipi?
78. Kufanana kwa maandishi ya KiYahudi na ya KiArabu, na lugha za Mashekhe
79. Kishtobe na Kumamoto ya KiJapani, na kombomwiko wa KiSpanyola
80. Kubuniwa alfabeti, na Fahali-Nyumba ya MaFinishan
81. Mavi ya Mzungu, na mtelezo wa chooni
82. Kudungwa kisu mtu 'ova' mara 50, na mwanamke kumzuiya mwivi asimuibiye
83. Watunguzi kutafta mavazi ya risasi zilotumika, na musaddas za mzunguko
84. Mtu kuuwawa, na kushukiwa 'autloz' kabla 'inloz'
85. Barua ya siri kwa mpenzi wangu kwenye kompyuta, na kuifuta kabisa kwa 'Dilit'
86. Seremala wamaliza mlango, na misumari ya vitwa vilopotea
87. 'Stempu' za taka za Uswizi, na kumtumia umtakaye kwa ndia ya posta
88. 'Raundabauti za Omani, na Vilemba vya Sultwani
89. Riyali moja ya KiManga, na kwesha lini petroli ya Omani?
90. Wanawake wacha M'ngu nti ya Taki, na kuvaa kwao mawigi
91. An epal a dee, na wimbo wa nasari
92. Mauwaji ya kikatili nti ya Siri Lanka, na Rajapaksa Kumaratunga
93. Loo Slang Jinz, na Alekzanda Makwini kwini kweli huyu
94. Mtoto kutokuwa na shabaha, na dominant ai na opozit hend
95. Mashini za kelele, na vizibio vya maskio
96. Gari kukupigia 'Pasi', na onyeka sije nikakugongla mbali!
97. "Majuu" mtoto 1 katika  4, na kunyokewa na maisha kuwa matajiri wakupindukia
98. 'Daiva' kuishiwa na hewa, na kuiangalia 'geji'
99. Mwendo wa 'supa model', na kuzirusha nyele za kubandika
100. Rangi ya kutu na mistari meusi ya Taiga, na kujifita kwake migombani
101. Kuanzishwa Kaka Kola, na kutumiwa kwa sherbeti na lozi
102. 'Rigo motis' ya maiti, na kuanza kufa kwake
103. Maradhi yaongozao Marikani, na kuwa na wivu na umpendaye
104. Kutumbukia mtoni huku "majuu", na kuogelea kaa uvukao Ngomeni
105. Kupiga gari 'stati' asubuhi, na kuliwata lishike moto vizuri
106. Tai au andaweya, Mfursi utamtambuaje?
107. Kukamata treni barabara, na smaku za elektro megnet
108. Simu za mkononi, na usabba wa umtukiaye
109. Kuzaliwa na kufa kwa binaadamu, na hizo "zaka zetu"
110. Haram za Giza, na ujenzi wa maalfu ya miyaka
111. Mashini za kuugundua urongo, na kunukizana midomo
112. Stimu za maklabu, na usomi wako wa neno 'Ambalesi'
113. Chai ya ndege, na uzembe wa ma 'eya hostes'
114. Jambia la bwana harusi, na nta za Mbwajumwale 
115. Dinari ya Kuweti, na Kauri ya za Giriama
116. 'Keeping up with the Kardashians" za "majuu", na "Vitimbi" vya wa "Matini"
117. Hamidi Kikuba, na kupapatua asmini
118. Inshuwarens ya 'thad pati', na Wazungu kurengana
119. Barafu ya Kizungu, na Pilpili hoho ya "Matini"
120. Mlango atokao Bob Mali, na Dirisha utokalo wewe
121. Totovu wa vuduu, na falaki za Pemba
122. Hija ya Maka ya Mkalasinga, na mabwamba'di wa Mkanyageni 
123. Mavi ya mbwa, na mwosho wa mara sabaa
124. Ekselereta ya ndege, na klachi ya matatu
125. Shati la kumtisha mwanamume mwenzio, na flana ya pinki
126. Siri ya nguo za wanawake, na uzuri wa nyumba
127. Mama wa Kisomali, na kumbatia yake
128. Uzuri wa mwanamke, na the biga the beta
129. Dhihaka za Muingereza na Muemerika, na watoto wa mjomba na shangazi
130. Kensa ya wanaume, na kupigwa finga na daktari asiyekua basha
131. Stileto za ughali, na mitawanda ya buni
132. Kuzoma Kizungu, na chuo cha Maalim Twalibu
133. Ma-Epal Mengo ya muwasho, na mayai ya Kenta lilopinduka
134. Lugha ya MaSkoti, na matamshi ya Aleks Faguson
135. Ukiagizia Inglish Brekfast, na weta maridadi
136. Mwana Falsafa Soktra"tizak", na skandalz za Alekzanda "Mtukufu"
137. Nyele za kubandika, na mawigi ya MaYoruba yatokayo Naijeriya
138. Taffash za baba kuwaangalia watoto, na bongo la mwanamke
139. Spidi ya jito kuona, na kiini mato cha mkono
140. Kuona kwa mbwa, na pua ya binaadamu
141. Vita vya 'tred maki' baina Uingereza na Sini, na kuingia kati Mfaransa kwa kunyimwa vyura
142. Ya leo na ya kesho, na lugha ya KiAimara wa Emerika Kusini
143. Kuumwa na jino, na kuramba pilipili
144. Visu vilokukalia kooni, na Kofta ya Mbaraka
145. Kuona kwa simba usiku, na kumwashia kwako taa
146. Kuzuru Afrika, na kuendesha gari usiku
147. Kuvaa Mzungu kikoi, na kaunda suti ya Mbajuni
148. Yemeni na Omani, na uume wao kutotawaliwa
149. Omo Pika Boksi, na kubahatisha asli ya uwaonao "majuu"
150. '5 O'klok Shedo', na 'Keyales Wispa' ya Joj Maikal
Mawala Surwa
A. Sfuria n'nini, na Safura n'nini?
B. Maradhi ya sukari, na sukari ya kumeremeta
C. Saa nne Kiarabu na kumfunza saa kwa Kiswahili mtoto wa "majuu",  na mfungo mosi ya Bathdee ya Nchume S.A.W.
Majawabu ya maswala
 
 
 
Hebu Tuanze
 
Mswahili wa "matini" yumbioni kwa kuandama usabasi, kuhusudu watu, kurushana urathi, kupiga mabarnaa, kutafta mlo wa bure maharusini (kwaitwa 'kumwaga vumbi' huku), na kuangalia viuno chakachani.
 
Na huyu Mswahili wa "matini" akiwa nyumbani kwake hana illa kuangalia mapya yaliyomfika kisabba na timvi mkubwa Bruki kwenye "The Bold & The Beautiful", au kuangalia mishono ya halmaria na rubini na dayet ziloingia za kina "Miss World", au kuangalia chakacha za kijameka na viuno vya kikongo kwenye "Music Time". Lengine la faida kulijuwa halijui.
 
Wengi katika Waswahili waliofika "majuu" wako mbioni, saa zote wako mzigoni, wamenyeka vibaruani (Mzungu hukwambia, "He's on the job 24 seven"). Kwa hivyo, akili zao zimpanuka na kukua, na kila kukicha zazidi kupanuka na kukua.
 
Lakini lazma tufahamu, chembelecho alvyonijibu jamaa mmoja Msomali Mswahili wa Magongo s'ku moja alipo nitenda nikamlaumu kwa kumtia kundini mwa Waswahili waso maana wakutiwa pipani, akanijibu chapchapu,  "Sio wote!" Nami nawaambia, sio wote Waswahili waliokuja "majuu" wamepata faida na kupanuka mabongo. Tufahamu kuwa pana wengi mno waliotoka maskani "matini" wawakuta wankuja na kuangukia maskani  huku "majuu". Wantoka maskani, wankuja maskani!
 
Ukija huku utakuta watu wanjaa geto la mtu, jamaa waambua gomba wakipiga na maji, nyumba i tele! Na videmu vya Kiswahili vyaingia kwenye mageto vikitoka, na wao ngomani wamo. Chembelecho Mzungu anenavyo, "You can take a man out of a village, but you cannot take a village out of a man." Hawa hawakustafidi kwa kuinua kwao. Faida waliyoipata kwa kuja "majuu" is a big, fat zero. Hawa na mbuzi wote ni gora moja; mbuzi ukimpigia gita, kweli atainuka ateze? Hatezi.
 
Haya, tuyaangalie baadhi ya mambo wayajuao watu wa "majuu" na wasoyajua mengi katika haya watu wa "matini".
 
A. Swalaa za kimnya huwaje, na ombi la Ayyub A.S.
Katika kushughulika kwake Mswahili wa "majuu", yeye hupata kujua mengi, si mambo ya kidunia, si mambo ya kiakhera. Tuangalie hii mifano michache ifuatayo. Tuanze kwa kuangalia mas'ala ya swalaa. Sote twajua ya kua swala za kiza zote 3 huswaliwa kwa sauti, na swala za mtana 2 huswaliwa kimnya kimnya. Lakini kimnya chenyewe kiweje? Si ukiskia kimya kiwe ni cha maktaba (laibrari), uwe wasoma kwa moyo kama wanavyoitakidi wengi. Lazma ndimi zitaharrak, zende.
 
Swala za kimya zikiswaliwa ukute kwa uchache, usome na huku ulimi uwende, na kwa kuzidi, usome katika swala ya adhuhuri au alasiri yako mpaka ujiskie kwa mbali kwa mashkio yako mwenyewe ukiisoma hiyo Alhamdu na Qul Huwal Lahu yako. Kusoma kwa moyo, kisiri siri, hiyo ni mediteshen, na mambo hayo hapana katika swala. Ndio mtume Ayyuub A.S. alipopawa mitihani mpaka akawa 'jabal min jibaalis subraa', Ayubu A.S. alimuomba M'ngu ampe mitihani yote ispokuwa ulimi wake auwate salama, ili apate kumsabbih Yeye Muumba wake S.W.T.
 
Wa "matini" haya, na mengi mfano wake, kuyajua hawayajui. Wao waulize nani aliyeatwa watakutukua wakufikishe mpaka mlangoni kwake. Pana katika Waswahili wa "majuu" waliotoka huko hawajui moja katika ya dini, walpofika huku wakatanabahi, na wakaanza kujibidiisha vilivyo kutafuta ilmu sampuli ya jambo hili tulolitaja hapa.
 
B. Alama 3 za mwanamke kuwa tayari kukinyaka
Twende kwenye ilmu ya wanawake. Najua nyii wa matini mwajiona nyoote ni mabingwa wa kutambulikana, machampiyoon kabisa, lakini muyajuayo ni ya tako la nani lakatisha vizuri zaidi harusini, jengine hamulijui. Hebu niwaulize, jee, mwanamke atajuwaje kaa mayai yake kwenye uzao wake yako tayari, mpaka akiundama na mumewe (au mshkaji wake wa kuibia huko mitaani kwenu huko "matini"), basi atakua yu tayari kushika mimba?
 
Vipi, ushalif'kiria hilo jawabu? Najua kaa unsoma sekandri na bado una kumbukumbu nzuri, basi utanambia mambo ya kuhisabu siku 14-16 kutokea alpoanza hedhi. Wewe kwanza ulifeli maths, kwa hivyo hizi hisabu usishindane nazo, hebu tuwaatie wenyewe Wahindi waendeshao maduka makubwa. Si wajua hisabu zetu kubwa ni za kummizia mate binti ya mtu tuu?
 
Najua hilo jawabu unshindwa nalo. Haa n'doo n'kupashe basi.  Alama zilioko za kujua yai la mwanamke litayari kushika mimba am laa ni alama 3. Ya kwanza, umoto wa mwanamke hupanda kidogo pindi akiamka asubuhi. Kipima joto (thamomita) huna? Najua huna. Hata mita ya maji nyii hamuna majumbani mwenu, itakuja kua hiyo thamomita!
 
Haya, alama ya pili ni kuumwa na tumbo, konde za matiti kufura na kuwa hazidariki kwa maumivu, na mwanamke kununanuna saa zote (kuwa 'moody'). Tukiwa twamzungumza Amina na Fahima labda alama hizi wanazo sku zote, na s'babu ni haweshi kula ma achari na mambirimbi mpaka wakaumwa na matumbo, na ikiwa kunung'unika na kufurizana ni ada yao saa zote. Kwa hivyo ukiishiriki alama hii utapotea maboya.
 
Twende kwenye alama ya tatu, mwanake hutoa sampuli ya 'maji' kutoka kwenye ule "ubale" wake mara nyengine, khaswa akimaliza kukojoa, na 'maji' haya huwa ni mazito na rangi ya maziwa. Ikifika wakti yai lake sasa lashuka kwenye uzao, na huwa yu tayari kushika mimba, basi 'maji' yale hubadilika yakawa mepesi, na rangi yake ikabadilika ikawa sasa ni nyeupe mfano wa maji, na huwa kama gundi inavyo ganda, au mfano bora huwa ni kama ule ute mweupe wa yai biti la kuku ulivyo mweupe na mnyato wake. Ndio hilo yai la binaadamu litayari, na kaa mwapanga nyii wazazi wawili mupate mtoto, sasa huwa ndio wakti mzuri wa kukutana, na usiniulize mukutane wapi!
 
Ilmu hii ulkua wewe kuijua huijui, ata uwe ni Dokta Lava wa Aga Khani, nyinyi kaeni mushiriki "The Bold" tuu sku zote, kisha muangalie mwisho wenu utakuwaje.
 
C. Ndege haipigi stati, utaishtua vipi?
Tuwate haya ya dini na ya kustarehe na mkeo au wakezo, twende mambo ya ndege. Un' ndege yako yakubeba mtu kumi. Ndio, najua hakika ndege kuwa nayo huna. Licha ya ndege, hata kuwa na dushi mwenyewe hapo nyumbani ukawa wamfuga huna, maana dushi ataka mtama saa zote. Utausaga mtama upate mofa ule wewe, au utakaa kazi ni kulisha madushi? Niko na wewe staa. Lakini hebu tujifanye tu, un'ndege. Haya, waipiga stati, inkataa. Jee, utaiwasha vipi?
 
Us'nambie ati utawaita jamaa wa mtaani waisukume. Uliskia hii ni matatu ya babako? Ndege haipigwi stati hivi babaz. Utakavyo fanya ni utaleta betri nyengine ya ndege (usibabaike, inkaa kama betri ya gari tuu), uunganishe waya, uishtuwe. Ndio ile 'jump-start' uijuwayo ukiona gereji za kishefa gari yashtuliwa. Waswahili musibabaike na ndege bwana. Ndege ni chombo chenye mashini tuu; gari na jahazi pia ni vyombo tu, na vyote hivi vina mashini na mabanka/maparapela kama ndege tuu.
 
Wayajuao wa "majuu" ni mengi, nyii kaeni mukiwashwa na mgongo umwambie mwenzio akukune tu. Huku utamwambia msafiri mwenzio ndani ya treni wenda mzigoni kweli ati akukune mgongo, na jamaa ukimuangalia ankaa kaa ji-saiko (psycho)?
 
D. Msuaki wa Mdaa, na Mato ya Kizungu
Katika wayajuwayo wa "majuu" ni kuwapeleka watoto wao kwa daktari wa meno kila mwaka. Wee unkaa "matini" umri wako wote hata huo mlango wa dentist huujui unkaaje wala unpakwa rangi ya mafuta au rangi ya tokaa. Wee uko kwenye msuwaki wa vijiti, na kama unaendelea sana, basi uko kwenye kutumia brashi ya Kizungu hiyo hiyo moja mwaka wa tano sasa, mpaka inkuwa yaomba toba ya ilahi, na pindi meno yakibadilika yaanza kua rangi ya buni kaa ya Kikikuyu, utake kuyang'arisha meno sasa yawe meupe, wakazana kuyasugua kwa mdaa au kwa tenga za makaa mpaka wavuja damu. N'shaona jamaa Ngomeni ajisugua meno kwa mtanga wa baharini. Nauliza jamani, kwani n'mashaza au ni meno tulonayo? Huku "majuu" pana msuaki wa kahrabaa (electric), na betri yake ya ndani ikisha nguvu waichaji tena (usione utakwenda kwa Bereki ukanunue betri za Eva Redi Paka Pawa), na ukiubonyeza kwa nguvu, wajizima wenyewe, maana Mzungu ashapima ya kuwa huwa waharibu ufizi (gamzi) wako.
 
Wengi wenu wa "matini" hamuli uyoga (mashrumz), hamjapanda ngazi za kwenda wenyewe (eskeleta), hamujaona thaluji (barafu) ikishuka, wala hamjaona mato ya Kizungu. Wazungu karibu wote wana mato ya rangirangi  - imma huwa wana rangi ya samawati, au ya kijani, au ya buni, au ya kijivu, na wachache ndio kama nyinyi wa "matini" huwa na mato meusi tu. Na rangi zenyewe nyengine huwa zimeiva, na nyengine huwa ni za mdaro tu, na wengine wana mato ya kutisha Wazungu wayaita "piercing eyes". Nyii mukiulizwa, "Huyo mume aliyekuja, ankaaje?" mwajua kujibu, "Am mato kaa glopu" na "Am mato kaa ya pweza" na "Am mato kaa mwivi."
 
E. Kusoma gazeti chooni, na kanda ya mkatano ya Kadeshian
Nadhani twaelewana mwandani? Wa "majuu" wa mbioni makazini, na wakipata dakka mbili za kupumua wengi wao hutafuta jambo la maana wakalifanya. Ndio utakuta Mzungu asoma gazeti chooni. Si starehe ile, laa, hapana bwana. Hana taimu nyengine ya kupumua na kujua yanaojiri ulimwenguni. Aona maadamu yu chooni ajikamua, basi wata apatilize kabisa aingie na gazeti aongeze maarifa. Ukifanya wewe haya huko "matini" utaambiwa, "Jee, kunani? Wawasomea majini wako taarifa ya khabari?"
 
Na wewe wa "matini" ukiwa wanya chooni pengine wapanga urongo wakumchenga jamaa ulomueka skwea jana, mulipoagana kwenda hukwenda. Na ifikapo jioni, wakalia T.V. wamuangalia Kadeshian, na kesho maskani muanze mjadala mkubwa, "Jee, huyu Kadeshian, kweli ana rasa shepu nzuri kuliko Sakina bandu wetu wa mtaani, ama laa?"
 
Umbaki kumuangalia Kadeshian na kumuhusudu, wala hujui kitu gani kilimfanya awe maarufu, au wewe wajua? Nambie basi. Mbona kimnya kinzidi? Alaa, hujui, si n'nakwambia mimi! Kadeshian alkua hakuna amjuae, lakini nyota yake ikapaa pindi alipo pigwa vidyo akatwa na mshkaji mmoja, na kanda hii chafu ikasambazwa Mashariki na Magharibi mwa ardhi. Ndio mshkaji wake wa sasa, Kanye West (kama ni Kanye East tena sijui), akachachawa alipoiona kanda hii, akenda mbio, mpaka mwisho akamtia mkononi, na hivi n'kwambiavyo Kadeshian ana mimba na harusi yao bado!
 
F. Jeket Potetoz, na 'House Full' ya Regal
Basi nadhani ushaelewa ya kuwa pana nusu ya Waswahili wa huku "majuu" hawakuishia maskani za majumbani (pan baridi kama tulivyoona, maskani za vibarazani hamna huku) wakapoteza taimu zao kama wapotezavyo ile nusu nyengine ya wa "majuu" walokuja wakaao fwaa tu, na karibu Waswahili wote waliobakia "matini".
 
Hawa nusu walokuja wakastafidi kwa kuja kwao "majuu", wao wajua, kwa mfano, ya kua viazi vya kuchoma visoshambuliwa maganda (vyaitwa 'jacket potatoes') ukivila vina vitamin C nyingi, na wajua ya kuwa snema ikijaa husemekana ni "Full House" wala si "House Full" kama ilvyokua ikiandikwa kwenye ubao zamani pale Regal Sinema. Riigal ilokua ubavuni mwa duka la viatu la Fimbo Footwear/Faruchi (Farucci) upande mmoja, na upande wa pili ndipo penye Bima Tawa ya leo.
 
G. Mkojo kikombeni, kutiwa tobwe mpirani, keepy uppy, 'ndoo nkutome' ya Madonna, na swalaa ya Norwe
Au ushawahi kukojolea kikombe cha chai kama mimi, kisha ukakiwata nde usiku kucha, asubuhi ukakuta kojo linfanya barafu rangi ya dhahabu? Hujafanya. Au wajua mtu akitiwa tobwe mpirani yaitwaje Kizungu? Yaitwa 'nutmeg'. Pengine wewe hata hujui hii nutmeg ni aina ya konde. Konde yenyewe ukiiskia Kizungu huijui abaa, ndiyo hiyo kungumanga yenu (inunue kwa AbdulKhaliq hapo Bondeni), isagwayo, kisha ikatiwa kwenye biriani mara nyengine, lakini maarufu hupewa bwana harusi akanwa na maziwa kusudi aweze zukwa vizuri akiingia nyumbani.
 
Nutmeg hiyo ya boli. Na kupepeta jamaini kwaitwa 'keepy uppy'. Usiniulize kuvalishwa kanzu mpirani Kizungu kwaitwaje, wala kuvalishwa kirinda kwaitwaje, bali niambie wewe kama kweli wajua! Nataka unifanyie na kazi nyengine pia, wewe wa 'matini'. Hebu kantaftie, huyu muimbaji Madonna (manake 'Bibi yangu wee!' au 'my lady', na ni jina la hishma Mataliani wamuitavyo mamake Isa A.S., Madonna = Virgin Mary), ile sdiria ya ukosefu wa adabu aloivaa steji ya 'n'doo nkutome' yaitwaje Kizungu? Na Norway kuanzia mwezi wa Mei mpaka Julai katikati hakukutwi kukawa magharibi wala ishai. Sasa swala huku zaswaliwa vipi? Hebu nenda kamuulize shekhe wako mskitini jee, manake najua wewe ilimu kuwa nayo huna.
 
H. Drying Room na Blackbrii, na Maswala 150 ambayo najua utayafeli tuu, nakwambia "Rii!"
Kwa hivyo nduu yangu pana mengi uso yajua. Wa "majuu" akiingia kazini pengine ankuja jogging au cycling, hupiga shawa chap chap, nguo zake zenye majasho akazitia 'Drying Room', wee hata huna habari chumba hichi n'cha nini, wee waona ndio unaingia hiyo sauna uiskiayo. Laa bwana, pana masakhaana pale (heaters), waanika nguo, ukimaliza shifti yako wenda zako nyumbani nguo zishakauka tena. 
 
Uko Afrika waskia Obama ana kisimu cha mkononi chaitwa Blackberry, wee waona labda chatoa matunda. Ata kukiita pia hujui kukiita. N'doo "majuu" uwaskize wenyewe huku - "blekbrii". Kuyajua mengi huyajui, lakini sku zote wee ni kishipa, mshindani.
 
Licha ya mambo ya kilimwengu, hata mambo ya kidini wengi wa "matini" hawayajui. Ingia Bashekhe sku ya Ijumaa utawaona watu wampindana wasoma Yaasini mara ishirin na moja. Na sunna ni kusoma Sura ya Pango (Suratul Kahf) yenye aya 110. Mtume SAW akiisoma kwenye mimbar sura hii mpaka maswahaba wote wakaihifadhi. Uisomapo sku ya ijumaa basi M'ngu hukutia nuru wewe mpaka ijumaa ijayo. Na pana hadithi maarufu ya anayehifadhi aya 10 za kwanza basi atasalimika na Dajjal. Dajjal kuja atakuja tu, na akija na wewe huko tayari jua uko mashakani, maana atawakufurisha wengi. Ndio Mtume SAW alisema hakuna mtume yoyote aliyetumwa illa aliuonya umma wake na kidudu mtu huyu Dajjal. Na wewe wakazana na Yaasini 21.
 
Watu wa "matini" hamuna mulijualo, poleni. Na kuonesha ukweli wa jambo hili, yafuatayo hapa tini enyi watu wa matini, ni maswala 150. Nusu ya Waswahili wa "majuu" wasokaa fwaa wajua majawabu ya maswala mengi mno katika haya, lakini walioko "matini" wengi hawayajui majawabu ya hata maswala 10 katika haya, na wakijua saana, basi hayapiti 15. Wa"matini" na wale taim westaz wa maskani huku "majuu", wao sku zote ni kujifanya tuu mach noo tu, lakini nawaambia tena, hamuyajui illa ya usabba tu, na pengine mukijua sana ni ya saba unusu na ya pesa nane tu. Hebu angalia mangapi uyajuayo. Tagua moja katika majawabu haya ya (a) au (b), mojawapo tu ndio sahih. Jawabu ziko mwisho wa huu "mtihani". 
 
I. Silence! Exam in Progress (150 questions, plus 3 others as bonus)
 
1. Tafauti ya samaki wa tafi na tangu?
a) Tafi ashutisha, na tangu atia riyahi.
b) Tafi haparwi kwa sababu hana magamba, na tangu magamba anayo. Red Snapper (tangu) in Jamaica
 
2. Serani kengele yake ni ya chuma cha reli. Kwa nini?
a) Ina mlio kuliko kengele za kanisani.
b) Ili isiibiwe na watoto. Mars Bar Bell Ringing
 
3. Waswahili wapenda kumuita mtoto 'mwana haramu' ambaye mimba yake ilitungwa bila ya mamake kuolewa na babake. Jee, Waswahili wana pointi hapa?
a) Mwanaharamu si ni mwanaharamu tu bwana, pana la zaidi?
b) Mtoto hana kosa. Bali mwenye kosa ni yule mama na yule baba. Kwa hivyo mbona Waswahili hawawaiti "Baba haramu" na "Mama haramu", wambakia wamhujumu na kumkejeli mtoto aliyezalika malaika wa M'ngu aso na hatia? Best of Fat Bastard
 
4. Waschana wavunja ungo baina ya umri wa miaka 8-13, na wengine wachelewa mpaka wafike miaka 16. Jambo moja muhimu linalo harakisha au licheleweshalo kuvunja ungo kwa mschana ni?
a) Aruka blada au haruki.
b) Ana uzito wa kutosha au bado kifefe. Charlie Brooker Sweet 16

5. Wanawake washuta mara ngapi kwa siku?
a) Namna gani shekhe, wanawake hawashuti bwana.
b) Mara 5 kwa uchache, na mara 30 kwa wingi, kama wanaume vilevile. The Farting Preacher

6. Waswahili wapenda wahed sitin (sababu pana kuowana hapa), je, nani alibuni mchezo wa kuchemsha bongo wa Shatranji (Chess), na nini maana ya Check Mate?
a) Chess lazma wanaibuni medieval knights wa Kizungu, na 'check mate' maanake ni 'Hands Up, mister.'
b) Wahindi ndio walioibuni, na maana yake ni 'Shah (mfalme) maat (ashakufa)'. Checkmate
 
7. Haya, munkaa pahali wataka mwambia mwenzio siri watu wengine wasisikie. Ufanyeje?
a) Mnong'oneze (whisper).
b) Mwambie kwa sauti ya chini, maana kunong'oneza kwaskizika rahisi zaidi. Careless Whisper

8. Ndege yatumia mafuta gani?
a) Mafuta spesheli kabisa.
b) Mafta ya taa. Hurricane Lamp
 
9. Mji wa Mombasa una umri gani, uliitwa nini kwanza, na ulianzishwa na nani? Na neno "Kenya" asli yake ni nini?
 
a) Mombasa maana yake ni kama nilivyomskia refyujii mmoja Msomali wa Merka pale Markiti, maanake ni "Bisbasa". (Alvosema in full ni, "Mombasa ananasa, bila pesa bisbasa" = Mombasa tamu kama mananasi, lakini bila ya pesa yawasha kaa pilpili); ulianzishwa na Mamazrui tangu babu yake babu yako hajazaliwa. Na Kenya maana yake ni "T.K.K." (toa kitu kidogo, yaani hongo kwenda).
 
b) Mji wa Mombasa ukijulikana kama 'Mvita' zamani, na una umri wa zaidi ya miaka 1,100. Walio uanzisha ni Mwana Mkisi na Shehe Mvita. Na neno "Kenya" yatokamana na Mlima wa Kenya wa rangi ya buni ulio na kilele chake cha barafu nyupe imfanana na manyoa meusi na meupe ya mbuni wa kiume. Wakikuyu wauita mlima huu Kirinyaga, WaEmbu wauita Kirinyaa, na Wakamba wauita Kiinyaa. Mzungu alpofika hapa akapaita "Kinyaa" ndio jina la nchi inavyojulikana mpaka leo.
 
10. Wenda zako Milima ya Simba (Shimba Hills) iliyoko Kwale kucheki wanyama na gari yako ambayo haiendeshwi na nguvu za magudurumu manne (haina 4WD). Na ni msimu wa mvua ya masika, na waogopea kukwama kwenye tope. Je ufanyeje?
a) Jaza upepo matai.
b) Punguza upepo wa matai yawe kama nusu tu.
 
11. Unlala na kunaingia moto nyumbani. Aghlabu (majority of the time, 9 times out of 10) kitakacho kuuwa ni nini?
a) Moto bwana - moto wauwa!
b) Sumu ya hewa ya carbonmonoxide - haina harufu wala huwezi kuiona, sailent kila. Carbon Monoxide Poisoning
 
12. Ukiangalia angani usiku uuwone mwezi mwembamba, jee, ni mwezi mpya au ni mkongwe, utajuwaje?
a) Ukiwa mpya mwanzo wa mwezi utakuwa shakli hii { ( } kisha uwe mbala mwezi huwa { O } na hatimae utakua shakli hii { ) }.
b) Mpya huwa ni hivi { ) } na mbala mwezi huwa { O } na mkongwe huwa ni hivi { ( }. Namna ya kukumbuka ni rahisi. Kiarabu waandika maandishi kutoka upande wa kulia kwenda kushoto. Tizama tena picha ya miezi mwanzo wa peji hii na jawabu hili litakua wazi kwako.
 
13. Mwanamume yoyote akimuona fulani, kiungo kimoja lazma kifure kiwe mara 2 ya kawaida yake. N'kipi kiungo hiki?
a) Wauliza tena? Shababu yoyote akimuona muimbaji Rihanna tu huwa palepale ashazukwa.
b) Baba yoyote akimuona mtoto mchanga palepale katikati mwa jicho lake (pupil) hupanuka pakawa mara mbili ya hali yake ya kawaida.
 
14
. Kipande kipi ndicho kitakacho mvutia panya zaidi umnase kwenye mtego wa panya?
a) Jubna (chiz).
b) Chakleti.
 
15. Nyoka hatari wa Black Mamba, ana rangi gani, kasi gani, na akikuuma akuuwa baada ya muda gani usipopata dawa yake?
 a) Ana rangi nyeusi (ndio hii 'black'), spidi ya misamba 5 kwa saa, na akikuuma waeza kufa baada ya masaa 10 kama hukupata dawa, au ukibahatika waeza kuishi ata bila ya dawa. 
b) Ana mwili rangi ya kijani cha zaituni (olive green), au rangi ya buni (brown), au rangi ya kijivu (ash grey), lakini ndani ya mdomo wake ni weusi wa makaa. Kasi ya mwendo wake yafika mita 5 kwa nukta moja (huyu ndiye Usain Bolt wa nyoka wote), na akikuuma wafa baada ya dakika 20 mpaka saa 1, na wakti mwengine ukiwa unshiba sima wafa baada ya masaa 3. Kattu huponi bila ya dawa. Deadly Black Mamba
 
16. Mboo ya binaadamu wa kawaida ina urefu gani ikilala? Na jee ikismama? (Kumbuka urefu wa rula skuli ni sentimita 30).
a) Sentimita 15 ikilala, na sentimita 30 ikiamka. 
b) Sentimita 9 ikilala, na sentimita 16 ikismama.
 
17. Kuma ya mwanamke wa kawaida ina urefu gani?
a) Ni shimo lisilo jaa shekhe.
b) Sentimita 10 hali yake ya kawaida, sentimita 15 akiwa yu tayari wa kufanya kitendo cha kuundama, na sentimita 17 hadi 25 ikivutika kwa mfano wakti wa kuzaa.
 
18. Mbwa ukampa nini katika hivi vitu viwili avile kwa wingi atakufla mbali?
a) Nyama ya nguruwe.
b) Chakleti.
 
19. Maji yajaa na kukupwa mara ngapi kwa siku? Kujaa na kukupwa huku kwategemea? Na ukinwa maji ya chooni?
 a) Ah, yategemea, mara nyengine mara moja, mara nyengine mara 5 hivi, ata ukimuuliza nahodha mmoja hodari  forodhani aitwa Captain Masudi atakwambia yayya haya. Yategemea mfungo. Na ukinwa maji ya chooni utasema sana.
 b) Mara 2. Na yategemea pale ulipo kama mwezi uko mlingoti ndio maji hujaa, na tena baada masaa 12 dunia ikizunguka mpaka mwezi uwe upande wa pili wa ulimwengu, nyuma ya pale ulipo. Na ukinwa maji ya chooni utakata kiu kama ukinwa maji ya karoni.
 
20. Mitaa ya Mombasa 10 haya, nini asli yake?
 a) Kibokoni, Baghani, Bomani, Mkomani, Kikwajuni, Mnazi Mmoja, Michenzani, Kijangwani, Ng'ambo, na Mwanakwerekwe. Imma palionekana mnyama mkubwa kama Kiboko (Kibokoni), au palkua na mti maarufu kama Mnazi Mmoja, au ni sehemu ya kipekee kama sehemu kavu ya Kijangwani, au paliishi mtu maarufu kama Mwanakwerekwe.
 
 
 
b) Sehemu zote zilotajwa (a) ni mitaa ya Unguja. Msa una:-
- Mji Wa Kale - hii ndiyo sehemu ya zamani kabisa Mombasa
- Kibokoni - palkua na jela wafungwa wakiadhibiwa kwa kuchapwa viboko
- Kaloleni - sehemu zilikua na mabanda ya Warabai na Waribe na maana yake ni "Katizameni"
- Floringi - ardhi yote ya mtaa huu ilikua mwenyewe ni Mgoa akiitwa Mr. Floring
- Majengo Sdiria - mama mmoja mwenye kifua kikubwa aliyeranga Majengo nzima atafta sdiria saiz yake akaipata hapa
- Madubaha - neno la kiarabu Madh-bah, nayo ni kichinjioni wakichinjwa ng'ombe na mbuzi kabla kichinjio kuhamishwa Kibarani
- Inglani - neno lakimijikenda "Ingirani" ('ingiyeni') lilobuniwa na mahamali wa Kimijikenda wakipitia mtaa huu kama shotkati wakti barabara ya Ndia Kuu (mainroad ya zamani) kutoka Forodhani kuja sokoni Salim rodi ilipofungwa kwa sababu ya kutengezwa
- Toa Tugawe - mtaa uko Kongowea ya ndani, na wahuni wa Kongo Bai Fosi wakisha msongonyoa mtu wakija sehemu hii kugawa vinyang'anyiro
- Kilindini - lindi ni shimo, kilindi ni shimo dogo, na malindi ni mashimo mengi. Sehemu hii ni ya maji makuu ndio bandari mpya ikajengwa huku
- Shika Adabu - mwanzo wa sehemu ya Likoni na pana jela baridi ya watoto waliobaleghe lakini hawasikii, na hapa hunyooshwa mpaka wakashika adabu
 
 
21. 'Meli' ni nini na 'manuwari' ni nini, na maneno haya - 'serikali', 'diwani' (kaunsla), 'sheha' (chifu), 'achari', na 'chai' zina asli gani, na maneno haya 'meza', 'leso', 'pesa', na 'mskiti' zatokamana na asli gani?
 
a) 'Meli' si ni jahazi la chuma bwana? Na 'manuwari' ni mijipandekizi ya mijimeli ya vita. 'Serikali', 'diwani', 'sheha', ni mambo ya Kiarabu haya yalikuja nao Wamanga, pamoja na 'leso' za Maskati za kufunga vibobwe, 'pesa' za kuwatuzia wakatishao viuno na huku wakipewa 'achari' wazidi mori, na miti ya Kimanga ikikaa na viji'meza' vyao wakinwa kahawa utungu na huku wakibarizi na kuvisannif viuno tu.
 
b) Hii ndiyo asli yake khasa:-
- Muingereza mtawala akipokea barua zatoka makao makuu London zijazo kwa majahazi ya chuma. Barua Mzungu aziita 'mail', na barua zikiingia huwa ndio 'meli' zinkuja. Meli barua zikawa ni meli majahazi ya chuma.
- 'Manuwari' ni man-of-war, meli za kivita zenye kubeba mizinga ya chuma ya kurepua meli nyengine au bandari na miji ya nchi nyengine.
- 'Serikali', 'diwani', 'sheha', 'achari' na 'chai' yote yana asli ya Kishirazi au Kifursi (Persian, Irani ya leo).
- 'Leso' ni hanjifu ya mkononi ya kujifutia jasho, 'pesa' yatokamana na peseta, na 'meza' ni yakuwekea vitu kama tuijuwayo, na yote ni maneno yenye asli ya Kireno. Wamanga wala Waswahili hawakuvaa leso zenye mafumbo tuzijuazo leo, na pesa hazikua za Mbeberu wala za Kinyata bali pesa zilkua ni za Mreno mwanzo, kisha zikawa ni kauri za baharini alokuja nazo Muingereza kutoka visiwa vya Kihindi vya Moldivz, na Wamanga na Waswahili wote wakila tini majamvini, hawali mezani. 
- Neno 'mskiti' latokamana na neno la Kireno ambalo limeazimwa kwa bin ammi zao zao Maspanyola na maana yake ni 'mbu'. Mskiti wa Kiibadhi Kibokoni asli yake ulkua ni Kanisa la Wareno, walipotolewa mji likageuzwa likawa ni mskiti wa watawala wapya kutoka Umangani kina Yarubi, na hawa wakapinduliwa na kina Al Busaidi huko Umangani, na liwali wao Mombasa Muhammad bin Uthman Al-Mazrui akaukataa utawala wa Omani na Zanziberi akaupigania uhuru wa mji wa Mombasa ili aendelee kuwa Sultani.
 
22. "Magarmachi chuu chuu chuu, chuu chuu chuu, mallee mallee mallee, kam kamecho kamechoo kamechoo, kipyar, kipyar, kipyar, magar choo!"; na "Kibe? Bado."; na mjiskatili; na kode; na blada; yoote ni mitezo ya watoto watezao mitaani. Je mtezo wa "Watoto nyara? Nyara ndiwa. Aipatae? Niyake. Asoipata? Siyake!" yasemekana ulibuniwa na nani?
a) Baba Ziro.
b) Majisu Mapanga.
 
23. Kuvaa sana kofia...
a) Kwaleta upaa.
b) Kwakukinga na jua. Watu wenye upaa mara nyingi huvaa kofia kuufita, sababu waona ndio mojawapo ya alama za uzee, sije watu wakawadhania "mashini zao" pia zinzeeka hazifanyi kazi. Stem Cell Hair Restoration Technique

24. Meli inaingia bandarini. Ikitaka s'mama sasa, itas'mama vipi?
a) Itapiga breki ya meli. Hii ni kama ya lori la Skeniya ikifanya kuchumpa ukaskia yashusha pumzi ghafla kwa sauti kubwa, lakini ya meli huisikii sababu iko chini ya maji.
b) Parapela lake lageuzwa lielekee mbele badala ya kuelekea nyuma, huku lazungushwa mduara wa kasi. Na meli ya biashara ina parapela moja, na ya kivita ina parapela mbili.
 
25. Kiumbe hatari zaidi Afrika anae uwa watu zaidi ni...
a) Mashetwani wa Kibokoni, bila ya shaka!
b) Kiboko.
 
26. Mwanamke akiwa na mimba huwa anlegea viungo. Kwa nini?
a) Si ajitendekeza tu? Ataka fanyiwa kila kitu, kwani mimba ni ugonjwa?
b) Mwili wake watoa homoni yaitwa Relaxin, ndiyo inayomlegeza viungo na mifupa ya mwili wote khasa vile viliozunguka mji wake ili kusudi mtoto aweze kuzalika kwa wepesi zaidi.
 
27. Muko kwenye Lend Rova liliowazi mbuga ya wanyama, kisha mukaishiwa na mafuta. Mushawasiliana na waokowaji kwa simu ya mrango, mwawangojea, jee, simba waweza kuwarukia ndani ya gari?
a) Haa sasa! Tena pigeni shahada kabsaa.
b) Simba aogopa kuingia ndani ya chombo chochote kilicho zungukwa kikamilifu kama kuta. Kwa hivyo, nyote muko salama salmini.
 
28. Wee ni mzamiaji (daiva) wazmia baharini, ukaja ukakatika na shaza umbali wa futi 20 huko chini - urefu wa kama mara 2 wa dipu ya birika la Mombasa Women's. Kama hukuhisi kule kukatika;
a) Utajuwa tu maana maji yatapiga wekundu kwa damu yako.
b) Hutajuwa kamwe, maana miale ya jua huvuliwa rangi nyekundu ikawa haipenyi tokea umbali baina ya futi 10 na futi 15 ikawa rangi nyekundu haionekani tena, bali huwa kama rangi ya kiza tu. 
 
29. "Shekh Abdalla" aleta tabu kidogo mpaka waif anug'unika na kulalamika kuwa humhudumii ipasavyo. Ufanyeje?
a) Tafta vitu hivi ule - kungu manga na maziwa kama ilivyo ukikaa nae mara ya kwanza baadan nikah. Ukiongeza kula haya pia ni bora zaidi - kunazi, kungu, mabuyu, mbirimbi, pepeta, zambarau, vitoria, mabungo, achari ya maembe, na muhogo wa kuchoma.
b) Kula tikiti, farwala (strawberries), ndizi, tangawizi, thomo, mbegu za tango, matunda ya kiwi, na lozi za mti wa lozi (si lozi za Mkungu).

30. Wataka panda feri Likoni na gari yako. Breki zinfeli, gari lintumbukia baharini. Ufanyeje?
 a) Ngojea Nguvu Mombasa itakuja kukuvuta wewe na gari lako.
 b) Utafanya yafuatayo:-
- Kwanza kabisa, kamata uskani kwa nguvu kwa mikono yako miwili, kisha jipinde mwili ('brace position') sababu ukisleki ule mfuko wa hewa (air bag) ukifunguka waweza kukuumiza vibaya.
- Pili, fungua ukanda wako wa usalama (kama basi ulkuwa unjifunga kamwe kwanza!). Uspofanya hivi utatokaje? Na kama pana watoto garini wasaidie wafunguwe kanda zao.
- Tatu, fungua dirisha chapchapu. Madirisha yakileo yakutumia umeme hufanya kazi kwa dakika 3 ndani ya maji. Kama hayafunguliki vunja dirisha kwa kutumia kitu kama nyundo kama unayo, au livunje dirisha kwa nguvu za mateke ya miguu yako.
- Usishindane kufungua mlango kwa sababu gari likiingia ndani ya maji mlango huwa haufunguki kwa nguvu kubwa sana za maji kukuzuia, hata ukiwa unkula pufya au uwe Taazan wa kuning'inia mitini. Mlango wagari lizamalo haufunguki mpaka gari lote lizame kabisaa ndio waeza kufungua mlango kwa rahisi kabisa. Na ukingoja gari lizame kwanza wafkiri kweli utapona wewe? Kwa hivyo vunja dirisha kijana!
- Toka garini uogelee ufuoni. Ukiwa hujui kuogelea basi wewe kwanza si mzaliwa wa Mombasa, na pili, wavuka wenda fanyaje Likoni?
- Kumbuka, gari lachukua baina ya dakika 1 na mbili kuzama. Kwa hivyo, usianyeanye! 
 
 
31. Teja ampiga ovadozi ya unga na kufla mbali. Jee, ovadozi immuuwaje?
a) Ikiwa ankula pilau kabla kutumia unga.
b) Apunguza kasi ya kuvuta pumzi, na anapovuta pumzi huzivuta kwa taabu; moyo pia wapungua kasi wapiga taratibu sana; ule weusi katikati mwa jicho wafinyika ukawa mdogo sana; mdomo wake na kucha zake zabadilika zawa rangi ya bluu; na misuli yake yatetema na aeza taataa. Aspopata matibabu ya chapchapu (fasti aidi) apotelewa na fahamu (coma) na kufa atakufa tu.
 
32. Muko Maddu mummuokoa mtu azamae. Mushamleta ufuoni, na mukimtizama pumzi havuti wala moyo haupigi. Je, ashakufa?
 
a) Ah, huyu ni wa Kikowani tu sasa.
 
b) Mpatilize na usaidizi wa kwanza (First Aid) palepale, maana moyo usiposhtuliwa baada ya dakika 4 tokea usangae ndio mtu yuwafa. Kwa hivyo, kwanza mpulizie hewa mdomoni chapchapu mara 2, kisha mshtuwe kifua chake kwa dakika 2 nzima, na katika kila nukta moja umbonyeze kifua mara mbili, na kila ubonyezi mmoja ukiskume kifua chake kama sentimita 6 (rula ndefu ina sentimita 30). Kwa hivyo baada ya hizo dakika 2 utakua ushamshtua kifua mara 240. Ukimaliza raundi hii ya dakika mbili nzima, mpulizie tena mara 2, na mshtuwe tena kifua kama ulvyofanya hapo awali, na huku mwaharakisha mwampeleka hospitali. Endelea kumpa usaidizi huu wa kwanza, wala kusangaa usisangae, mpaka aingie mikononi mwa madaktari. Usiseme ni wa Kikowani na wewe si M'ngu wala si daktari. 
 
 
33. Un'pesa mbili tatu wataka jenga mskiti Mazeras. Vipi utapunguza gharama?
 
a) Usijenge choo, wala usitie mifereji ya kutawadhia, wala usitie taa si za kikopo wala si za karabai pia.
 
b) Usijenge mnara wala kuba. Mnara kazi yake ni muadhini alkua apande juu kule akaadhini, sasa magoti ya watu si mabovu tu lakini maspika ya tele si Gede wala si Maganyakulo. Na makuba kazi yake ata hayajulikani kamwe, na walioanzisha haya makuba yenye shakli ya vitunguu kama makuba tuyajuwayo sisi ni maMughali wafalme wa Kiislamu wa India. Kwa hivyo minara na makuba yasipojengwa hapo basi zaidi ya nusu ya gharama za ujenzi zapungua palepale. Na ukisema mskiti si mskiti mpaka uwe na minara na kuba basi wewe hujaangalia historia bado. Mskiti wa kwanza wa Quba ulioko kusini wa mji wa Madina na Masjidun Nabawii mskiti wa mtume S.A.W. wa Madina yote yalikua miskiti simpal kabisa bila ya mapambo haya.
 
34 Kahawa mtini huwa rangi gani?
a) Wee hujuwi kahawa ni rangi gani bwana? Killa mtu ajuwa ni rangi ya buni (brown).
b) Huwa rangi ya kijani ikiwa mbichi, na ikiiva na kuwa tayari kutundwa hugeuka ikawa nyekundu kama nyanya ndogo nyekundu ilioiva vizuri.
 
35. Kahawa mbaya kwako sababu gani?
a) Yakufanya wee mwanamme uzukwe saa zote na kwako mwanamke yakuletea ashki ovyo ovyo.
b) Yapandisha presha.
 
36. Simu maarufu za iPhone zisizokua na vifungo vya kubofea, wafanya mambo yote kwa kukidara kioo chake kwa kidole, kwa nini hazifai Afrika?
a) Lazma uzungumze Kizungu tu, hazipeleki maneno yasokua ya lugha ya Kizungu.
b) Yataka chaji sana, na huko Afrika umeme hawishi kukatika. iPhone zahitaji kuchajiwa kila siku by oda japo simu yenyewe pengine unaizima sku nzimaa wala huitumii.
 
37. Ukila mayai kila siku:-
a) Yazidisha kolestrol mbaya, na yaleta presha na maradhi ya moyo.
b) Ni uzuri sana kukupa protiin, wala hayakudhuru kamwe.

38. Unaamka usiku na chumbani kwako giza. Wataka jua ni saa ngapi na waiangalia saa ya ukutani yenye mikono ya m'garo wa kijani-manjano. Huoni taimu mpaka:-
a) Uikodolee macho kaa glopu.
b) Uiangalie ile saa sio moja kwa moja lakini uitizame kwa kando kidogo, maana kwenye kiza katikati ya macho huwa pofu hakuoni, bali kuonao kwenye kiza katika jicho ni kando kidogo ya katikati ya jicho.
 
39. Waskia mtu huyu ni 'short-sighted' na yule ni 'long-sighted'. Sasa yupi ni yupi?
a) Short-sighted? Ni mtu mpumbavu asiyekuwa na hikma. Na long-sighted ni mzee ambaye ashapitia mengi, mwenye kuona mbali.
b) Short-sighted ni mtu aonae karibu tu, pengine asome buku vile, lakini mbali kuona haoni bila ya miwani. Long-sighted ni lazma awe na umri mkubwa, na aghlabu ni watu walio vuka umri wa miaka arbaini. Watu hawa waona mbali, lakini ukimpa mesej ya SMS anletewa na mtumbawe kwenye simu haisomi bila ya miwani, japo kwenda skuli ankwenda.
 
40. Ushakufa unzikwa kikowani.
a) Haya, tupeleke kilio matangani sasa.
b) Waoza chapchapu, miezi sita ngozi, nyama, mapafu na viungo vishaoza vinkwisha umbakia mifupa mitupu. Na baada ya miaka 20 mifupa pia ishasagika na kupotea, pengine libakie bufuu na meno tu. Ndio makaburini pakijaa rukhsa Kiislamu mifupa yalobaki uyazike kando ulete wengine - "Minka khalknaakum..."
 
41. Dereva maarufu aitwa 'Wan Twenti' alikua?
a) Dereva wa punda maarufu aitwa 'Gaucho' katika mashindano ya "Ambacha Ukucha Punda Huyao" katika Lamu Cultural Festival ya kila mwaka.
b) Dereva wa zamani wa Malindi Bus, na spidi yake akikanyaga lami haishuki 120 kilomitaz pa awa.
 
42. Tiizedi kikosi cha polisi wa usalama kinachotumwa kukiwa na mchafuko na ghasia wa raiyaa barabarani kama cha Kenya chajulikana kama?
a) Kikosi cha 'GSU' ambacho chaitwa 'Jeesyuu' au 'Guum Shekhe Uwende!' ukiwa mjini Darsalama, na chaitwa 'Sungusungu' ukiwa tarafa ya Temeke kwa Wanyamwezi.
b) Kikosi cha 'FFU' (Field Force Unit) ambayo wenyeji wakiita 'Fanya Fujo Uone'.
 
43. Gari kongwe lilochoka sehemu ya Shela ya Malindi linaandikwa?
a) Domo Kaya.
b) Babako Analo?
 
44. Huyu ni samaki tunu:
a) Tini ya mvungu.
b) Juu ya dari (ndivyo watoto wamuitavyo. Khasa aitwa jodari).
 
45. Ngumi ameumbiwa?
a) Muafrika.
b) Afrika nzima hapana taifa wala mila hata moja ya kukunda na kupigana kwa ngumi. Pana kutiana mipweke kwenye kirumbizi cha Amu na visiwani, kisha pana mashujaa wa Shaka Zulu wenye kutumia mikuki na ngao, na pana miereka ya Wanubi wa Sudani Kusini na miereka ya Mawolof wakaao na ndugu zao kina Kunta Kinte wa Kimandingo wa Senegal. Aliyebuni mchezo wa ndondi si mwengine illa ni Muingereza, kama alivyobuni michezo chungu nzima kama:-
- Kandanda
- Ragbi
- Kriketi
- Besboli
- Tenisi
- Tenisi ya meza
- Hoki
- Golfu
- Na michezo mingi mengine.
 
46. Bunduki maarufu ya AK47 yatefuwa risasi ngapi?
a) Zaidi ya alfu.
b) Ina risasi 34 tu, na yatefuwa risasi zote zikesha kwa nukta mbili tu.
 
47. Jambazi ankushkia cha moto ataka kukuhasiri, na huna namna illa ukache. Utakacha vipi, na ukijificha wapi anapotefua utasevu?
a) Bingiria; na jifiche nyuma ya mlango wa gari kama uonavyo kisnema.
b) Kimbia kizigzagi - watu wengi hawana shabaha nzuri, hata wawe wanajeshi; na mlango wa gari hauzuwii risasi, badala yake jifiche nyuma ya ukuta mzito kama vile nyuma ya nguzo ya saruji nzito na changarawe na vyuma (konkrit pila), au mti mnene kama vile muarbaini ulokomaa au mti wa mvule (teakwood), wala usjifite nyuma ya mgomba au mpapayu, na kama uko karibu na bahari au mto na wajua kuogelea basi ruka chomo uzamie, maana risasi hazina nguvu yoyote ndani ya maji umbali wa futi 10 (umbali wa dipu kabisa katika birika la Mombasa Women).

48. Mtu anshikiwa cha moto, aambiwa 'henz ap'. Akitefuliwa risasi ya kichwa imuuwe, ataiskia risasi kwanza ikialika?
a) Haa sasa! Mauti yaja kwa kishindo kikubwa.
b) Hataiskia. Risasi kasi yake inshinda kasi ya sauti mara tatu, kwa hivyo risasi itampiga bongo immalize kabla hajausikia mlio wake. AK 47 Underwater
 
49. Ngome ya Siyu, kisiwa cha Pate, ilijengwa na nani?
a) Si ni Sultan Barghash bwana?
b) Bwana Mataka, Msiu.

Haya, hebu sasa tuyaangaliemambo  ya dini kidogo tukae tuulizane.
 
50. Kina nani ndio wa kwanza ulimwenguni kuanza kunyoa ndevu kulingana na hadithi ya mtume S.A.W.?
a) Wazungu.
b) Mashoga waliopelekewa mtume Lut A.S. awaonye.
 
51. Unaingia mskitini na kwaswaliwa. Ukiangalia unkuta hamna nafasi illa kona ya kule mwisho, jee, uwapitie watu mbele yao ili ufike kule kona ukaunge safu au laa?
a) Usiwapite bwana utawavundia swala zao! Na ukijaribu utazuiwa kwa mkono unyooshwa stret kaa robot, na ukisistiza upite kimabavu waeza pagwa gumi au ukatiwa ndoo ukazirai.
b) Pita tu. Bora tu usipite mbele ya imamu maana hapo ndio utazivunda swala za maamuma wote.
 
52. Ni yapi hatufai kumzuia mtu yoyote kutumia kulingana na maneno ya mtume S.A.W.?
a) Ah, niambie wewe bwana, mimi nlikimbia sana chuo cha Maalim Shaishi.
b) Maji, moto, na choo. Maji mtu akikosa si aeza kufa? Na moto si umpe mtu awashie fegi, bali pengine ni wakti wa shitai ajikinge yeye na femeli yake na baridi wasife au wautumie kuwashia kuni wapike chakula wale. Na mtu akishikika ataka kwenda haja tusimzuie. Wataka mtu ajinyie shekhe? Na mambo haya si hatufai kumkataza Muislamu tu. Ata kafiri tusimzuie kutumia vitu vitatu hivi.

53. Kunwa tembo glasi mbili na kula riba shilingi mbili yote haya mawili ni madhambi makubwa, lakini lipi linamshinda mwenzake?
a) Zile glasi mbili shekhe. Mtume S.A.W. asema, "Alkhamru ummul khabaaith" - "Tembo ndio mama wa mabaya".
b) Hadithi sahihi hiyo ya (a), lakini dhambi kubwa zaidi ni zile shilingi mbili shekhe. Mtume S.A.W. asema, "Riba ina dhambi daraja 73. Daraja moja yake ni kama mtu kuzini na mamake."
 
54. Jee, mwanamke ashusha?
 
a) Hana mzigo wa kushusha, mbona wauliza swala la kijinga? Tena ondoka kamwe hapa, wee kwenu hukufundishwa adabu!
 
b) Ashusha. Mtume S.A.W. aliulizwa swala hili katika maswala 3 na aliyekua Yahudi Abdullah bin Salam hajasilimu hapo bado katika kumtahini mtume S.A.W. kama hakika yeye ni mtume kweli au ajifanyisha tu. Alimuuliza - "Huwaje mtoto saa nyengine akamshabbih babake na wakti mwengine akamshabbih mamake?" Na jawabu la mtume S.A.W. likawa, "Mshusho wa mwanamume ukimtangulia wa mwanamke basi mtoto atafanana na babake, na mshusho wa mwanamke ukimtangulia mwanamume basi hapo mtoto atafanana na mamake."
 
55. Mtume S.A.W. na maswahaba wake na matabiina waliokuja baada yao wakiweza matahajudi kwa wingi, nasi twashindwa na swala za alfajiri. Sababu?
a) Tun mijidhambi mingi.
b) Wote wakifuata sunna kubwa ya qailula - kulala kwa muda mfupi baada adhuhri. Ukienda Spain maduka yote saa nane yafungwa, kila mtu yuko siesta anlala. Na ndivyo wanasayansi pia wanavyotunasihi, kwani binaadamu akitaka kuwa na siha nzuri lazma saa 9 usiku awe anlala na ifikapo saa 9 jioni pia aweke ubavu, japo jioni apate kufumba macho ata kwa dakika 10 pia yatosha.
 
56. Anayesilimu?
 
a) Lazma atahiriwe akatwe mzunga, na lazma abadilishwe jina Joni aitwe Yahya.
 
b) Kutahiriwa ni sunna kubwa ya nabii Ibrahim A.S. na mtume wetu Muhammad S.A.W. akafuata sunna hii. Lakini asilimuye akawa bado ana mzunga wake huku hakumkafirishi, illa kila akimaliza kukojoa lazma ajisafishe kwa uzuri zaidi kutoa mabaki ya mkojo maana mkojo ni najisi. Na hakuna jina lililosilimu - makafiri zama za mtume S.A.W. walposilimu wakawa maswahaba wakubwa mno kama Umar bin Khataab na Khalid bin Waliid hawakubadilisha majina yao.
 
57. Shekh Lai katika darasa zake mskiti wa Mwijabu wakti wa Ramadhani sku moja aliulizwa, "Jee Mtume S.A.W. alkua akifanya kazi gani?" Shekh Lai akaona hili ni swala la stizai maana kila mtu ajua Mtume S.A.W. alkua na kazi gani, basi Shekh Lai akamjibu huyu aliyemuuliza afanyae kazi markiti, "Mtume? Alkua akiuza tamata, viazi, vitunguu, mboga..." Wenye kuskiza darasa (nao ni matineja watupu) waliteka mpaka wakabiringia nde ya mskiti. Lakini turegeshe tena swala hili, jee mtume S.A.W. alkua akifanya kazi gani?
 
a) Akisomesha watoto chuo kimoja mtaani Madina.
b) Mtume S.A.W. kama mitume wote kazi yake yakwanza alkua ni mchunga wanyama (shepherd), kisha akawa biznez man apeleka mali akiuza huku na kule, na alipopawa utume akawa ahubiria watu na akiwaonya ful taim.
 
58. Kiislamu, waweza:
a) Kuwa na mtoto wa kupanga ukamlea na kumfanya ni kama mtoto wako khasa.
b) Huwezi abadan. Kulea ('fostering') khasa mayatima ni jambo zuri mno litakalokutia peponi ukawa jirani ya mtume S.A.W., lakini kumfanya mtoto ni wako ('adopt') tunharamishiwa. Qur'ani yatwambia tuwaite watoto hawa kwa majina yao na ya baba zao waliowazaa. Na ukifa aweza kupokea kitu kutoka kwako ikiwa unmuandika kwenye wasia, lakini haingiii katika fungu la kukurithi kabsaa.
 
59. Mwenyezi M'ngu asema kwenye Qur'ani ya kuwa Suleiman A.S. alvyofika kwenye bonde lenye chungu, Suleiman A.S. alimskia chungu mmoja akiwaambia wenzake waingie kwenye nyumba zao sije Suleiman na jeshi lake likawakanyaga pasi na kutambua (Quran27:18 & 19). M'ngu S.W.T. alpomtaja chungu alimtaja kwa tamshi la kike. Je, Mzungu kulingana na utafiti wake ajua kwamba chungu wote wafanyikazi kama walivyo nyuki wote wafanyikazi wenye kutengeza asali, hawa wote ni:
a) Wakiume.
b) Wakike.
 
Haya, tuangalie mambo ya huku "majuu" sasa.
 
60. Wakaa Omani, wee ni kanzu za mskitini kwenda tu, mavazi ya kawaida Umangani.  Hatari iko wapi?
a) Utaambiwa unkua shekhe sasa, kwa hivyo fanyafanya ushike juzuu na kikoto uwende ukafundishe watoto chuoni.
b) Uspochunga utajishtukia ammi mwili wako um'panuka unkua huyyo tingatinga wapata hivi. Na sababu ni kua huvai suruali ukaziona zaanza kua hazikutoshi tena angalau ukapunguza mapudini na mafaluda nyumbani, na ukifika kwa Ankal Zahor na kwa Anti Zuwena ususie haluwa na viloso vengine.
 
61. Wanawake wa Kiyahudi walioolewa wavaa nini kitwani kufita nyele zao zisionekane na wanaume?
a) Hijabu.
b) Mawigi.
 
62. Kanada, Emerika, na nchi nyingi za Ulaya kuwapigia simu mapai ni 911 wala si 999, na sababu ni:-
a) Hawataki kutufuata sisi Waafrika, wataka kuwa Wazungu kivyao wapendao kuzungua watu, wakae watubabaishe tu.
b) Mtoto mdogo rahisi kutezea simu, akaishika na kupiga 999 na kuwapotezea taimu mapai, lakini apigae 911 huwa ni mwenye akili na andhamiria kweli kuipiga namba hii.
 
63. Bendera ya Emerika ina nyota ngapi, na ina mistari mekundu na meupe mingapi, na kwa nini?
a) Nyota zilioko ni 20 kama sigara 20 zilizomo ndani ya pakti ya sigara, si Emerika ndiko kulipoanza tumbaku ya Wahindi Wekundu (Red Indians) eti! Na mstari uliyoko ni mmoja, kuonesha huku ni kwa walami na mambo yote yanyooka kama barabara moja stret ya lami.
b) Nyota 50, kila jimbo ina nyota moja, na mistari iliyoko ni 13, na kila mstari ulikua ni jimbo la zamani la kwanza lililoasi amri ya Uingereza ya kuwalipa kodi na kuanza vurumai la kudai uhuru.
 
64. United Kingdom (U.K.) ndio Uingereza au Ulaya uisikiayo, na ni nchi moja.
a) Umpata.
b) Laa. U.K. ni muungano wa nchi 4 - Uingereza, Welz, nchi ya Maskoti, na nchi ya maAirish ya Kaskazini. Nchi ya Uingereza ni England, na Ulaya ni Europe.
 
65. Sama inkwisha, kwaigia msimu wa kharifu (autumn). Kwa nini msimu huu pia waitwa 'Fall'?
a) Ndio taimu wanaume wengi wanapo foli kwa mademu. Ni msimu wa mahaba.
b) Majani hupukutika katika miti na mimea yote ikawa haina jani hata moja kama iliyokufa, ispokua miti michache tu kama "miti ya krismasi".
 
66. Ukimwambia mtu "Hebu ni fleshie" huku "majuu" maanake ni?
a) Nipigie simu kisha uikate, nami nitakuregeshea simu tuzungumze.
b) Nivulie nguo.
 
67. Gazeti la 'Habari za Ulimwengu' linfungwa Uingereza sababu ya kutafuta habari za watu kinyume cha sheria. Njia moja ni 'pinging' yakumtambua mtu yuko wapi. Yafanyaje kazi hii?
a) Huu ni uganga Wazungu wanaotumia. Wenda kwa mtazamiaji akakupigie ramli akupe khabari zote.
b) Kila simu ina signal. Signal hizi hupokewa na milingoti kadhaa iliyo karibu zikarusha kwenye setilaiti. Kwa kugundua zile signal zimpokewa na milingoti gani mitatu iliyokaribu kabisa nawewe, mahodari watambua uko wapi khasaa, na wakikosea sana hawakosei zaidi ya umbali wa mita mbili.

68. Chawa "majuu" hakuna.
a) Hamna tawa wala vikoto wala peni la alaamisi.
b) Wanjaa, waitwa 'nits'. Ata watoto wa Waziri Mkuu wa Uingereza Devid Kemron huja msimu wakawa na matawa.
 
69. Wanawake wengi wanyoa nyusi kama malaya wa mwembe tayari, na kunyoa huku kwawavutia wanaume mabarabarani, na pengine hii ndiyo hikma ya Mtume S.A.W. kutuharamishia wanawake wetu wasinyowe nyusi. Huu unyowaji nyusi kwavutia vipi wanaume?
 a) Chapa ya malaya yoyote ni nyusi kunyolewa, kama beji ya skuli wajua huyu asoma Serani na huyu asoma Oshwal.
b) Mwanamke akiwa yuko kwenye "shughul" akifika kileleni nyusi zake aziinuwa bila ya kutaka kama Marilyn Monroe. Wenye kunyoa nyusi zao huwa zinainuka ziko shepu hii saa zote, ndio mana nyoyo za wanaume zikenda mbio.
 
70. Raisi na Waziri Mkuu wa nchi yoyote akisafiri, wakti wa kupanda ndege lazma apande chapchapu. Kwa nini?
a) Wakimbilia soda na keki za bure wakazifakamie.
b) Hii ni katika kujionesha kuwa wana nguvu kamili na siha nzuri, kwa hivyo, "Naondoka, lakini mimi bado ni Simba wa Mtaa n'tarudi karibuni, kwa hivyo usithubutu kukitamani kiti changu."
 
71. Siku ya kuadhimisha Haki za Wafanyikazi ('Leba Dee') yasheherekewa ulimwengu mzima tarehe 1 mwezi wa Mee kila mwaka. Sherehe hizi zilianza nchi gani, na nchi hiyo yaisheherekea siku hii lini?
a) Ilianza Urusi, na yaisheherekea siku hii tena sana!
b) Emerika, na haisheherekei siku hii Mosi ya Mee maana yakhofia mauwaji yalioanzisha kuadhimishwa siku hii mwaka wa 1886 mjini Shikago. Badala yake, washeherekea ijumaa tatu ya kwanza mwezi wa Septemba.
 
72. Wanawake wengi hushikwa na kensa ya matiti. Jee wanaume?
a) Namna gani shekhe, hebu tuhishimiane. Mwanamume anmatiti?
b) Yapatikana, pengine mwanamume mmoja katika kila wanawake 300 wanaopata kensa hii.
 
73. Niko ndani ya gari na miale ya jua yanipiga kupitia tuseme kiyoo cha mbele. Jee, nitapata vitamin D au sipati?
a) Wapata, tena ile pyuwa kabisa.
b) Hupati sababu glasi yoyote yazuia miale ya UVB yasipite. Na ikiwa vioo vyako ni vioo vyeusi (tinted) kama miti na mapajero yao, basi ndio hupati kabsaa!
 
74. Gari lenye kutumia petroli na gari lenye kutumia umeme yaja, utajuwaje na wewe hukuangalia barabara ukidakia?
a) Gari la kawaida la petroli si sote twalijua m'gurumo wake wa "n'g'aan n'g'aan"? Na gari la kutumia umeme saa nyengine lalia kaa transfoma bovu la barabarani, na saa nyengine lalia kama fattaki zikirepuka.
b) Gari la kawaida twalijua m'gurumo wake, na gari la kwenda kwa nguvu za spaki litakuvyoga tu wala wewe hutaliona maana halitoi sauti yoyote kabsaa.
 
75. Kipofu Afrika hukaa nyumbani, na akitoka lazma aandamane na mtu amuongoze sije akakatika na bamba linkaa vibaya kitotoroni, au akagongwa na gari barabarani, au... Jee "majuu", mambo gani 3 yamsaidia kipofu kutembea akenda zake madukani au kazini?
 
a) Wapewa mato ya baiyonik wakaonea nayo; wengine wapawa mtu spesheli amhudumie
 ampeleke mashopping na nin na nini; na wengine hawana haja ya kutoka kamwe bali watumia "National Blind Service" wawapigia simu tu na watu hawa ndio wawendea masupa maket wakawaletea mashoping yao au wakawaletea dawa kemist na mahitaji yao yote.
 
 
b) Vipofu hutoka peke yao wakafuata shughuli zao na husaidiwa na mbwa spesheli akamuongoza njia; au atashika fimbo nyeupe agotegote nayo kulia na kushoto akitembea ili asijigonge na kitu; na sehemu za kudakia barabara zikiwapa watu ishara ya ruhusa ya kudakia zalia mlio kama kengele na vipofu hutambua kuwa waeza kudakia pia.
 
76. Uko "majuu" na unaingia chooni. Ukimaliza haja kubwa watambaje?
a) Tishu shekhe. Na kama uko kwako nyumbani, basi tumia tishu kwanza, kisha tumia maji kutimiza sunna tu.
b) Maji ndani ya chombo chochote, ata kama ni kikombe cha karatasi cha Starbucks. Na ukiwa una maji lakini hayatoshi, basi tamba na maji kwanza, kisha umalizie na tishu mwisho. Hii ndiyo sunna tuliofundishwa na mtume S.A.W.
 
77. 0, 1, 2, 3, n.k. ni namba za Kizungu.
a) Kweli kabisa.  Mzungu ndiye mwenye ilmu yote dunia hii.
b) Laa. Namba hizi ni za Kiarabu. Mzungu namba zake ni zakiTaliani kama I, II, III, IV, n.k. Na sufuri (ziro) walkua hawana kabsaa.
 
78. Lugha ya Kiarabu ni lugha kama ya ilivyo lugha ya kazin zao Mayahudi sababu:-
a) Ni lugha za Kishekhe za kutumika miskitini na mahekaluni.
b) Ni lugha zinazoandikwa kutoka upande wa kulia kuelekea kushoto, na kawaida yake lugha hizi mbili haziandikwi na 'vowels' = a, e, i, o, u (au maarufu zaidi ni fat-ha, kasri na dhumma) kabsaa
 
79. Mswahili ukamfundisha Kispanyola au Kijapani, atashika ipi haraka zaidi?
 a) Kispanyola, maana ina asli ya Kilatino, na lugha ya Kiingereza (na Waswahili wote wankwenda skuli na wajua Kiingereza kidogo au sana) yatumia maneno mengi yaki-Spanyola kama avocado, cockroach, salsa, siesta, negro, vanilla, tornado, na El Nino.
 b) Kijapani. Maana maneno yote ya kijapani yesha na herufi mojawapo katika hizi 5 za 'a, e, i, o, u' kama Kiswahili, kwa mfano mji wa 'Kumamoto' ulio karibu na mji wa 'Kikuchi', au meli ya 'Kishtobe', au panga maarufu la 'Katana'.
 
80. Huku kuandika kwa 'Alphabet' kulibuniwa na watu gani?
 a) Mzungu bwana, vipi wauliza swala la kipuuzi kama hili, alaa!
 b) Waingereza wameazima kwa Mataliani (hicho Kilatini ukiskiacho), na Mataliani wameazima kwa Mayonani (Magiriki), na Mayonani wameazima kwa Mafinishan, watu walioishi sehemu za Lebanon, Falastin na Jordan. Hawa Mafinishan walikua wenye ustaarabu mkubwa, na walkua wana majahazi ya mabiashara miaka 3,500 iliyopita. Mafinishan watokamana na Sam mtoto wa Nabii Nuh A.S. , na ndio mababu wa Waarabu na Mayahudi (wote hawa watu wawili Kiingereza waitwa 'Semites' - watoto wa Sam). Neno "alpha" asli yake Kifinishan ni 'fahali', na neno "beta" ni 'beit' au 'nyumba'.
 
81. Mzungu akwambia ukitaka kujua kuwa una siha nzuri basi ukinya mavi yako:
a) Yawache alama za mtelezo kwenye choo (skid marks), au yaolee (floaters), au yawe meusi.
b) Yafanye herufu za kizungu (alphabet letters) kwa mfano 'S' au 'L'. Mtelezo na mwoleo (jawabu la 'a') ina maana pana kasoro fulani. Soma khabari kwenye mtandao ili ujuwe.
 
82. Wee ni polisi mchunguzi wa mambo ('investigeta') unkuta mwanamke anauliwa nyumbani kwake kwa kuchanjwa kisu mara 50 na vitu kadhaa kama dhahabu na pesa zimeibwa. Lazma:
a) Lengo la kuvamia ile nyumba lilikua ni kule kuiba, na yule mwanamke pengine alijaribu kumzuia mwivi asimuibie ikamtia mahamaki basi akamuuwa kinyama.
b) Lengo la kuvamia ile nyumba lilikua ni kumuuwa yule mwanamke, maana aliyevamia alkua na hasira kubwa mno ('kraimz of pashion') akamdunga visu na kumchanja kupita kiasi ('ovakil'). Kule kuiba ni geresha tu kuwababaisha wachunguzi wa jarima ('kraim investigetaz').
 
83. Pashatokea kutefuliana risasi baina ya makundi mawili ya mtaani. Mchunguzi wa mambo akifika ile sehemu, la kwanza atafuta mavazi ya zile risasi zilizotumika ('spent katrijiz'). Akiziona, huwa ashajua kwamba lazma:
a) Pantumika musaddas ya mzunguko ('revolva').
b) Pantumika musaddas ya kileo ('pistol').
 
84. Panauwawa mtu. Mzungu ajuwa watu wakwanza wakuwashuku ni watu hawa:
a) Majambazi  ('outlaws') halafu atawashuku kina bil qurbaa ('inlaws').
b) Watu wanaokuhusu kwanza ('inlaws') kisha ndio atawashuku majambazi ('outlaws'). Kikulacho? Si kinguoni mwako sku zote.
 
85. Haya. N'na kompyuta yangu. Nimemuandikia barua kadhaa mpenzi wangu. Pengine nikazichapisha ('print'), au nikamtumia kwa barua pepe, au nikazihifadhi ('sev'). Jee, njia pekee ya kuzifutla mbali zisipatikane tena ata ufanye nini ni:
a) Kwa kubofya ufunguo wa 'Futa' (' 'Dilit' kii') uzifute zote.
b) Lazma uikokoe Upelekaji Mgumu ('had draiv', inkaa kama 'wokman' hivi, ya chuma) uiponde ponde kwa nyundo.
 
86. Wee seremala wagongelea misumari katika kumalizia kuubandika mlango au dirisha kisha uupige/ulipige rangi. Kama wataka kazi safi kabisa ('pafekt finish'), utatumia?
a) Misumari ya vichwa vya mviringo ('round head nails').
b) Misumari isio na vichwa ('lost head nails').
 
87. Kuna siku maalum huku "majuu" taka za nyumbani zaja chukuliwa na watu wa manispaa. Swizalendi kila mfuko wa taka huuweki tu nje ya mlango wa nyumba yako bila ya kuubandika stempu. Kwa nini?
a) Ili umpostiye taka zako umtakaye kama unavyo tumana barua zako kwa umtakaye.
b) Hivi ndivyo ulipiavyo taka zako kwa hizi stempu za manispaa.
 
88. Mizunguko ya barabara ('raundabauti') kadhaa ya Omani una mapambo ya nini? Na kwa nini?
a) Vilemba vya Qabusi. Alaa, huyu ni Sultwani eti!
b) Vyetezo. Ubani wa moto ilkua ni biashara kubwa Umani zamani zikitoka kusini mwa nchi. Moshi wa ubani huu ukitumika kwenye dini nyingi "kupandisha" mbinguni du'a za waombaji wa dini mbalimbali, na wengine leo hutumia kwenye kusoma maulidi ya nchume na kupandisha maruhani.
 
89. Riyali 1 ya Kimanga ni dola ngapi za Kiemerika? Na petroli yesha lini Omani?
a) Riyali 1 ni sawa na dola za Marekani 100, na aliye kwambia petroli yesha Omani n'nani mzandik mkubwa wee? Hizi ni nchi za ne'ma, petroli haishi huku.
b) Riyali 1 ni sawa na dola 2 unusu za Emerika. Na petroli Omani yakisiwa yesha mwaka wa 2020 kama asemavyo Mzungu aliyeandikwa kazi ya utafiti huu na Qabusi mwenyewe (waiita hii "2020 Vision"). Ndio Omani pana ukosefu wa kazi kwa yang jenereshen, kila umskiaye ataka kitoa ende "majuu" ya Ulaya na Emerika sasa.
 
90. Wanawake wa Kiislamu wenye kutaka kujihifadhi nafsi zao nchi ya Taki wakienda vyuo vikuu wavaa:
a) Ninja katika kuzidi kucha M'ngu.
b) Mawigi, na sababu raisi wa kwanza wa Taki, Mustafa Kamal Atatuk, aliyeshika hatamu 1923 baada ya kuanguka Ukhalifa wa Uthmaniya, aliukataa Uislamu na mambo ya ukhalifa kabsaa, akawaharamishia wanawake kuvaa mahijabu maskuli, vyuo vikuu, na katika ofisi zote za kiserekali, na siku ya ibada na mapumziko ya Ijumaa akaifanya ni siku ya kufanya kazi, na Jumaamosi ndiyo badala yake akaifanya ni siku ya mapumziko.
 
91. Mzungu asema, "An apple a day, keeps the doctor away."
a) Huu ni wimbo wa watoto wa nasari (nursery rhyme) tu.
b) Ni wimbo wa nasari, lakini tufaha kweli lina mengi mazuri, ata ukitaka kata nguvu ya kutamani kula maakulati upunguze mwili basi pata tufaha ulile.
 
92. Hivi maajuzi palipatikana ushahidi wa filamu kuhusu mauwaji ya kikatili wa raiyaa wa KiTamili kuuliwa na wanajeshi wa Kisirilanka (Sri Lankan Killing Fields) katika vita vya wao kwa wao. Raisi gani wa zamani alipotizama filamu hii palepale aliangua kilio akalia sana?
a) PMR - Percy Mahendra Rajapaksa.
b) CBK - Chandrika Bandaranaike Kumaratunga.
 
93. Feshen ya kuvaa majinzi ya kuonesha matako - Wazungu waziita 'low slung jeans' au 'lowriders' au 'low-rise jeans' au 'hipsters' kwa wanaume na wanawake yahitaji majinzi yakoje na yalianza lini?
a) Majinzi haya lazma yaanze inchi 3 juu ya kitovu, na yalianzishwa na wafungwa wenye suruali bwelabwela zisizo na ukanda wakipelekwa jela ili wasitumia kanda hizo kwa kujinyongea.
b) Majinzi haya huanza inchi 3 chini ya kitovu, na yalianzishwa miaka ya 1960. Dezaina msenge wa Kiingereza aliyejinyonga mwaka jana akiitwa Alekzanda Makwin. Huyu ndiye aliye ihuisha sunna hii ya suruali hizi mwaka wa 2001.
 
94. Kuna watoto wengine ukiwaona hawana shabaha, kwa mfano hawana shabaha ya kurusha mawe, pengine huwa:
a) Mkono wenye nguvu wa kurushia huwa watetema.
b) Mkono wenye nguvu wa kurushia (kwa mfano mkono wa kulia) huwa waongozwa na jicho lenye nguvu la upande wa pili (kwa mfano jicho la kushoto). Mzungu akuita huku "dominant hand and opposite dominant eye", na ukimwambia mtoto achungulie tundu ya mlango ya kutia ufunguo basi sku zote atachungulia na hilo jicho lenye nguvu zaidi.
 
95. Wale wenye kukata miti au kufanya kazi zenye kutumia mashini zenye kelele huvaa vizibio vya mashkio ('iya plagz'), na vizibio hivi:
a) Huzuia sauti zote kabsaa, ukawa huskii chochote kama swala ya tahajudi ilivyo na kimya na utulivu mkubwa.
b) Huzuia kelele nzito tuu zenye kuharibu maskio, na sauti za kawaida hupita kwenye vizibio vile wakaskia sawasawa kama sahani na kawa.
 
96. Uko "majuu" waendesha gari wataka kona, na gari lililokukabili laja na huku lakuwashia 'ful laiti' likazima mara moja mbili, madereva wakuita "kukupigia pass" maanake ni?
a) Wewe! Onyeka! Usithubutu kukona mimi naja au nitakugongla mbali.
b) Nakupa ruhusa, pita wewe kwanza.
 
97. "Majuu" waeza pata mtoto 1 katika kila 4 wanaomaliza kusoma skuli sekandri na...
a) Waingia makazini na kuwa mamilioneya.
b) Bado hawajuwi kusoma wala kuandika.
 
98. Mzamiaji baharini 'daiva' hujuwaje yuko karibu na kuishiwa na hewa kwenye mtungi wake?
a) Ataangalia 'geji' ya mtungi.
b) 'Geji' haiangaliliki mpaka mtungi uuweke tini uusmamie, kwa hivyo ukiogelea iko mgongoni, utaionaje mbalahaji? Ataangalia saa - kama ni yakileo ya spaki atajua moja kwa moja, na kama ni saa yakizamani yenye mikono miwili atasoma 'bezel' iliyoviringa saa. 
 
99. "Majuu" utapata wanawake matineja watembea mabarabarani na mwendo wao ni wa kuwaigiza masupa model kina Tyra, Naomi na Gisele. Matineja hawa huwa watekesha mno maana hakuna mtu wa kawaida atembea hivi barabarani, lakini tineja ajiona ashafika. Mwendo huu mwanamke huutembea vipi?
 a) Atembea huku arusha nyele na kishungi chake upande wa kulia na kushoto, japo nyele si zake bali ni za kubandika za wigi.
 b) Atembeapo, ni kama kwamba nyayo zake zote mbili zakanyaga mstari mmoja uliochorwa barabarani, si kama mtu wa kawaida atembeapo  barabarani ambapo nyayo ya kulia hukanyaga upande wake wa kulia kidogo, na nyayo ya kushoto ikakanyaga upande wake wa kushoto kidogo.
 
100. Taiga ana rangi ya kutu na mistari meusi. Akikaa kwenye majani ya kijani kibichi sana kama migombani au ajifite katika nyasi zilokauka za manjano:-
a) Hafichiki, maana wamuona vizuri kama uonavyo wino mweusi kwenye karatasi nyeupe.
b) Hufichika kabsaa, akawa haonekani kamwe.
 
101. Kaka kola ('Coca-Cola') ilipoanzishwa vitu gani viwili vikitumika zaidi katika kinywaji hiki?
a) Sherbeti na lozi.
b) Koken (mihadharati) na kafin (kutokamana na kahawa).
 
102. Unkuta maiti na viungo vinkakamaa ('rigo motis'). Huyu maiti ankufa:-
a) Sasa hivi.
b) Baina ya masaa 3 na 12 iliyopita.
 
103. Maradhi gani ndio namba 1 inayowalazimu watu wakamuone daktari Emerika? Utaizuia vipi "necherali"?
a) Kumuonea wivu yule umpendae ('jelasi'). Ukitaka kukuzuia ni lazma uwende kwa mganga ukamfunge umpendaye mpaka awe hasikii wala haoni ila kwako tu.
b) Shinikizo la juu la damu ('presha'). Kuizuia necherali ni kwa kufunga (kama saumu za sunna), na kwa kupunguza uzito wa mwili wako.
 
104. Untumbukia kwenye mto/ziwa la maji baridi karibu kuwa barafu siku ya winta na wewe ni swima unayetambulikana. 
a) Utaogelea mpaka ufuoni kama uvukavyo Ngomeni sku zote.
b) Utashindwa kuogelea mita 30, na utakufa kwa shoki na hatataki kama hukuokolewa kwa robo saa.
 
105. Gari ukilipiga 'stati' asubuhi ni;
a) Lazma uwache lishike moto vizuri ili mafuta yapate kuingia kila sehemu ya mashini. Mashini ya gari itakua na maisha marefu ukifanya namna hii.
b) Amka twende. Hakuna cha wom up maana magari ya kileo yana direct fuel injection. Fanya risachi yako kijana!
 
106. Mfursi (Muirani) atavaa kila kitu ispokua hichi tu kwa kukataa kumuigiza Mzungu:-
a) Andawea.
b) Tai.
 
107. Treni zakamata vipi barabara ya reli?
a) Kwa smaku kwenye magudurumu yake, Wazungu wai iita "electro-magnet".
b) Kwa kufura/kujitokeza upande wa ndani wa magudurumu, Wazungu wauita "flange".
 
108. Simu za mkononi (mobaili);
a) Sku zote zakuletea mazuri, kama habari za umpendaye, na masaiba yaliyomfika umtukiaye alioko "majuu", n.k.
b) Zakupa habari nzuri na mbaya, na zaleta kensa kwa miale mibaya ya rediyo (redieshen), kwa hivyo punguza matumizi, na kama huna haja nayo izime.
 
109. Binaadamu akizaliwa na anapokufa;
a) Akizaliwa mikono huyafungua - kama aombaye "Tupe zaka zetu...", na akifa hufunga mikono kama ngumi - kama "Ziraili eeh, roho yangu naizuia, huitwai!"
b) Akizaliwa mikono huyafunga kama ngumi - kama kwamba "Naitaka dunia nzima iwe yangu", na akifa, huifungua mikono yake - kama kwamba "Naondoka ulimwenguni nenda akhera mikono mitupu".
 
110. Haram (piramidi) kubwa kabisa la mji wa Giza ulioko kilomita 20 kusini magharibi mwa Kairo, Misri, lilijengwa kwa muda gani?
a) Ah, maelfu ya miaka ammi.
b) Miaka 15, ikizidi sana, miaka 20.
 
111. Mashini ya kugundua mtu imma yuwadanganya au asema kweli yapima mambo mane. Ni yapi?
a) Una mafua au laa, waskia bukhari au laa, mdomo wako wanuka au laa, na unajanaba au hedhi ama huna.
b) Kasi ya moyo wako unavyopiga, kasi ya damu inavyotembea kwenye mishipa, kasi ya uvutavyo pumzi, na jasho likutokalo vidoleni.
 
112. Gari la ambalensi "majuu" sku zote huandikwa jina lake kinyume (Wazungu wakuita 'back-to-front') mbele ya gari - E C N A L U B M A. Kwa nini?
a) Ukishatoka maklabu ushapiga mtindi au ushazitia stimu tele uweze kusoma A M B U L A N C E sawasawa.
b) Likiwa lataka kukuovateki barabarani huku lawasha mataa na lapiga ving'ora, wewe ukiangalia nyuma kwa kioo chako upate kusoma sawasawa A M B U L A N C E ili ulipishe.
 
113. Uko kwenye ndege ni msafiri. Unaagizia chai. Wapewa, lakini sku zote huwa ladha yake hairidhishi. Kwa nini?
a) Wenye kuwahudumikia (maeyahostez) huwa hawana taimu wakuchemshie wewe tu mtu mmoja maji ya chai mpaka chai ikuridhishe. Wee hujui watu ni wengi na wote wako safarini, kwa hivyo mambo lazma yawe chapchapu?
b) Ndege ikiwa angani presha ya hewa hupunguwa, kwa hivyo maji yachemka digrii 90 sentigredi badala ya sentigredi 100 kama ilivyo kawaida ya chai kuwa nzuri. 
 
114. Maswala mazuri kwetu sisi Waswahili tupendao kuowa na kupigwa mlemba kitwani na kuvalishwa jambia kiunoni.
- Ni nchi mbili zipi zinazojulikana sana kwa majambiya?
- Thamani ya jambiya latokamana na nini?
- Jambiya lenyewe likivaliwa kiunoni ncha yake yaelekea upande wa kulia au wa kushoto?
- Na kwa nini jambia limpinda si kama visu vyengine vilvyonyooka? 
 
a) Hili ndilo jawabu swahihi:-
- Shela na Mbwajumwale ndio maarufu kwa majambia.
- Thamani yake ni shilingi alfu tatu, au alfu mbili mukiskizana.
- Nta ya jambia yaelekea kushoto maanake uko tayari kupigana na bilisi yoyote.
- Jambia limpinda manake wakti wa kuliunda na moto mkali chuma hubeta necherali.
 
b) Hili ndilo jawabu swahihi:-
- Umangani na Ushihirini ndio maarufu kwa majambia (Umangani sana laitwa 'khanjar').
- Thamani yake yategemea sana mpini wake (pale pa kushkia), na Yamani wautengeza mpini kwa pembe za faru na Omani waeza pata zintengezwa na pembe za ndovu. Sadik Al Ahmar kiongozi wa kabila kubwa la Hashid linalompinga raisi wa Yamani Ali Abdalla Swalehe ana jambia lenye thamani ya dola milioni 1.
- Majambia yote yapinda upande wa kulia kimila.
- Na jambiaya limpinda kwa sababu katika matumizi ya kupigana vita, lachafuachafua kwa kukata zaidi na kukhasiri zaidi lifikie figo na chango.
 
115. Pesa za Dinari zinazotumiwa na Kuwaiti, Bahreni, n.k. zatokana na asli gani? Na pesa za kauri (cowrie shells) zikipatikana wapi?
 
a) Dinari ni pesa za dhahabu za tokea kuanza Uislamu, kisha sasa zinkua pesa katika nchi nyingi za Kiarabu. Na hizi Kauri zatumiwa kwa mapambo na si zinjaa ufuo wa bahari wowote bwana? 
 
b) Dinari zilikua pesa za fedha za Warumi zilizotumika miaka 800 kabla ya kuja Uislamu. Na Kauri zilikua zikiletwa na Waingereza waliokua wakiwatumisha Wahindi wazikusanye katika visiwa vya Maldives, kisha kauri hizi zilikua zikisafirishwa na majahazi mpaka nchi za magharibi ya Afrika. Huko, Wazungu wakiwapa Waafrika kauri hizi kama pesa wakizinunulia watumwa wa kusafirishwa mpaka mashamba ya Emerika na Brazili. Kauri hizi hizi pia zilitumika kwetu Afrika ya mashariki kama pesa.
 
116. "Keeping up with the Kardashians"; "Cribs"; "Life in the Fab Lane"; "Sex and the City"; na "Desperate Housewives"; vipindi vyote hivi muviangaliavyo huko "matini":-
 
a) Waswahili walioko "majuu" hawaviangalii vipindi hivi kwa sababu wao ni kama hawa muwaonao kwenye vipindi hivi, waishi kwenye mijijumba kama muionayo katika "Cribs", na wana ma-makeup kama kina Kim Kardashian, na wana wafanyi kazi kama kina Kimora, na deli savis wao ni kwenda mashopping kama hawa "Desperate Housewives" na kulishwa mahoteli makubwa makubwa kama hawa viruka ndia vya "Sex and the City". Waswahili huku "majuu" actually live this kind of life, kwa hivyo hawana haja ya kuangalia maisha ya watu wengine kwenye vipindi kama hivi!
 
b) Waswahili, kama mu'dhamu mkubwa wa watu walioko huku "majuu", waishi kwenye mageto, wako kwenye msoto mtupu. Entatenment yao kubwa ni wakae majumbani baada ya machofu ya kazi ngumu kutwa nzima, wapolee na barafu za ukwaju waviangalie vipindi hivi hivi, huku roho zawatoka midomo wazi kwa kutamani kuishi wao haya maisha ya kina Kardashian.
 
117. Wanawake wetu wapendao kwenda maharusini lazma wapate mikadi, vilua na mashada ya asmini. Je, asmini hupapatua saa ngapi maalum ndio hazitundwi wakati huu? Na zikiwachwa mitini, zapapatua zikakaa hivyo hivyo au zajifunga baadaye? Na mwezi ukiwa tarehe gani ndio asmini zazidi kupapatua zaidi zikatoa harufu yake nzuri zikanenea kote?
 
a) Ah, ngoja n'kamuulize Hamidi Kikuba wa Jamatini Kuze, mambo haya mii n'tayajuaje? N'tashughulika n'pate gomba langu niandame vyandarua na mdundiko wa chakacha nkatie kozi au ntashiriki kuangalia ya kupapatua asmini!
 
b)  Asmini zapapatua baina ya magharibi na ishai mauwa haya yakakaa wazi usiku kucha. Ikifika asubuhi mauwa yake yajifunga tena. Kwa hivyo kutundwa kwake sku zote huwa ni mchana kabla magharibi zikapewa wenye kuzitunga vikuba vyao. Na asmini zikiwa bado zimitini basi hupapatua zaidi usiku mwezi ukiwa mchanga mpaka ukakua ukawa mbalamwezi.
 
118. Afrika ta'mini (inshuwarens) ya gari ni imma thad paati au komprihensiv. Je "majuu" hii ta'mini ikoje? Na pana ta'mini ya vitu vyenginevyo pia?
 
a) Ta'mini si ni ta'mini tu bwana? Kwani aliyeleta magari ni nani? Si ni hao hao Wazungu? Basi na ta'mini pia ni hizo hizo waloleta wao huku ni kama huko "majuu" basi.
 
b) Kinyume na Afrika ambapo ta'mini ni ya gari tu na dereva yoyote mwenye leseni aeza peleka hilo gari, ukifika "majuu" gari lazma liwe na ta'mini yake kama Afrika na dereva pia lazma awe na ta'mini yake kibinafsi. Kwa hivyo humpi tu mtu yoyote gari lako lililo na ta'mini alipeleke mpaka kwanza uhakikishe kuwa huyo dereva umpaye gari lako yeye anayo ta'mini yake yakibinafsi, na ta'mini yake isiwe thad paati bali iwe komprihensiv. Akiwa na thad paati atapeleka gari lake tu bas, hawezi peleka la mtu mwengine.
 
Mambo mengine watu wachukua ta'mini ni vitu vya nyumbani kama t.v. na dhahabu, ta'mini ya moogej ukifutwa kazi upate usaidizi, taamini ya siha upate matibabu hospitali, ta'mini ukisafiri ukipatwa na mkasa, n.k. Ta'mini ni biashara kubwa mno.
 
119. Barafu yaitwaje kizungu? Na pilipili jee? Na jee champali? Na kuweka kitu rahani? Na matangani?
 
a) Hebu skiza bwana. "Majuu" pana maaskirimu tu, hapana cha barafu za ukwaju wala barafu za maziwa. Na hii "pilipili usioila yakuwashiani" na mambo ya mbirimbi ni yahuko kwenu bwana, unsikia? Na Wazungu wote wavaa buti, huku kuvaa viatu vya kimaskini vya champali na kirikiri ni huko kwenu tu, baas. Na mambo ya kueka dhahabu zako rahani na mengine ya kimaskini mahohehaye ni huko kwenu tuu, husikii wewe?! Na mambo ya kushuka ukoo mzima kutoka Siu ukaja ukapaki kwa aliyefiwa Kongowea ni hukoo kwenu Afrika, uslete mambo haya huku "majuu" watu hawana taimu nayo wala hawayajui kamwe!
 
b) Barafu = ice lolly; Pilipili = Chilli pepper (yatamkwa chili pepa); Champali = flip flops;  kuweka rahani = pawn; Matanga = wake. Yote haya "majuu" yatele si kwa makapu bali kwa makontena haswaa.
 
120. Bob Marley atoka mlango gani? Na nini maana ya 'Rastafari'? Marasta waitakidi nini? Na "majuu" ukiwa wewe ni mtoto wa miaka 10 una rasta, utafkuzwa skuli hufkuzwi?
 
a) Bob Marley atoka mlango wa papa. Rastafari ni watu mabangi wenye manyele matimtimu. Marasta waitakidi kuwa bangi ndio mambo yote ndio wapenda msemo wa "Legalize Marijuana". Na una mtoto ana marasta? Skuli atafukuzwa tuu, mpaka ende kwa Bafuri kinyozi wa "No Mistake" akanyolewe makumbi yake, halafu isitoshe, apate na barua ya chifu aje nayo.
 
b) Wazazi wake wote wawili ni wazaliwa wa kisiwa cha Jameka lakini babake alkua na asli ya Muingireza na mamake katika wenye asli za watumwa wa Kiafrika. Ras (kichwa au kiongozi) Tafari (mwenye kuhishimiwa) Makonnen ndiye huyu huyu Haile Selassie alikua mfalme wa Ithiopia aliyependuliwa. Marasta waitakidi kua huyu Haile Selassie aliyewawacha watu wake kufa kwa njaa na ukame badala ya kuomba msaada wa chakula ni m'ngu, au ndiye Isa A.S. aliyerudi ulimwenguni mara ya pili.  Na "majuu" mtoto mwenye marasta kama za maumau awachiliwa asome maana serikali haiwezi kuingilia dini wala itikadi ya mtu wala mtoto.
 
121. Hii 'voodoo' na 'zombie' ni mambo gani haya? Na totovu aliwa kweli?
 
a) Ni shirki tupu ammi. Shirki hii yatoka kisiwa cha Haiti kama vile mambo ya falaki hedkota ni kisiwa cha Pemba. Totovu kuliwa haliwi, bali hutiwa kwenye glopu za taa akawa ni pambo tu majumbani mwa watu.
 
b) Vuduu yatokamana na dini ya uchawi ya 'vodun' ya kabila la maYoruba wa Nijeria. Mayoruba ni kabila nusu Waislamu na nusu Wakristo na yote haya makundi mawili yana shirki tele mpaka leo kama walivyo nayo Waswahili wengi. Watumwa walipopelekwa bara la Emerika, hawa Mayoruba na shirki zao hizi za vodun pia zikafika huko, na Haiti ndio ikawa ndio Maka Chocho yao, wasoma maulidi ya vodun mpaka leo.
 
Hawa mazombi ni watu waliopagawa, na hupagawa wakilishwa kiasi kidogo mno cha totovu wakawa hawajijui wala hawajitambui. Wakti huu ndio wale makuhani wa vuduu wanapo wapeleka watu hawa mizimuni wakawazika wakti watu hawa mazombi ("waliopagawa") wangali hai.
 
Totovu mmoja ana sumu yakuwauwa watu kadhaa, na ndio akawa totovu haliwi ulimwengu mzima ispokuwa na Majapani wanaomtengeneza akiwa bado yuhai maana wakti huu hatoi sumu mpaka afe kwanza, na ini lake ndio baya mno kwa hivyo Mjapani haligusi.

122. Nani aliyeianzisha dini ya Kikalasinga? Alikua na dini gani kwanza? Kisha akatembea akenda magharibi mwa India mpaka akafika wapi? Sasa Makalasinga waamini waungu wangapi? Waswali mara ngapi kwa siku? Na jee, wanazo tabaka (castes) kama Mabaniani?
 
a) Aliyeanzisha ni Bwana Sing, naye alkua Shekhe Mkubwa huko India, na alitembea Bombee akashika jahazi akaja Forodhani akakaa Mkanyageni miezi kadhaa. Sina hakika waamini waungu wangapi khasa, na kuswali waswali mara moja wakenda katika hekalu lao. Na tabaka wanazo, wana vijoho na mabwanyenye, wana na asli dhaifu na watumwa.
 
b) Guru Nanak ndiye alieanzisha dini ya Kikalasinga, na alianza kuwa na fikra za dini mpya 1499 alpokua na umri wa miaka 30. Guru Nanak alkua baniani mwanzo. Alitembea sana, na alifika mpaka Makka. Katika dini yake alisema M'ngu ni mmoja, na waumini waswali mara 5 kwa siku. Hawana kubaguana kwa tabaka kama Mabaniani, bali ni kama Uisilamu usemavyo watu wote ni sawa illa kwa kumcha M'ngu tu.
 
123. Mtoto mdogo watembea nae huku "majuu" mwida anaona mavi ya mbwa barabarani anyashika. Kimbia ukamuoshe haraka spidi tena upesi sababu -
a) Hiyo ni najisi tupu, tena muoshe mara sabaa!
b) Akijishika macho aweza kupata maradhi mabaya yatakayo mpofoa macho, na akiuguwa macho usimpatilize na mapema maradhi yatatembea mpaka kwenye bongo na yamuuwe khasa.
 
124. Ndege hewani yaendeshwa vipi?
 
a) Rubani wa ndege ni kama dereva wa matatu tu. Si matatu ina sukani, klachi, ekselereta, na breki? Ndege ni vivvi hivi, sema inaongezwa mbawa mbili tu.
 
b) Ndege lazma iwe mashini yaipeleka kwa kasi ndiyo iruke. Sasa mambo 3 ndiyo ya kontroli ndege:-
- Sehemu ya nyuma ya mbawa pana 'ailerons'. Hizi wazipeleka kwa uskani kama gari, kulia au kushoto, na kwafanya ndege ilemee upande wa kulia au kushoto, yaitwa ku-'roll' Kiingereza.
- Pili, pana mbawa mbili ndogo zinshikana na mkia. Sehemu ya nyuma katika vimbawa hivi venda juu na chini na Kiingereza zaitwa 'elevators'. Hizi ndizo zifanyazo ndege ielekee juu au iangalie chini, na huku kwaitwa ku-'pitch'. Kontroli yake iko kwenye kuuskuma ule uskani wenyewe mbele au kuuvuta kuelekea kifuani mwako.
- Tatu, mkia wenyewe ulio wima una sehemu ya nyuma inayokwenda kulia na kushoto. Hii yaitwa 'rudder' kama nyuma ya boti au mashua. Hii 'rada' yafanya ndege hewani igeuke kulia au kushoto kama kwamba yateleza hivi. Na ndege ikiwa kwenye ardhi hii 'rada' ndiyo yafanya ibete kulia au kushoto. Kontroli yake iko kwenye pedal mbili za miguu kama klachi. Hizi 'rudder' kwenye mkia yatumika pamoja na 'ailerons' kwenye mbawa kubwa kukonesha ndege hewani.
 
125. Wee mwanamume, wataka vaa shati au flana rangi gani uwatishe wanaume wenzio?
a) Shati au flana yenye rangi ya pinki.
b) Shati au flana yenye rangi hizi mbili - nyekundu na manjano. 
 
126. Nipe siri ya rangi ya nguo za wanawake.
a) "Uzuri wa nyumba si rangi jamani, fungua mlango uingie ndani, pengine utaikuta yavuja pahali." Pana lazaidi?
b) Siri ni nyingi nduu yangu, tizama hizi nne kwa sasa:-
- Mwanamke mnene atavaa nguo hizi ndio zimstiri kula kwake vitumbua vingi - nguo nyeusi au bluu daak (yaani 'dark blue').
- Mwanamke mwembamba atavaa kanzu yenye mauwa makubwa asionekane ni kifefe.
- Mwanamke mwenye nyonga za shakli nzuri (mahipsi yakuvutia) au matako ya buse mwenye haja ya kumtamanisha mumewe kwa kumtongoa shepu yote atavaa kanzu ya mistari yalolala (horizontal) meupe au meusi.
- Mwanamke kifupi nyundo atavaa kanzu ya mistari iliyo wima (vertical) meupe na meusi ili impe urefu.
 
127. Mama Kisomali  aitwaje, na kukumbatia Kisomali kwaitwaje?
a) Mama Kisomali ni "Wariyaa Mama!", na kukumbatia wakuita "Kummbat".
b) "Hooyo" ndio mama, na Wasomali hawana cha kukumbatiana wala maromansi ya mawardi wala ya kupelekeana chakleti, kwa hivyo neno kukumbatia halipo kwenye lugha yao abadan.
 
128. Uzuri wa mwanamke ni:-
a) Waswahili waona uzuri wa mwanamke ni weupe na singa, na of koz mandanda, the biga the beta.
b) Ukifika "majuu" fikra zako zabadilika, waanza kutambua kua shepu ya nyonga zake ni muhimu na yavutia, na kujaa kifua pia, ndiyo hiyo figa 8 eti. Mandanda watambua hayana umuhimu huuo, bali ni mzigo tu wakukalia. Kama hujaja "majuu" fikra zako hazifiki kiwango hiki, wee uko kwenye kuangalia mafurushi ya mahando tu.
 
129. Tafauti ya jokes na tabia ya Muingereza na ya Muemerika ni nini?
 
a) Ah, hawa ni watoto wa mjomba na shangazi, wote ni wamoja bwana.
 
b) Muingereza mara nyingi ana "Dry Humour" - atakuelezea maneno ya kuchekesha lakini uso umfreeze, na Muemerika mara nyingi ni kinyume cha hivi.
 
Na Muingereza atapenda mtu asio na kitu apate (supports the underdog) lakini illa yake ni huyo andadogi akishapata tu atamuonea uhasidi mpaka avundikiwe. Muemerika wapenda mtu aliyefanikiwa - star au hero - wapendelea azidi kun'gara.
 
Na maarufu katika usemi wao Muingereza akwambia, "You know what I mean?" na Muemerika atakwambia, "You know what I'm saying."
 
130. Kensa kubwa ya wanaume yaitwaje? Kawaida daktari aicheki vipi ukienda kwake kwa chekap ya kila mwaka?
 a) Kensa si ni kensa tu? Na haya maneno ya kensa ni maneno mabaya ata usiyataje bwana.
 b) Yaitwa 'Prostate' cancer yenye kuwashika wanaume waliozidi umri wa miaka 50. Hii prostate ni kiungo kiko chini ya kibofu cha mkojo, na kazi yake ni kuyapa manii maji yake yasaidie manii kuogelea katika safari yake ya kuungana na yai la mwanamke. Prostate yachekiwa na daktari atie kidole tundu ya nyuma ahisi kama hiyo prostrate imfura au iko hali yake ya kawaida. Na kwa sababu hii yakutiwa kidole ndio wanaume wengi hudinda kuchekiwa!
 
131. Viatu gani vya kike ni vya ughali kweli, na soli yake ni rangi gani?
a) Mitawanda. Rangi yake ni ya buni maana zatengezwa na mbao.
b) Christian Louboutin, maarufu ni Louboutin tu. Soli yake ni rangi nyekundu.
 
132. Kuzoma na kufanya sura mbovu kwaitwaje kizungu?
a) Mzungu hakusoma chuoni kwa Maalim Twalibu, kwa hivyo atajuwa mambo ya kuzomana?
b) Gurn.
 
133. Jamaa mmoja nilikwenda nae kumuangalia jamaa alipata ajali ya dafrau. Jamaa mwenyewe kwao wanazo mashallah. Tukapewa matufaha matamu mno kula. Basi rafki yangu aliwashwa na tumbo kwa kutozowea kula matufaha, siwajuwa watu wa kula kungu na kunazi hawa? Ni kama jamaa wa Majengo sku moja canter la mayai lilipinduka, jamaa wengine wamsaidia dereva aliyejeruhika na jamaa wengine bizi waiba mayai, wayavunda wakiyala mabiti mabiti hapo hapo saba saba. Anyway, matufaha yaku sampuli ngapi?
 
a) Iko epal la kawaida na epal mengo.
 
b) Matufaha yako sampuli nyingi, mengine mazuri kwa kuyala, mengine kwa kupikia, na mengine yatumiwa kutengeneza mvinyo. Katika matufaha maarufu ni ya kijani ya Granny Smith hutengezewa zaidi epalsos (apple sauce); Red Delicious ni matufaha mekundu matamu, mazuri kwa kuliwa; Golden Delicious ni matufaha rangi ya manjano matamu sana na mazuri kwa kupikwa kwa tanuri (oven); na Gala lina rangi mchanganyiko ya wekundu na manjano, matamu ya kuliwa.
 
134. Maskoti wa Skotlandi wazungumza lugha gani? Wewe Mswahili waeza kuwafahamu?
a) Wazungumza Kiskoti, lugha yao. Mswahili mpaka aisome lugha hii ndio aweze kufahamikiana nao.
b) Wazungumza Kiingereza. Mswahili hatowafahamu wakizungumza kwa sababu lahja yao nzito sana. Mskize mudiri wa timu ya Man U Alex Ferguson akihojiwa hapa. 
 
135. Unaingia kafee Uingereza, uanaagizia "A full English Breakfast", utaletewa nini?
 
a) Utaletewa na weta alovaa maridadi kabisa slesi mbili za tosti zilopakwa blu band ya Ulaya, mayai matano ya bata mzinga, glasi moja ya maziwa, debe zima la orenj juus, na napkini motomoto zenye harufu ya limau kupangusia mkono ukimaliza kula.
 
b) Waeza anza na konfleks na glasi ya maji ya machungwa, kisha ukakalia masosej (nyama ya nguruwe) na mayai ya kukaanga. Mara nyingi hapakosekani Pudini Nyeusi ('Black Pudding' iliyotengezwa na damu ya nguruwe iliyoganda na mafuta yake), maharagwe ya mkebe (baked beans), na mkate wa kukaanga. Na kama unaagizia Full English Breakfast kokote Scotland, utapewa yote haya na uongezewe na "Haggis" ambayo ni mchanganyiko wa moyo, maini, na mapafu ya kondoo, yatiwe chumvi, vitunguu, na poriji, kisha yote haya yatatiwe na matumbo ya huyo kondoo na yachemshwe kwa muda wa masaa 3. Utatapikizana shekhe!
 
136. Mfikiriaji maarufu wa falsafa wa Kioyonani (Greek) aitwa Sokratiz aliyekua na upara na macho balbu ya kukodoka na akitembea mguu chuma, na Mmasedonia maarufu Alekzanda "Mtukufu" aliyetawala Uyonani na nusu ya Ulimwengu mzima mpaka Misri na India, na wapiganaji mashujaa maarufu wa mji wa Sparta waliopigana na dola kubwa ulimwenguni la Kifursi (Persian Empire, Irani ya leo) na wakapata ushindi, woote hawa walikua:-
a) Waume kweli kweli.
b) Mashoga wapendana na waume wenziwao. Ndio Waarabu wamuita Sokratiz "tiizak" (maanake "tuu yako"), na wajuwao wakwambia Alekzanda alkua na maskandalz yasosemeka.
 
137. Nyele za kibinaadamu za kubandika (mawigi) wanawake wengi wapendao kuzivaa, mawigi haya mingi yatoka wapi?
a) Yatoka kwa makabila ya Mayoruba wa Naijeria na Mandingo wa Mali wakinyolewa nyele zao makaburini katika sherehe zao zakiganga.
b) Yatoka India kwenye mahekalu ya Kibaniani wanaponyolewa nyele walizoziwekea nadhiri, na nyengine zatoka Koreya kusini.
 
138. Kwa nini baba akikaa kuwaangalia watoto huskia tafash chapchap hana subra, lakini mama au mwanamke yoyote yule aweza kuwaangalia watoto na akafanya kazi zote bila shida yoyote?
 
a) Si ndivyo akina baba walivyo, hawana subra sini.
 
b) Bongo la mwanamke laweza kushughulika na mambo 5 pasi na shida; akamskiza mtoto wake Zahra amuelezea yaliyotokea skuli, na huku amfunga mtoto wake mwengine kibinda, na mwida huo huo aangalia vitimbi vya "kipochi" Brooke kwenye 'The Bold & The Beautiful' na huku atia dania kwenye mchuzi, na bado aendelea kuzungumza usabasi kwa simu na Asiya aliyoko Dubei. Huku kwaitwa ku-'multi-task'. Mwanamume maumbile yake aweza kufanya jambo moja tu kwa wakti mmoja.
 
139. Kuona kwa jicho au haraka ya mkono, ipi iliyo na spidi zaidi?
a) Jito bwana. Ukipiga jito tu ushaona mpaka kwa jirani.
b) Mkono. Wanao fanya kiini mato (magik triks) wakuonesha mkono mtupu, ukitahamaka mkono una karata na wewe unkodoa mato wala huyapepesi na kuona huoni. Ndio Mzungu akakwambia, "Believe nothing that you hear, and only half of what you see."
 
140. Mbwa aona vipi?
a) Maili kumi.
b) Haoni vizuri. Rangi aonazo ni za samawati na manjano, haoni rangi nyekundu. Ukiwa mbali kidogo ukatulia aeza asikuone kamwe, lakini ukiwa wenda akuona zaidi kuliko binaadamu. Kiungo kinacho "ona" zaidi kwenye mbwa ni pua yake. Mbwa askia harufu kama mara 900 kuliko binaadamu, na hashikwi na mafua akawa na kamasi basi akawa wiki nzima haskii harufu. Kwa hivyo mbwa kuona kwake hategemei macho yake kukuona, bali "akuona" kwa pua yake. Na maskio yake yana ukali wa kuskia mara 40 kuliko sisi binaadamu.
 
141. Uingereza ilipigana vita na Sini (China) miaka mia kabla vita vikuu vya pili, na baada ya miaka 17 ikapigana vita vya pili na safari hii Ufaransa ilimuunga mkono kumpiga Msini. Sababu ilikua?
 
a) Sini ilianza kutengeneza baskili za chuma cha Reli (Raleigh) zenye 'tred maaki' za Uingereza, na vita vya pili vilipiganwa na Muingereza kwa sababu hiyo hiyo na Ufaransa ikaingia kati kwa sababu WaSini walikataa kuwauzia Wafaransa vyura vyakula vya tunu mno viliwavyo mjini Paris.
 
b) Uingereza ilimaskinika kibiashara na ikapeleka huu unga wa heroin wa nchi tawala ya India kuiuza Sini. Sini ilipoona heroin hii haina vitamini yoyote bali yaleta mateja wakaamua kuipiga marfuku. Ndio chanzo cha vita vilivyoshindwa na Uingereza. Vita vya pili vilikua ni paat tuu tu ya ugomvi huu huu.
 
142. Yaliyo pita na yatakayo kuja. Vipi fikra ya mambo haya mawili ilivyo tafauti baina ya lugha ya Wahindi Wekundu ma Aymara wa Chile na Peru ukilinganisha na lugha nyengine?
 
a) Sasa pana tafauti kweli? Si ya jana ni ya jana na ya kesho ni ya kesho Kiswahili na Kizulu na Kikarachiwala na .....
 
b) KiAimani, mambo yaliyopita yako mbele yako, hayako nyuma yako. Na mambo yatakayo kuja hujayaona bado, basi yako nyuma yako. Kwa hivyo Ma-aimani katika fikra hizi wana komon sensi kubwa, mantik tupu. Yaliyo pita wayajua na wayaona waziwazi kama yaliyo machoni mwako, na yatakayo kuja yako kishogoni mwako, nyuma yako, yakuvizia na kuyaona huyaoni, na kukujia yatakujia ghalfla bin vuu, kama mauti yajavyo, hupigiwi simu wala huletewi barua pepe.
 
143. Jino laniuma mamangu mzazi! N'tumie nini litulie?
a) Masala.
b) Karafuu.
 
144. Koo yakuwasha, waskia kaa visu vinkukalia. Ufanyeje?
a) Tafta Strepsilz kemist usonde. Au Kofta dukani kwa Mbaraka.
b) Koroga chumvi kibao na maji, kisha skutua mara kadhaa. Hakikisha maji ya chumvi makali ukiskutua karibu yakuingie kooni mara kadhaa. Regelea mara mbili tatu kwa siku. Kuumwa na koo itakua bai bai tena.
 
145. Vipi kiasi cha kuona kwa simba katika usiku wa giza?
a) Waona ukiwaashia tochi.
b) Waona mara sabaa bora kuliko sisi. Kwa kutumia mn'garo wa mwezi au nyota, waona umbali wa mita 10 hadi mita 15. Na usiku usokua na mwezi wala nyota, pengine mawingu yalofunga kabisa, watumia hisia za kuskia na harufu ya pua kukamata punda milia, swara, twiga na nyati.
 
146. Mimi mtalii nenda zangu nchi ya Kiafrika kutembea. Nipe nasaha kuhusu gari na usiku.
a) Hakikisha gari unlikodisha AVIS.
b) Usiendeshe gari usiku Afrika. Cars and the night don't mix in Africa. Chansi ya kugonga au kugongwa ni kubwa sana. Usalama wako ni wa bahati na sibu. Madereva walevi usiku ni wengi, na magari yasiyofaa kutumika barabarani yanjaa, kwa mfano hayana taa kabsaa, au yana taa moja wee waona motabaiki yaja kumbe kanta laja, au taa za kuashiria kukona hazifanyi kazi, au gari lenda lakini halina breki atumia breki ya geya, n.k. Watafta kifo au kujeruhiwa? Peleka gari usiku usiiku tu Afrika!
 
147. Je, Wazungu wote hawavia vikoi?
a) Kwani ni Washihiri au Wabajuni wale? Mzungu sku zote ni kaunda sut.
b) Ma-skoti wavaa. Waiita 'kilt'. Na wakivaa aghlabu hawavai andaweya. Utamaduni huu wao wauita, 'Going Commando."
 
148. Yemen na Oman hazikutawaliwa?
 
a) Hawa ni wanaume shekhe, walitawaliwa lini? Hawakutawaliwa abadan!
 
b) Walitawaliwa tena walitawaliwa sana, na histri yao ni hii:-
 
Omani 
- ilitawaliwa na MaQaramita (wenye kuandika kwa khati ndogo) ambao ni maShia wa Bahren miaka 931-934.
- Dola ya ki-Uthmaaniya (maTurki) 1581-1588
- Wareno (Portugese) 1515-1650 
- Japo Maskati na Omani walikua dola yenye nguvu na ardhi Mombasa, Zanzibar na Gwadar (Pakistani), kiboko yao ilikua Uingereza. Uingereza ikipiga ngoma Omani yateza chakacha.
- Omani ikamaskinika sana, na baina ya 1850-1870, Wamanga alfu 47 walihamia kutoka Maskati kwenda Unguja, Maskati ikabakia na Wamanga elfu 8 tu.
 
Yamani
- Ilitawaliwa na Mahabashi (kumbuka Abraha na jeshi lake la ndovu lilovamia Makka)
- Ikatawaliwa na Mafursi (Ma-Irani)
- Ikatawaliwa na Makhalifa wa kishia wa Misri
- Ikatawaliwa na Dola la Uthmaniaya (ma Turki)
- Ikapata uhuru baada ya vita vikuu vya kwanza na kuvunjika dola la Uthmaniya, ikawa na mfalme katika kina Hamidadd
- 1962 Yamani Kaskazini ikawa Jumhuriya (yaani hapana tena mfalme, pakawa na raisi sasa)
- Muingereza akaizuia Yamani Kusini 1962-1967, akawa Muingereza apiga tabla na Myamani ateza Sub-ha
- Yamani Kusini wakapata uhuru na kuwa na siasa za Ujamaa kama za Nyerere aliyepotosha watu
- Yamani Kaskazini na Yamani Kusini zikaungana kwa 'Al-Wahda' 1990
 
149. Uko "majuu" waona watu wakupita, waeza bahatisha asli zao kwa kuwatizama tu?
 
a) Nibahatishe kwani hii ni "Omo Pick A Box"? Muulize tu atakwambia.
 
b) Utawatambua hivi:-
- Ukimuona mwanamke mweusi matako fleti na nyonga zisizo na shakli ya kuvutia, fleti (hii ni 'figa wan'), atokapi?
Lazma ana asli ya Kijameka.
 
- Ukimuona mwanamke mweusi anshiba nyuma, atokapi huyo?
Lazma atoka Afrika, kama mwanamke wa Kiganda aloshiba matoke.
 
- Mwanamke akivaa jeket refu winta, usimuone uso wala ngozi ya mwili na ankupa mgongo, waona nyele zake tu nyororo na zan'gara na kila unywele uko pahala pake, ana asli gani huyo?
Lazma ana asli ya Kiafrika - anvaa wigi huyo.
 
- Uko kwenye treni wapita Wazungu waume kwa wake wana nyele rangi ya dhahabu (blondi), wangapi ni necheral?
1% au 2% tu, waliobakia wote watia rangi.
 
- Unampita mwanamume au mwanamke, imma ni Muhindi au ni Mbangoli, utajuwaje?
Mbangoli mweusi kidogo, na sku zote ni huyo mfupi katika wao.
 
- Mkorea na Mchina, ukiwaangalia tafauti iko wapi?
Mkorea ana mifupa ya matavu (cheek bones) yaliyotongoka zaidi.
 
- Mwanamume mwafrika ummuona anvaa suruali yake anaipandisha juu ya kitovu, na aandamana na mwanamke annyoa nyusi zote anchora na kalamu na ana full make-up kila ukimuona ata akenda kununua kibiriti dukani na haripiti nguo abadan, watokapi watu hawa?
Ni Wakongo kutoka Zaire.
 
- Waingiliana na Mwaafrika kwa muda, utatambua vipi kama atoka Naijeria au Gana bila ya kumuuliza?
Mnaijeria ni stret-fowad kama Mzungu, na Mgana ana ajenda nyingi kama Mswahili.
 
- Uko kwenye basi anaingia Mwaafrika ahanikiza samaki basi zima, atokapi huyo?
Atoka Gana.
 
- Kapal - mume na mke, wako kulee, watembea barabarani. Utajuwaje ni Maithiopia au ni Wasomali?
Mara nyingi kapal wa Kisomali mwanamke hutangulia mbele mwanamume akatembea nyuma, na Maithiopia wenda sambamba.
 
- Una shaka mwanamume ni Muithiopia au ni Msomali, utajuwaje?
Muithiopia ankaa kopi kama Mswahili, rangi nyeupe mpaka nyeusi na shakli moja, na mwanamume wa Kisomali ufito na sura kali nyembamba zisopotea.
 
- Una shaka mwanamke ni Muithiopia au ni Msomali, utajuwaje?
Muithiopia ukimuangalia mguu hana supu, hakushiba hamstring, na Msomali ana wowowo wazimu na mara nyingi mdomo wake uko wazi kama mwenye kustaajabu saa zote.
 
- Haya, watu wawili wanaingia. Waambiwa wote ni Wanyaruanda. Mtutsi ni yupi na Mhutu ni yupi?
Mtutsi ana pua ya upanga, na Mhutu pua yake si ya shoka, bali ana pua nene.
 
- Anaingia jamaa singa na mweupe. Ni Mbarawa au ni Muarabu utajuwaje?
Mbarawa ankaa ana wasiwasi wasiwasi hivi.
 
- Wanaingia watu wawili. Mmoja waambiwa ni Mmisri na mwengine ni Mualjeria. Yupi ni yupi?
Alo na kitambi, anyoa nyusi, anuka vitunguu na ana majidai kama ekta mkubwa wa picha Nazi Snema ni Mmisri. Mualjeria sana mwembamba, serias wala usimletee joksi huyo.
 
- Wanaingia watu wengine wawili kwenye basi, moja anuka harufu ya vitunguu na mweninge kari poda, watokapi hawa?
Mturki anuka vitunguu kwa Shish Kabab zao, na Muhindi anuka bizari zao, kama Mswahili utamjua anavyonuka usabasi.
 
- Wamskia mwanamume au mwanamke Mzungu, ammuona mtoto wao anaumia goti na waliita "Nyii" watokapi hawa?
Hawa ni kina "Nyeti" watoka Urusi, "No" kikwao wasema "Nyet".
 
- Panaingia Muingereza na panaingia Muemerika ndani ya treni, tafauti yao waspozungumza?
Muingereza meno yake manjano kwa chai nyingi, na Muemerika meno yake pafekt na ya n'gara kwa kwenda kutengezwa na kung'arishwa kwa daktari wa meno.
 
 
150. 5 O'clock Shadow ni nini?
a) Hiki ni kile kivulivuli chako ukismama juani saa kumna moja jioni.
b) Mwanamume akinyoa ndevu asubuhi, kisha ikifika jioni ashamea ndevu kwa mbaali, hii ndio 5 O'Clock Shadow. Muimbaji kuchu Joj Maikal wa nyimbo ya 'Keyaless Wispaz' ndiyo aliofanya kivuli hiki cha saa 11 jioni kuwa maarufu.
 
Je, mtihani unauonaje, mgumu sio? Haya, maswala 3 haya surwaa ya A,B,C, ya mwisho kabisaa, jitahidi mwandani! Maswala mawili ya kwanza yahusu maradhi, na swala la mwisho ni la wakti (wakti ukate kabla haujakukata, chembelecho rafki yangu mmoja, marhem sasa):-
 
A. Sufuria ni nini, na safura ni nini?
a) Wee huijui sufuria? Kwani huli wewe? Ni chombo cha kupikia. Na hiyo safura, ata sijui n'kwambieje. Maradhi mabaya sana, hata kuyataja usiyataje! Ndio tukatazwa tulpokua watoto tusile chumvi nyingi sini.
b) Sufuria ni ya kupikia utaipata jikoni (yatokamana na neno 'sufur' = ziro, na shakli yake ikiandikwa kirakamu au kinamba 'O' ndiyo hiyo kama sfuria), na safura ni kule kufura kwa mwili, Mzungu akuita 'oedema.' Waeza kuona miguu au mikono ya mtu infura ukafkiri ana matende guu (elephantiasis). Wenye maradhi ya sukari, kwa mfano, wakianza kuharibika figo zao, au mfano mwengine wenye presha ya juu wakianza moyo wao kufeli, hufura mwili. Wazee wetu walkua wajua athari ya kula chumvi kupita kiasi, wakituonya tusile. Chumvi nyingi, kama wewe hujatambua bado, ni sumu.
 
B. Maradhi ya sukari yatumaliza sisi Waswahili. Upimapo sukari ya mwili, kipimo cha swiha chataka kiweje?
a) Kilo moja kama ni sukari ya kumeremeta, na nus kilo kama ni sukari guru, kama ilivyo ukenda dukani kwa Yusufu.
b) Mtu asiye na sukari ambae hajala akipimwa damu ana kiwango cha 4, na muda mfupi baada ya kula ana kama 7.8 kawaida, lakini mtu mwenye sukari kabla ya kula ana baina ya 4-7 kabla ya kula na ana kama 8.5 baada ya kula. Ukimpima mamako na ana 17.9 basi wajuwa hatozimia tuu huyu sasa hivi, bali pana hatari ya kufeli figo akafa kamwe.
 
C. Saa nne wasemaje Kiarabu? Na ukimfundisha mtoto kusoma saa Kiswahili pengine mwakaa huku "majuu", utamfundisha vipi? Mfungo Mosi waanza lini? Bathidee ya Nchume (SAW) ni lini? Na goride la maharusi laanza taimu gani?
 
a) Haya ni maswali ya kuniuliza? Saa nne Kiarabu si ni "Saa arba'a"? Ukimfundisha mtoto kusoma saa Kiswahili s'ku zote mfundishe kwa kikoto. Na Mfungo Mosi si huja kabla ya Mfungo Pili? Na Nchume (SAW) si anzaliwa 26 Aprili, mwaka wa 570 baada ya kuzaliwa Nabii Isa (A.S.), kwa hivyo angalia kalenda yako utie alama na mapema, bathdey yake itakua 26th April, na kila mwaka tarehe ni hii hii, unskia? Na goride la maharusi si laanza ukishamtoa mke chooni kabla ya kumtia chumbani?
 
b) Saa nne Kiarabu ni "Saa 'ashara" kama Kizungu.
 
Ukimfundisha mtoto huku "majuu" kusoma saa Kiswahili mwambie aangalie ule mkono mdogo waashiria namba gani, kisha aangalie ile namba iliyoelekeana na namba hiyo ndio saa kwa Kiswahili, kwa mfano "10 O'clock" inaelekeana na namba 4 katika saa, kwa hivyo wakti sasa ni Saa Nne.
 
Lugha ya Kiswahili tu katika dunia hii ina kuhisabu taimu kwa kutumia mantik. Kukiingia kiza Mswahili aanza kuhisabu, "Saa moja usiku" wakti lugha zote nyengine za Ulimwengu wako kwenye "Saa saba". Na usiku wesha "Saa kumnambili", ili kusudi ikifika Saa Moja asubuhi watu wajitayarisha kwenda zao maskuli na makazini, lakini walimwengu wengine ati wako kwenye "Saa Saba". Simpal, stret foward logik.
 
Mfungo Mosi ndio sisi Waswahili twaanza mwaka mpya, nao ni ukisha mwezi wa Ramadhani tu. Hapo sisi twala Idi na huku tuko kwenye kalenda ya mwaka mpya tena, lakini Muarabu hafuati kalenda hii yetu. Mfungo Mosi Muarabu huwa ndio mwanzo yuwaanza mwezi wake wa 10 wa Shawwal.  New Year ya Arabuni haianzi mpaka uandame mwezi wa Muharram ambao ni mwezi wa Hija ukimalizika kwanda. Kwa hivyo sisi tunamtangulia Muarabu kwa miezi 3 kamili katika kusherehekea mwaka mpya.
 
Bathdey ya Nchume (SAW) n'lini? Tarehe 12 ya Mfungo Sita, hakuna asiyehisi. Mfungo 6 ni mwezi maarufu mno. Waarabu wauita Rabiul Awwal, mwezi wao wa 3 kulingana na kalenda yao. Makka Chocho huhuika wakti huu kwa marashi na kaswida za Maulidi, kila umuonae antinga kizibao chake.
 
Wakti huu wa Mfungo 6 pia ndio utaingia mskitini uskie, "Uzawijuka Nasira Binti Kharusi bi mahrihaa alfen dolaar..." na sinia za haluwa zikizungushwa mskitini. Mfungo 6 ni wakti wa vyandarua vya maharusi na goride la Simba Ropa. Nakuuliza, hapo ulipo upo upo?
 
Katika kujua majira Mswahili anshinda kila mtu ulimwenguni, lakini katika kupoteza wakati Mswahili anshika bendera! "Paukwa? Pakawa! Hapo zamani za kale..."
 
Majawabu ya mtihani
Majawabu yote ya (a) ni ya makosa, na yote ya (b) ndio ya sawa.
 
Videos: