Menu

   

PDF Print E-mail
Waswaha Abroad
 
 
(C) The Full Picture: - 4. Dini
 
muslim hijab
 
Yaliyomo:-
 
a. Miadhini na miskiti
b. Kutukiwa Uislamu (Islamophobia)
c. Kalenda ya swalaa, na kufunga Ramadhani
d. Swala za Ijumaa, na khutba za "Majuu"
e. Shiftwork na kufunga Ramadhani, na Idi isyo na bashasha, na mitihani ya Sama
f. Mkatano
g. Kukaza wanao kuhusu (incest)
h. Nadi na mihadharati
i. Kutokwenda Haji
j. Hapana cha kuandika Wasia
 
a. Maharim wako
b. Safari na Emoshinal Sapot
c. "Majuu" waume hawakimbilii kuoa
d. Wanawake kutafta mabasha
e. Hijabu ni ya roho
f. Kutafta waganga
 
a. Vyuo vya Waswahili hakuna
b. Vyuo vya wengineyo, malipo yake, na uzito wake
c. Wawasomesha mwenyewe
d. Skuli na mafundisho yake ya astaghfiru
e. Hakuna cha "Home Aone"
 
a. Tiivii
b. Mtandao
c. Mitezo ya Xbox na vifaa vyengine vya mawasiliano
d. Maswaiba
e. Father's Day na Mother's Day, na malavu ya Vaentaini
f. Nyama za haramu
g. Uchafu mabarabarani
 
5. Videos
 
 
4.  Dini huku "majuu"
 
Kabla kwenda mbali, ongeza ilmu hapa kwa kitabu hiki:- Islam, A Brief History by Karen Armstrong.
 
Naam, tuanze sasa. Hapa tutaangalia "majuu" inavyo waathiri imani zao hawa Waswahili, na tutaangalia inavyo muathiri mwanamme, halafu mwanamke, kisha inavyo wathiri watoto, na hatimaye inavyo waathiri wote hawa, yaani baba, mama na watoto kwa jumla.
 
 
1. Mwanamme
 
a. Miadhini na miskiti
Mwakaa huko "matini" and you take things for granted. Si alfajiri si ishai, pana muadhini utakukumbusha swala, japo kuna wengi hawaswali illa ijumaa mpaka ijumaa. "Majuu" kote, ispokua Arabuni, hakuna cha muadhini wala cha mteka maji mskitini. Majuu ni nchi hazina mizizi ya Uislamu tokea awali, kwa hivyo miadhini kwa kipaza sauti (spika) hayaruhusiwi kamwe.
 
Na miskiti yenyewe yapatikana miji mikubwa tu kama Toronto, New York, London, Birmingham, n.k. Ingia kijiji cha Loosdrecht kilichoko Holland chenye nyumba 62 hupati mskiti, au pita kijiji cha Keene cha watu elfu 22 kilichoko mkoa wa New Hampshire nchi ya Emerika na hutakuta mskiti. Kwa hivyo ishi sehemu hizi - na pana Waswahili wengi wanaoishi sehemu kama hizi - na maisha yako utayamaliza wala hutaswali kipindi kimoja cha swala mkitini wala hutaswali swala moja ya ijumaa.
 
b. Kuchukiwa Uislamu (Islamophobia)
 Ukienda Switzerland utapata miskiti injengwa kama mfano wa nyumba, haina kuba wala mnara. Kama wewe ni mpita njia si mwenyeji, hutajuwa kamwe kuwa pana mskiti pale. Na sababu ni kuwa minara impigwa marfuku, yaambiwa ati "yaharibu" mandhari ya Switzerland, na katika kampeni ya kupinga athari za kiislamu hivi karibuni walisambaza makaratasi waonesha mskiti wenye minara iliyokaa kama makombora au mizailz, kusudi kutia watu hamasa wapinge katika kura yao athari za Uislamu na miskiti. Huku ndiko katika kule kuuchukia Uislamu, au Islamophobia.
 
Watu wachukia Uislamu na sababu kubwa ni ubaguzi wa rangi (racism) na vyama vya kisiasa kugeuza watu akili kutumia magazeti (media brainwashing) khasa baada ya matukio mabaya ya kumnamoja septemba ya magaidi wachache na siasa zao zisizokua na msingi wa Kiislamu za kuuwa wasio na khatia. Almuhim, sumu hii ya kuchukia Uislamu iliyoenezwa na magazeti na vyama vya kisiasa huku "majuu" ndiyo iliyofanya kua huwezi kujenga mskiti ulio na mnara Switzerland leo kikanuni (by law), lakini Kanisa laweza kuwa na jisalaba maili mbili laelekea mbinguni isiwe neno. Maswizi wantekwa akili kikamilifu.
 
Na Faransa hawataki upige ninja (waiita "burka") au watozwa faini pale kwa pale, au wenda zako jela, au wapokonywa uraiyaa uregeshwe kwenu. Hijabu vaa barabarani, lakini ukifika skuli au jengo la manispaa lazma uivuwe. Na kumbuka hii ni nchi iliyopigania freedom katika mapinduzi ya 1789 mjini Bastille!
 
Kwa hivyo Ufaransa pana uhuru wa mume au mke kuvaa sdiria na chupwi ukaranga mji mzima, lakini hapana uhuru wa kujistiri kwa kuvaa hijabu. Ukitaka vaa hijabu yako nyumbani upike maharagwe na mabiringanya, lakini ukitoka nyumbani mwako hiyo hijabu ivue. Hijabu zinkua ni hijabu za roho tu. Kama uhuru ni huu, jee u-dikteta unkaaje? Na kumbuka kuwa Waislamu si watu ishirin na mbili huku - Ufaransa pana Waislamu wasiopunguwa milioni 5 katika nchi hii ya watu milioni 65.
 
Kushika dini ni kama kushika kaa la moto huku “majuu”. Baada ya September 11, mambo yaliharibika sana. Wanawake waislamu wengine Emerika wakavua mabuibui na hijabu zao kwa khofu, na hivyo hivyo Ulaya. Wanaume wengine wakanyoa ndevu, na Mohamed akajiita Mo. Islamophobia hiyo. Kuogopa/kumbagua Muislamu pasi na kufahamu hii dini - pure prejudice ndiyo hii.
 
Hii ni overview. Sasa basi, tuangalie undani kidogo. Kama wee mwanamume hujitahidi huku "majuu", swala utaiwacha. Hakuna miadhini, hakuna kukumbushana. Si wajua imani huzidi na kupungua saa zote? Imani yako huku "majuu" itapungua na waeza ritadi kamwe kama walvyo ritadi wengi mno waliokuja huku miaka thalathini na arbaini  iliyopita.
 
c. Kalenda ya Swalaa na Kufunga Ramadhani
 Kama hakuna miadhini, lazma uwe na kalenda ikuonesha Jenuari tarehe moja kizungu, na kiarabu siku hiyo ni tarehe 12 Rabiyul Awwal. Ewe! Ndiyo bathdey ya nchume S.A.W. tena! "Allahumma swalli alaa Muhammad! Allahuma swali wasallim aleih!" Ukae utamani marashi ya Haji Mwamadi hapo wee.
 
OK, kalenda ishakupa tarehe ya kizungu na ya kiarabu, sasa uwangalie kifungu cha taimu, ikupe wakti wa swalaa. Alfajiri ni saa kumna moja unusu, adhuhuri ni… Bila ya kalenda kama hii utaswali vipi? Huswali. Kalenda hii ndio itakwambia Ramadhani itaanza lini, au mwezi mtukufu huu utakupita wala saumu hutofunga. Kwani atatoka jirani yako Kapinsky akuambie mwezi wa Ramadhani huo ushaandama?
 
Kalenda huna? Kama huna kalenda labda uwe una saa ya muadhini nyumbani mwako - kila kipindi cha swala kikifika saa hii yaadhini ujue taim imfika uswali nyumbani, au kama umbahatika pana mskiti karibu na kwako uwende ukaswali mskitini.
 
Lau huna kalenda wala saa basi uwe na T.V. yenye channel ya Kiislamu ya nchi uliyoko uwe unaiwasha saa zote, waitizama. Na nchi nyingi huku "majuu" hazina channel hizi locally, maana kukiadhiniwa magharibi Makka utaswali vipi Toronto ambapo bado ni usiku wa manane, hakujapambazuka kamwe?
 
Kwa hivyo kalenda hizi za Kiislamu ndizo zitakazo kwambia mfungo sita ni lini, siku nyeupe ni zipi, n.k. Bila ya kalenda Idi itakuingilia wala hutajuwa kamwe, maana hutaskia mzinga wa Ngomeni wala matakbira ya miskitini. Kama huna kalenda bibi wee basi jua ya kua utakaa na saumu yako ilhali ya kua dunia nzima yala vinono.
 
Na miaka miwili sasa pana Smartphones zenye apps (applications). Utazinunua hizi apps na uzi-download, na utapatak kwenye simu yako kalenda ya Kiislamu na kila kipindi cha swala kikifika simu itakuadhinia. Ikiwa wa yataka haya ya dini basi namna iliyoko ni kama hii. Na simu ikisha chaji? Jua yakua na wewe huswali.
 
Na tusisahau jambo moja muhimu. Ukishajua taim za swala, uko kazini, au uko car park shopping mall, au uko nje ya mji barabarani wapeleka gari, infika taim ya swalaa, kibla kiko wapi? Vigumu sana kutambua, maana "majuu" si kama Msa, waelekea mashariki kwenye bahari/jua linapochomoza kisha wapiga quarter left turn upate kibla. "Majuu" ni almost impossible kujua kibla kiwapi sababu ya misimu (seasons) - jua saa sita kwa mfano haliko mlingoti wima saa sita winta - liko at an angle, na pengine liko dizain ya jua la alasiri au Magharibi huko "matini".
 
Kwa hivyo sharti uwe na compass mkononi, au compass ya mswala, au kwenye smart phone, au una map uchemshe bongo ujuwe kibla kiko wapi. Saa zote "majuu" wachemsha bongo for the simplest of tasks, hujifanyii tu.
 
d. Swala za ijumaa na khutba za "majuu"
 Na je kuswali kwenyewe? Mskitini pengine uutafute uuwendee ijumaa mpaka ijumaa, ikiwa basi kazini uko off ijumaa. Wengine wetu tushakwenda swali khutba ikawadia kidogo, pengine imamu anchelewa dakika tano au ana hamasa basi khutba anairefusha dakika mbili, basi ikabidi tutoke miskitini turudi kazini maana sije tukaletewa taabu bure.
 
Na khutba yenyewe jee? Mskiti wa Kihindi una khutba za Kihindi, wa Kimoroko una Kiarabu kichafu cha lahja ya Kimoroko hakifahamiki, mskiti wa Kisomali una khutba za Kisomali si 'aaniga' zake hizo, mskiti wa Kinaijeria una khutba kwa lugha ya Kinaijeria, n.k. Faida wapata? Hupati. Waondoka na thawabu inshalla bila ya kuonyeka kwa kufahamu mawaidha.
 
e. Shiftwork na kufunga Ramadhani, na Idi isiyo na bashasha, na mitihani ya Sama
 Ramadhani pengine uko shift work wafanya kazi mpaka ma-alfajiri. Tarawehe ikiwa utaamua uswali utaswali peke yako gange. Na hakuna pahali kazini makhsus pa swalaa. Utatafuta sehemu, pengine ya ngazi ya kukimbilia moto (fire escape) ndio ufunge swala yako huko.
 
Na Idi ifikapo waeza kuwa uko kazini uikose kamwe, na kama unwahi kwenda mskitini waeza ingia mskiti ukaskia kimya kikuu, hakuna cha kupiga takbira kwa sauti wala cha kupigana pambaja na wenzio mskitini wala cha kutabasamu na yoyote. Kimnya kimnya utadhani mumfiliwa. Huu ndio utamaduni wa "majuu".
 
Na mukitoka miskitini hakuna cha kupeleka watoto Makadara wala cha kwenda kwa jirani kutoa mkono wa Idi. Mwakaa nyumbani mupigie simu wazee Afrika kama bado wahai basi, mupike birri mule, na muangalie TV. Haya, siku hiyyo, ishapita. 
 
Basi wewe mwanamume uliozaliwa Afrika ukaja huku "majuu" utakosa swala, darsa, mawaidha, na nasaha. Bila shaka imani yako itadhoofika tu. Na ukiwa umeowa ni hatari, na ukiwa ni bachla boy hatari zaidi, maana si mitoto mizurimizuri utakayo yaona Ulaya na Emerika. Malatina wa Kikolombia na Kipueto Riko, maBrazili, maSpanyola, mablondi wa kiLithuenia, maPalestina, Wahindi wa kuteza nachi, n.k. Walimwengu wote wapatikana huku, kwaitwa 'melting pot'. Mitoto ya ng'aaara!
 
Na winta si mwajifinika gubigubi? Sama ikifika Jun/Julai/Ogast huwa ni bikini kwenda, basi Ramadhani iwe katika miezi hii, pana cha kufunga hapo? Mfano ni Ramadhani ya 2011 iko mwezi wa sama wa Ogast kwa Ulaya na Emerika, wakti wa masdiria na ma G-stringi kuruka, ukifunga lazma "mato tini"  wenda huku wajipiga na kuta, laa sivyo utafunga ndaa tu.
 
f. Mkatano
 Na kutiana huku "majuu" ni jambo la kawaida. Waeza ingiana na toto kazini, au madukani shopping, au kwenye traffik barabarani, au uko ngoma, au carnival kwenye chakacha za kilatina. Ni kama ule msemo wa Kizungu, "Any time is tea time", huku "majuu", msemo ni "Any time is sex time", 24 seven. Wamwambia dem, "But don't you see the ring on my finger? I'm a married man." Hapo dem atakuuliza, "What’s that got to do with me?" Yaani yeye ataka mkuni tu, hana haja ya mahaba ya 'long term relationship' wala pesa zako. Mitihani baba.
 
Yaani mambo yalivyo ni waeza kupambana na dem kwenye kuruka majoka, dem ampiga red wine yake hapo klabu ana nyege ile mbaya, basi hapo akajitongoza mwenyewe, ukenda ukalipiga mikwaju garini au kichochoroni na mukamalizana huko hata majina hamujuwani! Hakika ya mambo wajuwao wajuwa na wasiojuwa hawaambiwi.
 
Na nyii oneni Wazungu wote ni intelijent tu. Ukweli ni kuwa wengi hawajui ati condom yazui viini vya ukimwi, na wengi wafkiri ukimwaga nje ndio mwandada hashikwi na mimba. Ujuha na majuha wanjaa, lakini nyii fkirini tu Wazungu smati. Waeza okota ukimwi mjini Vankuuva chap chap kuliko kijiji cha Vanga.
 
Kisha pana kitendo chaitwa 'dogging' huku. Utakwenda usiku na ndinga yako kiunga cha mji maalum chajulikana na mashabik wa mambo haya, au kwenye hadika kubwa, au kona fulani mupaki gari. Dem yoyote atakayejiskia utakaemuona - hamujuani - mwachajiana ndani ya ndinga. Hapo jamaa wengine - hamujuani pia - watakusanyika walizingire gari lenu waangalia jinsi munavyopurana, kama 'live, free sex show'. Kila mtu na raha zake, waliofanya uzinifu, na walioshuhudia uzinifu ule. Mambo ya kihayawani kabisa. Dogging hiyo. 
 
Msekeso mwengine wa ajabu ni 'roasting' au 'gang banging'. Hii ni umlete dem pengine nyumbani kwako umkate. Ukimaliza swaiba yako nae pia ale vitu. Akisha yeye… ukitahamaki mtu 11 washamla dem mmoja. Gang banging hiyo. Haya yako, si kwenye nyumba za watu wa kawaida mitaani, wala si nyumba za kishefa za ma futbola wa Uingereza, wala si mabasketbola wa Emerika. Mambo yako kila pahali.
 
Au uingie kwenye mtandao. Pana website kibao. Mwatiliana, mwida si mwida mwakutana mjini, mwenda pub (bar), mtindi na mjani, mwachkuana sehemu au nyumbani au kwenye gari, shughul. One night stand hizi. Mashia waziita "Mut'ah" - kontrakt za 'temporary marriage' ya one time shot au pengine uwe na huyu "mke wako" kwa wiki baas, kisha kila mtu ashike njia ende zake. 
 
"Majuu" hii. Mkatano hauna mipaka. Kwa hivyo, patakuwa na dini kweli?
 
Na wengine wetu kwa kutafuta tonge kwa njia rahisi twaingia katika kila mtego wa Iblisi. Pana swaiba yangu Khalfani alitoka Msa na sajda yake kubwa kama kungu, kipindi cha swala hakimpiti. Aona laifu ngumu Afrikete na kazi yake ya kutengeza mafriji mabovu, basi akaja akapambana na toto la kifaransa zuri Sheli bichi akaruka nalo. 
 
Khalfani huu ni mwaka wa 19 wako mji wa Angers, kama kilomita 250 kutoka Paris. Ana watoto 6, wote M'ngu anwajaalia ni mabinti, wengine ni wanawali na mdogo kabisa ana miaka miwili, basi mama na watoto wote hawatoki kanisani. Khalfani hana illa majuto - chembelecho Wazungu, to win the world and lose your soul, je, is it worth it?
 
g. Kukaza usioweza kuwaowa (incest)
Mpigo huu wa watu wasioweza kuowana kujuwana kimwili utele Afrika. Pawe pana ammi au mjomba amkaze mtoto wa nduguye. Au ndugu wa kiume - hasa wakubwa - kuwabaka na kuwanajisi nduguze wadogo, wawe ni wavlana au waschana. Na pia papatikana mpaka baba kumlala bintiye.
 
Wengine watapanda hamaki wayakatae haya, lakini ukweli ni kuwa mambo haya yako, wala si uzushi. Wazungu wasemao kweli wakisia baina ya 10%-20% ya femeli vitendo hivi viovu vishatendeka/vyaendelea kutendeka. Sasa basi, kwa Waswahili waliokuja "majuu", mtezo huu uko au hakuna? Uko, tena unzidi kuliko huko "matini".
 
Utakuta ndugu wavlana na waschana walala rumu moja; au utakuta ndugu wavlana walala kitanda kimoja. Mambo haya Uislamu umeyakataza haya. Ikiwa hali ni hii, jua kua pana 60% chans watoto wataparagana hawa. Na kaeni mukijua ya kuwa nyumba za huku "majuu" hazina nafasi - pengine femeli ya baba na mama na watoto 5 wana vyumba viwili tu. Kwa hivyo ni hatasri si hatari? Hatari kubwa iliyoko.
 
Au utakuta bradha akaa na sistake na wake katika nyumba moja, au kaka hakain hapo lakini aingia nyumbani kwa marefu na mapana. Sasa basi, ukosefu wa swala na miadhini kwaleta sahau ya dini. Basi bilisi huingia jamaa akamlala/akawalala watoto wa sista.
 
Au upate buda ana binti yake aliyekuja nae huku "majuu". Binti achipua, na bilisi akamvaa baba bachla boy sasa baada ya kumtaliki mamake binti, akamuingilia na kumuharibu mwanaye mwenyewe. Pengine baba apiga maji au ana uraibu mwengine wa mihadharati. Au upate baba wa kambo anwachiwa watoto wa waif wako nyumbani. Mtoto atakhasiriwa kisha awe blackmailed into silence kwa vitisho mbalimbali.
 
Yote haya yapo. Tusikasirike bure tukapandwa na pufya, mambo haya yaako tokea Afrika, ajuwae ajuwa na asiyejua usimuulize. Na mtu akipata faragha "majuu" mambo huzidi kuvurugika. Pana kesi kadhaa ziko. Na juu ya visho vya Afrika vya mama kutambua kinachoendelea lakini aogopa aibu na kusemwa mitaani, huku "majuu" pana wengi mno katika Waswahili waogopa kuwapeleka mbele hawa wanaume waovu kwa sababu waogopa kutiliana fitina na kuchongewa warudishwe "matini".
 
Kuna kesi tatu nazijua - mojawapo ya Sweden hivyohivyo watoto 5 waliharibiwa na mjomba kisha mjomba akakimbia Emerika. Sistadoo hakumletea kuogopa kesi, lakini alimpasha mkewe kakaye kiumbe muovu. Mkewe naye aliamua kumezea kwa sababu mume ana kazi nzuri ndie alipae moogej. Kwa hivyo pochi linshinda maneno, kitu kinshinda utu.
 
Au utapata mume na mkewe imma waishi pamoja na bradhake mume, au bradhake mume hatoki mle nyumbani. Mume ankwenda kazini, watoto wako skuli, waif afanya chapati jikoni na leso moja naTenge aimba kwenye CD. Fitna itapita haitopita hapo? Ukisema n'nazidi na bilisi ni mimi kumbuka mtume S.A.W. aliulizwa kuhusu kutangamanika mke wa mtu na nduguye mume, akasema huyu "ndiye sumu kabisa."
 
Au kazin aje na short pants ajumuike na waif wa bradha. Patapita fitna hapo au hapapiti? Patapita. Kesi ngapi tuzijuazo za maKanada, Emerika, Dammam, Dubei, n.k.? Kesi nyinigi. Kazin kazin makes a dazin. Kuna kesi za mke akamfumania mumewe amlala "nduguye" walionyonya titi moja. Hawa si hawaowani? Ama kweli wanyonya titi moja na huyu jamaa akanyonya matiti mawili!
 
Na maswahiba pia. Umpeleke waif Emerson Hall kuna harusi huko, kisha rafkiyo Kasimu atam-drop nyumbani sababu wewe wenda gange. Ukishtuka 9 months leeta waif an-drop mtoto Kasimu kopi. Wampa simba nyama akutungie, haya basi.
 
Au umpate baba wa 54 anamuowa waif wa 23, na watoto wa baba huyu same age au wakubwa wa waif mpya na wakaa nyumba moja, huoni pana hatari hapa? Shababu akianguka nae kweli utastaajabu wewe? Huwezi kustaajabu ammi.
 
Mambo haya yako "matini" na "majuu" yako zaidi! Kumbuka huku hapana miadhini, hapana cha swalaa, hapana kukumbuka kufa shekhe.
 
h. Nadi na mihadharati
Ulaya gati si haramu, kwa hivyo gomba kuliwa laliwa na Waswahili. Si London, si Ireland, si.... Watu waambua nadi, na waambua majumbani mwao. Problem zilezile za Afrika zawaandama huku "majuu" - mume akaadimika nyumbani au akawa hafai mpaka mke akatafuta wakumfaa nde, n.k. Emerika tu ndio miraa haramu. 
 
Na uraibu hawishi kwenye miraa. Tembo huku ndio kwao - bars na pubs. Dublin, Ireland, kwa mfano, kila baada ya nyumba mbili au tatu wapata pabu ya kuuza Guinness, na wako Waswahili wanwao mtindi kama wanavyokunwa watu maji. 
 
Isitoshe, "majuu" pana makoken na maheroin - kumbuka Waswahili wengi waliokuja "majuu" walkua ni watu wa mabomu na mabrauni na mabugizi. Wakija huku waendelea na yayya haya, na mihadharati yaliyo zaidi ya haya. Na usione ni "majuu" ya Ulaya na Kanada na Emerika tuu, ukiangalia Omani mambo ya brauni na bugizi yako vilevile, kwani si Irani na Afghani iko umbali wa pua na mdomo tu? Bali nawajua watu khasaa walioshikwa na kufungwa, wengine ni mateja na wengine ni wauzaji wa mabrauni Jidda na makokeni Dubei.
 
i. Kutokwenda haji
Walioko "majuu" ya Emerika wengi wana moogej. Moogej si ina riba, na riba impingwa na lugha kali mno ndani ya Qur'ani? Hawa hawana cha hajji maana wana deni la riba. "Majuu" kwenginkeko wengi walipa kodi, nyumba si zao. Pasentej kubwa sana katika hawa waweza kujikaza wakalipa kodi ya mwezi mmoja wakafunga safari wakenda hijja, lakini ukweli ni kuwa, wengi mno hija hawendi. Ukimuuliza Mansuri n'vipi haji mwaka huu, akwambia, "Ah, bado sijaitwa." Na Mansuri mwenyewe ana 60, haa, ngoja Izraili akuite basi.
 
Ni kama Slemani nliye muona hani muni Costa Del Sol, Spain. Atoka New York, anamuowa mswaha wa Dublin, ankuja nae wala fungate Malaga tunshukia hoteli moja. Katika stori tukaja mambo ya haji. Asema hajenda bado, lakini "iko siku". Iko siku vipije sasa, ilhali yakuwa kuowa ni sunna, lakini kuhiji kwa mwenye uwezo kama yeye ni faradhi? Waeza kweli kukaadhiniwa ukaingia mskitini ukaswali sunna zote, ukimaliza ukatoka usiswali faradhi? Haiwezekani, kwa hivyo mas'ala ya haji, mbona twafanya kinyume?!
 
Kama hapana hijja kwa mwenye uwezo hapana Uislamu hapo. Na angalau ile hijja itakuregesha kwenye kumkumbuka M'ngu, uangalie tena upya hali yako kibinafsi, kisha uangalie hali ya waif na watoto wako na maslahi yao ya kidini. Huna haji? Basi hapana revishen ya maisha yenu huku "majuu".
 
j. Hapana kuandika Wasia
Afrika ukifa urathi otamatik wajulikana apewe nani kwa kiwango kipi kulingana na sheria ya Kiislamu. "Majuu" hakuna mahakama ya Kadhi. Yalobakia ni uandike wasia, uusiye mali yako yagawanywe vipi. Bila ya hivi pengine unkufia kazini na ulipwe fidia (kompenseshen) mambo yatakwenda kwa kanuni ya "Majuu". Kwa hivyo, wasia unakua muhimu uandike maagizo kabla hujenda safari isiyokua na kurudi.
 
Lakini, Waswahili wangapi kuishi waishi "Majuu" lakini hawakuandika wasia (will)? Karibu wote! Pengine ana nyumba, gari, ma T.V., pesa katika akaunti benki, n.k. Mali yote haya yenda kwa waif, au kwa galfren, au kwao na watoto wako, au kwao na wanaharamu wako. Wajua wazee wana thluthi nzima (one third) katika urathi? Mama na baba wagawanye nus bin nus. Na wanaharamu hawarithi kitu, ata konde ya ukwaju pia hawairithi.
 
Sasa uspokua na wasia, na sisi hatuweki wasia, na tukiwa nao huo wasia, basi hatufuati mafundisho ya M'ngu na mtume wake S.A.W, na wewe M'ngu ashakukhitari uko dunia nyengine, huoni una maswala magumu ya kujibu kule? Maana unwadhulumu wazazi wako haki zao.
 
 
 
2. Mwanamke
a. Maharim wako
Mtume S.A.W. alisema, hijja ya mwanamke haiswihi bila ya maharim wake. Mwanamke hafai kwenda kuitekeleza nguzo hii muhimu peke yake au na wanawake wenziwake peke yao. Na hijja ni Ibada kubwa. Lakini juu ya hayo, ni sharti mwanamke ende na nduguye, au babaye, au…, laa sivyo, mwanamke hana hijja bali apata dhambi kamwe. Hebu fkiria, wanawake wangekua wajiendea hijja tu peke yao, si kozi zingechacha? Bila ya shaka. Hikma hiyo.
 
Sasa basi, utakuta baba ampa ruhusa binti yake atoke Lamu ende akasome Nairobi University peke yake. Ukimwambia, "Lakini Mtume S.A.W. asema…" atakwambia hayo tuyawate kwanza. Sasa kule Nairobi University mtoto wa kike peke yake, atapigwa miti hapigwi miti? Tena atapigwa sana! Maneno ya reality haya, na utawaskia wanawake mbio wataruka, "Untufanya sisi wanawake hatuna self control?"
 
b. Safari na Emotional Support
 Maumbile ya mwanamke lazma apate social interaction - kuingliana - zaidi kuliko mwanamme. Mwanamke ataka more emotional support - kuliwazwa, kubembelezwa, n.k. - kuliko mwanamme. Hii wazi kabisa, ata mzungu msomi hawezi kubishana nawe. Kwa hivyo hii vulnerability ya mwanamke - udhaifu wa maumbile yake - ndiyo hikma ya mwanamke asitangamane ovyo masokoni na wanaume, yee akawa auza leso hapa na Yusufu auza kungu ubavuni mwake. Fitna itapita tuu.
 
Mutakubali au mutakataa lakini ajuae ajua na asiyejua hajui. Mtoto wa kike ende akasome "majuu" peke yake - iwe ni Poland, iwe ni India, iwe ni Los Angeles, iwe ni San'aa, au iwe ni boarding school ya wanawake watupu Kakamega, lazma mwanangu atakumtwa tu! Penda usipende, kubali usikubali, lazma kubikwa atabikwa!
 
Kuna mzee mmoja atiwa Hamadi matata sana. Kusoma ansoma lakini Hamadi ankaa Kanada sana - zaidi ya miaka arbaini - mpaka ambadilika mawazo. Hamadi akija Msa kazi yake ni kwenda sokoni asubuhi akanunue viazi na vitunguu vya kupikia huku ambeba kiondo ampelekee mkewe. Ukimwambia, "Hamadi ee, wanaume hawabebi viondo, hii ni Afrika bwana, alaa!" yeye aona ajabu, asema Kanada abeba kiondo sku zote. Watu wakimwambia Hamadi, "Basi beba huko Kanada tu, ukija huku usikiibebe", yee mshipa auliza, "Kwani kuna ubaya gani?"
 
Basi Hamadi huyu ana binti yake Hudaa mwenye akili sawasawa ya kusoma - ammaliza mpaka kolej ana na CPA ya akaunting khaswaa, lakini Hudaa mwenyewe mwenye miaka 26 ni retarded upande wa social interaction, hashiki mita watu wakimpigizia maneno au wakimramba kishogo. Namwambia, "Hamadi, sioni ni aidia nzuri kumtaftia Hudaa kazi manispaa" annijibu chapchapu, "Waogopa atachariwa?!" 
 
Hudaa hashiki mita za abal hakama za watu, atauweza usekretari kweli? Secretary keeps secrets of the office, jee Hudaa atajuwa vipi wakti gani afumbe mdomo asibobokwe? Au akitongozwa na kukosewa adabu, how will she deal with it? Hao wanawake walio sawa haweshi kukosewa adabu na wengi kunyonywa huko maofisini na mameneja, itakuwa huyu Hudaa mtoto wa Hamadi "Kiondo"? Sikumnasihi tena. Utampigia mbuzi gitaa, kweli atainuka ateze? Hatezi.
 
Hamadi mtu mzima lakini ankosa akili, na chuoni alikimbia sana. Kwa hivyo ilmu ya Mn'gu ansema nini na mtume wake S.A.W. anaamrisha nini hana, and adding insult to injury, hata common sense pia hana. Utamkanya asiyekanyika? 
 
Na binti akitaka soma India au Malaysia au Poland, muoze basi ende na mumewe. Au funga safari uwende nae, au ende na kakaake wakasome pamoja. Ukibishana hubishani na mimi shekhe, wewe wampinga Mtume S.A.W., hunipingi mimi. Na ukinletea "logic" atakaye msimamia katika maisha yake ni nani kama hana ilmu ya kidunia basi anayekupa wewe rizki ni nani, wajipa mwenyewe au akupae ni  M'ngu?
 
Na wanawake wangapi wansoma walivyo soma mwishowe wanaishia kuingia jikoni na kulea watoto? Ata "majuu" hawa 'career women' wengi huishia namna hii hii. Mwanamke atakimbia maumbile yake kweli? Haya kimbii. Au ansomea uwakili akifika Afrika mawakili tele hawana kazi imbidi awe mwalimu wa nasari? Kumbuka, asome Bombay au asome Johannesburg, kurudi harudi bikra, simple mathematics. Wangapi waliosoma Thika boarding ya wanawake tu wakatoa mimba tatu tatu?
 
Sasa jiulize, pana mabinti wangapi waliohamia "majuu" haswaa? Waliokuja maKanada na maEmerika, maUlaya na maDubei na maSuudia na… Wengi wankwenda guu mosi guu pili peke yao. Wengine wankimbia bwana zao khaswaa, wakifika tuu wankuja jiatisha wenyewe. Talaka wanzitoa wao wanawake kuwapa waume zao.
 
Wakifika huku "majuu" wataka emotional/financial support huku, wapambane na Sharmake Msomali, au Seifuddin Mpakistani, au Akinwale Mnaijeria, au Kooffi Mghana, au Demitrius Mrashia, au Borowski Mpolish, au Van Daam Mdachi, au Heinz Mjarmani, au Peter Muingereza, au Jordan Muemerika, au Fernandes Mlatino, au D’Souza Mgoa, au Patel-bhai Baniani, au Rankine Mjameka, n.k., wee wafkiri patabakia cha virgin Mary hapa? Zindukana!
 
Na kama mwanamume lazma ajikaze sana ndio aswali, na lazma ajikaze mno asizini, je waonaje hali ya mwanamke mwenye maumbile khafifu, awe na uhuru wa kuingia na kutoka? Utajaza hapa ________.
 
 
c. Majuu waume hawakimbilii kuoa
Ukija huku Ulaya na Emerika utakuta watu hawakimbilii kuoa. Kwa nini? Sababu ni mbili. Sababu ya kwanza ni maisha ni ghaali sana. Sistem ya Kizungu ilivyo, na tunavyo itaba wengi katika sisi wa "matini" tuliokuja juzi na jana, ni kuwa bachela enda tia mzigo wake, na pesa apatazo enda akastarehe nazo atakavyo baada ya kulipa kodi, taa na maji, haya mahitaji ya lazima. Zilzobakia zote ni chapaa za kurusha roho, enda ziwasha moto. Ukiowa babaa hata usiulize hisabu utakazo kuwa nazo, utatokwa na mvi sasa hivi. Tushaangalia kwengine matumizi na hisabu kali mno zilizoko huku "majuu" katika pirika za kuendesha maisha. Ukiowa huwa akiba huna, maisha tait, ni mas'ala ya 'hand to mouth' uisikiayo.
 
Sababu ya pili wanaume hawakimbilii kuowa huku "majuu" ni hizo "rights" karibu zote zenda kwa wanawake. Hizi huwa si "rights" tena bali hizi huwa ni "wrongs". Maana mukikorofishana wakti wowote, ata kama mume yuko katika usawa na mke ndiye aliye na makosa, au mke ndiye aliye na mshkaji anamleta ndani ya nyumba yenu, wale watoto wenda kwa mwanamke sku zote. Na kama muna nyumba ya kukodisha au wailipia wewe mwanamume moogej, basi wewe mume ndiye utakayetoka nyumbani umuachie mke.
 
Mzungu akwambia, "Ladies and Gentlemen." Mwanamke huyo, ashapawa umbele. Kinyume na mila na dasturi zetu. Hata M'ngu katika kuumba alimuumba Adam kwanza, kisha akamuumba Hawaa. Funzo hilo, mantik. Ikiwa utakataa, ulete ubishi, unione imma mii ni zuzu badala au n'na mawazo ya kizamani, kaa ukijua mjinga ni wewe, hapana mwengine bwana. Iangalie lugha ya Qur'ani, na lugha ya hadithi, aashiriwapo mtu aswali, au atoe sadaka, au aoge janaba, au aingie peponi, huwa twaambiwa sote waume kwa wake, lakini kalima inavyo tumika sku zote huwa ni ya kiume, si ya kike. Na utakuta wazungumzao lugha ya Kiswahili wasiokua Waswahili wawataba Wazungu, ukiwaona mikutanoni wawaskia wafungua khutba zao na, "Mabibi na mabwana." Si Kiswahili hiki. Mume humuowa mke, hawaowani bwana!
 
Uislamu jee wasemaje? Wasema mume na mke wakiachana watoto akae nao mke wakiwa watoto ni chini ya miaka saba. Wakiwa ni wakubwa wa umri huu, basi watoto wapawe uhuru wa kuchagua watakaa na nani - mama au baba. Lakini mwanamke akiolewa wakti wowote basi watoto wenda kwa baba yao, no question. "Majuu" hakuna haya. Men are losers, always. Na wengi mno katika wanawake wetu dini hawaijui, na kama waijua, hawaitaki. Wataka kuonesha inda na "pawa" tu, ilhali yakuwa wapinga kauli ya Mwenyezi M'ngu S.W.T. na Mtume wake S.A.W.
 
Kwa hivyo mke hakutaki tena ashakupa wewe talaka akwambia toka ndani ya nyumba "yake". Virago vyako ashakufungia kwenye mfuko wa taka ankuwekea nde ya mlango. Haya, nyumba ushatoka umuatia yeye. Na moogej shekhe uendelee kuilipa vile vile mpaka uimalize, kama ni miaka 20 au 30, wala kuikaa hiyo nyumba wewe huikai, na vitu huvili wewe bali vyaliwa na mskaji mwengine. Ni man-tik hiyo au ni woman-tik hiyo? Hii ndiyo reality ya "majuu".
 
Kwa hivyo jamaa "majuu" hawana moto wa kuoa. Jamaa wataradhia uhuni wa "hit and run." Na mademu wetu waliozaliwa Afrika si twajua majority wapenda pochi? Kwa hivyo kupenda mambo makubwa - wavae nguo za ghali na mabegi ya Louis Vuitton na kuandama maharusi n.k., yule bachla boy ataona laa, haoi Mswahili wala haowi gharama zake. Basi jamaa atakaa na dem wa Kijameka kihuni, wakilala wakiamka wao ni 'lav you lav me' wakitahamaka wakaa kinyumba na uboli  ashamjaza au anamuowa (ili ati asizae mwanaharamu) wala kusilimu demu hasilimu.
 
d. Wanawake kutafta mabasha
Kwa hivyo madem wetu waangukia kutafta mabasha wa asli nyengine wakapigwa miti huko. Pana wanaoirusha kwa washkaji wa kiGhana wasio tahiriwa, wapo waliozaa na washkaji wa kiJameka, pana wanaoishi na maboifrendi kinyumba wakiDachi, n.k.
 
Kwa ufupi, mschana aishi na kukulia katika mazingira haya ya "majuu" yasiyokua na dini, na kwao Afrika pengine alkua hashkiliwi kamwe kuvaa buibui akienda mabichi, ankuja huku ikifika summer time watu wako uchi na yeye pia akupigia skin tait, mini skat, au shorts, na aishi peke yake, basi jua ya kuwa kuparagwa ataparagwa tu, no question.
 
Hawa ni katika walio kuja na wana miaka 15 mpaka miaka 35. Basi pana na walio wadogo wa hawa ambao hawakwenda chuoni Afrika kabsaa, na waliozaliwa hapa sasa. Kumbuka baba most likely hana cha kuswali, na kufunga ni bahati kubwa, na akiwa baba haswali basi huwa hana cha mawaidha, jee mama nae atakuwa hali gani? Na mama ndiye mwalimu wa kwanza kwa watoto wake. Basi utajaza wewe hawa Waswahili yang jenereshen huku wako hali gani.
 
Na pana wale wanawake ova 35. Wengi walikuja huku hawajaolewa, au wanwatwa tokea huko au wanwatwa huku, basi wao ni "free hold" sasa. Hawana cha darasa wala cha kuswali, wewe wafkiri hali yao ikoje? Ndio utaskia "Jiwe moja, halieleki chungu" - mwanamke ana washkaji kadhaa awa-droo pesa kwa kuwapa mwanya. Kwa ufupi biashara ni kupiga umalaya. Reality hiyo.
 
e. Hijabu ni ya roho
 Na kuhusu vazi la Kiisilamu la kujistiri, ata usiulize. Katika wanawake 100, utawapata pengine wawili au watatu tu wavaao mabuibui wakajistiri, na wengine kumi utawapata wanvaa hijabu na koti refu au kanzu ndefu ya kuwakaba kifua, au jinz limemkaba wowowo karibu lipasuke. Kwa hivyo, thamanini katika mia hawana athari yoyote ya Kiisilamu, wao wataka ku-"fit in". Buibui walilivua chooni ndani ya Kenya Airways walpokua wakija. 
 
Na bali kuna wengine wana inda khaswaa, walkua wakikamia kuzivulya mbali hizi hijabu - nyele wazi zintiwa blichi, mini-skirt na micro-skirt hizo, na mpaka hot pants zioneshazo bum cheeks (nusu ya matako). Ukiona stori hizi ni maskhara, uliza aliye "majuu" atakwambia haya ni maneno ya kweli. Na hawa ni wana watoka Vibokoni na Mikanyageni hawa, usione watoka Bombolulu au Maganyakulo.
 
Na nyele wazi wanawake "wetu" watembea nazo huku "majuu", na si Ramadhani, si matalamtana, wakuta mwanamke antia nyongeza za nyele za kubandika. Zaitwa hair extensions. Nyele za plastiki zikitumika hapo zamani, sasa watu wako katika 100% human hair, na mtindo uloingia sasa ni wa Brazilian hair. Nyele wazinunua hizi, $500 kwa rahisi, zenda mpaka $5,000. Wenda saluni, waoshwa nyele zako, kisha hizi nyele za watu washonewa nazo wewe. Ukakaa nazo wee, miezi 2 hadi miezi 6. Si baadhi ya wenetu tuu, au mableki wa huku, Wazungu wengi mno wanazo maana wengi wao nyele zao ni "mbaya" au huwa ni fupi hazimei zikashuka shingoni na mabegani, licha ya kufika mgongoni au kiunoni. Kweli pana cha kuoga janaba hapa au cha swalaa kweli? Hapana.
 
Na hawa wenetu, utakuta wake waloolewa na wanawake waso funga ndoa, na yote mapote mawili haya wakizaa, waeza staajabu ukaskia anzaa mtoto wa kike amuita Tyra, Rhianna, Naomi na Tamara. Majina ya ma Supa Modelz matupu haya. Mwanamke si ana nguvu huku "majuu" kuliko mumewe? Na ukiangalia mama Mswahili, baba pia Mswahili, lakini hapana cha majina ya Shadya wala ya Hudaa hapa. Wala hujaja kwa walioolewa na makafiri moja kwa moja, kama Aisha aloolewa na Mzungu wa Rotadamu hapo Holland, anaanza kwa kubadilisha jina la babake si Aisha Muhammad tena, bali ni Aisha Van Voorst, na amuita binti yake aliyemzaa Heidi, na Hanifa aloolewa na Msirilanka baniani hapo Korki, Ailend, amuitae mtoto wake Madhuri, na Mansura hapo Liechtenstein, ubavuni mwa Swizalend, aloolewa na Mjeru asie amini M'ngu, amuita mtoto wake Devid, n.k. Pana cha swala na cha zaka na cha saumu ya Ramadhani hapa kweli? Utajaza.
 
f. Kutafta waganga
Musione ni wanawake wa huko "matini" tu wenye "kuwaendea mbio" waume zao "watulie". Wanawake wa huku "majuu" pia ni hal kadhalika waingia kwenye shirki vilevile. Pana "waganga" wa Kiswahili - makoni - watafta mafala wakuliwa wawale. Wakaitwa mume hayuko nyumbani wakajaza mahirizi ndani ya mito, nyuma ya pazia, mpaka skrubu za T.V. zikafunguliwa pakatiwa hirizi humo ndani mwa T.V. - maana mume saa zote akiwa nyumbani si huelekea kibla cha T.V. akaiangalia? Bas, aielekee hirizi. Mtu "akawekwa pahali pake".
 
Waganga wa Kiswahili hawatoshi. Pana waKisomali, na waKinaijeria, na wengi mfano huu. Nilimuona madha mmoja wa kikwetu katika hafla aitwa Wahida mjini Minneapolis, Emerika. Huyu madha ana maradhi ya wasiwasi kidogo. Akamuona "shekhe" wa Kisomali anvaa kanzu ya mskitini na kofia ya vito. Basi Wahida akamwambia huyu "shekhe" kua ana wasiwasi wasiwasi na kitwa hakishi kumuuma.
 
Huyu "shekhe" wa Kisomali akamwambia, "You know sister, you have jinn in your head. No problem, I can take it out, easy wallah. You come this address, my house, only you. Come after this barrty (party) tonight, and in morrning, wallah no sheedan (sheitan), everything OK." Shekhe amwambia Wahida maneno haya na huku ammizia mate. Sijui kama Wahida basi alikwenda au alifanya akili.
 
Na si huko kwenu waganga tele? Utawanona mitaani kama nyumba iliyoko karibu na Dil Bahar, mwengine kwenye fleti ubavuni mwa mskiti Konzi, mwengine nyumba mbili mwa mskiti wa Mkanyageni, mwengine... Na advertisement ziko kila mahali. Barabarani Nakumatt Likoni utaona vibao vinaandikwa:-
 
Mganga - hakuna jambo linishindalo.
Mobile 0733 123456
 
Au uwende Mtopanga uone kibao barabarani chasema:-
 
Twapiga Ramli ya Kioo - Nyumba Hii
 
Huku "majuu", utapita na njia zako bas steshen au tren steshen ukamuona mtu bleki anvaa kanzu tepwetepwe la ki West African na kofia nyekundu akakupa 'biznez kaad'. Ukiisoma waona:-
 
Al Haji Madiba
Gifted African Spiritual Healer and Advisor.
I have a solution for black magic, love voodoo, sexual impotency, business transactions, exams, court cases & immigration cases.
I can help you reunite with your loved ones, split unwanted relationships and gambling.
Quick results guaranteed.
Get results first, pay later.
Call this number now:- 123456789.
 
Asili haiwati usuli, na wengi katika Waswahili walio ignorant, khasa wanawake, mambo haya hawakuyaata Afrika, bado wanayo! Shirk na kufru tupu walizonazo. Na chuoni wengi hawakwenda kamwe na ubaya wa u-koni huu (uganga) hawaujuwi.
 
 
 
3. Watoto
a. Vyuo vya Waswahili hakuna
 Watoto utawataftia madrasa, na mitaa mingi katika hii miji huku "majuu" hamna miskiti, skefu hizo madrasa, utavipatapi vyuo? Na ikiwa viko, basi ni vyuo vya Kisomali, au vya Kinaijeria, au vya Kibangoli, au vya Kialjeria, au vya Kimisri, au… Utakuta wote wana lafdhi zao "funny" hivi - kama 'zaa' badala ya 'dhaa' n.k., na wengi waleta mila zao katika dini, na wengi katika watoto wao wana ubaguzi wawabagua watoto wako, mwida mwalimu awafundisha kwa lugha zao kama Kihindi na Kisomali, n.k.
 
Kwa hivyo, vyuo miji mingi hapana, na vikiweko, mitaa mingi hapana, na vikiweko, watoto wako watafundishwa dini na bid'aa na dasturi za nchi za wenye hivi vyuo. Waswahili hawana vyuo - si sisi hatwishi kubaguana, kusingiziana, kuzozana na kutiliana fitina? Wengine walianzisha vyuo, lakini havikukaa, watu walizuliana na kukorofishana sku mbili tu.
 
b. Vyuo vya wenginevyo, malipo yake, na uzito wake
 Na ikiwa wataka wapeleka hivyo vyuo vya Kinaijeria n.k., jee malipo utayaweza? Tupeane mifano. Kwa mwezi (yaani jumaamosi na jumaapili 4, nayo ni jumla ya siku nane tu hizo) ulipe kama waishi mji wa London £20. Haya, basi uwe una watoto 4 wataka kusomeshwa, ni pesa ngapi hizo? £80, ambazo ni 10,000/= za Kenya. Yoyote anaishi London hana pesa hizi zende chuoni tu mtoto afundishwe alif bee kwa masaa 3 au manne tu.
 
Na wengine pesa wanazo, lakini they're short of time. Ni ile game of muscial chairs  tena - baba gange mama yuwa babysit, kisha mama gange baba yuwa babysit, Monday to Friday. Wikendi ikifika wazee wanchoka kweli kweli, sasa iwe ni mambo ya pengine buda kwenda mzigoni na mama awapeleke watoto chuoni na chuoni kwenyewe ni 1 au 2 hours away? Rahisi wazazi kuvunjika moyo watoto wasione mlango wa madrasa.
 
c. Wasomeshe mwenyewe
 Basi ufanyeje? Msomeshe mwenyewe. Haya basi, kama wewe mzazi basi wajua kusoma, na chuoni ulikimbia sana zamani! Na pengine baba ajua kusoma Qur’ani lakini mama hajui. Na baba saa zote yuko kazini, akirudi watoto washalala, na wakiamka watoto hao wenda zao skuli. Watoto watajua dini? Kuijua hawatoijua.
 
Na kama baba ajua kusoma Qur'ani na pia akajitahidi akawafundisha watoto kuisoma, haina maana ya kuwa maadam watoto wajua alif bee na wajua kuisoma juzuu nzima ya amma kwa moyo basi watoto hawa waijua dini, laa bwana. Uislamu pana kujua nguzo za Kiislamu na nguzo za imani, pana kujua ujumbe wa Nabii Ibrahimu na Luqmani na mawaidha aliyomnasihi mwanawe, pana kujua historia ya usunni na ushia, na pana kuwaelezea watoto wako uharamu wa nguruwe na uharamu wa ugaidi na kuuwa pasipo haki. 
 
Kwa ufupi pana kazi, na wengi katika sisi Waswahili ilmu yenyewe hatuna na kuitafuta hatuitafuti. Nilimuona binti mmoja anaolewa Afrika na yeye mwanamwali boko. Chuoni ansoma na amma hakumaliza. Almuradi mumewe naye pia chuoni ankwenda lakini ilmu hakupata, akawa huyu mume apita akimtangazia mkewe aibu zake maduka ya samaki na vibanda vya marungi mpaka mwishowe akamuata. Ex amtangazia alimpata si bikra.
 
Halima atangaziwae na ex wake Rajabu ampatikana ashabastishwa kwao wanazo, basi alipomtoka mumewe kwa khasama kina Halima walileta wafanyi kazi 12 wakabeba kila kitu ndani ya nyumba yao - maana vyoote hapo, t.v., fanicha, mpaka masufuria yannunuliwa kwa pesa za Halima - basi maboi 12 wansafisha nyumba yote yakupangisha, hata karatasi ya gazeti hawakuiwacha.
 
Mwisho wa kwisha huyu Halima akapata safari akenda zake Norway. Nae kule akapambana na korkosi wa Kiswahili aliyezaa nae watoto 3, mwishowe Halima akaatana na mumewe kwa kumuitia mapai mume akatolewa nyumba. Haa niambie, kweli Halima huyu atawafundisha watoto wake mas'ala ya manii na madhii na wadhii au kuoga janaba? Au namna ya mwanamke kujitoharisha baada ya hedhi kwa sunna ya mtume S.A.W.? Au tafauti ya shetwani wa kijini na wa kibinaadamu?
 
Halima hawezi kuwafundisha watoto wake chochote maana hajui cha kuwafundisha maana ilmu hana, kama korokosi aliyempata Norway na ex wake wa awali Rajabu aliyemtangazia aibu zake Afrika.
 
Au kisa cha dem mwengine nilikua nikimjua zamani sana Afrika. Akaniambia sku moja ya kuwa yeye akhiyari afe kwenye ndege, ianguke na ipasuke au iungue. Nikamuuliza kwa nini? Akaniambia sababu atakua jivu na hatozikwa kwa hivyo hatopata adhabu ya kaburi. Na huyu Firdausi anzaliwa Mwembe Kuku na ansoma chuoni kwa Auni. Haya, fahamu ya Firdausi ni hii, haya niambie fahamu ya watoto wake ikoje na Firdausi sasa aishi Denmark mwaka ni wa 18 tena huu?
 
Au dem mwengine anzaliwa Afrika ankuja huku ana eit, sasa ni pandekizi la mama la miaka 32 liko Toronto, laniuliza, "Ati ankal, wako kweli vitunusi?" Jimama jizima hili, lishatoa mimba za haramu mbili so far laniuliza habari za vitunusi! Na lilikua dead serious likiniuliza swali hili.
 
Waswahili kweli wanayo ilmu ya dini ya kisawasawa hata wakiamua wajikaze wawafundishe watoto wao majumbani huku "majuu"? Je, kweli watawaeleza yaliymo kwenye Taurati na ya yaliyomo kwenye Qur'ani pia? Watawelezea watoto wao yapi na wengi wao sehemu ya dini ndani ya mabongo yao pana vacuum tupu? Kweli patatoka chochote cha maana cha kuwafundisha watoto wao ispokuwa pengine ikifika Iddi kuwafundisha kusema "Minal aiddiin" na kujibu, "Minal faziziin, siniina baadal siniinina, awwam baada awwam" tu, bas.
 
d. Skuli na mafundisho yake
Ufaransa pana Waislamu milioni 5 na watoto hawarushusiwi kuvaa hijabu wala buibui kama ilivyo Turki miaka mingi mno; kote huku, wewe binti unkuja nazo wazivua mlangoni. Mtoto asome mpaka miaka 18, na sku zote havai hijabu skuli, akimaliza masomo kweli ataivaa? Abadan havai.
 
Watoto nao wafundishwa kwamba femeli si mume na mke peke yao; yaweza kuwa mume na galfriend wasio owana, waishi kinyumba, na kuzaa na watoto. Au yaweza kuwa baina ya mume na mume mwenziwe, wakitaka, wakapanga watoto. Au femeli yaeza kuwa baina ya misago wawili. Na hii misago yaweza kuzaa wenyewe kwa kupata mshusho wa mwanamume wasiyemjua "sperm donor" au wakapata mtoto wa kupanga, mmoja katika misago hawa akawa "baba" na mwengine akawa "mama".
 
Kwa hivyo mtoto ana miaka 5 skuli afundishwa kuwa msenge au kuwa msago si jambo baya bali ni maumbile khasaa ya kibinaadamu. Je sasa, mafundisho ya Kiislamu akienda chuoni jumaamosi na jumaapili kweli yana chansi ya kumuingia mtoto kweli? No chance.
 
Na pia mafunzo mengine wapatayo skuli ni kuwa "single parent" ni jambo la kawaida. Huyu "mzazi wa kipekee" sana huwa ni mama asiyekuwa na mume au aliochana na mume wake. Watoto wafundishwa kuwa hili ni jambo normal. Kwa hivyo, una binti yako akaririwa jambo hili skuli, sku gani ataona ni muhimu aolewe na ajaribu kukaa kwenye ndoa astirike kama Uislamu unavyofundisha?
 
Au school plays. Watoto wa 'dress up' - drama au plays hizi. Watoto wadogo wa kiume wa miaka 6 waeza vishwa marinda na mavazi ya kike na ma lipstiki, na watoto wa kike wakavishwa majinzi na mashati kama wavlana. Ukiuliza ni vipi hii role-reversal, utaambiwa na walimu hii ni drama tuu, ni matezo tu. Mtoto wa kiume aambiwe, "You look cute like a real girl." Akifika miaka 13 akisema yeye ni chakla, utamlaumu nani?
 
Au hizi mixed schools. Kijana na binti wakaa ubavu kwa ubavu. Una thatiin au fotiin, waanza baleghe na mapele pele ya uso, na dem mwenzio aanza hedhi na kutumia 'Always with Wings' na mwakaa deski ubavu kwa ubavu, jambo hili la kutangamana namna hii ni 'normal' kweli? Mutasoma mambo ya skuli, au mutafundishana biology ya reproduction nyinyi? Uislamu wapinga haya na ni mantik, lakini huku "kuendelea", hamuoni something is very wrong here?
 
Na mujtama woote huku "majuu", jambo la galfren na boifren ni jambo super normal hapa. Tena isitoshe kuwa ni normal, kama huna mshkaji mwapakana mate breaktime kwenye playground basi lazma utashkiwa chuni uambiwe, "You are weird, man!" Peer-pressure itakulazimu na wewe utafte mshkaji japo madrasa wafundishwa M'ngu hayataki hayo.
 
Na skuli ni kuanzia saa moja, au saa mbili, au saa tatu asubuhi mpaka pengine saa tisia, kumi au kumi na moja jioni. Sasa niambie, mtoto gani atakaye swali skuli na kwenda nyumbani lanch hawendi? Mtume S.A.W. asema, "Aswalaa imaadud diin" - 'Swala ndiyo uti wa mgongo (backbone) wa dini'. Sasa hii 'kiss kiss brektaimu' itakufanya utokwe na madhii yaingie surualeni, au pengine utokwa na manii khasaa kwa hivyo mpaka usafishe nguo/uwoge janaba,  kwa hivyo kweli patakua na kusimamishwa swala skuli? Neva.
 
Na wewe wauliza, mtoto akizikidhi swala jee? Winta taim alfajiri ni saa moja asubuhi, alasiri ni saa nane, magharibi ni tisia unusu, ishai ni saa kumi na moja jioni. Swala zote wakati wake ukiingia yeye yuko skuli. Kweli akirudi nyumbani atazikidhi swala zote tano kwa mpigo mmoja, deli savis? Tusindanganyane.
 
Na kuna jambo jengine nyii mulioko "matini" hamulijui kamwe. Mtoto wewe waona ni wako lakini si wako wewe, mtoto ni wa serikali. Mfano mtoto ankosa heshima na adabu, mkanye lakini huna ruhusa ya kumtia kofi wala kumtia mbati. Hayo yawate Afrika.
 
Kuna kidem kimoja cha Kiswahili nakijua, hapo kilikua kibinti cha umri wa miaka 14 sku zile. Sku moja kinnvaa koschumu skuli chataka kufanya swimming mwalimu akakiona kina alama ya kufinywa begani. Kikiulizwa chikasema kilimtolea mamake ufidhuli kidogo akakifinya, basi mwalimu akapeleka ripoti social service ya kiserikali hiki ki-Husna kikachkuliwa.
 
Basi kibinti kikapelekwa 'safe house' kikakaa kule miezi sita, wazee wake hawana ruhusa ya kuwasiliana nae huyu "abused girl". Basi Husna akapewa "freedom" kule, akafundishwa kujipaka ma-makeup, kwenda ma auti usiku, kuwa na washkaji, n.k. Ata kesi ilposmama kotini mschana akakhiyari mwenyewe kurudi kwa wazee wake, lakini kwa sharti la kuwa ana uhuru wa mapana na marefu.
 
Kwa hivyo wazee wa Husna hawakuthubutu tena kumpandishia sauti na kumuudhi, licha ya kumdara. Hivi Husna mwenyewe ana umri wa miaka 27 leo, na watoto alionao ni 4, wote anwazaa na baba tafauti tafauti, hajaolewa hata mara moja.
 
Kwa hivyo, watoto tokea wana umri wa miaka 5 wafundishwa skuli wakikemewa na kutishwa au wakichapwa wapige special namba wawaite soshiyal savis au wapige 911 (999) wawaite mapai. Chembelecho kisa cha mzee Amri wa mtaa wa Kelbuu kule Maskati Umangani. Ati mapai walimletea kujua mzee Amri wakti kijana wake wa miaka 13 asiyesikia alpokwenda kwa mapai kumshtaki mzee Amri alipom-discipline, na mapai ati wakamtia dim Mzee Amri.
 
Mzee Amri hakubishana, alitia Land Cruiser yake moto akenda nyumbani akawakusanya watoto wake wote kutokana na wake zake wanne - watoto 18 kwa jumla - akawabwaga wote kituo cha polisi akawaambia mapai, "Haya, basi twaeni mas'ulia kwa wote hawa, muwaangalie na muwalee munavyoona ndio sawa." Huyyo, mzee Amri akakitoa. Eh, si ilibidi mapai wamtafute na kumtaka msamaha mzee Amri, wakasallim amri.
 
Kwa hivyo "majuu" mtoto ni wako lakini si wako. Wewe ndio "you are towing the line", si watoto. Wewe mzazi ndio wajiogopea sije ukamuudhi kijana au binti wako ukanyang'anywal mbali. Wewe si baba au mama tena - unkua ni 'sperm-donor' au 'egg-donor' tu. Serikali ndio baba na ndio mama. Kama wewe hujuwi, uliza walioko "majuu" wajuao wakupashe kwa nini watoto wao hawana adabu.
 
Na kuna kesi kadhaa, ati kischana cha miaka 13 kinshika mimba, chamwendea mwalimu wake kwa siri, chamuelezea. Mwalimu atamuitia skul naas (school nurse) ampe tembe amize, kisha ende chooni akai flush mimba, pankupya, chepta klozd. Wewe mzazi kuulizwa rai yako huulizwi, wala msiba huu uliomkumba binti yako kupashwa khabari hupashwi. Kwa ufupi, mtoto "ana rights zake"; na ikiwa ni mwili, mwili ni wake yeye si wenu nyinyi, kwa hivyo, amri ya kuilea au kuiharibu ile mimba ni yake yeye kibinti cha umri wa miaka 13 (au 12 au 16 au...), si amri yenu nyinyi wazazi wake. Ushaona wazimu bin kichaa huu?
 
Na kumbuka skuli wana maswahiba wengi walio makafiri. Na nyinyi mulio "matini" hamujuwi maana khasaa ya hili neno "kafiri" ni nini. Hawa si Manaswara. Wengi mno katika Wazungu wa Ulaya si Manaswara. Majority ya watu walio chini ya miaka 50 hawendi kamwe makanisani, si Ijumaa pili wala si krismas. Wendao pengine ni 5% tuu, na majority ni makafiri wasioamini M'ngu kamwe! Kwa watu namna hii, ile tarbia ya kidini ya Kimasihi au ya Kiislamu, hawana kabsaa.
 
Kwa hivyo Krismasi ikifika kwao huwa si siku za ibada hizi bali ni hepi time tu ya kwenda ma-shopping na kupeana zawadi, na Pasaka (Easter) ni taim ya kupeana "mayai" ya chakleti, na Thanksgiving ni siku ya mapumziko (public holiday) na wakti wa kula bata mzinga, na sherehe mia nyenginzo huwa ni namna hii. Majority ya watu huku hawaamini pana M'ngu kamwe!
 
Kwa hivyo, kweli watoto wako watajua sera ya Mtume S.A.W. kweli ilhali ya kuwa tredishen waionayo nyumbani ni tredishen ya mama akitoka ajifukiza kwa udi wa mawardi na akipata simu ya Afrika yakua ammi yao Rishadi M'ngu anamkhitari akae asome "Yaasin" hiyo mumbo-jumbo yao ya kiAfrika halafu aweke na khitima awashe makaa na atie ubani wa moto asome tawasuli.
 
Na kando ya hatari ya huu "uhuru" wa kutombana utakavyo, pana hatari nyengine ya kuingia kwenye ukafiri khaswaa. Maskuli kwafundishwa nadharia (theory) za Chalz Daawin aliyekaa kama tumbiri. Kafiri huyu alisema wanaadamu twatokamana na manyani. Watoto wasiokwenda madrassa, na ata wanaokwenda, wafundishwe ukafiri huu si wengine watapotoka? Asiyekwenda chuoni akatambua tumeumbwa na mikono yake M'ngu S.W.T. kama dini itufundishavyo, huoni waeza teleza wakaingia kwenye kufru? Hatari kubwa.
 
e. Hakuna cha "Home Alone"
Watoka wenda dukani kununua samli huwezi kumuacha mtoto wako wa miaka 10 peke yake nyumbani. Fanya hivyo na jirani sabasi akikusemea utashtakiwa. Ndio watoto "majuu" wachkuliwa kila pahali kama vihenbegi. Hakuna cha mama aliyetalikiwa ankwenda harusini arudi usiku wa manane na amuacha mtoto wake wa miaka ata ya 15 peke yake. Ndio ukaona watoto wadogo "majuu" wakajua mambo ya kiutu uzima haraka wala hawajafisha.
 
Na mara nyingi "majuu" lazma uzijue sharia ova wakili. Ujuwe mtoto humuachi peke yake mpaka ashafika umri wa miaka 16 na isitoshe, umjaji ashakuwa na mechurity fulani. Au ndani ya gari mtoto lazma apewe kiti chake spesheli afungwe na ukanda wake kulingana na urefu wake. Mambo chungu nzima lazma uyajuwe, lakini usisahau, muache mtoto "home alone" kama hushtakiwi na kufunglwa mbali.
 
 
 
4. Baba, Mama na Watoto
a. Tiivii
Hakuna nyumba isiokua na T.V. Ni kawaida kuwa na T.V. mbili au zaidi. Mama huku aanglaia "Desperate Housewives" sitting room, watoto waangalia "Teenage Trouble" vyumbani mwao, na wewe baba huna khabari uko chumbani kwenu waangalia chakacha ya kijameka kwenye MTV, au kama wewe "ni shekhe", basi watizama boli.
 
Wewe, waif, na watoto mwapata mafundisho gani kwenye vipindi hivi? Ugahba, uvutaji wa mjani, na mkatano. Hii ni reality. Kuwe na madrasa au pasiwe na madrasa, uchafu huu ndio utakao wavaa nyoote. Na waif hendi kuswali ijumaa na hajenda darasani au kuskiza waadhi kwenye mtandao sasa ni mwaka wa 24, jee kweli patapatikana athari ya Kiislamu ndani ya nafsi zao au ndani ya nyumba yenu?
 
Au vipindi Uingereza kama Eastenders au Holby City vinavyo angaliwa na watu wengi mno wakiwemo Waswahili, pana mashoga kupanda kitandani wakabusiana. Kijana wako wa miaka 8, jee ni sawa aangalie? Na jee kwako wewe baba, pia ni sawa wewe uangalie? Ni kama Afrika, femeli nzima ikimuona Richi ambusu Brooke Loogan, baba ajifanya, "Audhu Billah" - lakini aangalia huku macho balbu.
 
Au vipindi vya mziki kama vya MTV. Uwaone kina 'Pussy Cat Dolls' waimba, "Don't you wish your girlfriend was hot like me", au Britney Spears aimba "I'm a slave for you", au Beyonce aimba "Naughty Girl", au Rihanna aimba "I'm Unfaithful", au  Akon aimba, "I Wanna Fuck You". Na mitoto mizuri mizuri invaa G-string kuruka, nambie wewe, bintiyo kesho atavaa hijabu kweli? Na mkeo akatazika asivae high heels? Na shababu wako kweli atashika masomo? "Majuu" hii.
 
Bali kuna vipindi vya mkatano khasaa, watu wapigana mikuni, baada ya saa tano usiku mpaka chee kila wikendi, tena chenal za bure! Na tineja ana T.V. yake chumbani, mama anchukuliwa na usingizi siting room, na baba yuko nait shifti, atarudi nyumbani saa 1 ya asubuhi, haa niambie, pana uwongofu hapa au pana kupotoka tu?
 
Si vipindi tu vya ulaanisi. Bali advertisment kibao za kuchafua watu akili. Advertisement waeza kuona ya gari linshiba nyuma upande wa buti (Renault Megane) ukaona mwanamke nae akatisha matako na nyimbo yaimba, "Shake that ass!"
 
Na jee advertisement za mtindi? Kibao. Kama ya "Tuska Export - Nyama Choma!". Waona glema (glamour), ma night life, na tembo. Powerful connection hiyo.
 
Na advertisement za tembe za kutoa mimba. Kalale na utakaye lala nae, lakini akikinyaka tembe za kukitema ni hizi mwandada. Zaitwa 'Morning After Pill'.
 
Na pana advertisement za kuchukua mikopo - easy loans. Ununuwe fanicha, gari, uwende holiday, n.k. Na uchukuwe ma-credit cards, na ukiingia katika bahari hii na riba yake, uko kwenye khasara, hutoki kwenye matatizo ya deni.
 
Au ata muangalie kipindi cha "Deal or No Deal" - ni kama kama "Omo Pick A Box". Utaona ni kipindi kisichodhuru, innocent, lakini kwa hakika ni kipindi cha kamari. Na kuna waraibu wa kamari "majuu" kibao, gambling addicts mpaka wende Gambling Anonymous utafte matibabu. T.V. zina advertisement kibao za kamari - mashindano ya farasi, magari, mabaiki, lottery, n.k.
 
Na waona watoto wadogo watilie cartoons waangalie? Pana vibonzo kuvaa nguo seksi, pana kushumiana hapo, pana... Hapana salama ata ni sharti ukae nao watoto muangalie vibonzo pamoja.
 
Na pana vipindi vya dayet. Toka mama wenye mikono tepwetepwe ya "bingo wings" wataka daet, mpaka mabinti zao wataka "size zero" kama kina Naomi na kina Kate Moss. Na watoto wa 5 mpaka 12 wataka wembamba wa "Victoria Secret Angels". Upate mtoto wa miaka 6 hali akashiba - ataka kuwa "anorexic". Mwengine apakie ale ale wee, akisha tu akimbilia chooni ajitie vidole vya mdomo na kooni atapike alivyokula ili asinenepe - yaitwa "bulimia".
 
Na kuna vipindi kibao vya kuonesha namna ya kutumia madawa ya kulevya. Mtoto hajui mjani ni nini afundishwe kusokota bangi; mtoto hajui tafauti ya brauni na kokeni sasa ajuwe mpaka tafauti ya stimu zake; mtoto hajui vibugizi ni nini sasa ajuwe Roche 5 na Valium ni nini; mtoto hajuwi tafauti ya Speed na Ecstacy wala Yabaa sasa ajuwe. Na Crystal Meth haijuwi kipindi kimfundishe, kimfundishe na Crack Koken ni nini. Na wee wamwambia asianze kuvuta fegi na wee mwenywe ndani ya gari na ndani ya nyumba fegi wavuta.
 
Na jee vipindi vya kujikwatua? Namna ya mschana kutia make-up, namna ya kuvaa Push Up bra kwa wenye matiti madogo, na feshen zilizoingia mjini za T shirt za waschana wa miaka 6 zasema, "Too Many Boys, Too Little Time' na "I'm A Pornstar", n.k.
 
Au uwangalie vipindi vya kujitoa roho, "suicide". Mtu ana depreshen akajiuwe. Mwengine ajiona aanza kupiswa ale sumu aage dunia. Zaa jenereshen hapa wee wafkiri watafika hadi hii au hawafiki na wao wakuona wewe ni Mwafrika uliye nyuma wao ni  Wazungu.
 
T.V. iko kila rumu, mpaka jikoni pana T.V. mama hataki kukosa "Keeping Up With The Kardashians", na nilikwenda kwa swaiba mmoja ana 14 inch T.V. chooni, atizama akinya. Ndio T.V. ikaitwa "Iblish Namba Wan." Jee, "majuu" pana cha salama na bilisi ni huyu?
 
b. Mtandao
Hayo yote ya T.V., na yaliyo mabaya zaidi, yapatikana kwenye Mtandao (internet), buree. Mpe mtoto kompyuta ndani ya chumba chake na ushampa leseni ya kuharibika. Na watoto wana laptops na wana na smart phones, kwa hivyo kontroli wewe mzazi huna. Na si wao tu, nyinyi wazazi hamuko immune. Mutaanza taratibu taratibu kuangalia hiki na kile mukitahamaka mwaangalia machafu bila ya mipaka.
 
Na "Facebook". Nkiiona picha na profail yako tu, nakushtua kwa 'nudge' bas, twaanza mawasiliano. Tutongozane wee, ukitahamaka jamaa ashamlala dem. Licha ya watoto, ingia kwenye hiki "kitabu cha sura" na utaona watu wazima waliohusudiana zamani lakini maisha yalikwenda vengine, wakaowa na kuolewa na watu wengine, wengine wakahama mij, na wengine wakatoka nchi khasaa, wao ni marafiki wa muhibu wao wa zamani japo wao ni watu makamo sasa na femeli zao na watoto wao. Wakipata chansi tu washalalana na hawa long-lost lovers. Kweli si kweli? Kweli tuputupu.
 
c. Michezo ya Xbox na vifaa vengine vya mawasiliano
Watu "majuu" hawaangalii sana snema au vidio. Sasa ni vidio gemz. Hakuna mtoto asiyekua na Playstation au Xbox 360. Hizi ni kama DVD player, waya zendazo kwenye T.V., na remote kontroli yake. Basi kijana antoka skuli aeza cheza gem apigana na watu kama "Call of Duty 2: Modern Warfare" 5 hours non-stop. Au "FIFA World Cup 2011" au...
 
Na baba nae? Hal kadhalika. Aeza cheza kwenye Playstation 3 yake "Grand Theft Auto IV" ya kufurushana na magari na kutefuliana risasi Los Angeles, au "James Bond" video game, au...
 
Na mama nae aeza kuwa na Wii yake acheze "Brain Game" au "Exercise That Bum!" au...
 
Watu wapoteza wakati wao - masaa mengi kila siku washiriki upuzi. Badala ya watu femeli kukaa kula pamoja na kuzungumza au kushauriana wamuona baba yuko bizi kwenye internet, kijana yuko kwenye Xbox 360 yake, binti a chat kwa SMS yake wala hujui a chat na nani, na mama nae aangalia "The Bold and the Beautiful" - wote pengine wako siting rum, lakini wote wako mbali kimawazo wamo katika dunia zao. 
 
d. Maswaiba
Wazungu wasema, "No man is an island." Hii ni kweli kwa wote, waume, wake, na watoto pia. Mwanamume awe na marafiki enda ku chill nao wikendi. Wakacheze snooker, wakaangalie boli, n.k. Marafiki mara nyingi si Wasilamu, kwa hivyo kwa hawa, hapana mipaka, wao wafanya mambo yote. Wazini, walewa, n.k. Wee mwanamume andamana nao tu, na sooner or later, utaingia ndani ya ngoma yao. Ndio mtume S.A.W. akatutahadharisha tujichunge sana na marafiki waovu.
 
Na wanawake hal kadhalika. Na ukisema wasiwe na marafiki illa Waswahili, bado hawajapata salama. Zile illa 27 za Waswahili zitakuja kuplee hapa, ukishtuka mwanamke amuandalia mumewe gati na soda na ubani na mziki, halafu mke aaga enda muona rafki yake Maimuna kumbe waif yuko chemba kwa Maimuna akumtwa na mshkaji!
 
Na watoto jee? Marafiki ni kina Robert na Suzanne, pana cha salama wende kwao masaa 5, au walale overnight waje asubuhi?
 
e. Father's Day na Mother's Day na malav ya Valentain
"Majuu" watoto wakifika miaka 16 au 18 washatoka nyumbani watia gange na kukodisha nyumba zao wenyewe. Washapata "freedom". Basi kama wana boi-/gal-fren wao waishi nao, wajishughulikia nafsi zao. Waeza maliza mwaka mzazi haulizwi kheri wala shari. Akipigiwa simu mara moja kwa mwezi basi ni bahati kubwa. Kwa sababu hii, Wazungu wakaweka hii "Mother's Day" na "Father's Day" kujaribu kuwahimiza watoto wawanunulie zawadi wazee wao, na kama wankuwa wakongwe na wamo ndani ya nyumba za wazee wakawatembelee huko.
 
Na hivi ndivyo Waswahili wanavyoelekea. Mafundisho ya Kiislamu ya hadithi ya kuwa, 'Pepo iko chini ya akina mama', na aya ya kuwa, 'M'ngu ameamrisha usimuabudu illa Yeye, na uwatendee wema wazazi wawili' watoto wa huku "Majuu" ilmu hii ya Madrasa hawaijui. Ndio washika mila za kikafiri - mtoto hamkumbuki mzazi wake mpaka siku hizi mbili! Ilhali ya kuwa killa siku kwa Muislamu ni "Mother's & Father's Day!"
 
Na pana "Saint Valentine's Day" Februwari 14. Valentine ni watu watakatifu (saints) wa Kitaliani waliouwawa katika kutetea dini yao ya Kikatholiki. Kuoneshana mahaba baina watu wapendanao wawili hakuhusiani kamwe na na hawa mashahidi wa Kikristo, na kumpelekea chakleti na mawrdi na kadi unayemtongoza si sunna ya Mtume S.A.W. wala faradhi ya M'ngu S.W. bali yapingwa vikali na Uislamu. Watu wamo na sisi tumo tu pasi na kufahamu tu?
 
Au pana hizi sherehe za bathdee. Wapi yasema mtume S.A.W aslisherehekea bathdee yake akafanya keki akaiwashia mishumaa na akaiwashia kandili? Hapana aya wala hapana hadithi. Hapana illa uzushi tu.
 
Ndio watu wakawaida wasiokua Waislamu wana bathdee zao, na pia wana bathdee kubwa kama Wakristo wana maulidi ya mtume Isa (A.S.) Disemba 12 (na wanahistoria wote waikataa kamwe tarehe hii!); bathdee ya wavlana wa Kiyahudi wakibaleghe umri wa miaka 13 wana ‘Bar Mitzva’ na wavlana wa mashekhe wa Kibaniani (mabrahmini) wakibaleghe wana ‘Upayana’ wakavishwa vijikamba vitakatifu kwenye vitengele vya mikono; Emerika pana ‘Sweet Sixteen’; Waschana wa Kilatino wana ‘Kwinseyanera’ wakifisha miaka 15; na Majapani wana maulidi kubwa watoto wakifisha miaka 20.
 
Bathdee zote hazikuamrishwa kwenye Uislamu; sherehe tulizonazo ni mbili kwa hisabu, Eid ya Mlo (Eidul Fitri) baada ya mwezi wa kufunga wa Ramadhani, na Eid ya Haji (Eidul Adh-haa) iliyo siku baada ya Iblisi aliyelaaniwa kutoa kilio kikubwa kwa mkusanyiko wa waumini wanao omba maghfira na kusamehewa Arafa.
 
 
Hizi ni sherehe za kuzaliwa, na pana sherehe za kufa pia. Kwa mfano a ‘wake’. Huu ni usiku kabla ya maiti kuzikwa, pengine ashamaliza wiki 3 mochari. Azikwa kesho na usiku wa leo watu washerehekea wakanwa tembo na kupaati hapo wee.
 
 
Pana jamaa mmoja kazini. Sku moja hakuja. Bosi akampigia simu. Jamaa akipokea asema kwa kilio na kwikwi kua anfiliwa. Bosi akampa pole, kisha akaulizwa aliyekufa ni nani? Jamaa acajou aliyekufa ni mbwa wake. Na jamaa ni bleki huyu. Hakukaa sana kazini bali alifutwambali.
 
 
Kwa hivyo “majuu” Waswahili tunasherehe mia ni kidogo, na zote twaigiza watu wengine. Watoto wenyewe wengi wankulia na kuzaliwa huku “majuu”. Wengi wao Uislamu hawaujui kamwe, kisha twawatwika sherehe zisizokua na misingi ya Kiislamu, na nyengine zisokua na kitwa wala maguu. Jee, huku ni kuongoka huku?
 
f. Nyama za haramu
Afrika mukishaskia nyama za haramu mwaona ni nguruwe tu. Au pengine nyama ilojepwa. Pana haramu namna nyingi jamani!
 
Nenda "Burger King" nyama iliyoko si ya halali. Ya halali huchinjwa kwenye shingo damu ikamtoka mnyama yule ikabakia nyama isioyokuwa na damu mfu. Mzungu asema kuchinja huku ni unyama, si ubinaadamu. Ati yule mnyama aumia. Kwa hivyo Mzungu ampiga a bolt gun - ataekewa gani kwenye kichwa kisha ukitefuwa chatoka chuma kama tumbuu ya mlango kwa kasi kubwa sana ikamuingia ndani ya ubongo wake. Wasema huku kwaleta kifo cha ghafla kwa hivyo yule mnyama ha-safa!
 
Nyama hiyo ni haraaaam. Kwa hivyo nenda Nijmegen iliyoko Holland, au Hamburg iliyoko Ujeru, au Sandvika iliyoko Norway, au Lublin iliyoko Poland, au Limerick iliyoko Ireland, au Calgary iliyoko Kanada, au Tacoma iliyoko Emerika, au Montevideo iliyoko Uruguay, au Wagga Wagga Ostrelia, jua ya kuwa mlio wa gude ni mmoja. Wanyama wauliwa kinyama kwa hizi tumbuu za bunduki, na nyama hizi ni najis, haraam.
 
Lakini Waswahili wengi kuzila wazila wala roho haziwapigi. Yuko Frankfurt anaona kuku wa kuchoma barabarani anunua akala ata habari hana. Wanyama halali lakini uuwaji wao ni wa haramu. Basi kuna wale walao nyama za haramu moja kwa moja, nyama ya nguruwe, wala habari hawana. Ukila nguruwe, kweli utafunga swala uswali baada yake?
 
Ata tunshindwa na Baniani mmoja mwenye duka Venkuva, Kanada. Niliingia dukani mwake nkaona nyama ya kuku infanywa burgers. Aniuliza ntapendelea kuinunua? Namjibu mimi sili illa nyama ya halali. Anamibia, "I'm not halal, but this meat is halal."
 
g. Uchafu mabarabarani
Utaingia dukani kununua maziwa na mtoto wako na pana magazeti na majarida ya mkatano on display. Sasa, uwende dukani peke yako sku zote?
 
Au mtoto aone gazeti kwenye basi alifunguwe - page 3 yaonesha mwanamke matiti wazi. Sasa utafanyaje? Haya kata hiyo picha ya Page 3 na akisoma, kijana wako au binti wako aona advataizment ya 'Marie Stopes' yasema, "One up the bum and you won't be a mum" - yaani ukitia/ukitiwa nyuma hushiki mimba. Ndio mafundisho ya Uislamu haya?
 
Mukitembea femeli barabarani hamukosi kupambana na advertising posters za uchafu. Wanawake nusu uchi Carnival ya Rio de Janeiro Brazil wakatika samba, na advert yenyewe ni ya shirika la ndege lina 'ofa' ya tikiti rahisi. Advertizment kibao, na nyingi ni za ulaanisi.
 
Au mwatembea park (ma gaden) mwida mwapambana na maandamano ya mashoga na misago. Yabidi mugeuze njia chapchap, laa sivyo utamuanzia kuwaelezea wapi kijana na binti kuhusu mambo haya na ata miaka 7 hawajafika?
 
Au muone maadamano ya wanawake wavaa kimalaya na nguo zao zasema, "We're all sluts".
 
Au pengine park mumpambana na "Naked Bikers" - waume kwa wake tupuu wapeleka baskili hawakuvaa hata soksi!
 
Au munkwenda bichi muone halaiki ya watu, waume kwa wake, wako tupuu waingia ndani ya bahari ili wavunje rekodi ya watu wengi zaidi kuogelea tupu au pengine ni katika kule kukusanya pesa za sadaka - charity swim hiyo. Sama ina vituko "Majuu".
 
Mukiamua mwenda zenu nyumbani mushike treni mupambane na "No Pants Day" - madem treni nzima hawakuvaa skati wala suruwali, wana chupwi tu. Haya mwatoka. Pandeni basi mukute waume wawili wako viti vya nyuma wabusiana. Haa shukeni sasa nendeni kwa miguu na nyumbani ni maili 10.
 
Walio "matini" wengine wayatamani haya, lakini kuwa na watoto kwanza kisha utatanabahi kuwa mambo haya ni hatari kubwa. Si ekshen spiks lauda den wadz? Mwana akishaona vituko hivi si ni hatari? Bali ata kwa wewe baba na mama imani yako yadhoofika pasi nawewe kutanabahi kamwe!
 
Au mbali na parks na mbali na mabichi, waeza tembea sehemu zenye "ustaarabu" - pana ma theatres zenye kuonesha drama ndani yake, ukampata binti yako wa miaka 10 asoma title ya hiyo play mlangoni mwa hiyo theatre yasema, "Puppetry of the Penis" - la haula. Ukikata kona waona theatre nyengine yasema, "Vigina Monologues." Hii ndiyo "Majuu."
 
Mazingara yalioko huku "majuu" ni namna hii, na maskuli marafiki namna hii, je wafkiri wewe Mswahili uliye kuja tafta maisha huku “Majuu”, wafkiri laif yako itakua vipi? Kuswali pengine huswali, waif havai buibui wala hijabu, watoto hawendi madrasa. Binti yako akiwa na mshkaji akikuletea mimba uilee, utastaajabu kweli? Huwezi kustaajabu.
 
 
Videos: